Kuwahusu Karamagi, Rostam, na wenzao...

leteni habari jamani.... Invisible tunakutegemea mpaka jioni ya leo kiwe kimeeleweka!!!
 
Mkuu habari hii jana nimehangaika nayo sana. Kila kitu jana kiliendeshwa kisiri mno, waandishi walishindwa kuelewa kinachoendelea na wengine wakadai hakuna kitu kama hicho.

Nilikuwa na mwandishi eneo hilo na kila nikiwasiliana naye alinambia kashindwa kabisa kuelewa kinachoendelea. Maelezo ya kuwa Meghji, Msabaha na Karamagi walikuwa tayari washahojiwa niliyapata mapema sana lakini inaelekea kama kitendo cha kuwahoji kilifanyika basi kilifanyika kisiri na mashtaka yao walisomewa kisiri sana.

Lemme check the status...


Kaka kama utakumbuka niliripoti jana kuwa hawa watu Walisomewa mashtaka jana na wakashindwa kulipa dhamana waliyoambiwa watoe.Siioni ile post yangu la
 
Mkuu habari hii jana nimehangaika nayo sana. Kila kitu jana kiliendeshwa kisiri mno, waandishi walishindwa kuelewa kinachoendelea na wengine wakadai hakuna kitu kama hicho.

Nilikuwa na mwandishi eneo hilo na kila nikiwasiliana naye alinambia kashindwa kabisa kuelewa kinachoendelea. Maelezo ya kuwa Meghji, Msabaha na Karamagi walikuwa tayari washahojiwa niliyapata mapema sana lakini inaelekea kama kitendo cha kuwahoji kilifanyika basi kilifanyika kisiri na mashtaka yao walisomewa kisiri sana.

Lemme check the status...


Kaka kama utakumbuka niliripoti jana kuwa hawa watu Walisomewa mashtaka jana na wakashindwa kulipa dhamana waliyoambiwa watoe.Siioni ile post yangu
 
Mh! Nipashe gani lililoandika habari hiyo? Nipashe ninalolisoma mimi hapa sasa hivi lina habari kuwa Feleshi amekwamisha mashitaka dhidi ya Karamagi. Sasa kama mashitaka yamekwamishwa, amefikaje mahabusu?
 
leteni habari jamani.... Invisible tunakutegemea mpaka jioni ya leo kiwe kimeeleweka!!!
Iko hivi:

Meghi ni kweli alihojiwa na alikuwa anaandika maelezo. Inadaiwa ni dhidi ya upitishwaji wa malipo kwa Kagoda.

Karamagi DPP kadai hakuna proof ya issue za Buzwagi hivyo nadhani kwa kauli hiyo HANA KESI.

Msabaha na Lowassa wana kesi ya kujibu juu ya Richmond.

Rostam yupo Nairobi kwa sasa na hajawa na kesi ya kujibu.

Ni hayo tu
 
Mh! Nipashe gani lililoandika habari hiyo? Nipashe ninalolisoma mimi hapa sasa hivi lina habari kuwa Feleshi amekwamisha mashitaka dhidi ya Karamagi. Sasa kama mashitaka yamekwamishwa, amefikaje mahabusu?

Ndio maana nimeomba watu mconfirm, mtu aliyeniambia yuko Dar na sikuamini mara moja, mpaka aliponiambia iko kwenye nipashe,

Kwa kuwa NIPASHE ya kwenye Internet bado haijatoka ndio maana nikaomba watu walioko TZ, wadhibitishe kama ni kweli Nipashe imeandika hivyo!!!

Kwa Tanzania ya sasa, kila kitu kinawezekana, Usanii juu ya usanii
 
Iko hivi:

Meghi ni kweli alihojiwa na alikuwa anaandika maelezo. Inadaiwa ni dhidi ya upitishwaji wa malipo kwa Kagoda.

Karamagi DPP kadai hakuna proof ya issue za Buzwagi hivyo nadhani kwa kauli hiyo HANA KESI.

Msabaha na Lowassa wana kesi ya kujibu juu ya Richmond.

Rostam yupo Nairobi kwa sasa na hajawa na kesi ya kujibu.

Ni hayo tu

Hapo kidooogo narudisha IMANI niliishajisemea Safari hii INVISIBLE katulisha KASA.
 
Mhhh sasa tusubiri tuone mwisho wake. Tunaomba alie na habari kamili kuhusu haya atusadie tuufahamu ukerli wa habari hizi.
 
Bado tuna muda wakusubiri nini kili jili jana hapo Kisutu.
Kuna watu lazima wanajua ni nini kilijili jana tunaombeni data zenu jamani watu tumekaa na kimuhe muhe muda wote huu roho juu juu tu.
 
Mapigo ya moyo yanaanza kuongezeka tena kama jana, hili swala la kesi kufanyika kwa siri linakuwaje? Mbona wengine wote wamewekwa hadharani? Ni nini kinafichwa hapa? Kama hili swala ni kweli kabisa basi nimeshaona dalili zote za kipigwa changa la macho. Wananchi tuna haki zote za kujua makosa waliyoshitakiwa nayo maana walichofanya ni kutumia jasho letu kujinufaisha. Kimsingi sisi wananchi ndio washitaki.
 
Habari hii haina ukweli as far as mama Meghji is concerned. NImetoka kuzungumza naye sasa hivi na yuko nje anaendelea na shughuli zake. Hayuko Keko. Hii habari sikuigusa toka jana kwa sababu.

Mapambano haya yana njia nyingine na inashangaza jinsi watu wasivyoelewa mapambano haya.

Inasikitisha sana.
 
Mkuu Invisible

Kama hili kweli limetokea na limefika Nipashe kabla ya hapa JF...na sisi itabidi tuunde tume kuchunguza kwa nini Wana JF mliopo jijini mnatuangusha...mkicheza na sisi tutawafikisha hapo hapo Kisutu..!!!
wa kwanza kukufikisha ni wewe kaa mkao wa kula!hehe
 
Habari hii haina ukweli as far as mama Meghji is concerned. NImetoka kuzungumza naye sasa hivi na yuko nje anaendelea na shughuli zake. Hayuko Keko. Hii habari sikuigusa toka jana kwa sababu.

Mapambano haya yana njia nyingine na inashangaza jinsi watu wasivyoelewa mapambano haya.
Inasikitisha sana.

Mkuu hapo nimeshindwa kukupata umemaanisha nini naomba ufafanuzi kudogo. Njia nyingine zitakuwa zip hizo mimi nimebaki njia Panda. Ni kweli jana hakutoa neno lolote kuhusu hii issue lakini lao umekuja na Sentesi tata kidogo. Naomba ufafanuzi mkuu!
 
Nadhani huyu ni Karamagi

Kigogo anusurika Kisutu

• Ofisi ya DPP yadaiwa kumuokoa dakika za majeruhi

na Happiness Katabazi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MMOJA wa mawaziri aliyepata kuingia katika mkumbo wa watu wanaofikishwa mahakamani wakikabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za serikali amenusurika, Tanzania Daima imegundua.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima ilizipata jana zinaeleza kuwa, mwanasiasa huyo ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo moja lililo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, alinusurika kupelekwa mahakamani jana kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, waziri huyo wa zamani aliyepata kuhusishwa na mkataba wenye utata wa uchimbaji wa madini alikuwa afikishwe mahakamani kwa kosa la kutumia vibaya madaraka yake wakati akiwa waziri.

Chanzo cha habari cha kuaminika kilichozungumza na Tanzania Daima kinaeleza kwamba, hatua ya Ofisi ya Mwendesha Mashitaka nchini (DPP) kumnusuru mwanasiasa huyo, imewashtua baadhi ya maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambao kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa wamekuwa wakilichunguza sakata linalomhusu mwanasiasa huyo.

Mtoa habari wetu aliieleza Tanzania Daima kwamba, kabla ya kuwasilishwa kwa DPP kwa ajili ya uchunguzi zaidi, maofisa wa TAKUKURU walikuwa wamejiridhisha kuhusu kukamilika kwa shauri hilo na kumuacha DPP akichunguza uzito wa ushahidi uliowasilishwa.

"Leo ilikuwa apandishwe kizimbani kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka yake na kulisababishia taifa hasara kubwa lakini katika hali ya kushangaza Ofisi ya DPP imegoma kupeleka mahakamani kesi hii," kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa ili kuelezea taarifa hizi, Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Elieza Feleshi, alikanusha kuingia katika undani wa suala hilo zaidi tu ya kueleza kwamba hawezi kamwe kufanya kazi kwa shinikizo au kwa kusikiliza taarifa za kuzusha.

Feleshi, alisema kila kitu anachokifanya kinatokana na uchunguzi uliofanyika na taasisi mbalimbali zinazohusika na uchunguzi na yeye hupatiwa mafaili ya wahusika ili kujiridhisha kama kuna ushahidi wa kutosha kuwafikisha mahakamani.

‘Eehe bwana wee, mambo hayo unayoyasikia umeongea na vyombo vya uchunguzi na vikakupa taarifa? Maana siku hizi kila mtu anasema lake, mimi sifanyi kazi kwa namna wanavyotaka watu pasipo kufuata sheria," alisema Feleshi.

Alisema yeye anafanya kazi kulingana na taaluma yake, ndiyo maana kila faili analoletewa ni lazima alifanyie uchambuzi wa kina ili kuepusha kumuonea mtu au kulitumbukiza taifa katika matatizo ambayo yanaweza kuepukika, iwapo ataachiwa afanye kazi yake kulingana na taaluma aliyonayo.

Alisema kila kukicha kumekuwa na taarifa zisizo sahihi kuhusu watu kufikishwa mahakamani katika kesi mbalimbali, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaifanya Ofisi ya DPP iwe katika wakati mgumu wa kujibu maswali ya watu mbalimbali.

"Watanzania wasiwe na wasiwasi kwani kila kitu tunachokifanya, kitaonekana kwa jamii, ni jambo la kuvuta subira na kuona nani atafikishwa mahakamani na kwa kosa gani kuliko kueneza uvumi usio na tija kwa taifa," alisema Feleshi.

Alisema wiki iliyopita alishaeleza wazi kuwa DPP atawafikisha mahakamani watuhumiwa wote ambao ushahidi wao utakamilika ili mahakama iweze kuthibitisha wana hatia au la.

"Sioni sababu ya kila siku kuulizwa maswali yale yale kuhusu kesi nitakazozifikisha mahakamani, kama mtu ana kiu ya kuona watu watakaofikishwa mahakamani, basi avute subira," alisema Feleshi.

Tukio hili lilikuja ikiwa ni siku moja tu tangu Waziri wa Fedha wa zamani, Basil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, kupandishwa kizimbazi juzi wakikabiliwa na mashitaka 13 ya kutumia vibaya madaraka yao, kwa kusaini mikataba na kulisababishia taifa hasara ya sh bilioni 11.7.
 
DPP adaiwa kumkingia kifua Nazir Karamagi

2008-11-27 12:07:13
Na Abdallah Bawazir


Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), amezuia kupelekwa mahakamani aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi.

Karamagi anatuhumiwa kutumia madaraka vibaya katika kusaini mkataba wa mgodi wa madini wa Buzwagi.
Imedaiwa kuwa, DPP alichukua hatua ya kuzuia kufikishwa mahakamani kwa Karamagi kutokana na ushahidi dhidi ya tuhuma zinazomkabili kutojitosheleza.

Kesi dhidi ya Karamagi, ilikuwa iwasilishwe katika Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kukamilisha kazi yake.

Habari kutoka ndani ya kikao watendaji wa serikali na wafadhili wanaochangia bajeti ya serikali kilichofanyika Dar es Salaam jana, zilisema kuwa Takukuru walikwisha baini matumizi mabaya ya madaraka katika sakata zima la Buzwagi, lakini DPP akakataa kesi dhidi ya Karamagi isifunguliwe.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mabalozi wote ambao nchi zao zinachangia bajeti kuu ya serikali na Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali.

Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya kikao hicho, kilieleza kuwa, wafadhili walielezwa kuwa, Takukuru ilipeleka majalada ya kesi mbili kwa DPP, ikiwemo inayowahusu mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona ambayo ilitajwa juzi katika Mahakama ya Kisutu pamoja na la Buzwagi.

Ilielezwa kuwa, liliporudi jalada la mawaziri hao wawili wa zamani, lilipitishwa kwa ajili ya kupelekwa mahakamani, lakini la Buzwagi DPP alisema hakuna ushahidi wa kutosha kuifikisha kesi hiyo mahakamani, hivyo kulifunga.

Inadaiwa kuwa, uamuzi huo wa DPP, umeikasirisha Takukuru, ambayo ndiyo iliyokuwa ikikusanya ushahidi ili kesi hiyo iweze kufikishwa mahakamani kwa kuanza kusikilizwa.

Chanzo hicho cha habari cha kuaminika, wafadhili walielezwa kwamba, majalada ya kesi nyingine nne kubwa, zikiwemo zinazoihusu kampuni ya uchimbaji madini ya Meremeta na Deep Green, bado yapo kwa DPP yakisubiri uamuzi wake.

Pia Mabalozi hao waliwaomba kushawishi nchi za Ufaransa, Uswisi, Afrika Kusini, Mauritius, Hong Kong kutoa ushirikiano ili kesi hizo tatu ziweze kukamilika.

Ilidaiwa kuwa, nchi hizo zimekuwa hazionyeshi ushirikiano mara maaofisa wa Takukuru wakihitaji taarifa.

Jitihada za Nipashe za kumpata DPP, Elieza Feleshi jana ziligonga mwamba, kwani baada ya kuwasiliana naye alieleza kuwa, yupo kwenye kikao na kutaka apigiwe baada ya nusu saa.

Lakini baada ya muda huo kupita na kupigiwa, alipokea msaidizi wake ambaye alieleza kuwa, bado yupo kwenye kikao na hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kikao hicho kilikuwa bado kikiendelea.

Nipashe ilipowasiliana na msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria, Omega Ngolle kuhusiana na suala hilo, alisema angeeleza kwa undani suala la jalada la Buzwagi, lakini hakufanya hivyo alipopigiwa simu baadaye.

Sakata la mkataba wa Buzwagi kusainiwa nje ya nchi kwa mara ya kwanza liliibuliwa Bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Zitto alidai kuwa, waziri huyo wa zamani alikwenda kusaini mkataba huo, London nchini Uingereza, kwa kutumia mfumo wa mikataba wa zamani wakati serikali ikiwa inajadiliana na wawekezaji kurekebisha mikataba ya madini nchini.

Suala hilo alilieleza katika mkutano wa nane wa Bunge mjini Dodoma, ambapo alihoji hatua ya Nazir Karamagi kusaini mkataba huo nje ya nchi.

Baadaye, Zitto aliwasilisha hoja binafsi bungeni, akiomba kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge, kuchunguza hali hiyo.

Zitto alieleza kushangazwa na uamuzi wa Karamagi kusaini mkataba wa madini kati ya serikali na kampuni maarufu ya madini hapa nchini ya Barrick Gold Mine kwa ajili ya mgodi ya Buzwagi nchini Uingereza badala ya Dar es Salaam.

Mbali ya kuhoji uhalali wa Karamagi kusaini mkataba huo, kinyume cha maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete ambaye aliagiza kupitiwa upya kwa mikataba yote mipya ya madini, Zitto alikielezea kitendo hicho kuwa kinaongeza wasiwasi wa kuwepo kwa ushawishi wa rushwa.

Hata hivyo, hoja hiyo ilitupiliwa mbali na Bunge na hatimaye Zitto aliishia kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa kile kilichoelezwa amelidanganya Bunge kuhusiana na madai yake hayo.

Alipewa adhabu hiyo kwa madai ya kutoa kauli ya uongo Bungeni dhidi ya Karamagi, inayohusu kusaini mkataba na kampuni ya Barrick, juu ya mradi wa Buzwagi, jijini London nchini Uingereza.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom