Kuwahusu Karamagi, Rostam, na wenzao...

oneni watu waudaku mnavyo hijack the topic.. I hate that about JF.. OK in short Mzee Mkapa hit it off once sijui na huyo Rita.. Yeye akaona sifa akawa anajipaisha na alipoachwa kuchaguliwa in the 1st cabinet alipata kichaa akalazwa ikabidi kaka yake Kweka atoke UK kuja kumuona.. Then Mkapa ndio akampa shavu la Unaibu... Its not a big deal.. Wapenda udaku I hope mmeshiba.. Sasa naomba tusubiri data za topic husika sio kuandika vapour.
 
Mzee Warioba naomba kwa heshima zote asipelekwe Kisutu sababu watakua wanataka kutuondolea mzalendo na kumchanganya na haya majambazi.

Pse pse watu wa system tunajua mnatumia mtindo gani hapa ili kuepusha kitu kikubwa, tafadhali msimpotoshe muungwana na mnajua kilichotokea leo mpaka Karamagi akapona sababu ya ujinga wenu.

Mwacheni mzee warioba wa watu ambae sio FISADI kabisa, na tunajua EL anatumia mbinu gani hapa.

Nakuunga mkono mkuu, hata kama yuko implicated katika mwananchi na meremeta, bado hawezi kukaa kundi moja na manyang'au kama Rostam, Karamagi, Yona na Mramba. Haki itendeke pleaseeee
 
Taarifa tulizozipata zinadai watajwa wote wapo huru.
Nadhani topic hii inatakiwa kufungwa kwa sasa.
 
Kama imefikia hatua ya hawa wakuu kufikishwa mbele ya sheria napata naona kwa mbaaali tumaini likirejea..Tunahitaji zaidi ya haya tuyaona.Na nikitafakari kwa mbali naona ishara mbaya kwa mkuu wa kaya wa awamu ya tatu.Ni kama vile wamemwambia hata wewe tunaweza kukufikia!
 
Wapendwa wana JF, naomba mwenye copy ya hotuba ya rais wakati wa kufungua bunge aiweke hapa... haya yote yalitabiriwa if you read that speech between the lines. Aliwaonya viongozi wenzake, akasema wasimuone ancheka ana msimamo na pia aliwaambia tusije laumiana mbele ya safari. Tatizo lililokuwepo ni kwamba wananchi tunataka mambo haraka haraka bila umakini.. mwenzetu JK ana utulivu .. ndio ametuacha tuchonge wewe halafu ndio papu anafanya mambo... pesa za EPA karudisha na sasa wote waliorudisha na ambao hawajarudisha rupango... soma Guardin ya leo kuna mahojiano ya Mkurugenzi wa Mashitaka.. Cha msingi sasa hivi ni kumuunga mkono sio kushangaa.. JK has proved evry one f us very very wrong

Mpaka tuone kinachofanyika dk za mwisho kuwa hawa watu wanakula miaka na si kupelekwa KEKO tu kwa kukosa Dhamana. Wakila miaka yao hapo ndipo tutaweza kum-judge JK na serikali yake kwamba wamefanya kazi nzuri. Hatutaki changa la macho kwa sababu ya uchaguzi ujao. Uchaguzi ukiisha na kesi zinatupiliwa mbali.
 
Kutokana na mtoto wa mramba kufanya sherehe ya kufuru wakati ule , inasemekana huyo mtoto alizaliwa na anna mkapa sasa hapo sijui ilikuwaje kuwaje ila ule mguu uliharibiwa baada ya huyu mwanamama kurusha stuli

Shy unazungumzia sherehe ipi? Mtoto wa Mramba kwa mama Mkapa ni kiume na alishaoa zamani sana, usije ukawa unamzungumzia huyu binti aliyesendofiwa juzi
 
Hivi akina MNYIKA, ZITTO, Dr SLAA wapo wapi?? mbona hawasemi kitu kwenye hii thread?? si hii tu hata ya Mlamba nimejaribu kuipitia koote lakini hawa waungwana hakuna hata mmoja aliyesema kitu, naanza kuwa na wasi wasi huenda there is something going on behind huko nyuma ya pazia
 
Vipi, hawa jamaa mafisadi walitishia usalama wa Kikwete kwa hiyo akaamua kuwarudi mapema? Nashangaa sipidi yake imekuwa ya haraka sana siku za hivi karibuni, wakati siku za nyuma huko alikuwa akisuasua sana hata pale palipokuwa na ukweli wa wazi kabisa. Sasa hivi naona kaamua kuweka gia ya nguvu na kukanyaga mafuta moja kwa moja bila kulegeza; hebu tusubiri mwisho wake, isijekuwa ni mbio za sakafuni tu.
 
Ndugu wana JF,

Uendeshaji wa kesi hizi ni UFISADI pia,

Inasemekana kuwa ni kweli Kesi dhidi ya Karamagi, Zakia na Msabaha iliendesha jana Kisutu, na wako Keko sasa hivi!!!

Walioko TZ wanaweza kudhibitisha hilo, kwa kuwa inasemekana Gazeti la Nipashe leo limeandika!!!!

Sorry kama thread kama hii imeshawekwa hapa janvini na mtu mwingine.

Word to you guys.
 
Yaani mpaka habari inaandikwa kwenye gazeti (tena Nipashe), tena hapari ni kuhusu Zakia, Karamagi na Msabaha hakuna mwanachama wa JF aliekuwa kuripoti hapa....!!!!!!!!!!!

Hii haiwezekani hata kidogo. Wana JF waliopo Tanzania hawawezi kutuangusha kiasi hiki...hapana sitaki kuamini...!!!

Mpaka dakika hii naamini huu ni uzushi.
 
Ndugu wana JF,

Uendeshaji wa kesi hizi ni UFISADI pia,

Inasemekana kuwa ni kweli Kesi dhidi ya Karamagi, Zakia na Msabaha iliendesha jana Kisutu, na wako Keko sasa hivi!!!

Walioko TZ wanaweza kudhibitisha hilo, kwa kuwa inasemekana Gazeti la Nipashe leo limeandika!!!!

Sorry kama thread kama hii imeshawekwa hapa janvini na mtu mwingine.

Word to you guys.

Mkuu habari hii jana nimehangaika nayo sana. Kila kitu jana kiliendeshwa kisiri mno, waandishi walishindwa kuelewa kinachoendelea na wengine wakadai hakuna kitu kama hicho.

Nilikuwa na mwandishi eneo hilo na kila nikiwasiliana naye alinambia kashindwa kabisa kuelewa kinachoendelea. Maelezo ya kuwa Meghji, Msabaha na Karamagi walikuwa tayari washahojiwa niliyapata mapema sana lakini inaelekea kama kitendo cha kuwahoji kilifanyika basi kilifanyika kisiri na mashtaka yao walisomewa kisiri sana.

Lemme check the status...
 
Mkuu Invisible

Kama hili kweli limetokea na limefika Nipashe kabla ya hapa JF...na sisi itabidi tuunde tume kuchunguza kwa nini Wana JF mliopo jijini mnatuangusha...mkicheza na sisi tutawafikisha hapo hapo Kisutu..!!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom