A
Anonymous
Guest
Sisi watumishi wa Idara ya Afya tulioajiriwa tarehe 23 Juni 2025 katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji, tunatoa malalamiko yetu rasmi kuhusiana na kutolipwa kwa pesa zetu za kujikimu ambazo kisheria na kiutaratibu zilipaswa kulipwa mara baada ya kuajiriwa.
Hadi kufikia sasa, tumetumikia kwa kipindi cha takribani miezi nane hadi tisa tangu kupokea ajira hizo. Pamoja na muda huo wote kupita, bado hatujalipwa pesa za kujikimu, hali inayotuathiri kiuchumi na kisaikolojia, hasa ikizingatiwa kuwa tulianza kazi katika mazingira mapya bila maandalizi ya kifedha.
Tumejitahidi kutafuta ufumbuzi kwa kufuata ngazi zote za uongozi ndani ya Manispaa, ikiwemo kuwasiliana na Katibu wa Afya pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya. Hata hivyo, jitihada hizo hazijazaa matokeo, kwani hatujapatiwa maelezo ya wazi, ya maandishi wala ratiba maalum ya lini malipo hayo yatafanyika.
Kinachoongeza sintofahamu na kuumiza zaidi ni kwamba idadi ya idara nyingine ndani ya Manispaa hiyo hiyo tayari zililipwa pesa zao za kujikimu tangu mwezi Oktoba 2025, ikiwemo Idara ya Elimu. Aidha, tumeelezwa kwa kauli zisizo rasmi kuwa walimu walilipwa mapema kwa sababu chama chao kina nguvu, na kwamba watendaji wa mitaa na kata wao wanasimamiwa moja kwa moja na Maafisa Utumishi, hali inayorahisisha upatikanaji wa stahiki zao.
Maelezo haya yanazua maswali ya msingi kuhusu usawa, haki, na utaratibu unaotumika katika kushughulikia stahiki za watumishi wa umma, hasa pale ambapo idara zote ni sehemu ya mfumo mmoja wa serikali. Inatia wasiwasi kuona Idara ya Afya ikiendelea kusubiri bila majibu ya kuridhisha, ilhali idara nyingine zimeshalipwa kikamilifu.
Kwa misingi hiyo, tunaomba mamlaka husika zitupatie maelezo ya kina na ya wazi kuhusu sababu za kuchelewa kwa malipo ya pesa za kujikimu kwa watumishi wa Idara ya Afya, pamoja na kuchukua hatua za haraka kuhakikisha haki yetu inalipwa bila kuendelea kutuathiri zaidi.