Kuwahusu Karamagi, Rostam, na wenzao...

Kuwahusu Karamagi, Rostam, na wenzao...

Nadhani sasa hivi nni muda muafakawa kusikiliza Hotuba za Nyerere..
nawaomba msikilize nukta 77 mpate kufurahisha roho zenu maanake hizi nyufa zimezidi haswaa...
Bofya hapa.
 
I wonder where is Mzee Kingunge who dared to lie to Tanzanians infront of Camera kuwa walioibua hii ni waongo na lengo lao ni kuleta distraction. Sasa hapa naona DPP anaweza kututhibitishia kuwa Mzee alitudanganyam if that is the case kuna haja ya kuangalia uwezekana wa kufikishwa mahakamani kwa conspiracy ya kujaribu ku-cover up wizi wa mali ya taifa. Nina hakika watu wa DPP mnasoma hili ni moja kati ya mambo yanayoweza kufanyiwa kazi. Kama watu wa TV mnarekodi hiyo ingekuwa poa sana kama mngetuwekea hapa na kuisikiliza kauli ya mzee kingunge na jamaa waliotangaza kuwapeleka kina Slaa mahakamani.

Unajua Bongolander hili ndilo tatizo kubwa la viongozi wetu wengi!! mzee Kingunge bado anafikiri tunaishi kwenye zile zama za kulindana na kufichana!
Na ukweli ni kwamba mchezo huu umeturudisha nyuma sana kama taifa na kwa kweli hata yeye anapaswa kufikishwa mahakamani kwa matamshi yake yale ya kutaka kuficha ukweli na kulihujumu taifa.
Pili hata mtoto wake Kinjekitile anapaswa kufikishwa mahakamani kwa kutumia jina la baba yake kujipatia contract ya kukusanya mapato pale kituo cha mabasi yaendayo mikoani kupitia kikampuni uchwara!! maana haya ndiyo mambo ya rushwa tunayoyakataa kila siku.Tangu lini Kinje akawa ni expert na ujuzi wa kukusanya kodi???????
 
Nadhani sasa hivi nni muda muafakawa kusikiliza Hotuba za Nyerere..
nawaomba msikilize nukta 77 mpate kufurahisha roho zenu maanake hizi nyufa zimezidi haswaa...
Bofya hapa.

Asante mkuu, infwakt, jana niliisikiliza , nikawa nabikiri jinsi ya kuileta hii mada hapa, sasa sijui kama inawezekana Invisible kumuomba nukta77 au tukapata copy yetu tukaiweka kwenye items za jamiiforums. kama tulivyo weka zilipendwa, bongo flava etc.
 
Kuna taarifa ambazo nimepata sasa hivi kuwa Karamagi (tayari), Rostam Aziz, Meghji na Warioba (hawa wako njiani) watasomewa mashtaka leo.

Stay tuned

Duh! Na Warioba naye ndani ya list, hii kali.
 
Yaani mambo yamekuwa mambo.......muheshimiwa mtanashati kachoka vijembe, Kaamua kukunja shirt sleeves na kufanya kazi sasa. This time nikisikia amepaa ameenda vekesheni nitamsapoti, maana naona angalau amefanya kazi japokuwa kidogo. Tunamsubiria Kambale mwenyewe BWM anaswe kwenye nyavu za dagaa mchele.....Wakimdaka nimeshaahidi pale kambi ya fisi...ulabu kwangu siko hiyo...
Ok hamna mengi ya zaidi...narudi chemba kuendelea kumonita ishu jinsi inavyokunjuka.....
 
Waungwana,

Kama serikali inakubali kwamba mkataba wa Buzwagi uliosainiwa na Karamagi umeliingizia Taifa hasara kubwa, sasa inangoja nini ili kuufuta mkataba huo ili kuepukana na hasara zaidi na pia kusaini mkataba mpya ambao utakuwa na maslahi kwa Watanzania? Sioni kwanini serikali isubiri kipindi kirefu kabla ya kufanya mabadiliko ya mkataba huo na mikataba mingine ya uchimbaji wa madini.
 
Nadhani sasa hivi nni muda muafakawa kusikiliza Hotuba za Nyerere..
nawaomba msikilize nukta 77 mpate kufurahisha roho zenu maanake hizi nyufa zimezidi haswaa...
Bofya hapa.

Aisii unajuwa nini Nyerere kweli alikuwa ana akili .saizi ndio nalitambua hilo .
Asante mkuu kwa kutuwekea rekodi hiyo.
 
Habari hii haina ukweli as far as mama Meghji is concerned. NImetoka kuzungumza naye sasa hivi na yuko nje anaendelea na shughuli zake. Hayuko Keko. Hii habari sikuigusa toka jana kwa sababu.

Mapambano haya yana njia nyingine na inashangaza jinsi watu wasivyoelewa mapambano haya.

Inasikitisha sana
.

Mkjj, kama hutojali weka wazi zaidi hapo penye red!!!!!

Pia ningemshauri Invisible, awe anatoa pande kwa JF member mwingine kupost thread ambayo hana uhakika nayo!!!!!!
 
Waungwana,
Inasikitisha hata hapa JF tunashangiria bila hata kufikiri kwa undani, sasa hawa Mramba na Yona ukitazama makosa yaliyoorodheshwa ni madogo mno kiasi unajiuliza walikuwa wapi tangu siku zile kuwashitaki? Kama kweli mama Zakia ni juzi juzi tu alikiri kuuidhinisha malipo kwa kigezo eti alidanganywa na Balali, sasa yuko wapi mpaka sasa kufikishwa mahakamani? hivi un aweza kusaini bila kusoma?
Tatizo la EPA linazunguushwa kwani muhuzika mkuu Rotsam Aziz hajaguswa mpaka sasa, watanzania tunataka kujua kwanza, ni vipi ilikuwaje huyu jamaa awe jirani na Apson na baadae wakawa marafiki wakubwa na ni vipi huyu jamaa ali penetrate klwenye intelincy ya Tanzania?
kuna huyu jamaa Ngowi yeye ni afisa UWT na mwenyewe kazini sasa hivi anajiita EPA, na anasema yeye alifuatwa na wakubwa kwenda kuchukua pesa za EPA, sasa huyu anatakiwa akamatwe na aisaidie serikali kumpata aliyekuwa anawatafuta watu wa kuja kuchota pesa za EPA.
Waungwana msije shangaa kusikia hawa Yona na Mramba wamefuatwa kutiwa adabu kwa sababu labda wamehamia kwa mtu fulani ambaye anajindaa 2010.
Kama nia ya Vasco da Gama ni kusafisha tuataka hawa RA na EL tuwaone mahakamani, Richmod inajulikana vizuri na ni jinsigani m toto wa EL ameshiriki, na kama ni kutumia madaraka vibaya wote tunajua Yona katumiwa na BWM kwa nini asimuuite hata kwenye kamati ya bunge ahojiwe?
Ndugu tulitazame kwa makini hii ni kama opera inaenda kujisafisha wanaachwa wanaotakiwa hasa na wanaojua ukweli wa mambo.
Leo inasikitisha tunaanza kuletewa hoja za ukabila zisizo na kichwa wala kiuno ili kuficha ukweli wa mambo
Aluta continua mapambano yanendelea.
Mkereketwa,
 
JAMANI MIMI NAMSUBIRI ROSTAM AZIZ TU.....Nasita kusema mengi kwa sasa...

Ila hongera ndugu zangu walio nyuma ya pazia katika MCHAKATO WA KISUTU. Kazi bado ni kubwa mno but atleast kuna kamwelekeo fulani kanajijenga...

Salam

Tanzanianjema
 
...au katoa vitisho ya kuyaanika yote yaliyojiri wakati wa kampeni za kumtafuta mgombea toka CCM!?

Date::11/29/2008
Chadema wachachamaa faili la Karamagi kufungwa
Na Joyce Mmasi
Mwananchi


Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vyetu, kitendo cha DPP kutupilia mbali faili hilo hakikuwafurahisha maafisa wa Takukuru ambao walikuwa wanajiamini kuwa walikuwa ushahidi wa kutosha kuthibitisha mashtaka yao, huku wakiamini kuwa kitendo cha Karamagi ‘kuwaelimisha' watalaam na kubadili ushauri wao wa awali, ni sawa na kuwashinikiza-hivyo kuingia kwenye kundi la matumizi mabaya ya madaraka yake.


Hmmm! Hapa kuna mkono wa Mkuu.
 
Date::11/29/2008
Chadema wachachamaa faili la Karamagi kufungwa
Na Joyce Mmasi

WAKATI Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) imefunga faili la uchunguzi dhidi ya waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wa kutosha kumshtaki, kitendo hicho kimekichefua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Habari ambazo Mwananchi Jumapili limezipata zinaeleza kuwa uchunguzi dhidi ya Karamagi kuhusiana na tuhuma za kutumia madaraka yake vibaya kusaini mkataba wa mgodi wa Buzwagi tayari limefungwa.

Vyanzo vya habari kutoka kwenye ofisi ya DPP na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) zinasema vielelezo vilivyowasilishwa havikuwa na nguvu za kumfikisha Karamagi mbele ya mkono wa sheria.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, maoni ya ofisi ya DPP ni kwamba mbunge huyo wa Bukoba Vijijini alifuata ushauri wa watalaam kusaini mkataba huo, licha ya kwamba tarehe ambayo alipokea ushauri huo ndiyo aliyosafiri kwenda London, Uingereza kusaini mkataba huo.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, watalaam washauri wa madini ambao pia walikuwa wameunganishwa na Karamagi kwenye uchunguzi huo wa Takukuru, awali walimshauri Karamagi asisaini mkakataba huo kwa vile haukuwa na maslahi kwa taifa, lakini waziri huyo ‘akawaelimisha' wakaafikiana naye na kuruhusu amwage wino kwa niaba ya serikali.

Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vyetu, kitendo cha DPP kutupilia mbali faili hilo hakikuwafurahisha maafisa wa Takukuru ambao walikuwa wanajiamini kuwa walikuwa ushahidi wa kutosha kuthibitisha mashtaka yao, huku wakiamini kuwa kitendo cha Karamagi ‘kuwaelimisha' watalaam na kubadili ushauri wao wa awali, ni sawa na kuwashinikiza-hivyo kuingia kwenye kundi la matumizi mabaya ya madaraka yake.

Jambo jingine ambalo wapasha habari wetu wanalieleza ni kwamba, kitendo cha Karamagi kuondoka kwenda London tarehe ile ile aliyopokea ushauri wa watalaam, kina maana kwamba suala hilo lilikuwa tayari limeshaamuliwa na kusingekuwa na kurudi nyuma.

Wakati hali ikiwa hivyo, Dk Slaa jana alilieleza gazeti hili kuwa DPP anatakiwa kumshataki Karamagi bila visingizio vyovyote vya kumkingia kifua na kama ana tatizo la ushahidi yeye na chama chake watamsaidia.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, DPP, Elieza Feleshi, alisema kuhusu suala hilo aulizwe Dk Hosea (Edward, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru) kabla ya kumuuliza yeye. Hata hivyo juhudi za kumpata Dk Hosea hadi tunakwenda mitamboni hazikufanikiwa.

Dk Silaa aliyeonekana kukerwa na suala hilo, alisema imeanza kuonekana hali ya kulindana kwa visingizio kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kumshtaki Karamagi.

"Sasa unaposema huna ushahidi wa tuhuma za Karamagi unataka nini zaidi, kama mtu alitoka hapa akakimbilia London kusaini mkataba, kuna ushahidi gani zaidi ya huo mkataba uliosainiwa London," alihoji Dk Slaa.

Alisema hata hivyo mtu aliyetoa tuhuma hizo kwa mara ya kwanza bungeni ni Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye anao ushahidi wa tuhuma zile, na akasema ingekuwa vizuri Zitto aombwe amsaidie DPP ili Karamagi aweze kuunganishwa na wenzake mahakamani.

"Mihuri iliyotumika ipo, aliibeba na kwenda nayo London, muda aliosaini unajulikana, ushahidi kuwa alikikiuka taratibu kwa hatua yake hiyo, upo, sasa watuambie wanataka ushahidi gani ili tuwasaidie," alisema.
 
kuna taarifa ambazo nimepata sasa hivi kuwa karamagi (tayari), rostam aziz, meghji na warioba (hawa wako njiani) watasomewa mashtaka leo.

Stay tuned

hao wote ni washenzi tu, hivi tanzania hakuna watu wa kujitoa mhanga kwa ajili ya kuokoa vizazi vijavyo?
 
hao wote ni washenzi tu, hivi tanzania hakuna watu wa kujitoa mhanga kwa ajili ya kuokoa vizazi vijavyo?

Ikiwa watu wantupia mawe msafara tutegee wanaojiripua karibuni maana watu wamchoka mkuu
 
Jamani.. someni sheria ya DPP... atazuia vipi kumpeleka mtu mahakamani wakati yeye ndiye mwenye majukumu ya kuleta mashtaka au kufuta mashtaka? Yaani kajizuia kufanya kazi yake yeye mwenyewe?

Mkuu Mwanakijiji, DPP lazima atoe idhini kwa kesi zote za rushwa zinazofunguliwa na TUKUKURU.

THE PREVENTION AND COMBATING OF CORRUPTION ACT, 2007-11
PART VIII; MISCELLANEOUS PROVISION, Sect. 60

Sanction of D.P.P
Prosecution for an offence under this Act shall be instituted with written consent of the Director of Public Prosecutions.


Pia, sio DPP peke yake mwenye majukumu ya kuleta mashitaka.

THE PREVENTION AND COMBATING OF CORRUPTION ACT, 2007-11
PART II; ESTABLISHMENT OF THE BUREAU,

Functions of the Bureau Sect. 7 (f)
The Bureau shall, subject to the directions of the Director of Public Prosecutions, prosecute offences under this Act and other offences involving corruption;

Institution of criminal proceedings, Sect. 9 (1)
The Director General (of the Prevention and Combating of Corruption Bureau) or a person authorized by him …shall institute criminal proceedings against…


Na zaidi ya hapo, mbali na kesi za TUKUKURU, mtu yeyote ana uwezo wa kufungua kesi ya jinai bila idhini ya DPP

THE CRIMINAL PROCEDURE ACT, 1985-9
CONTROL OF CRIMINAL PROCEEDING, PART IV ( b )Sect. 99 (1)
Conduct of Prosecutions

Permission to conduct prosecution
Any magistrate inquiring into or trying any case may permit the prosecution to be conducted by any person…


Ila katika kesi za jinai kwa ujumla, kuna wakati ambapo ni lazima upate idhini ya DPP: Section 94 exceptions pamoja na Section 397( f )(4) exceptions za Criminal Procedure Act

THE CRIMINAL PROCEDURE ACT, 1985-9
CONTROL OF CRIMINAL PROCEEDING, PART IV ( b )
The Director of Public Prosecutions

Offence by foreigners, Sect. 94 (1)( a )
Proceedings for the trial of any person, who is not a citizen of the United Republic, for an offence committed on the open sea within two hundred nautical miles of the coast of the United Republic measured from the low-water mark, shall not be instituted in any court except with the leave of the Director of Public Prosecutions.

Police Ordinance Amendment Sect. 397( f )(4)

No prosecution resulting from the excise of powers under this section (section 34, Police Ordinance Act) shall be commenced without the leave of the Director of Public Prosecutions
 
Kuhani, pointi ya maoni yangu ni kuwa aliyesema kuwa DPP "azuzia" na wale waliosema "amkingia kifua" n.k Karamagi wameshindwa kuelewa nguvu za DPP. Point yangu ni kuwa DPP amefanya kitu alicho na nguvu nazo kisheria. Maana yake, DPP hawezi kuzuia kufanya kazi yake ya kisheria.

DPP anapoingilia kesi, anapoamua kuondoa mashtaka yeyote kwenye mahakama yeyote nchini au anapoamua kutomshtaki mtu "hazuii" bali anafanya kile ambacho kimo ndani ya nguvu zake kisheria.

Naweza nikajaribu kufafanua kivingine.
 
Well, kama hakuna ushahidi wa kutosha nadhani kisheria inabidi kina Dr. Slaa na Zitto ambao wana Ushahidi zaidi waufikishe TAKUKURU ili hilo file lifunguliwe Upya. hakuna sheria inayokataza file lililofungwa kutofunguliwa baada ya ushahidi mpya kupatikana.
Na wakati huo huo ni lazim a tukubali kwamba DPP wanaweza kukataa kusimamisha kesi ikiwa hakuna ushahidi wa kutosha ktk mashtaka yaliyowakilishwa na sio ushahidi ambao tunao sisi midomoni mwetu...
Na nadhani kina Dr. Slaa na Zitto wapo ktk nafasi nzuri zaidi ya kudai hilo file lifunguliwe maadam limekwisha fikishwa mbele ya sheria.
Tatizo ilikuwa kulifikisha DPP kutokea Takukuru, kwa hiyo hapa kidogo nadhani inawezekana kabisa kuibua kesi upya!...
 
Kuhani, pointi ya maoni yangu ni kuwa aliyesema kuwa DPP "azuzia" na wale waliosema "amkingia kifua" n.k Karamagi wameshindwa kuelewa nguvu za DPP. Point yangu ni kuwa DPP amefanya kitu alicho na nguvu nazo kisheria. Maana yake, DPP hawezi kuzuia kufanya kazi yake ya kisheria.

DPP anapoingilia kesi, anapoamua kuondoa mashtaka yeyote kwenye mahakama yeyote nchini au anapoamua kutomshtaki mtu "hazuii" bali anafanya kile ambacho kimo ndani ya nguvu zake kisheria.

Naweza nikajaribu kufafanua kivingine.

Hebu nipeni mwanga. Kama sikosei sheria mpya iliyounda PCCB pamoja na kuongeza makosa kutoka manne hadi 24, imeipa PCCB nguvu ya kufungua kesi iwapo DPP atashindwa kutoa kibali ndani ya kipindi fulani, je, nguvu hizo haziwapi mamlaka ya kuendelea na kesi hata kama DPP atakataa? Je, DPP anapofunga jalada ina maana ushahidi ukipatikana PCCB wataogopa kulipeleka tena jalada? Je, kwanini DPP asiwaambie PCCB kwamba jalada lenu lina mapungufu kadhaa... ambayo mukiyarekebisha tunaweza kufungua kesi, vinginevyo hatutashinda mahakamani, au kwanini DPP asiseme, kwa maelezo ya fulani na fulani, tunashauri apatikane fulani (ambaye hajahojiwa) ili tuweze kuboresha mashitaka dhidi ya watuhumiwa (Kama ilivyokuwa kwa Kagoda-hint)? Ninavyoona kuna kitu kinafichwa na si suala la kisheria hapa. Again "CHANGA LA MACHO"
 
Halisi,
Navyofahamu mimi DPP husema tu kuwa wajomba hapa hamna kesi hakuna ushahidi thabiti dhidi ya mhusikakufungua kesi hii, hivyo ni jukumu la PCCB kutafuta ushahidi zaidi ktk baadhi vipengele ambavyo ktk mazungumzo wa uwakilishi (Chemba) vilitamkwa kuwa sio ushahidi unaotosha kwa mshtakiwa kuhusika na...

Binafsi nadhani kesi zilizofunguliwa zinahusiana sana na uzembe ama negligence (kupuuza), jambo ambalo haliwezi kuangukia ndani ya criminal terms na hasa corruption..Na mara nyingi hukumu ya Uzembe na Kupuuza ni kufukuzwa kazi, hiyo imetoka - mtuhumiwa hakuiba ama kuhujumu uchumi wa nchi makusudi.
Tatizo kubwa linakuja pale inaposemekana kuwa Karamagi alienda London ikifahamika kiofisi kwamba alikwenda kuweka sahihi Mkataba wa Buzwagi na kama nakumbuka hata Rais mwenyewe alikiri kuwa Kisheria Karamagi alikuwa na madaraka ya kufanya alofanya bila kumtaarifu rais, hapo ndipo picha inapoharibika zaidi..
Ni loopholes kama hizi ndizo viongozi Mafisadi wamekuwa wakizitumia kwa muda mrefu na kwa bahati mbaya sheria zote zilizowekwa zimezingatia zaidi Ujambazi yaani hujuma za vitendo kuliko kutumia wino.
Kifupi mkuu hakuna mwizi anayeweza kujihusisha moja kwa moja wakati kuna mianya ya kutumia ujanja, kupokea hisa badala ya cash ambayo haiwezi kujulikana kirahisi unless shirika zima liwe ktk darubini.
 
Kama Kesi ni Matumizi mabaya ya Madaraka, Ushahidi hapa chini unaoonyesha kuwa alichofanya Kamaragi ni sawa na wakina Mramba na Yona, nitarejea kuwaeleza ni kwanini DPP anapata kigugumizi:

NAZIR MUSTAFA KARAMAGI

Nazir Mustafa Karamagi ni Waziri wa sasa wa Nishati na Madini. Aliingia kwa mara ya kwanza katika Baraza la Mawaziri la Rais Jakaya Kikwete kama Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko. Lakini kufuatia Kashfa ya Umeme wa Richmond iliyomwondoa Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo Dr. Ibrahim Msabaha na Naibu wake Lau Masha, Mheshimiwa Karamagi alihamishiwa Wizara ya Nishati na Madini. Katika kipindi cha karibu mwaka mmoja ambao Mheshimiwa Karamagi ameshikilia madaraka yake ya sasa amehujumu taifa la Tanzania kwa kusaini mkataba wa ujenzi wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga na kampuni ya Pangea Minerals Limited ambayo ni kampuni tanzu ya Barrick Gold Corporation ya Canada. Mkataba huo ulisainiwa Churchill Hotel, London, Uingereza tarehe 17 Februari 2007. Kwa vile kusainiwa kwa Mkataba huo ndio ulikuwa chimbuko la hoja ya kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge iliyopelekea Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Z. Kabwe kusimamishwa kufanya shughuli za Bunge kwa miezi mitano, ni vema madhara na/au manufaa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya Mkataba huo kwa Tanzania yachunguzwe kwa makini kama ifuatavyo:

I. MUDA WA MKATABA

(i) Kwamba Waziri Karamagi atatoa Leseni Maalum ya Uchimbaji kwa Pangea Minerals ya muda wa kuanzia wa miaka ishirini na tano (25). Leseni hiyo itatolewa haraka iwezekanavyo na kwa vyovyote vile ndani ya muda usiozidi siku sitini (60) tangu Pangea Minerals kuwasilisha maombi yao ya Leseni Maalum ys Uchimbaji. Aidha, Pangea Minerals “… watakuwa na uhuru wa kuongeza muda wa Leseni hiyo kwa masharti hayo hayo kwa miaka mingine ishirini na tano (25).” Na endapo muda huo wa nyongeza ukiisha na Pangea Minerals wakaomba kuongezewa muda zaidi, “… basi iwapo Waziri ataona ni kwa maslahi ya taifa kuwaongezea muda kama walivyoomba atawaongezea muda wa ziada atakaoona unafaa.” Kwa masharti haya ya mkataba, Pangea Minerals wana haki ya kuendelea kuchimba dhahabu kwa miaka hamsini au zaidi kufuatana na mahitaji yao na matakwa ya Waziri wa Nishati na Madini na kwa masharti yale yale yaliyowekwa siku ya kusaini mkataba;

II. MAPATO YA SERIKALI

Mkataba wa Buzwagi unadai kwamba “Kampuni inachukulia suala la kutobadilika badilika kwa kodi na sheria za fedha za Tanzania kama sharti la msingi katika uwekezaji wake kwenye Mgodi na kwamba Kampuni itakuwa na uhakika kwamba kodi na utaratibu wa kifedha ulivyo wakati wa kusaini Mkataba utaendelea kuwa hivyo kwa Kampuni wakati wote wa uhai wa Mradi” wa Buzwagi. Katika kuhakikisha suala hili, Mkataba huu umeweka masharti yafuatayo kuhusiana na masuala ya kodi na/au ya kifedha:

(i) Kwamba Pangea Minerals watalipa kwa Serikali kodi zifuatazo:

(a) Asilimia 3 (3%) thamani ya madini baada ya kuondoa gharama za uzalishaji kama mrahaba kwa madini yote yatakayochimbwa eneo la Buzwagi isipokuwa almasi ambayo mrahaba wake utakuwa asilimia 5 (5%) ya thamani ya almasi hiyo baada ya kuondoa gharama za uzalishaji;

(b) Ushuru wa stempu (stamp duty) kama ulivyoainishwa na Sheria ya Ushuru wa Stempu Na. 20 ya Mwaka 1972 kuanzia tarehe ya kuanza kwa mkataba wa Buzwagi. Hata hivyo, kuna uwezekano wa Pangea Minerals kutolipa hata senti moja kama ushuru wa stempu kwani kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Ushuru wa Stempu kimetoa angalizo kwamba “hakuna ushuru wowote utakaolipwa kutokana na waraka (instrument) wowote uliosainiwa na, au kwa niaba au kwa taarifa ya Serikali ambapo kama kifungu hiki kisingekuwapo, basi Serikali ingekuwa na wajibu wa kulipa ushuru huo kuhusiana na waraka huo. Neno ‘instrument’ limetafsiriwa kuwa linajumuisha “kila nyaraka ambayo kwayo haki au deni/wajibu l/imetengenezwa au imedaiwa kutengenezwa au kuhamishwa, kupunguzwa, kuongezwa, kufutwa au kurekodiwa.” Kwa tafsiri hii, ni wazi kwamba Mkataba wa Buzwagi ni ‘waraka’ (instrument) ambao kwayo haki na wajibu wa Serikali na Pangea Minerals imetengenezwa, kuhamishwa na/au kurekodiwa;

(c) Dola za Marekani laki moja na ishirini na tano elfu (US$ 125,000) kwa ajili ya Mfuko wa Uwezeshwaji (Empowerment Fund) zitakazolipwa kila tarehe 31 Desemba ya kila mwaka kuanzia mwaka wa uzalishaji. Ni muhimu kuelewa hapa kwamba ‘Mwaka wa Uzalishaji’ umetafsiriwa katika mkataba huu kuwa ni kipindi ambapo uzalishaji wa dhahabu safi au isiyosafishwa utafikia kiasi cha wakia 20,000. Kwa maana nyingine Pangea Minerals hawawajibiki kulipa kodi ya Mfuko wa Uwezeshwaji iwapo uzalishaji wa dhahabu hautafikia wakia 20,000 kwa mwaka;

(ii) Kwamba kodi yoyote, ushuru wowote, ada yoyote au malipo mengine ambayo Kampuni, wenye hisa wake, washirika au wadeni wake watatakiwa kulipa kutokana na mapato, ikiwa ni pamoja na mapato ya gawio, yatokanayo na uchimbaji madini unaofanyika chini ya Leseni Maalum ya Uchimbaji vitalipwa kuanzia tarehe ya mkataba kufuatana na matakwa ya Sheria ya Kodi y Mapato ya mwaka 2004 na Sheria ya Ushuru wa Forodha ya mwaka 1976. Ni muhimu kuelewa hapa kwamba Sheria hizo mbili zilifanyiwa marekebisho makubwa na Sheria ya Mabadiliko ya Sheria za Fedha Na. 27 ya mwaka 1997. Chini ya marekebisho hayo kodi, ushuru au ada zinazozungumziwa katika kifungu hiki cha Mkataba ziliondolewa au kupunguzwa kwa kiasi kikubwa au kufanywa kuwa tegemezi wa wakati makampuni ya madini yatakapoanza kupata na/au kutangaza faida. Kwa maana nyingine, Serikali inaweza isipate fedha yoyote kutokana na kifungu hiki cha Mkataba wa Buzwagi;

(iii) Kwamba kiwango cha jumla ya kodi zote ambazo Pangea Minerals italipa kwa halmashauri za wilaya au serikali za mitaa kwa ujumla hakitazidi Dola za Marekani laki mbili US$ 200,000) kwa mwaka. Aidha Kampuni haitalipa kodi za halmashauri na/au serikali za mitaa:

(a) ambazo zinazidi viwango vya sehemu nyingine za Tanzania;

(b) ambazo zimetokana na faida, mauzo au uzalishaji unaotokana na uchimbaji madini; au

(c) ambazo zimetokana na thamani ya ardhi inayotumika kama mgodi, kwa miundombinu ya uchimbaji madini au mitambo;

(iv) Kwamba Pangea Minerals haitawajibika kulipa kodi zifuatazo kutokana na shughuli zake za uchimbaji madini:

(a) Ushuru, ada au mchango wowote wa lazima zaidi ya vile ilivyoelezwa katika aya ya (iv) isipokuwa kwa kodi, ushuru, ada au michango midogo midogo ambayo kwa pamoja haitazidi Dola za Marekani elfu kumi (US$ 10,000) kwa mwaka;

(b) Malipo yatozwayo chini ya Sheria ya Madini au kanuni zake yanayozidi Dola za Marekani elfu mbili (US$ 2,000) kwa kilometa ya mraba kwa mwaka. Kwa maana hiyo, kodi ya kiwanja inayotakiwa kulipwa kwa eneo lote la Mkataba wa Buzwagi lenye ukubwa wa kilometa za 24.49 ni Dola za Marekani elfu arobaini na nane mia tisa na themanini (US$ 48,980) kwa mwaka;

(c) Kodi ya matumizi ya barabara iliyowekwa na Sheria ya Kodi za Mafuta na Barabara ya mwaka 1985 itakayozidi Dola za Marekani laki mbili (US$ 200,000) kwa mwaka;

(d) Kodi yoyote ya mauzo, matumizi au ongezeko la thamani isipokuwa kama ilivyowekwa chini ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ya mwaka 1997. Hapa vile vile ni muhimu kuelewa kwamba Sheria Na. 27 ya mwaka iliyofanya marekebisho ya sheria mbali mbali za fedha iliondoa kabisa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa mauzo ya madini yote yanayouzwa nje ya Tanzania kama dhahabu au almasi, n.k. Ndio maana kifungu hiki cha Mkataba wa Buzwagi kimesema wazi kwamba Pangea Minerals ina haki ya kunufaika na nafuu za VAT zilizopo katika Nyongeza ya Tatu ya Sheria ya VAT kuanzia tarehe ya Mkataba;

(v) Kwamba Pangea Minerals italipa kodi ya zuio (withholding tax) kutokana na malipo kwa watu wengine kama inavyotakiwa na sheria husika, isipokuwa Kampuni haitawajibika kushikilia kodi:

(a) Kwa kiwango chochote kutokana na malipo ya mkopo au deni la riba inayotakiwa kulipwa kwa fedha za kigeni kwa ajili ya mikopo, ikiwa ni pamoja na mikopo ya washirika wake, iliyokopwa nje ya Tanzania kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini. Kwa maana nyingine, malipo ya mikopo mikubwa ambayo makampuni ya madini yamekuwa yanadai kulipa kwa wadeni wao wa nje na kwa hiyo kushindwa kupata faida ya kulipa kodi ya mapato kwa Serikali ya Tanzania nayo haitalipiwa kodi ya zuio;

(b) Kwa kiwango chochote kinachozidi asilimia 5 ya malipo ya jumla kuhusiana na huduma za kiutaalamu au ada za menejimenti;

(vi) Pale ambapo asilimia 5 ya malipo ya jumla kwa ajili ya huduma za kiutaalamu au ada ya menejimenti inashikiliwa na Pangea Minerals imezuiliwa, kodi hiyo ya zuio itahesabika kuwa ni sawa na malipo yote ya kodi ya mapato inayotakiwa kulipwa na mtu anayetoa huduma za kiutaalamu au menejimenti. Maana ya kifungu hiki ni kuwawezesha watoa huduma za kiutaalamu au menejimenti kutolipa kodi ya mapato ambayo kisheria ni asilimia 30 ya mapato yao;

(vii) Kwamba Pangea Minerals itaruhusiwa kukata asilimia 80 ya mtaji uliotumika kwa mwaka uliotumika mtaji huo na baada ya hapo itakata asilimia 50 kwa mwaka isipokuwa tu kwamba Serikali ya Tanzania itatakiwa kufanya marekebisho ya sheria ili kuyafanya makato haya yakubalike chini ya sheria za Tanzania. Kifungu hiki cha Mkataba kina maana kwamba endapo Serikali haitafanya marekebisho ya Sheria husika, basi Pangea Minerals itaendelea kukata asilimia mia moja ya mtaji uliotumika kwa mwaka wa kwanza!

(viii) Kwamba mnunuzi wa madini yoyote yaliyochimbwa katika eneo la Mkataba hatalazimika kuzuia kiasi chochote kutoka katika bei ya mauzo.

Itakumbukwa kwamba wakati akijibu hoja ya Mheshimiwa Zitto Kabwe juu ya kuundwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza tuhuma zake dhidi ya kusainiwa kwa Mkataba wa Buzwagi, Waziri Karamagi aliliambia Bunge la Jamhuri ya Muungano juu ya faida zifuatazo zinazotarajiwa kutokana na kusainiwa kwa Mkataba wa Buzwagi:

(a) Malipo ya mrahaba na kodi nyingine za kiasi cha Dola za Marekani milioni 198.9;

(b) Makato ya kodi ya mishahara ya wafanyakazi (pay as you earn) ya kiasi cha Dola za Marekani milioni 50.3;

(c) Ujenzi wa laini na matumizi ya umeme ya Mgodi na maeneo yanayouzunguka ya Dola za Marekani milioni 30;

(d) Manunuzi ya huduma mbali mbali wakati wa kujenga miundo mbinu, mitambo na wakati wa uzalishaji ya kiasi cha Dola za Marekani milioni 568.4;

(e) Jumla ya mapato yote yatakayoingia kwenye uchumi wa taifa katika kipindi cha uhai wa mgodi ni takriban Dola za Marekani milioni 818.3;

(f) Ajira 630 kwa Watanzania; kuongezeka kwa pato la taifa la fedha za kigeni; miundo mbinu ya kiuchumi na kijamii, n.k.

Hata hivyo, vifungu vilivyotajwa hapo juu vinaonyesha kwamba nje ya malipo ya mrahaba na kodi ya zuio, sana sana Serikali ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kahama, itakuwa inalipwa jumla ya Dola za Marekani 583,980 kwa mwaka. Na kwa kuzingatia taarifa ya Waziri Karamagi kwamba Mgodi wa Buzwagi unatazamiwa kuwa na ‘uhai’ wa miaka kumi, Serikali italipwa Dola za Marekani 5,839,800 nje ya mrahaba na kodi ya zuio kutokana na utajiri wa madini yote yaliyoko eneo la Buzwagi. Ukweli ni kwamba kiasi hicho kinaweza kupungua zaidi kwa kuangalia maelezo ya aya za ii(c), iv na v(a), (b) na (c) katika Waraka huu. Kuhusiana na madai ya Waziri Karamagi juu ya malipo ya mrahaba na kodi nyinginezo ya Dola za Marekani milioni 198.9, taarifa aliyoitoa Naibu wake William Ngeleja inaonyesha kwamba katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, Serikali ya Tanzania imepokea Dola za Marekani milioni 78 tu kama mrahaba na kodi nyingine kutoka kwa migodi yote 6 ya dhahabu ambayo inafanya kazi hadi sasa. Kwa kiwango hicho, Buzwagi ambao Waziri Karamagi mwenyewe aliuita kama ‘Marginal Mine’, yaani ‘Mgodi Mdogo’ ni wazi kwamba matarajio ya Serikali kuhusu manufaa ya Mgodi wa Buzwagi hayana msingi wowote katika hali halisi.

III. UHAMISHAJI WA RASILMALI YA TAIFA

Mkataba wa Buzwagi pia utakuwa na madhara makubwa kwa uchumi wa taifa kwa sababu utapelekea kuhamishwa kwa rasilmali ya taifa letu kwenda nje ya nchi (capital flight). Kwa muda wote wa uhai wa Mkataba, Pangea Minerals “… ina haki na itaendelea kuwa na haki ya”:

(a) Kubakisha nje ya nchi fedha za mauzo ya madini yanayomilikiwa na Kampuni na, ilimradi tu inatimiza wajibu wake wa kufanya malipo ndani ya Tanzania, Kampuni itakuwa na haki ya kuhamisha na/au kupeleka fedha hizo za mauzo ya madini popote inapotaka na kwa namna yoyote inayotaka;

(b) Kuingia katika makubaliano ya mikopo nje ya Tanzania inayohusu shughuli za uchimbaji na kubakisha nje ya nchi fedha zinazotokana na malipo ya mikopo hiyo;

(c) Kufungua na kuendesha akaunti za fedha za Tanzania au za kigeni endapo akaunti hizo zinatumika kwa ajili ya fedha zinazotokana na/au zinazohusu shughuli za uchimbaji madini;
(d) Kufungua na kuendesha akaunti za fedha za kigeni nje ya Tanzania zinazoweza kuingiziwa fedha bila kizuizi chochote na kuhamisha fedha hizo kwa uhuru na bila kizuizi na bila masharti ya kuzibadilisha fedha hizo kwa fedha za Tanzania na/au kurudisha Tanzania sehemu yoyote ya fedha hizo ilimradi tu Kampuni inaweza kutoa taarifa kwa Benki Kuu ya Tanzania juu matumizi ya akaunti hizo kuhusiana na shughuli za uchimbaji madini kama itakavyotakiwa na Benki Kuu;

(e) Kusafirisha na kuuza kwa wanunuzi wa nje madini yoyote na mazao yanayohusiana nayo yatakayochimbwa na/au kupatikana katika eneo la Mkataba.

Masharti yaliyotajwa katika (a), (b) na (d) yanahitaji vibali vya Benki Kuu ya Tanzania. Hata hivyo, kifungu cha 5.2 cha Mkataba kinailazimu Serikali ya Tanzania kumfanya Gavana wa Benki Kuu kuiandikia Kampuni barua itakayotoa vibali vyote vinavyotakiwa chini ya Mkataba huu ndani ya siku thelathini (30) kutoka tarehe ya kusainiwa kwa Mkataba. Na endapo vibali hivyo havitatolewa kitendo hicho “hakitaathiri au kuzuia Kampuni kutumia haki zake au kufaidika na manufaa yaliyoko kwenye Mkataba huu”! Vile vile Serikali na Waziri Karamagi wanatakiwa kuchukua hatua zote kuruhusu kitendo au kitu chochote cha kuhakikisha kwamba Kampuni inakuwa na haki na manufaa yaliyotolewa na Mkataba huu. Aidha taarifa zozote zinazotakiwa kuchapishwa ili kuhalalisha haki na manufaa ya Kampuni chini ya Mkataba huu zitachapishwa lakini kutochapishwa kwa taarifa hizo “… hakutaizuia Kampuni kufaidika na manufaa yoyote yanayotarajiwa chini ya Mkataba huu.” Kwa masharti yaliyotajwa katika sehemu hii, ni vigumu kuelewa na/au kukubali kauli ya Waziri Karamagi Bungeni kwamba Mgodi wa Buzwagi utaingiza mapato ya takriban Dola za Marekani milioni 818.3 kwenye uchumi wa taifa katika kipindi cha uhai wa mgodi huo!

IV. MANUNUZI YA BIDHAA NA HUDUMA

Katika hotuba yake Bungeni Waziri Karamagi alidai kwamba moja ya faida zitakazopatikana kwa kusainiwa Mkataba wa Buzwagi ni “kununua huduma mbali mbali za wakati wa kujenga miundombinu mingine kwenda mgodini, ujenzi wa mitambo na wakati wa uzalishaji ambao unatarajiwa kugharimu takriban USD 568.4 milioni.” Ushahidi wa Mkataba wenyewe unapingana na hoja ya Waziri Karamagi. Kwanza, kifungu cha 7 kinasema yafuatayo: “Kampuni itatoa upendeleo wa kununua bidhaa na huduma zilizoko Tanzania ilimradi bidhaa na huduma hizo zina ubora wa kimataifa, zinapatikana kwa wakati na idadi inayotakiwa na zinauzwa kwa bei ya ushindani zinapofikishwa Tanzania.” Vile vile Kampuni kwa kushauriana na Waziri itaweka utaratibu wa zabuni utakaowawezesha wakandarasi kushindania zabuni hizo kwa kuangalia mazingira ya Tanzania. Hakuna chochote katika kifungu hiki cha Mkataba kinachoelezea kiasi cha fedha kitakachotumika katika kununua bidhaa na huduma ndani ya nchi na kama bidhaa au huduma zenyewe zitazalishwa Tanzania au zimenunuliwa nje kwa matumizi ya ndani.

Pili, kifungu cha 8 cha Mkataba pia kinaitaka Kampuni na makandarasi wake kutumia bidhaa, vifaa na ugavi vilivyozalishwa ndani ya nchi kadri inavyowezekana wakati wa ujenzi na uendeshaji wa Mgodi na miundombinu yake. “Hata hivyo”, kifungu hiki kinatahadharisha, “Kampuni na makandarasi wake watakuwa na haki ya kuagiza, bila kizuizi, vitu vyote vinavyohitajika kwa usanifu, ujenzi, kuweka mitambo na uendeshaji wa Mradi, ikiwa ni pamoja na mafuta, spea na sehemu za spea … ilimradi tu ushuru wowote unaohusu uingizaji mafuta, ikiwa ni pamoja na mchango wa ushuru wa barabara hautazidi Dola za Marekani 200,000.” Aidha, “ushuru wowote wa forodha utakaotozwa kwa bidhaa na/au vifaa vilivyoagizwa nje utakufuatana na matakwa ya Sheria ya Ushuru wa Forodha Na. 12 ya mwaka 1976 kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Fedha Na. 27 ya mwaka 1997.” Kama tulivyoonyesha, Sheria Na. 27 ilifuta masharti mbali mbali ya ulipaji wa ushuru wa forodha kwa ajili ya bidhaa na/au vifaa vinavyotumika au kuhusika na uchimbaji madini. Kifungu hiki pia kinapingana na hoja ya Waziri Karamagi juu ya manufaa yatakayotokana na manunuzi ya bidhaa na/au huduma.
V. ‘UTAKATIFU’ WA MKATABA

Mkataba wa Buzwagi unaitaka Serikali kuhakikisha kwamba vifungu vya sheria vinavyohusu manufaa, haki na wajibu wa Kampuni na/au wanahisa wake hazibadilishwi wakati wowote wa uhai wa Mkataba:

(a) Muda wa Leseni Maalumu ya Uchimbaji au matumizi ya ardhi ya eneo la Mkataba ikiwa ni pamoja na matumizi ya ardhi yoyote iliyoko nje ya eneo la Mkataba kwa miundombinu, utunzaji au usafirishaji wa bidhaa zake;

(b) Kuingiza Tanzania wafanyakazi wa nje, mashine, mitambo, magari ya usafirishaji na vifaa vingine muhimu kwa ajili ya ujenzi wa Mgodi na uendeshaji wa shughuli za uchimbaji madini;

(c) Misamaha ya kodi, ushuru, ada na michango ya aina yoyote;

(d) Ulinzi wa kuhamisha mtaji, faida na gawio na ulinzi dhidi ya utaifishaji ;

(e) Upangaji wa bei au mauzo ya dhahabu;

(f) Kubakisha na kuhamisha nje ya nchi fedha za kigeni;

(g) Wajibu wa kulipa mrahaba, kodi ya mapato na namna ya kuzihesabu kodi hizo;

(h) Jambo lolote ambalo ni la msingi kwa hali ya kiuchumi ya Kampuni.

Mkataba unatamka kwamba vifungu hivyo vya Mkataba ni vya ‘msingi’ na ‘vitakatifu’ na kwamba endapo vitabadilishwa na “… kuiweka Kampuni katika hali mbaya ya kiuchumi kuliko ilivyokuwa wakati wa kusaini Mkataba, basi Serikali kwa mashauriano na Kampuni itachukua hatua za lazima kuhakikisha kwamba haki au maslahi ya Kampuni hayaporomoshwi au kupunguzwa kimsingi”!

VI. UTATUZI WA MIGOGORO

Kufuatiwa hoja ya Mheshimiwa Zitto Kabwe juu ya kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mazingira ya kusainiwa kwa Mkataba wa Buzwagi, kumejitokeza mjadala mkali juu ya utashi wa kimaadili na/au madhara ya kisheria ya Mkataba huu kusainiwa London nchini Uingereza. Tumezungumzia kwa kirefu viwango vya maadili na/au utashi unaotakiwa kwa viongozi wa umma chini ya Sheria ya Maadili ya viongozi wa Umma na hatuna haja ya kurudia mjadala huo. Mjadala unaohusu madhara ya kisheria ni wa muhimu vile vile. Mahali unaposainiwa mkataba (locus contractus) ni muhimu sana kisheria kwa sababu endapo mkataba wenyewe uko kimya juu ya utaratibu wa kutatua migogoro inayoweza kutokana na utekelezaji wa mkataba wake basi sheria za mahali uliposainiwa ndio zinazotumika.

Mkataba wa Buzwagi umefafanua juu ya utaratibu wa kutatua migogoro inayoweza kutokea kutokana na utekelezaji wa Mkataba huu. Kama alivyosema Waziri Karamagi Bungeni, Mkataba wa Buzwagi unataja kuwa sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo itaongoza mkataba huo.” Kauli hii ya Waziri Karamagi ni sehemu tu ya ukweli wa jambo hili kwani kuna ukweli mwingine ambao Waziri Karamagi hakuutaja. Kwanza, Mkataba huu utatawaliwa na sheria za Tanzania “na taratibu za sheria za kimataifa zinazohusika.” Jambo hili limetiliwa nguvu zaidi na kifungu cha 13 cha Mkataba kinachoamrisha kwamba mgogoro wowote “utatatuliwa kwa upatanishi kufuatana na Kanuni za Upatanishi za Tume ya Umoja wa Mataifa ya Sheria za Kimataifa za Biashara (UNCITRAL).”

Pili, mahakama za Tanzania hazina mamlaka ya kusikiliza na/au kutatua migogoro chini ya Mkataba huu kwani jukumu hilo imepewa “Mahakama ya Upatanishi wa Kimaifa ya London kufuatana na Kanuni za Upatanishi za UNCITRAL zitakazokuwa zinatumika wakati wa kusaini Mkataba huu.” Chini ya utaratibu wa Mkataba huu, kila upande unapaswa kuteua mpatanishi mmoja na wapatanishi hao wawili watachagua mpatanishi wa tatu ambaye ndiye atakuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Upatanishi. Aidha, kesi ya upatanishi huo itafanyika London na lugha itakayotumika ni Kiingereza. Vile vile hukumu yoyote itakayotolewa na Mahakama ya Upatanishi itazifunga pande zote na Serikali inafuta haki zake za kudai ulinzi dhidi ya mashtaka kwa nchi huru (sovereign immunity) na inafuta madai yoyote ya ulinzi huo kuhusu mashauri ya kukaza hukumu hiyo … na ulinzi kuhusu ukazaji wa hukumu dhidi ya mali yoyote ya Serikali inayotumika kwa ajili ya shughuli za biashara.”

Tatu, ni muhimu kuelewa kwamba ingawa Mkataba wa Buzwagi unasema kwamba utaongozwa na sheria za Tanzania, sheria zenyewe hazilindi uhuru wa taifa letu na mamlaka ya kikatiba ya taasisi zetu za kutatua migogoro. Kwa mfano, Sheria ya Madini Na. 5 ya mwaka 1998 - ambayo ndiyo sheria itakayoongoza Mkataba huu – inatamka kwamba migogoro yoyote kati ya mmiliki wa Leseni Maalumu ya Uchimbaji na serikali utatatuliwa kwa kufuata kanuni au taratibu za Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID). Kituo hiki ni moja ya taasisi za Benki ya Dunia na kina makao yake makuu New York, Marekani.

Chanzo: Orodha ya Mafisadi
 
Back
Top Bottom