Kuna watu wanasema tuliombee taifa la Israel mm hata siwaelewi

wankuru nyankuru

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
491
763
Wapendwa napenda tena kuwaita toka ndani ya moyo wangu, mje msimame na taifa la Israeli wakati huu, nina mengi sana ya kusema juu ya taifa la Israeli, watu wake, na jiji la Jerusalem, Si kwamba nimepewa mzigo tu wa kusimama kwa ajili ya taifa la Israeli, lakini nina connection na bond isiyovunjika na taifa la Israeli, kwangu Israeli ni taifa rafiki, pia ni taifa ndugu kwangu, nimeunganishwa na hili taifa, liko ndani ya moyo wangu, upendo nilionao kwa ajili ya hili taifa ni upendo usioelezeka, nimelikumbatia hili taifa, hata kama adui anataka kurusha mishale juu ya Israeli na wayahudi, inipate mimi kwanza, lakini isiifikie taifa la Israeli wala watu wake ambao Mungu amenipa na nina wapenda sana.

I do real have a special connection with Israel, Israeli inapoingia kwenye shida, na mimi huwa ninapata mahangaiko sana ndani yangu, ni kama vile ndugu zangu wako kwenye shida, huwa kuna wakati namuuliza Mungu ni kitu gani hiki?

kwa watu wanaofahamu wanajua Israeli ipo karibu sana kuingia katika vita, iko kwenye hali ya kivita.

Mpango wa Palestina wa kudai taifa huru la palestina katika mipaka kabla ya vita ile ya mwaka 1967 Israel iliposhinda na kuliunganisha tena jiji la Jerusalem ni mpango hatari sana kwa uhai wa taifa la Israeli,

katika Muda wa siku chache zijazo, macho ya ulimwengu wote yataelekea mashariki ya kati, kuna mambo ambayo kwa kweli ukiyaangalia kwa macho ya Rohoni, yanasukuma kutimilika kwa nabii muhimu sana katika Biblia, wale student of Bible prophecy na wale wanaofuatilia habari ya Taifa la Israeli kwa karibu wanajua kitu ninachosema.

Vile vile natoa wito kwa serikali au taifa la Tanzania, Rais, na wizara ya mambo ya nje, na washauri wake wa mambo ya nje, taifa la Tanzania lisiingie katika muunganiko wa mataifa ambayo yatapiga kura kulitambua taifa la Palestine katika mipaka kabla ya vita ile ya mwaka 1967. Taifa la Tanzania lisipigie kura wala kushiriki kui endorse makubaliono yoyote ambayo yanalitambua taifa la palestine na kuugawa mji wa Jerusalem na nchi ya Israeli.

Taifa la Tanzania kama mwanachama huru wa Umoja wa Mataifa, huwa linapiga kura pamoja na mataifa mengine ambayo yako katika baraza kuu la umoja wa matiafa na pia ni wanachama wa umoja wa mataifa.

Maandiko ninayosoma yananiambia hasira kali ya Mungu ipo kwa ajili ya mataifa ambayo yamekusanyika au yanakusanyika kwa ajili ya kuukandamiza na kuionea sayuni, kuionea Jerusalem, na taifa la Israeli.

Kwa watu wanaotaka kuungana nami kwa maombi, hebu kwa walau masaa machache au dakika chache tu, soma Isaya 62:1-7 pata muda wa kumwambia Mungu kitu juu ya Israeli. Mimi sitaki kuona Israeli inaingia katika matatizo, kwahiyo nina jukumu la Kuomba sana kwa ajili yake, na kulitia moyo taifa la Israeli, lisifadhaike, wala kupoteza tumaini, eh Israeli, sema unazo nguvu, kwa maana Mungu wako yupo karibu sana nawe apate kukutetea na kukupigania, yeye aliye mlinzi wako hatalala wala kusinzia.

Inuka eh Bwana uitetee Israeli mataifa yaliyo ulimwenguni na watu wa kabila zote, dini zote, na watu wote wapate kuona ya kwamba wewe hujaiacha sayuni bali upo karibu sana na sayuni, eh, Mungu wangu majira na Nyakati za wewe kuonekana sayuni zimetimia, inuka eh Bwana mataifa waone ya kwamba wewe Ndiye Mungu wa Israeli. Na Israeli ni mtumishi wako.

isaya 62 (1-2) ili neno nalipenda kulisimamia. kwa maana atakae ibariki israeli nae atabarikiwan nae alilaanie nae atalaaniwa. basi sasakwaajili ya sayuni sitanyamaza na kwaajili ya yerusalemu sitatulia hata haki yake itakapotulia kama mwangaza na wokovu wake kama taa iwakayo.Na ombea amani, mshikamano, na upendo katika taifa teule na mipaka yake yote, Roho mtakatifu malaika wakawe walinzi wa sayuni.Nuru ya mungu ikaangaze makabila yote ya israel. Silaa zote zinazoenda kurushwa zikanifikie mimi kwanza, pia misukosuko yote na umwagaji damu isitokee tena kwa taifa lile teule la Mungu. Najiunganisha na kujifungamanisha na taifa la israeli kila siku ya maisha yangu AMINA.

Ahsante sana kaka Lwitiko Katule kwa kutukumbusha wajibu wetu, maana agizo linaema atakaeibariki Israeli nae atabarikiwa. Kwahiyo kaka mimi nami nimmoja wapo kati ya watu wanaoguswa kuiombea Israeli si kwasababu ya baraka zilizoahidiwa bali kwasababu ni agizo kutoka kwa Mungu kuwa tuiombee Israeli. Barikiwa Israeli taifa teule la Mungu anaeabudiwa na watu wote wamchao Bwana Yesu Kristo. Kuta za moto wa Roho Mtakatifu zikazingire pande zote za nchi ya Israeli. Asisinzie akulindae. amina.

Mungu kamwe hajaisahau Israel ipo siku moja atairejesha katika majukumu aliyo nuia kama taifa alilolichagua. Warumi 11

Mungu akubaliki mleta mada hii kwani watu wengi hawaelewi hata viongozi wa wa nchi mimi huwa nasema Tanzania iko kwenye laana kwa sababu hatuwezi kuwa na madini,mbuga za wanyama, bahari,maziwa,gesi,nk bado tukawa ni masikini kiasi hiki ni laana ya viongozi kutetea uhuru wa taifa la palestina maana biblia inasema ukilaani israel kwa namna yoyote ile utalaaniwa wewe ambaye huelewi unadhani israel ni sawa na mataifa mengine pole israel ni taifa teule la Mungu na lile ni taifa lao halali hakuna uhuru wa palestina pale Mungu awabaliki

kwa habari ya israel kila mkristo anaejua wokovu wetu na jinsi kanisa linavyowindwa na mbwa mwitu kama biblia inavyosema hanabudi kusimama na israel kwani Mungu wetu ni Mungu wa israel amina

Ukisoma vizuri maneno chini kabisa, “Inuka eh Bwana uitetee Israeli mataifa yaliyo ulimwenguni na watu wa kabila zote, dini zote, na watu wote wapate kuona ya kwamba wewe hujaiacha sayuni bali upo karibu sana na sayuni, eh, Mungu wangu majira na Nyakati za wewe kuonekana sayuni zimetimia, inuka eh Bwana mataifa waone ya kwamba wewe Ndiye Mungu wa Israeli. Na Israeli ni mtumishi wako”

ni maombi ambayo siyakuwatakia waarabu mabaya, ila ni ya kumwita Mungu au kumkaribisha Mungu aje kuitetea Israeli. Akali nina mengi sana ya kusema juu ya taifa la Israeli , na Jiji la Jerusalem, ambayo huwa Roho Mtakatifu hanipi nafasi ya kuongea kwa kila Mtu, kuna Mengine hata huwa nadiriki kuyaongea kwa rafiki zangu wa Kiyahudi walioko Israeli ambao huwa nawasiliana nao mara kwa mara, lakini Roho mtakatifu huwa ananinyamazisha, na kuniambia kwa habari ya kutii na kukaa kimya

Primi kitu ninachofuata ni kile Roho Mtakatifu anachonisemesha sana kwa habari ya taifa la Israeli, hii ni portion yangu, nisipowajibika kama mlinzi ambaye ninajukumu la kutoa ulinzi kwa kinywa changu, nina kitu cha kumjibu Mungu, kwasababu nitaulizwa. Inawezekana wapo watu waliopewa mzigo wa kuombea mataifa ya kiarabu, sikatai, lakini mimi ninawajibika katika kipengele nilichopewa, kila mtu na mraba wake. huu ni wito ambao ninataka waombaji ambao Mungu amewawainua kwa kuombea amani ya Jerualem na taifa la Israeli wapate kuinuka. Kama haujabeba mzigo huu ndani yako, hutaweza kuelewa uzito wa hiki ambacho nimekiandika, lazima Roho Mtakatifu akupe msaada katika hili.Harafu hakuna ambaye anawatakia mabaya waarabu, hii ni tafsiri amabyo siyo sawa ya kwamba mtu anaposimama na Taifa la Israeli basi anawatakia waarabu mabaya. Sijui hii tafsiri umeipata wapi, ukisema umeipata kwenye kile nilichoandika, nitakataa, kwasababu sijasema kitu chochote kuhusu kuwatakia mabaya waarabu. Hebu soma vizuri na kutafakari kitu nilichokiandika, na kama kuna kitu unahitaji ukielewe niambie mimi nitakielezea kwa jinsi au kwanini nimekiandika hivi, ili nikupe kile halisi kilicho ndani ya moyo wangu, badala ya wewe kuja na tafsiri yako kwa habari ya kile nilichokiandika. Ubarikiwe sana

Nijuavyo mtumishi tunapaswa kuombea amani mataifa yote, kuibariki israel ni jambo jema kama nchi ambayo Bwana wetu Yesu kristo alizaliwa lakini fahamu upanga hautaondoka katika nchi ile mpaka Kristo atakaporudi kulichukua kanisa lake na ndipo israel wote watakapookolewa, tusifurahi na kuwatakia mabaya waarabu hawa bali pia tuwaombee maana mungu hapendi watu wafie dhambini bali wote waokolewe na kumjua yeye. Hebu nikuulize swali mtumishi- Je ikitokea Israel ikaishambulia Tanzania wewe utachukua hatua gani ikiwa wewe ni Mtanzania?. Mungu akubariki na neema ya Bwana iwe juu yako.

PSALMS 122:6 “Pray for the peace of Jerusalem! May they prosper who love you [the Holy City]!”

“For Zion’s sake I will not keep silent, for Jerusalem’s sake I will not remain quiet, till her righteousness shines out like the dawn, her salvation like a blazing torch” Isaiah 62:1

Psalms 122:7 – 9

May peace be within your walls and prosperity within your palaces! For my brethren and companions’ sake, I will now say, Peace be within you! For the sake of the house of the Lord our God, I will seek, inquire for, and require your good.

ANDIKA MAONI YAKO

Blog at WordPress.com.
 
Dini ni upofu Mkuu,usipokuwa makini lazima use teja .....kiufupi vita si kitu chema kwa mataifa yote,watoto,wanawake,wazee,vijana na wanajeshi wanakufa.....inaumiza sana ila sina cha kufanya...sipendi watu wauane sema sina la kufanya...maana kama Mungu mwenyewe yupo kimya Mimi ni nani nizuie damu zisimwagike.Inaumiza sana😭😭😭😭
 
Back
Top Bottom