Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,702
22,743
HABARI MPYA: Kamanda wa Polisi Dodoma amesema yeyote mwenye taarifa kuhusu wahusika waliompiga risasi Tundu Lissu waiwasilishe polisi.

Kwa sasa wamepata taarifa kuwa gari iliyoonekana ni gari nyeupe aina ya Nissan.

Naye mkuu wa mkoa wa Dodoma amesema polisi wameshaanza kufanya upelelezi kuhusu wahusika na kusema watu waendelee kusubiri taarifa kutoka kwenye jeshi hilo

Amesema hawatapenda kuona mikusanyiko sehemu yoyote ya Dodoma mjini kwa sababu jeshi la polisi bado linafuatilia asili ya tukio lenyewe na mikusanyiko ya watu inaweza kutumika vibaya.
Pia wataendelea kuwafaamisha raia kwenye kila hatua watakayofikia



adc7684e7b5f47745028ccb004d3f1db.jpg


[HASHTAG]#Mwananchileo[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom