Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa pesa hiyo unaweza kufanya biashara ya vitumbua au mama niwekee.
 
Inabdidi uandike business plan na uikoleze ushahidi halisia yaani unakwenda kuulizia ww mwenyewe mfano kujua kweli hivyo vitu unavyodhani vinauzika kweli kwenye hali halisi vinauzika-ulizia walau wanawake 30-50, mfano unaweza kuwauliza ni vitu gani ambavyo wanavitumia mara kwa mara au kama wangepewa nafasi ya kununua vitu vya kike wangenunua nini unaweka orodha wanatick kimoja au viwili then unakuja kuona vipi vimechaguliwa zaidi, jaribu kuwa specific zaidi-i.e. nguo za ndani km..., vipodozi km...?

Na kwa bei gani hao wateja wako unaowa-target wanasema wanaweza kununua kwa cash au mkopo! Je wapi utanunua hivyo vitu vya biashara-je umezunguka maduka kama 10 kulinganisha bei za jumla? utauzia wapi-kwa musimu au muda mrefu? Je gharama za usafirishaji?

Gharama za utekelezaji wa mradi wako- labour cost? Risk zake zipo? Mimi wazo langu hebu fikiria kutengeneza ice cream kisha uuze kwenye mazingira ya shule hasa shule za msingi au uende kiwandani kwa bhaharesa uulizie kama bei ya ice cream zao kwa jumla, uone wewe utauza kwa bei gani na faida.
 
Angalia aina ya Biashara unayotaka kufanya na soko zuri lilipo, kama ni ya chakula, tafuta maeneo yenye wahitaji wengi wa chakula, mfano, kwenye shule, hasa shule za Sekondari, madereva, makondakta, wauzaji wa sokoni, wauza mitumba, bites, juice, matunda, maeneo kama ya ufukweni, kama ni hivyo vitu vya wanawake, maybe nguo, viatu, mikoba n.k,

Kuna Maeneo kama Mwenge, maeneo ya around na Vyuo, nguo za watoto wadogo au matunda, maeneo ya karibu na hospitali kubwa n.k
 
Ndugu yangu doreen22 na london wamekupa mwanga sasa anza kazi but
tafuta zile amri za ujasiriamali, mi ntakupa chache tu;

    • ubunifu(andaa mpango wa biashara yako)
    • kujituma
    • fanya kazi mwenyewe(usiajiri mtu kwanza)
    • tunza mahesabu vizuri
    • uvumilivu
    • kubali hasara penye faida
    • ujasiri(usiogope)
    • kubali changamoto(usidharau)
    • pigania kuongeza mtaji inapobidi
    • heshimu wateja wako
    • fanya tathmini ya biashara yako kila wakati na ukibaini maendeleo chanya endelea nayo, kama ni hasi anza kufikiri upya juu ya mpango wako na uendelezaji wake.
"usikubali kufeli mtihani nje ya chumba cha mtihani"
 
Uza bidhaa zako kwa bei ambayo wananchi wanaweza kuimudu vizuri na hiyo bei iwe ni yenye kukupa faida wewe pia, ili mtaji wako uweze kukua na kukuwezesha wewe kukuza biashara yako na kuendesha maisha yako vizuri, safari moja, huanzisha nyingine!, sorry simaanishi Bia!,

But mwendelezo wako wa kibiashara, usiogope, usitishwe, maana binadamu wengi kwa kukatisha wenzao tamaa, ni kiboko, kisa wao yamewashinda, wakati si ajabu ni kwasababu ya kutokuwa makini na serious katika wanachokifanya, we pambana, steringi kwenye movie ya maisha yako ni wewe mwenyewe, kama Prof.Jay alivyosema
 
Mtaji mdogo sana na inabidi uwe mvumilivu sana kwenye swala zima la kupata faida nzuri, kama sio muuza sura nenda boma sokoni wanapouza mitumba wanaanza kufungua sa10 usiku wahi mashati ya kiume jinzi model then uanze kutembeza kwa madenti vyuoni ata kwa watu binafsi, pale uwa wanauza bei rahisi sana kuliko watu wanavyopigwa mtaani,waweza nunua labda shati kwa elfu tatu ukalipiga mpaka elfu kumi...try ilo
 
Kama uko Dar, naomba nikuagize kariakoo ukaniulizie bei ya pili pili aina ya paprika, nasikia kuna wahindi huwa wanaisaka sana ila hawajui wapate wapi kwani kwa miaka ya nyuma kulikuwa na kampuni inanunua kwa jumla, Mwaka huu kuna wakulima wamelima na hawajui wapeleke wapi. Please kama uko serious, nenda karioakoo alafu uje humu tena tufanye biashara.
 
Sasa kwa wale wanaopiga kelele za kujiajili huu ndio wakat muafaka wa kumpa mawazo mkuu.ctegemei aachwe uchi huyu ila kuna wandugu ambao c tukilalamika ajira wao utaskia vijana mjiajili.
 
Nunua videsktop viwili ufungue biashara ya kompyuta games kwa watoto
NB:kwa huku kwe2 uswazi lakini kama we wa mikocheni au pande zile zenye ikulu ndogondogo biashara itasanda mdau
 
Inafaa uianze wewe kwanza

Mbona sikuelewi.. Niianze mimi kivipi. Nina biashara zangu ambazo mtaji wake ni zaidi ya 200m wewe ndiye ulieanzisha thread ukaomba ushauri wa aina ya biashara kwa mtaji wako wa laki 3 na kuna mtu ukamjibu kwa unataka kufanya biashara kuhusiana na vitu vidogovidogo vya wanawake.

Napenda nikutaarifu wewe moyo wako kwamba sijafurahi na majibu yako kwenye thread yangu, pia nakuona wewe si mwelewa, na kwa taarifa yako biashara ya kupaka rangi na kusafisha kucha akinadada inayofanywa na vijana wengi wanaozungukazunguka na wengine wameweka vijiwe sehemu mbalimbali ambazo sio rasmi sana inalipa sana na mtaji wake ni mdogo sana. Fanya uchunguzi na usikurupuke kutoa majibu ya hovyo kwa watu usiowajua.
 
Kuna watu wanapenda kuvunja moyo wenzao!!!
Mtu anauliza unamjibu kwa dhihaka.


Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD

Kuvunja moyo kivip mkuu? Nenda kinondoni uone watu vitumbua na maandazi vinavyowatoa!! Au kama vp ngoja tumshauri kama unavyotaka wewe,moyo wangu agiza magari japan uwe unauza hapa bongo yanalipa sana!!
 
Back
Top Bottom