Kuvaa shati moja kila siku sio umaskini

Kuvaa shati moja kila siku sio umaskini

Tunakuwa Maskini kwa sababu ya kuwekeza kwenye vitu ambavyo havina faida

Wakinga wanafanikiwa kwa sababu ya nidhamu ya Pesa.

Mtu anavaa nguo Moja lakini anawekeza kwenye biashara. Utasikia sina Hela ya kula kumbe kuna sehemu kawekeza hela yake.

Ukweli ni kwamba bila kujitoa Huwezi kuwekeza. Endelea Kuwekeza kwenye muonekano utawakumbuka BUSINESS IDEAS ACADEMY.

Wakati unafuga nywele wenzako wanafuga Kuku, bata, mbuzi na ng'ombe.

View attachment 3297934

Unapanda maua ya mapambo wenzako tunapanda Mboga Mboga

Anza leo kuwekeza hata kwenye maarifa:
View attachment 3297931

Kujipatia kitabu cha Mawazo 112 ya biashara unaweza kututafuta whatsapp: 0612607426 au kwa email: business.ideas613@gmail.com
Mtu hanidanganyi kwa hiyo idelogy mfu.

Kuvaa 'kauka nikuvae' hata kama unajitafuta, ni udwanzi, ni uchafu wa asili wa mtu.

Mfano huu haustahili kuigwa na mtu aliyestaarabika.

Inamaana watu wote wenye maendeleo hawavai na kubadili nguo?

Kila mtu ana kipaumbele chake na mbinu zake za kuserv pesa.
 
Mleta bada hii ideology yako inategemea na context.
Kwa mfano wewe ni shuttle airport, unavaa shati limepauka na kiatu kimetoboka na kibeberu cha kutosha, wateja utawapata kwa manati. Kuna deal au kazi zinategemea na smatness yako

Ulitakiwa useme ishu sio shati moja, bali nidhamu katika matumizi ya fedha, kwa kutofanya matumizi yasiyo ya lazima na kuongeza mapato.
 
Mtu hanidanganyi kwa hiyo idelogy mfu.

Kuvaa 'kauka nikuvae' hata kama unajitafuta, ni udwanzi, ni uchafu wa asili wa mtu.

Mfano huu haustahili kuigwa na mtu aliyestaarabika.

Inamaana watu wote wenye maendeleo hawavai na kubadili nguo?

Kila mtu ana kipaumbele chake na mbinu zake za kuserv pesa.
Hiyo maana yake ni kwamba kipindi cha mwanzo cha kujitafuta labda kuanzia miaka 17-30 usiwe mtu wa kuwekeza kwenye mavazi na vitu vinavyoshuka thamani.

Lakini kwa mtu ambaye amezidi miaka 30+na lazima ujijali na upendeze na kama una watoto hakikisha mabegi yao ya nguo yanajaa na wewe unakuwa na code za mitoko siku ukiamua unanunua suti ya laki mbili unatupia kuutishia umasikini nadhani umenipata boss!
 
Unamsifia anayekula chips kavu za buku upo serious kweli mkuu? Badala ale vizuri kwa afya yake anajitesa kwa kula machips na maziwa anakamua mwenyewe anashindwa kunywa glass moja ya maziwa?

Huko kujitesa kwa kula chips kavu kutakuja kumtesa baadae kugharamia kuweka afya yake sawa na madawa ya hospitalini.
Ni lifestyle yake tu, na suala la afya mara nyingi ni Mungu tu, hata uwe unakula milo 10 kwa siku afya yako ikiyumba ndo basi tena.

Kuna watu ambao toka wamezaliwa hawakijui kitanda cha hospitali ni kutumia mitishamba tu na dawa za asili na wanaishi mpaka wanakufa wakiwa wazee!
 
Ukijua sababu kuu, kwa nini tunaishi? unaweza kuona hii dhana ya tutafute hela huku tukijinyima inakuwa haia maana.

Inatakiwa, mwanzo wa maisha yako mpaka unakufa, unatakiwa kuishi kwa furaha; kwa sababu hapa duniani hatuishi kwa mashindano.​
Pesa yako inabidi itimize mahitaji yako kwanza ya msingi kama mavazi,malazi na chakula(afya).
Ukiona unaforce kuwekeza wakati una nguo moja ujue kuna muda utaivuta tu hiyo pesa ulikoipeleka.
Angalau angeongelea vitu visivyo vya lazima kama ulevi na ngono kupitiliza. Chamsingi ni kupambana kukidhi mahitaji na kuwekeza
 
Nisahihi lakini Mimi naboresha zaidi,Hii ni nzurii umri below 35.Ukivuka hapoo kulaa maisha kwa kidogo ulichopata Duniani mwaisa.
 
Ni lifestyle yake tu, na suala la afya mara nyingi ni Mungu tu, hata uwe unakula milo 10 kwa siku afya yako ikiyumba ndo basi tena.

Kuna watu ambao toka wamezaliwa hawakijui kitanda cha hospitali ni kutumia mitishamba tu na dawa za asili na wanaishi mpaka wanakufa wakiwa wazee!
Kula milo 10 sio afya. Nini unakula ndo muhimu.

Wewe ni mmoja wa hao watu ambao hawajawahi kutumia dawa za hospitali au unaongea tu hadithi za kusadikika
 
Iko hivi ngoja nikwambie mimi nimeishi ukinga huko makete ndani ndani, kijana akifikisha miaka 16 au 17 anapewa akili ya pesa alafu anaingia kwenye utafutaji.

Hata waganga wa kule masharti yao ni hayohayo kijana anaambiwa avae kiatu kimoja tena cha elfu 5 chakula cha elfu 1 kwa siku ametumia hela nyingi ni elfu 6 au 7 haizidi hapo.

Hakuna kunywa pombe ovyo, hakuna kucheza kamari wala kuhonga mtu kama huyo lazima amiliki hela babu.

Lakini makabila mengine hayaelewi hizo mambo ukienda kutafuta unaambiwa tu pambana mwanangu!
Umenena kweli tupu,walihamia Tukuyu kupasua mbao wengi walivunja masharti ya pombe!Wameishia ulofa.
 
Mtu hanidanganyi kwa hiyo idelogy mfu.

Kuvaa 'kauka nikuvae' hata kama unajitafuta, ni udwanzi, ni uchafu wa asili wa mtu.

Mfano huu haustahili kuigwa na mtu aliyestaarabika.

Inamaana watu wote wenye maendeleo hawavai na kubadili nguo?

Kila mtu ana kipaumbele chake na mbinu zake za kuserv pesa.
Kwa kazi ya usalesman ukiwa mchafumchafu,utadoda na vitu vyako!
 
Kwa hiyo mtu atembee peku ili anunue mbuzi? Haya anatembea peku kachomwa na msumali nwenye tetanus matibabu milioni 2, au kagongwa na nyoka kwenye kiisigino Anti-venom gharama laki 6 kwa sindano moja. Ila kupanga ni kuchgua.
 
Back
Top Bottom