Kwa waliosoma Azania sekondari.

Wagumu walikua TA (Tambaza), ASS (Azania Soma Sana) walikuwa mabishoo.

Hapa ndipo penyewe!! walikuwa wanavaa kaptura na mikanda miwili na chini lazima ipigwe turn over!! kitambaa kile cha kaki kilikuwa kinawashwa pasi na sio kupiga pasi!! maana mbele kama kisu hapo usikutane nae anaelekea fire kupanda basi na mfuko wake wa rambo nyuma mabinti wa jangwani. Anavyodunda utakataa ;-) kama anaishi kule kwetu uwanja wa fisi! hapo bado hajafika mtaani kuonyesha kila mtu kwamba anasoma Azania..................
 
Namkumbuka H/Master Andrew Kwayu, Mama Temba akitufundisha 'Namba ', 'Kicheche' akitufundisha siasa.
Bible Scripture aiidha pale Don Bosco au ktk jengo moja pale karibu na Muhimbili Hosp.
Ugomvi ktk soccer sie na Tambaza Boys miaka ya nyuma ilikuwa kitu cha kawaida. Siku moja ulitokea ugomvi mkubwa pale ktk uwanja wa shule Muhimbili P/School, tukavulumishiwa mawe na vijana wa O Level, refa alikuwa Padri mmoja wa Ki-Phillipino toka Bon Bosco, baada ya hali kuwa mbaya alichomoa bastora na kupiga risasi mbiili juu! Hiyo ikawa salama yetu.
Nakumbuka ilikuwa tukichoka ku-bukua, tulikuwa tukiingia Pale Paramedical Muhimbili kucheza disco.
Kipindi hicho tukiwa na akina Akilimali Kighoma Malima, Patrick Mkandya, Ismael Kulengwa(Mzee wa kambi), Asimwe Kabunga, Lusajo, Arnold Nzali; Tito William, Muhindi Musyangi, Nelson (Easy E), Rweyemamu (Mom), Adronicus Buberwa, Kantalamba, Abraham Chenelo na wengine wengi.
 
enzi hizo! Azania ilikuwa bomba sana na lebo yetu ya ramani ya africa, ukipita mtaani hasa kwa mabinti unajitahidi lebo inaonekana!
Mwl. Miti mingi yupo wapi siku hizi?

Unamkumbuka yule mzee wa kichagga, mwangalizi wa mabweni aliyekuwa anakaa peke yake pale karibu na bweni la O' Level?
Hata jina nilishasahau! Punishment kipindi kile ilikuwa kulisha yale maviti moto karibu na jiko la shule.
 
Ama kweli watu mnasahau mimi na umaarufu wote simo kwenye list!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????.
 
Unamkumbuka yule mzee wa kichagga, mwangalizi wa mabweni aliyekuwa anakaa peke yake pale karibu na bweni la O' Level?
Hata jina nilishasahau! Punishment kipindi kile ilikuwa kulisha yale maviti moto karibu na jiko la shule.

Unamzungumzia mr yengela?Yule alikuwa tungi ol the time..afu akija na demu sie tunapanda ghorofani kuchungulia akipiga game daah!!
 
Wagumu walikua TA (Tambaza), ASS (Azania Soma Sana) walikuwa mabishoo.

Dah mi nlisoma pote Azania o level na Tambaza A level!!
Mtaani tulifaulu saba tu,na kipindi hicho hakukuwa na shule za kata so bichwa kubwa kitaa nlikua naonekana bonge la jinias!
 
Ulikuwa raha sana
basi mie mtaani nilitoka peke yangu, aisee niliwatesa watoto wa manzese!!!

Kuna kwayu,yengela,mchwampaka,madam mabano,madam shirima,biology lab unamkuta mwalimu omari daaaah we had a great time jameni!
 
....sijui ulikuwa mwaka gani azania, miaka niliyokuwa mie jangwani vidume vya azania vilikuwa vinajigonga sana kwa wasichana wa jangwani......hadi kula chipsi walikuwa wanakuja kula jangwani kwa Z ilimradi wapate kampani ya wasichana.
 
Ulikuwa raha sana
basi mie mtaani nilitoka peke yangu, aisee niliwatesa watoto wa manzese!!!

We ulisoma azania o level ama a level?Ulimaliza mwaka gani?Ulikuwa darasa gani?Mi nlikua darasa N form 1na 2 na darasa R form 3 na 4..
 
....sijui ulikuwa mwaka gani azania, miaka niliyokuwa mie jangwani vidume vya azania vilikuwa vinajigonga sana kwa wasichana wa jangwani......hadi kula chipsi walikuwa wanakuja kula jangwani kwa Z ilimradi wapate kampani ya wasichana.

Wakati nyie mlikuwa mnakuja kusomea forest mmesahau?
 
Afu nani anakumbuka jolo?Dah ilikuwa sh mia mbili tu siku umeiona hasa kwa tuliokaa hostel!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom