Ni muda tu wamewapa serikali lakini watatoa habari tuKwa wanaofuatilia masuala ya diplomasia, wanatambua kuwa mara nyingi balozi za Marekani, Uingereza, Canada na Umoja wa Ulaya nchini Tanzania huwa mstari wa mbele kutoa matamko pindi viongozi wa upinzani wanapokamatwa. Kumbukumbu ya karibuni ni balozi hizo zilipoijia juu serikali ya Magufuli kufuatia kukamatwa kwa Marehemu Maalim Seif na viongozi mbalimbali waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana...