Rais Samia: Madiwani na Wenyeviti wa Halmashauri wanachukua Mikopo ya 10% kwa Vikundi Feki

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120

Rais Samia amesema Serikali inashughulikia namna itakavyotoa tena Mikopo ya 10% ya Halmashauri kwaajili ya Vikundi ambayo ilisitishwa baada ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2022/23 kuonesha kulikuwa na ubadhirifu mkubwa

Akizungumza wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu Dar es Salaam, Rais Samia amesema kuna baadhi ya Watu hawadaiwi Fedha hizo kwasababu ni Watumishi wakiwemo Madiwani na Wenyeviti wa Halmashauri na Wanaounda Vikundi Bandia wanapewa Pesa wakati Vikundi havipo

Rais amesema Fedha hizo zilitengwa kwaajili ya Wananchi lakini zikaanza kutolewa kinyume na taratibu kutokana na baadhi ya Wasimamizi kukosa Uadilifu kwenye majukumu yao
 
Back
Top Bottom