Kwa waliosoma Azania sekondari.

jchofachogenda

JF-Expert Member
Jan 8, 2012
537
123
Jamani wana Azania wenzangu naomba tujikumbushe kipindi kile tukiwa shuleni.Nakumbuka kipindi hicho ukifaulu kwenda Azania unaheshimika mtaa mzima.Ndio shule pekee ya serikali iliyokuwa na wanafunzi wa kiume pekee katika mkoa wa Dar es salaam.Si mnakumbuka nickname yetu ya shule ya Azaboys?Tulikuwa tunajiita wagumu hivyo masholi wa Jangwani sekondari hatukuwafagilia.Tulikuwa tunawasumbua sana walimu wetu kwa kukimbia masomo ya darasani na kwenda tuition.Je unamkumbuka yule mwalimu wa nidhamu aitwae Mchwampaka?Unamkumbuka mkuu wetu wa shule aitwae Andrew kwayu?Naomba mnikumbushe mengine wana AZABOYS.
 
Azania haikuwa spesho skuli banaa! Mi nilifaulugi spesho skuli, nilikuwaga na akili, sijui zilienda wapi! Aaaggghhhrrr, bhange haina adabu! Ila nimeacha siku hizi...

Oh yeah...ulifaulugi spesho skuli ipi?

Na vigezo vya kufaulu spesho skuli vilikuwa ni vipi? Manake mpaka sasa sijaona uspesho wowote toka kwa hao spesho wanafunzi :lol::lol::lol:

Bado wanakula mavumbi tu kama hawana akili nzuri lol
 
Kula bata haihusiani na akili banaa! Ukiangalia vizuri utaona uspesho, na kigezo kilikuwa marks nying za mitihani. Acha wivu basi jamani! Mi nilifaulugi ilboru,lol
 
Kula bata haihusiani na akili banaa! Ukiangalia vizuri utaona uspesho, na kigezo kilikuwa marks nying za mitihani. Acha wivu basi jamani! Mi nilifaulugi ilboru,lol

Kheee! Kumbe na wewe Kongosho....yaaaalaaah!!!!

Ila unajua nini, yale mafeki jamaa aliyoniuzia yalikuwa ya uongo! La sivyo tungebanana wote Mzumbe:poa
 
NN utakuwa professional mchakachuzi.
Ulianza mafeki la saba?

Bora mie nilianza fomu foo.

Kheee! Kumbe na wewe Kongosho....yaaaalaaah!!!!

Ila unajua nini, yale mafeki jamaa aliyoniuzia yalikuwa ya uongo! La sivyo tungebanana wote Mzumbe:poa
 
Nakumbuka miaka ile ya 80s mtu wangu mmoja alikwenda Forodhani kitaa kizima aliheshimiwa!!
 
Nilikuwepo

Ezi za Kwayu headmaster
second mistress yule mama aliamia wizarani ..
Discipline master MchwaMpaka

Kwa zamani kweli ilikuwa sifa fulani ..sidhani kama ni anymore..au mimi niko out of touch.Maana naona wazazi wengine hawapeleki tena watoto wao shule hizo japo wamechaguliwa...na pia cha msingi ni matokeo ya mwisho ktk maisha shule ni mwanzo tuu
 
azania zaman bwana....................siku iz kila mwanafunzi anajitia kabo snoop visuruali vinawabana. hakuna wagumu wala afu wamekuwa vilazaaa.
 
Azania haikuwa spesho skuli banaa! Mi nilifaulugi spesho skuli, nilikuwaga na akili, sijui zilienda wapi! Aaaggghhhrrr, bhange haina adabu! Ila nimeacha siku hizi...
Huo ni wivu na roho mbaya,unajifanya hujui kuwa Azania sekondari ilikuwa special school kwa wavulana katika mkoa wa Dar.Ngoja nikukumbushe na kama unabisha kamuulize Kapuya au Mungai mawaziriwetu wa elimu enzi hizo.kwa wasichana walikuwa majirani zetu wa Jangwani.Ili uende Azaboys ulitakiwa kupata maksi 120/150.Sasa nakutajia special nyingine Tanzania kwa enzi hizo.kwa wavulana,Ilboru,Mzumbe,Kibaha,Mkwawa,Tanga technical na Tabora boys.Kwa wasichana,Msalato na Tabora girls.Hizo shule nilizotaja ilikuwa huchaguliwi mpaka upate maksi 140/150 au zaidi.Je una hoja?
 
Back
Top Bottom