Interlacustrine R
JF-Expert Member
- Jan 22, 2022
- 6,010
- 12,354
Soma King James Version ambayo huwa haina ukakasi sawa na hizi Biblia nyingi za siku hizi zinazochakachuliwa na Manabii wa uwongo.Ama kwa hakika sijawahi kuelewa kwanini Kuna tofauti kuhusu agano la kale na jipya.Mkuu Undava King kama ulivyosema,Jews walimkataa yesu ilhali wao ndio watu wa kwanza kupata ufunuo kutoka kwa Mungu.Agano la kale liliandikwa kwa Hebrew language ambapo katika song of solomon 5:16 wamepotosha neno la nabii Muhhamad kwa kutafsiri as "all together lovely".Ndio maana Hadi leo wakristo hawatambui kuwa Muhhamad ni nabii.
Kwa nini nimesema hivi,Jews sio kwamba hawamuamini yesu pekee hata Muhhamad hawamuamini na sababi ni ugumu wa nyoyo zao tangu enzi za nabii Musa.Katika vitabu vyao vya kale vilivyoandikwa in Hebrew Yesu yupo pamoja na Muhhamad (Wazungu wamepotosha kwa kutafsiri jina la Muhhamad Kama "all together lovely".
Mkuu Nibiru asante kwa post yako.Mimi huwa najiuliza kuwa kuna baadhi ya watu wanasema Mungu wa Ukristo ni tofauti na Mungu wa Uislamu sasa mbona katika Biblia Mungu wa agano la kale ni tofauti na Mungu wa agano jipya.
Most people tuna claim Mungu ni mwanzo na mwisho.Yeye anajua past,present na future inakuaje Mungu atoe amri katika agano la kale na atoe adhabu alafu katika agano jipya aone kuwa watu hawawezi kufuata amri?Ina maana alikua hajui watu hawatofuata amri zake?
Katika agano la kale Mungu alisema hakuna kula nguruwe lakini katika agano jipya Peter anapata vision kuwa ale chochote kwa kua alichokiumba Mungu sio najisi.Sasa hapa Kuna Miungu miwili au Mungu anakua kigeugeu.
Je Mungu wa agano la kale alileta dhana ya Trinity?
Haya katika Quran 92:3 Allah anaapa kwa aliye umba kike na kiume.Ilhali katika Aya nyinginezo Yeye ndio aliyemuumba binadamu.
Nisiwachoshe wakuu reference zipo nyingi sana about these errors both in Quran and Bible.
ERRORS EVERYWHERE!!!
HAKIKA KAMA UNATAKA KUWA MTU MWENYE HEKIMA BASI MUNGU WAKO AWE MOYONI MWAKO THEN BALANCE MAFUNDISHO YA QURAN NA BIBLIA 50/50 NA CHUKUA YALE TU YENYE FAIDA.
Ephraem_EE.
Waebrania 13:8
"Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele."
Yakobo 1:17
"Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka."
Mungu hajawahi kubadilika, huwa habadiliki na hatabadilika kamwe!
Mathayo 5:17
"Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza."
Yesu alisema hakuja kubatili torati bali kutimiliza(perfection/kuboresha) ktk utimilifu wala si (ukamilisho/compliment) wa sheria.
Mungu mwenyewe aliyekukataza usizini ndiye aliyekukataza usiibe na hakuna hata dhambi aliyoihalalisha wala kuitetea kuwa ni ndogo kuliko zingine.
Sisi Binadamu ndiyo huwa tunabadilika lakini kamwe! Mungu muumba mbingu na nchi huwa habadiliki milele zote, Amina.