Kwaherini JF

Status
Not open for further replies.
Umenena vizuri sana Mkuu.
Kiukweli,
Muda wote tujiweke tayari kuondoka.
Tuishi maisha matakatifu.

Ugomvi wa kijinga na watu tuache,tufocus kwenye ibada.
Muda wowote na saa yoyote ikija tujiamini kwamba tunaenda mahala pema peponi.
 
YEAH NAAMINI HUYU SISTA ANAWEZA KUA ANAUMWA CANCER, ITS TRUE, NAKUMBUKA YULE WAZIRI, ALIKIA ANATOA STORI YA MAISHA YAKE ANADAI, SIKU HIYO ALITOKA DODOMA AKAPANDA NDEGE KWENDA DAR PALE MUHIMBILI ALIKUA AMEENDA CHECK UP, HAKUA NA TATIZO LOLOTE LOLE MWILI WAKE ULIKUA SAFI KABISA.

ILIKUA NI KAWAIDA YAKE KUFANYA CHECK UP, SASA KAFIKA MUHIMBILI, AKAMKUTA DOKTA KISENGE WAKATI HUO NDIO ALIKIA DOKTA WAKE WA CHECK UP, WALIFANYA CHECK UP, NA BAADAE ALIONDOKA KIA ATATUMIWA MAJIBU KWENYE SIMU. AKIMWAMBIA DEREVA WAKE WAWASHE GARI KURUDI DODOMA, WAKIWA NJIANI ALIPIGIWA SIMU NA DOKTA KISENGE, AKIULIZWA UKO WAPI MUHESHIMIWA, AKAJIBU YUPO NJIANI ANAELEKEA DODOMA KWENYE KIKAO, DOKTA KISENGE AKAMWAMBIA AGEUZE GARI HARAKA, AANZE SAFARI KWENDA INDIA MANA AMEBAINIKA NA CANCER, CHA KISHANGAZA HUYO WAZIRI HAKUA NA DALILI YOYOTE ILE KIA ANA UMWA.

IKABIDI AMWAMBIE DEREVA AGEUZE GARI KURUDI DAR WALIPO FIKA, AKAONANA NA DOKTA KISENGE, HAPO HAPO SAFARAI YA KWENDA INDIA IKAANZA, UNAAMBIWA KAFIKA INDIA BADO HAAMINI KINACHO TOKEA, AKASHANGAA ANA NYOLEWA NYWELE ZOTE NA MAISHA YA KITANDANI YA KAANZIA HAPO, HII STORI ILINIFIKIRISHA SANA KAMA KUNA MTU ANAMFAHAMU HUYU WAZIRI ATWAMBIE JINA LAKE JAPO MPAKA LEO BADO ANAISHI, STORI NIMEISOMA MAHALA HATA MIEZI MITATU HAIJAPITA, ALIKUA AKISIMULIA YEYE MAPITO YAKE, UNAAMBIWA INDIA ALIKAA KAMA MWAKA, ANAWASHUKURU WATOTO WAKE MKEWE NA FAMILIA YAKE KWA UJUMLA KUSIMAMA NAE.
 
Wazo zuri
 
Majina ya hawa Joanah mawili yananivuruga.
Huyu ni yule akikue ba profile picture mwanamke kavaa vit3nge

Au yule kuna mwanamke kavaa ki blouse cheusi

Back to the topic. Dying is not the end. Right now tengeneza njia...
 
Kama wewe ni mfatiliaji wa mziki kuna msanii anaitwa BRACKET anatokea NIGERIA aliwai patwa na CANCER na akapona vizuri Tu ( kumaanisha CANCER ilikuwa stage ya mwanzo aliwai pata matibabu). Kwahiyo pia mleta mada asijikatie tamaa anaweza pona vizuri tu.
 
Kama ana kansa ,ina maana alienda pale OCRI ,na kama ameenda hapo means ameanza tiba kwa hatua iliyofikia hiyo kansa
 
Duuh kuna umuhimu wa kufanya checkup mara kwa mara
 
Nigeria mbali,Babuu wa Kitaa,yule pale ni Balozi wa kansa na ana Taasisi yake ya kupambana na Kansa
 
Hey people,

Uzi huu ni wa kuwaaga wanaJF wenzangu

Nimekutwa na cancer ambayo kimsingi nimepewa taarifa kwamba ndani ya miezi miwili sitakuwepo

Naumia lakini sina jinsi
Take Courage Dr. Sio Mungu.
Pengine kuna kitu Mungu anataka kujidhihirisha kwako.
 
Mimi sijakata tamaa lakini kuna nafsi inaniambia sifiki mbali
Believe me, ukiweza kuishinda hiyo nafsi utaishi.

Kuna roho ya uzima na roho ya mauti,.

Roho ya uzima utaihuisha utapojiamini, amini hutakufa utaishi kwa msaada wa Mungu unaemuamini, roho ya uzima ni kama battery ya simu, ikiisha chaji utaichaji kwa kusoma biblia, sikiliza gospel na mahubiri.

Roho ya mauti inapata nguvu utapokuwa na hofu, ukiwa na hofu utaididimiza roho ya uzima na kuihuisha roho ya mauti, usiwe na hofu.

Hata ukisoma biblia, neno USIOGOPE limerudiwa mara nyingi sana, hii ni kwasababu shetani hutupata kupitia hofu tunazokuwa nazo maishani hasa tukipitia changamoto tofauti.

Humu ndano wote tunapenda uishi, basi amua kuishi kwa kuishinda hofu ukimtumainia Mungu, ya daktari huu sio wakati wake tena, huu ni wakati wa imani, AMINI.
 
Nimesoma comment zote hadi hiinya mia tano na zaidi, nimejifunza vingi mno.
Kuna watu wamepitia magumu sana , kiasi cha kusema dunia haina huruma , dunia ni kama vile haimuhitaji mwanadamu.


Anyway Joanah kwa baadhi ya Replay zako kwenye uzi huu hapana shaka kuna ukweli .

But imani yangu bado ipo pale pele , utaishi maadamu dunia na jamii ishakupokea na unahitajika, kama kilicho kuleta duniani kimeshakamilika basi utaondoka kwa amani , na hii ni sote, lakini kama ni bado nina hakika ukijaliwa uzao utamshuhudia mtoto wa mtoto wako , naomba ikifika kipindi hicho ukumbuke comment hii.

Pole, tu pamoja nawe, na tokea sasa kuwa na furaha na amani.
 
Barikiwa sana
 
Nakufa ndoa yangu ikiwa changa ambayo hatujapata uzao wowote 😭😭

Nakufa namuacha baba yangu
Nakufa namuacha mama yangu

Ee Mungu

Ni kweli kifo kipo Joanah, kama ilivyo kwa kila mmoja wetu wakati ukifika.

Narudia tena, huu sio muda wako wa kufa, hautakufa bali utaishi, ndoto ya kituo cha afya itimie, upate watoto na uwaone wakikua uweze kuwa shuhuda wa matendo makuu ya Mungu
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…