Kuwahusu Karamagi, Rostam, na wenzao...

Kuna wakati huyo Dr Hosea alitangaza mkataba wa Richmond haukukuwa na kosa lo lote la kisheria. DPP anaweza kusema hakuna ushahidi lakini sisi walalahoi hatumwamini. Lao moja wote hao.

Tunaibiwa kisheria. Labda si kosa, kisheria, kuwaibia Watanzania kwa kushirikiana na wawekezaji, kama wanavyofanya akina Karamagi. Nyie mlie tu.
 
Well, kama hakuna ushahidi wa kutosha nadhani kisheria inabidi kina Dr. Slaa na Zitto ambao wana Ushahidi zaidi waufikishe TAKUKURU ili hilo file lifunguliwe Upya. hakuna sheria inayokataza file lililofungwa kutofunguliwa baada ya ushahidi mpya kupatikana.
Na wakati huo huo ni lazim a tukubali kwamba DPP wanaweza kukataa kusimamisha kesi ikiwa hakuna ushahidi wa kutosha ktk mashtaka yaliyowakilishwa na sio ushahidi ambao tunao sisi midomoni mwetu...
Na nadhani kina Dr. Slaa na Zitto wapo ktk nafasi nzuri zaidi ya kudai hilo file lifunguliwe maadam limekwisha fikishwa mbele ya sheria.
Tatizo ilikuwa kulifikisha DPP kutokea Takukuru, kwa hiyo hapa kidogo nadhani inawezekana kabisa kuibua kesi upya!...

Kama DPP ameona hakuna ushahidi tosha wa kumfungulia FISADI Karamagi kesi basi naamini itakuwa vyema Dk. Slaa na Mh. Zitto wafungue kesi bila kupeleka ushahidi TAKUKURU. Wakipeleka ushahidi TAKUKURU ngoma itakuwa ni ile ile inarudi kwa DPP kabla ya fisadi kupanda kizimbani.
 
Ndio maana kuna mahali nimeshauri kwamba Upinzani sasa ndio hasa wakati waku-take charge, maana kisheria wana haki ya kusimama kwenye sheria na kutoa ushahidi unaohitajika.

Ya kusema hakuna ushahidi hilo DPP anajidanganya, maana utaacha wa Richimonduli waliokimbia bungnei bila kufukuzwa kwa sababu ya kukosa utetezi kisheria leo uje useme hakuna kesi ya kuwahukumu mahakamani, are you kiddiong me or what!

- Utawaacha vipi Lowassa, Karamagi, Msabaha, Mgonja, Rostam, Manji, na Noni, eti hakuna ushahidi that is non-sense, tunawakumbusha tu huko wahusika kua tunasubiri na hawa kutinga kwenye sheria, imeshafahamika mjini leo nzima kuwa kesho ni zamu ya Mgonja, they better be for real!
 
Kwa nini iwe sasa zamu ya Mgonja kabla ya Rostam na Karamagi? Ama JK anaipendelea Kilimanjaro?

Na nina swali la nyongeza: Indume Yene amependekeza Slaa na Zito wampeleke Karimagi kwa Pilato wao wenyewe. Ni nani atamkamata? (Maana tunataka wakamatwe, na sio waitwe mahakamani). Nani atakuwa Prosecutor?
 
Sasa Mkapa,Apson na Kingunge twawataka.Lowassa pia tunamuhitaji maanke kama kesi ya Mramba ni kutumia madaraka vibaya,basi lowassa ashtakiwe kwa kutumia madaraka vibaya na uzembe akiwa ofisini huku akilisababishia taifa hasara

kabisaa Lowasa alitumia madaraka vibaya kwa Richmond, na kikwete pia kwa kukiuka sheria kuna sheria gani inayomtaka mwizi kurudisha mali ili asamehewe? Rais yuko above law? mh Mramba mbona hakuambiwa alipe hela alizotutia nazo Hasara?? Mh mi nina mashaka mwenzenu
 
Kwa nini iwe sasa zamu ya Mgonja kabla ya Rostam na Karamagi? Ama JK anaipendelea Kilimanjaro?

Na nina swali la nyongeza: Indume Yene amependekeza Slaa na Zito wampeleke Karimagi kwa Pilato wao wenyewe. Ni nani atamkamata? (Maana tunataka wakamatwe, na sio waitwe mahakamani). Nani atakuwa Prosecutor?

Ipo sheria inaruhusu kuwa na private prosecutors. lakini the trick ni kuwa mpaka mahakama iruhusu private prosecution ndio mashitaka yanaweza kufunguliwa.
Upo mfano wa hilo, kuna mtu anaitwa Alfred Ngotezi, anagombania kumshitaki Mbunge wa Buchosya, samuel Chitalilo kwa utaratibu huu, mpaka leo kesi ya kutaka kuruhusiwa kutumia private priosecutor ndio inaunguruma. Wakishinda ndio watafungua kesi ya msingi.
Chini ya utaratibu huu, mtu akitakiwa kukamatwa anakamatwa na vyombo husika kama kawaida na wito wa kuitwa mahakamani unatolewa na mahakama kama kawaida
 
Mgonja kwa sasa ndio key saspect ktk kesi zote hizi kama ambavyo angekuwa balali.

Lakini mpaka sasa sijaelewa kuhusu serikali inavyomchukulia huyu mgonja yeye ni shaidi au mtuhumiwa namba moja.

wengine wote watakuja baada ya mgonja.
 
Ndio maana kuna mahali nimeshauri kwamba Upinzani sasa ndio hasa wakati waku-take charge, maana kisheria wana haki ya kusimama kwenye sheria na kutoa ushahidi unaohitajika.

Ya kusema hakuna ushahidi hilo DPP anajidanganya, maana utaacha wa Richimonduli waliokimbia bungnei bila kufukuzwa kwa sababu ya kukosa utetezi kisheria leo uje useme hakuna kesi ya kuwahukumu mahakamani, are you kiddiong me or what!

- Utawaacha vipi Lowassa, Karamagi, Msabaha, Mgonja, Rostam, Manji, na Noni, eti hakuna ushahidi that is non-sense, tunawakumbusha tu huko wahusika kua tunasubiri na hawa kutinga kwenye sheria, imeshafahamika mjini leo nzima kuwa kesho ni zamu ya Mgonja, they better be for real!

Kwa jinsi ninavyoziamini post zako naisubiria kwa haamu hiyo kesho nipate kuchekelea, maana huyu Mgonja anajiamini sana sijui kwa nini
 
Itanguwa ngumu sana kumshtaki mgonja... na ata akishtakiwa itakuwa kuwanyamazisha wapoiga kelele.. He will never be found guilty. Jueni hivyo tu.
 
Imetolewa mara ya mwisho: 02.12.2008 0006 EAT
• Karamagi: Richmond iachiwe Serikali

*Aonesha kukerwa na siasa za chuki

Na Mwandishi Wetu
Majira

ALIYEKUWA Waziri wa Nishati na Madini ambaye hivi karibuni amekuwa akihusishwa na uchunguzi katika kashifa kadhaa ikiwemo suala la mkataba wa madini wa Buzwagi na sakata la Richmond,Bw. Nazir Karamagi, amevunja ukimya na kuzizungumzia kashifa zinazomkabili.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Bw. Karamagi kwanza alisisitiza kuwa anaamini msingi wa shutuma zote anazoelekezewa sasa ni ajenda za siri walizo nazo wabaya wake.

"Inasikitisha kuona watu wamejawa na mawazo ya kuhujumiana. Siasa zimejaa chuki na visasi, ndio maana nimeamua kuwa kimya," alisema Bw. Karamagi na kutokuwa tayari kuingia kwa undani kuwataja wabaya wake hao.

Juzi gazeti hili lili lilikuwa na habari ya uchunguzi iliyoeleza uwezekano wa Karamagi na vigogo wengine wa Serikali kukabiliwa na uwezekano wa kushitakiwa.

Karamagi amekuwa akihusishwa na kushitakiwa baada ya faili lake kuhusu uchunguzi wa mkataba tete wa Buzwagi kufungwa na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma (DPP) kutokana na kukosekana ushahidi wa kutosha.

Taarifa za kiuchunguzi zimekuwa zikisema kufunguliwa kwa kesi dhidi ya mawaziri wa zamani, Bw. Basil Mramba na mwenzane, Bw. Daniel Yona kumeonekana kuwa njia kwa vigogo zaidi kufikishwa kortini iwapo wakati wakiwa mnadarakani uamuzi wao katika masuala mbalimbali ulililiingizia Taifa hasara.

Akizungumzia sakata hilo Karamagi alisema hapendi kulizungumzia kwa undani katika kipindi hiki bali anadhani ni busara iachiwe Serikali.

"Suala kwamba nilihojiwa au la si busara kulisema kwa sasa, lakini nami nakumbuka kuwa Serikali ilitangaza kuwa kuna uchunguzi inaufanya kuhusu hilo, tuiachie yenyewe wakati ukifika itasema imefikia wapi," alisema Karamagi na kufafanua kuwa tatizo la tuhuma nyingi kwa wanasiasa nchini pia linatokana na watu kutowaamini wazawa.

"Ninavyoona hatujawaenzi wafanyabiashara wazawa. Kumekuwa na maneno mengi pale mzawa anapoonesha kujituma katika shughuli zake lengo likiwa kumkwamisha, hili haliwezi kutusaidia," alisema Bw. Karamagi ambaye alilazimika kujiuzulu baada ya ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuonesha kuwa pamoja na kwamba hakuwa wizara hiyo wakati mkataba wa Richmond ukisainiwa, lakini alionekana 'kuikingia kifua' kampuni hiyo wakati ilipokuwa ikibanwa itimize wajibu wake.

Pamoja na Bw. Karamagani viongozi wengine wawili waandamizi walijiuzulu kufuatia kashifa hiyo ambao ni aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na ambaye wakati wa kusainiwa mkataba wa Richmond Juni 23, 2006 ndiye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Ibrahim Msabaha.
 
Hakuna siasa za chuki bali Watanzania tumechoshwa na viongozi mafisadi wanaoingia mikataba bila kufanya utafiti wa kina na mara nyingi kuweka maslahi yao mbele badala ya yale ya Taifa. Mkataba na Richmond ulisainiwa kisanii ili kuwanufaisha marafiki zenu na nyinyi wenyewe bila kujali kama kampuni hiyo ilikuwa na uzoefu au la katika utaalam wa kusambaza umeme. Hata mlipogundua kuna utata kuhusu uwezo wa kampuni hiyo mlikaa kimya huku kampuni hiyo ya kifisadi ikiendelea kulipwa mabilioni ya pesa toka TANESCO pamoja na kuwa walikuwa hawazalishi chochote.

Mikataba ya uchimbaji wa madini mbali mbali ikiwemo dhahabu, Tanzanite, Almasi na n.k nayo imesainiwa kwa kuweka mbele maslahi ya viongozi mafisadi na matokeo yake haina maslahi yoyote kwa Watanzania. Tuna rasilimali chungu nzima kwanini tuendelee kuwa maskini miaka nenda miaka rudi wakati rasilimali zetu zikiendelea kuwanufaisha wageni na viongozi mafisadi. Kuwa mkweli wa nafsi yako usitafute mchawi wa kumtupia lawama.
 
Sasa Mkapa,Apson na Kingunge twawataka.Lowassa pia tunamuhitaji maanke kama kesi ya Mramba ni kutumia madaraka vibaya,basi lowassa ashtakiwe kwa kutumia madaraka vibaya na uzembe akiwa ofisini huku akilisababishia taifa hasara
 
Back
Top Bottom