Kuwahusu Karamagi, Rostam, na wenzao...

Huyo ni Karamagi, na nimesikia kuwa swala hilo la DPP kuzuia mashtaka ya Karamagi linaweza kumtokea puani yeye mwenyewe kwa vile pressure ya kuwashitaki viongozi wote waliohusika na mikataba mibovu iko juu sana kiasi kuwa bado Karamagi hajapona.
 
Kama kweli DPP kafanya hivyo, basi hata hao walio salia katika makosa ya kusign mikataba ya nchi kihuni na kifasadi inaweze kuchukua mkondo tofauti na ule uliowapeleka Mra Mbaazi na Yoo ona. Viginevyo issue Karamagi kupelekwa kwa pilato iwe pale pale na kilichofanyika ni kumpa muda wa kuongea na ndugu na jamaa kwa kirefu wakati ushahidi ukiwekwa sawa.

Mungu bariki ujasiri wa DPP ili azidi kuwatendea haki Wadanganyika
 
Ilielezwa kuwa, liliporudi jalada la mawaziri hao wawili wa zamani, lilipitishwa kwa ajili ya kupelekwa mahakamani, lakini la Buzwagi DPP alisema hakuna ushahidi wa kutosha kuifikisha kesi hiyo mahakamani, hivyo kulifunga.
 
Jamani.. someni sheria ya DPP... atazuia vipi kumpeleka mtu mahakamani wakati yeye ndiye mwenye majukumu ya kuleta mashtaka au kufuta mashtaka? Yaani kajizuia kufanya kazi yake yeye mwenyewe?
 
The dataz nilizozipata sasa hivi ni kwamba hawa wawili wako chini ya ulinzi maalum wa serikali, wakisubiri siku yao rasmi.

1. Rostam yuko chini ya ulinzi maalum mahali pa siri.

2. Jana Karamagi alijaribu kusaifiri kuelekea USA, akazuiwa uwanja wa ndege na kunyang'anywa documents zake zote, na kuchukuliwa "somewhere"

....Mods iki-exipire iunganisheni, tunatafuta habari zaidi baadaye wakuu!
 
Kama ni kweli basi ile issue ya kumpindua ........... labda kuna ka..............
 
This is definetly Karamagi. I wish wangefanya ya Chenge na EL kabla ya hawa wengine.
 
Ahsante kwa dokezo.

Sisi tulio mbali tumetega masikio yetu makubwa kama ya Nipashe ili tusikose jambo lolote.
Bondo ni nafuu yake tumbo, habari, tetesi na fununu ni msosi wa sikio.

Sikio litalalaje njaa na makelele yote haya??
 
Kuna habari kutoka gazeti la alasiri la leo ya kwamba Manji kakimbia. Amekimbilia Nairobi Kenya. Nimeshindwa kuifungua habari yote mtandaoni. Tuhabarisheni mlio nyumbani please!
 
Kuna watendaji wa serikali ya CCM ambao bado wako kwenye kaptula za kulalia wenyewe wanaita pajama na nyuso zao hawataki kuosha au kupangusa matongotongo na denda midomoni mwao.

Nadhani MH Rais anatakiwa kuotesha ukoka kwenye kibarua cha huyu mheshimiwa aitwaye DPP.

Swala la Deep Green linaihusu CCM na watendaji wake wakuu.
Ili MH Rais na CCM wajinusuru ni lazima hawa akina Karamagi,Rostamu na visiki wengine muhimu watolewe kafara ya damu na nyama zao ili kukomesha dhambi, sivyo laana ya dhambi waliyoitenda kama chama itawazoa wangu wangu bila kujali vyeo vyao na dhamana waliyo nayo kwa taifa.

MH DPP umekalia jiwe la moto, tena uchi bila kaptula, ni suala la muda tu makalio yatawaka pilipili.
 
Jamani.. someni sheria ya DPP... atazuia vipi kumpeleka mtu mahakamani wakati yeye ndiye mwenye majukumu ya kuleta mashtaka au kufuta mashtaka? Yaani kajizuia kufanya kazi yake yeye mwenyewe?


Ndio kwani haiwezekani kujizui kufanya kazi.Kama unatakiwa ku act na haufanyi hivyo ni kujizuia kufanya kazi.
Sehemu kubwa ya ushahidi umetoka takuru kama yeye anachukua forever ku close check na kumpeleka mtu mahakamani ni anaujizuia kaka DPP .
Kuchelewesha hukumu ni kuchelewesha................
 
Wazee wameithibisha story ya MWANAHALISI nini?... Mbona waarabu wa pemba wanachenjiana live?
 
Wakuu tunaendelea kuzifuatilia habari ni ngumu sana, mawazo yangu hapa toka jana yakutokuwa na uhakika na kama hii deal ni kweli au mazingaombwe tu yamewaudhi sana wakulu flani ambao ndio walionipigia simu na kunipa hizo dataz, wakaniamba nitizame maneno ya juzi au jana ya Pinda, kuwa wananchi watulie wasiwe na wasi wasi,

Wamenihalkikishia kwamba kwenye hili haponi mtu, lakini leo asubuhi niliongea na mkulu mmoja ambaye ni tomaso kama mimi, kwa hiyo nitarudi baadye kumalizia kule kwingine na kuona kama nitafanikiwa kupata zaidi on this, lakini tushirikiane wakuu kujua kama hawa wakulu wameonaekana mahali au vipi zaidi.

Baadaye!
 
Back
Top Bottom