Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

hahahaha uzi una vituko sana kila aliye changia akiwa under 30 aliyapata aliyo yahitaji mtoa mada hahahah
Yani kila mtu anavyo vyote anavyo vitamani mtoa mada
 
Nini gari, kuna wanaomiliki kampuni za maana.
Wakuu naomba kuuliza hivi humu jamiiforum kuna kijana yeyote ambaye yupo chini ya miaka 30 ambae anamiliki gari na nyumba.Yani ambae ametafuta kwa jasho lake bila kupewa au kurithi.

Nimeuliza hivi kwa sababu mimi nina miaka 25 na ndoto zangu ni kumiliki gari na nyumba kabla Sijaoa.Lakini kila siku zinavyo sogea naona ndoto inakua ngumu kutimia.

Nikipita barabarani au kwenye kumbi za starehe naona vijana wadogo wamepaki magari yao, basi roho yangu inaumia sana.

Hivi inawezekana kweli au ni ndoto za mchana hizi ninazo ota.
 
Nina 24 nimemaliza mwaka jana ndo nyumba yangu ipo kwenye lenta, mambo yamebana ila mwakan namalizia, ikiisha nanunua mchuma. Nilianza biashara ya mazao nikiwa first year

Inawezekana.

Sent From Ikulu-Magogoni street
 
Ngoja nikueleze kidogo, nilimaliza chuo kikuu nikiwa na miaka 26 tayari nilikuwa na biashara yangu ya insurance agency na gari nilikuwa nayo aina ya Nissan March.

Nilifanya marketing nikapata kazi kubwa kwenye kampuni fulani sitaitaja wana malori na tanker trucks nilipokatia bima nilipata faida milioni 40 na ushehe maana alikuwa na lorry zaidi ya mia.

Nilijenga nyumba ndogo nikahamia kwangu mbezi juu interchick. Mwaka uliofata nilipata tena hiyo kazi nikabadilisha gari na miradi ikaanza nikaona nimesimama ilipofika nina miaka 29 nilioa na mpaka sasa nimerudi kwenye profession yangu ya Uwakili na maisha yanaendelea.

So amini kwenye hilo
Mkuu naomba nije pm tuyajenge
 
Nimesoma comments za wachangiaji wa huu mjadala, wengi sana ni waongo ama hawakumuelewa mleta hoja.

Jamani, bila back up ya familia ni ngumu sana kumiliki gari na nyumba kwa under 30! Si semi hawapo, ila sio wengi kiivyo kama walivyo jinasibu humu.

Wengi familia zetu ni zile ukipata kazi tu, macho yote kwako kitu kinachokuchelewesha kuwekeza

Fikiria bei za viwanja hapa mjini, tafakari mishahara ambayo wengi wanaanza nayo! Halafu angalia uhalisia wa namna watu wanavyochangia mjadala huu! Labda kama tunaongelea kujenga huko kijijini kwenye viwanja vya wazee!

Kwa wale wakishua, at the age of 22 - 25 wengi hapa bado hawajawaza kujitegemea tuseme ukweli!!!! Wengi hapa wanakuwa wamekazana na dady i want this, mom I want that, oh dad I want to study masters sijui of what and what na wanakuwa bise na magari na nyumba za wazazi wao!

In reality, ni wachache sana at the age of under 30! Namaanisha, under 30! Wanakuwa na vitu vyote hivyo! Ni wachache sana!
Kwa wale ambao nilisoma lao wakaishia std 7 wengi sasa wana nyumba na gari

Sent From Ikulu-Magogoni street
 
Mbona huu uzi waliochangia wengine under 30 wanasema wana gari ila plofile zinaonesha umri umeenda
 
Mkuu kabla haujamiliza chuo ulikuwa na gari na kampuni....mtaji wa kuanzisha kampuni na kununua gari ulitoka mfukoni mwako au support ya family??
Mtoa mada kasema vitu vya kwako si support (kupewa mtaji) au vya kurithi...hapa tunazungua wale waliostruggle wenyewe tu hao wengne ni out of this
Ni pesa yangu bro, kufungua kampuni hauhitaji kuwa na mamilioni. Nilikuwa nalima mahindi na maharage toka ujanani mwangu nikiwa nyumbani kwetu na ninauza. Nimekuwa nahangaika na biashara za kila aina ndugu yangu.

Ni ngumu sana kuelewa ila nataka nikuhakikishie sijawahi kuoewa hela nianzishe biashara maana wazazi wangu wamefariki nikiwa na miaka kumi na tatu tu.

Leo mie ni wakili wakujitegemea ila niliamua kusoma tu hata hivyo biashara nyingine ndio zinanifanya niishi maisha haya.
 
Mkuu humu kila mtu atakwambia anavyo wakati wengine ni family relay au wa kuishi kwa shemeji. Cha msingi pambana tu utavipata achana na story za watu wa JF wengi ni waongo
kuna porojo ziko humu, kila mmoja maisha mazuri under 30 ana kila kitu

ukifatilia uzi wa matengenezo ya magari kule huwaoni asa haya magari yepi? wanayo sema

uzi wa ujenzi huwaoni hata kuulizia bei ya marumaru dizaini mpya.

Oooh nna 23 nna vyote ivo, ***** naona gari na nyumba vimekuwa matako sasa kila mmoja anavyo

Nna 28yrs sina chochote.
 
Mimi cjafanikiwa kujenga..ila namiliki biashara zaid ya moja..ikifika September nikaanza ujenzi kwenye kiwanja changu nonstop tena ndani ya mkataba wa kampuni fulani hv ya ujenzi inayofanya vizuri hapa mjini..mahesabu yake kutokana na ramani itagharimu mil 52.5 na ujenz utachukua muda wa mwenz 1 na wiki mbili. Kuhusu gari sina presha nina uhakika nyumba ikiisha sina miez 3 nitahakikisha navuta brevis moja ya adabu. Maisha ni malengo.umri wangu ni miaka 26 tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana tena sana tu. Japo gari na nyumba kwa upande wangu si maendeleo.
Mara ya kwanza kupata pesa nilinunua Shamba la miti ya miaka 3...hapa nilipo imebaki miaka 4 ili nivune, nadhani mzee Mkapa atakuwa jirani yangu pale rushoto maana sitokubali tena kuishi jiji la joto na makelele hapa Dar...ila ukiniona kama Lofa flani hivi wala hunidhanii kabisa.
 
Mm nilifukuzwa nyumbani nikiwa 19 yrs nikaowa wen i was 21 nikiwa na escudo bro nikahama bara zima la africa na wife nikiwa 26 yrs nimejenga kigamboni tuna watoto 2 na sijutii uamuzi wakuowa na changamoto zake she is all i needed in life and she has sharpen my mind get a wife utapata vyote .....and more

Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom