Ujenzi wa Bandari ya Abiria Mpigaduri(Zanzibar), Upande wa Tanzania bara nasi tuwekeze kwa Bandari nyingine ya kisasa ya Abiria

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,958
12,556
Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar kupitia shirika Lao la Zanzibar Ferry Development wamesaini mkataba wa ujenzi wa bandari ya boti za abiria, ndege maji (Sea Plane) na sehemu ya kupaki na kufungia boti eneo la Mpigaduri lengo kuu ni kupunguza msongamano wa abiria Malindi Port (Darajani).

Huu ni mradi wa kupongezwa Sana kwa Rais Dr H. Mwinyi katika miaka ya karibuni, hii inabidi iamshe upande wa Tanzania bara na kujenga bandari ya boti za abiria na sehemu ya kufungia boti. Maana eneo la sasa limezidiwa na halina parking za kutosha,idadi ya wasafiri kuongezeka.

Kwenye uchumi wa Blue uwekezaji unapofanyika Zanzibar unaleta athari chanya upande wa Tanzania Bara. Kujengwa kwa Mpigaduri Port kuna fanya watalii na wageni wanaokuja Dar au Zanzibar kupita sehemu zote hivyo upande wa bara pasipo boreshwa panakuwa kero kwa wageni na watalii.

Bagamoyo panafaa kuwekwa bandari ya abiria kama ya Mpigaduri. Bandari itakayo hudumia boti za abiria, boti ndogo, ndege za baharini(Sea plane) na sehemu ya michezo ya baharini (Eneo la Marina Park).

Tukiwa na bandari ya abiria eneo la Bagamoyo itachochea zaidi watalii wanaokuja Bagamoyo,Hifadhi ya Saadan,Fukwe za Pangani,Mkwaja mkoani Tanga kwenda kutalii Zanzibar na waliopo Zanzibar kuja upande wa pili. Watalii wanaotoka Dubai, Mombasa na South Africa na yacht zao itakuwa ni rahisi kufika eneo lenye maegesho ya boti mara kwa mara.

References

View: https://youtu.be/X44Kf9AiNHI?si=VyIwMwo6oNJpN72R

View: https://youtu.be/fRlptjAt1A8?si=WAuXq292Ayi-tFy2
 
TPA imesema mwaka ujao wa Fedha itajengwa Gati 3 Mpya ikiwemo ya abiria
 
Back
Top Bottom