Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,834
- 18,835
Wakuu niaje, kuna mikopo ambaypo fedha zake hutengwa kwenye asilimia 10 ya mapato ya halmashauri, mikopo hii inaelezwa inatolewa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
sasa kwenye bajeti ya mwaka huu imependekezwa kwenye huo mkopo badala ya kutolewa asilimia 10 ya mapato, itolewe tu asilimia 5 na hiyo asilimia 5 nyingine itumike kujenga maeneo maalum kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo (machinga) kufanyia biashara zao.
lakini hili limekumbana na upinzani mkali kutoka kwa wabunge wengi wa CCM kuwa hii mikopo inasaidia sana vijana na wanawake na kuiondoa italeta balaa janga kubwa sana.
sasa hii mikopo inatolewa na ina msaada kiasi hicho kweli kama inavyosemwa? maana nilisikia pia kutoka kwa Rais Samia mwenyewe, kuwa hii mikopo inatolewa kwa kujuana na rushwa na inatumika na wabunge kuhonga watu wao ili wawapitishe tena.
je nauliza kuna mtu aliyeweza kupata hii mikopo? au kuna mtu unayemjua aliwahi kupata huu mkopo? ama uliwahi kuomba huu mkopo ukanyimwa na ukapewa sababu gani.