Kwa waliosoma Azania sekondari.

daaah Azaboy, mie namkumbuka yule jamaa aliyekua anauza karanga kwa kupima na kisoda! Sijui alikua anatuwekea nini kwenye karanga zake...ni lazima kila day ujisikie kuzionja tuuuu
 
....sijui ulikuwa mwaka gani azania, miaka niliyokuwa mie jangwani vidume vya azania vilikuwa vinajigonga sana kwa wasichana wa jangwani......hadi kula chipsi walikuwa wanakuja kula jangwani kwa Z ilimradi wapate kampani ya wasichana.

Tutajie mwaka uliosoma Jangwani kwa kuwa miaka tuliosoma sisi Azania hatukuwashobokea masholi hata kidogo.
 
azania.jpg
Jikumbushie...
 
Wagumu walikua TA (Tambaza), ASS (Azania Soma Sana) walikuwa mabishoo.

sio kweli hata kidogo Azania hatukuwa mabishoo na kama tungekuwa mabishoo tusingeletewa Discipline master mkali mpaka akawa maarufu Dar es salaam yote namaanisha Mchwampaka.Walichotuzidi Tambaza ni kwamba walikuwa wanaweza kuanzisha vurugu sehemu yoyote na hadi kusabasha kumuua mtu. Unakumbuka walivyomuua yule kondakta wa daladala mwaka 1994.Huo ndio ulikuwa mwisho wa o'level Tambaza,tukabaki vidume sisi tu Azaboys.Walizidisha sana ndumu wale.
 
daaah Azaboy, mie namkumbuka yule jamaa aliyekua anauza karanga kwa kupima na kisoda! Sijui alikua anatuwekea nini kwenye karanga zake...ni lazima kila day ujisikie kuzionja tuuuu

Haloo umemkumbuka yule muuza karanga!alikuwa na taiming ya muda yule.Saa nne tu katia timu,unamkumbuka yule ticha mlevi alltime?Tukumbushe na mengine aisee.
 
Huo ni wivu na roho mbaya,unajifanya hujui kuwa Azania sekondari ilikuwa special school kwa wavulana katika mkoa wa Dar.Ngoja nikukumbushe na kama unabisha kamuulize Kapuya au Mungai mawaziriwetu wa elimu enzi hizo.kwa wasichana walikuwa majirani zetu wa Jangwani.Ili uende Azaboys ulitakiwa kupata maksi 120/150.Sasa nakutajia special nyingine Tanzania kwa enzi hizo.kwa wavulana,Ilboru,Mzumbe,Kibaha,Mkwawa,Tanga technical na Tabora boys.Kwa wasichana,Msalato na Tabora girls.Hizo shule nilizotaja ilikuwa huchaguliwi mpaka upate maksi 140/150 au zaidi.Je una hoja?

uongo!
Azania haikuwa, na haijawahi kuwa special schule. Ni uoga wa wanafunzi wa Dar kuichagua, kama ulikuwa na guts za kujaza kwenye fomu ya SELFORM, halafu ukapata reasonable marks, wanakupeleka pale. By the way, Azania nimesoma, na special school pia nimesoma, Kibaha Boys.
 
Unamzungumzia mr yengela?Yule alikuwa tungi ol the time..afu akija na demu sie tunapanda ghorofani kuchungulia akipiga game daah!!

Yengela a.k.a. Chapombe...
Afu yule baba hana mbwembwe, akiishiwa hela hata kangara anapiga kama kawaida.
 
....sijui ulikuwa mwaka gani azania, miaka niliyokuwa mie jangwani vidume vya azania vilikuwa vinajigonga sana kwa wasichana wa jangwani......hadi kula chipsi walikuwa wanakuja kula jangwani kwa Z ilimradi wapate kampani ya wasichana.

halafu walikuwa hawapiti geti lao. Lazima waingilie geti la jangwani washangae visketi ndio waende kwao. Lol. Bora sahivi wamewekewa ukuta wa kuwatenganisha na jangwani.
 
wachumba na mashemeji nawamisije!

Sasa umesomeka,nilikuwa sijakusoma hapo mwanzo.Kumbe ulikuwa shemeji yetu,na nimegundua umesoma Jangwani kwa jinsi ulivyoreply comment ya prety.Lakini najiuliza ni Yuda(msaliti)gani huyo alievunja katiba ya shule yetu ya kutoshobokea Sket(masholi)na wewe kucheza nae mechi isiyo na jezi kwa wakati huo?Tungemjua huyo shule angehama.Hebu tuambie ni nani huyo?je ni mwana Jamii Forum?usiogope kwani shule tushamaliza.
 
Siamini kama ulisoma jangwani husninyo daaaaah!!Ukute nlishawahi kudate naww..
 
Mimi nilikuwepo enzi za headmaster:Kisamo.Makumu wake:Mzee Mejja na wakati huo A-level kuna combination ya PCM tu na tulikuwa tunajiita tupo hotelini maana misosi ilikuwa balaaaa.
 
sio kweli hata kidogo Azania hatukuwa mabishoo na kama tungekuwa mabishoo tusingeletewa Discipline master mkali mpaka akawa maarufu Dar es salaam yote namaanisha Mchwampaka.Walichotuzidi Tambaza ni kwamba walikuwa wanaweza kuanzisha vurugu sehemu yoyote na hadi kusabasha kumuua mtu. Unakumbuka walivyomuua yule kondakta wa daladala mwaka 1994.Huo ndio ulikuwa mwisho wa o'level Tambaza,tukabaki vidume sisi tu Azaboys.Walizidisha sana ndumu wale.

Get your story straight ile vagi ilikuwa 1993, hakukuwa na Tambaza Boys 1994. Mchwampaka alikuwa maarufu kwasababu ya ukali na sura yake...(unakumbuka neno u...wa paka?). Sababu kubwa ya kusamaratishwa kwa TA boys ilitokana na kuvunjwa kwa ukuta wa Muhimbili primary ambao ulijengwa ili kutenganisha shule hizo mbili kwa kisingizio cha kulinda watoto wa primary.

Wanafunzi wa TA walikasirika kwasababu walikuwa wanaenda muhimbili primary kucheza basketball (kwasababu kiwanja cha Tambaza kilikuwa cha udongo) ndipo walipoamua kuuvunja. Vigogo waliokuwa na watoto wao pale wakaamua kuifunga shule yetu mwezi July 1993 shule ilipofunguliwa (Oct 1993) walimu wote wa Tambaza wakawa wamehamishwa na baadae (1994) wakawasambaratisha wanafunzi nchi nzima.

All in all Tambaza ilikuwa ni shule nzuri yenye vifa vya maabara kuliko shule yoyote Tanzania na ilikuwa na walimu wazuri wanaofundisha tofauti na Azania ambapo walimu walikuwa hawafundishi kabisa yaani wanafunzi wanaakaa siku nzima bila hata ya mwalimu mmoja kuingia darasani. Miaka ya themanini wanafunzi wa mzizima na Shaban Robert walikuwa wanakuja kufanya practical za London GCE Tambaza kwasababu kulikuwa na vifaa vya uhakika.
 
Nashukuru kwa utetezi wakn wako hasa ukizingatia waswahili husema kila mwamba ngoma ngozi huvutia kwake. Nimeshangazwa na kauli yako eti Mchwampaka alikuwa maarufu kwa sababu ya sura yake.Umaarufu wa Mchwampaka ulikuja kutokana na kudhibiti wanafunzi wakorofi hilo halina ubishi.Mbona hujakataa kuwa mmewahi kumuua Kondakta?
 
Back
Top Bottom