Kuna mchezo unachezwa na wapo wanaopenda kucheza mchezo huo. Mchezo unaochezwa na wenye kucheza hucheza. Mchezo huo huchezwa na wale wenye kuupenda mchezo huo. Ukikaa pembeni wanakushangaa kwanini hutaki kucheza na ukiingia kucheza utakavyo watakuuliza 'mbona huchezi kama sisi'? Ukiwaambia mchezo wenu haufuati kanuni wala mlio wa muziki watakuambia haijalishi wewe cheza tu alimradi uonekane unacheza. kuna mchezo unachezwa na wapo wanaopenda kucheza mchezo huo. Ukialikwa kucheza utacheza au utabakia kutazama? Au utajaribu kutaka mchezo ubadilishwe ili wengi waufurahie kwa kufuata kanuni, na mirindimo yenye kuendana na uzuri wa mchezo wenyewe?
Ndugu zangu, kuna mchezo unachezwa, na wapo wenye kupenda kucheza mchezo huo!
MMM
Mzee Mwanakijiji, with due respect, we all know politics is a dirty game, and we all knows the games people play!.
Kabla ya mchezo wowote, rules of the game zinakuwa put forward, timu zote ninakubali kuwa zita play by the rules, on the middle of the game, unakuta rafu za ajabu na refa anazifungia macho ili game iendelee wewe ushindwe. Kwenye rules of the game, pia wamekuwekea provision kama utayaona hayo unayoyaona, unatakiwa ufanye nini within the rules ili kuusimamisha mchezo na wewe kutendewa haki, haki yako ni kusimama kucheza na kubaki uwanjani kushinikiza fair play vinginevyo pambano livunjike.
No matter how bad your situation is, don't loose your temper, you can make it worse!. Hata kama mnajua refa hawatetei haki, bado ni lazima kupeleka timu uwanjani na kutumia kanuni kumlazimisha refa kutenda haki, na sio ku play no show, wenzenu watajipatia ushindi wa mezani!.
Isome kwa makini kanuni ya 86, kwa nini Chadema hawakuitumia kuusimamisha muswada huo?. Hivi unajua kuwa hotuba ya kambi ya upinzani ni pre-requisite ili muswada wa serikali usonge mbele?. Kwanini Mhe. Lissu hakuitumia kanuni hiyo ya 86 kutosoma hotuba ya kambi ya upinzani, hivyo muswada lazima ungekwama kuwasilishwa kwa mara ya pili na ungelazimika kurudishwa kwenye kamati?!.
Kwa vile Chadema had a chance, but lost the chances they've been given tena kwa kuwafungulia mlango wa kuendelea na safari, huko kususia wataachieve nini?.
Kwenye mapambano yoyote, au vitani, kuna ile strategy ya "no retreat, no surender", hapa ni kupigana mpaka risasi ya mwisho, na tone la mwisho la damu linamwagika, at the end of the day, unakuwa umekufa kishujaa kama Ghadafi!.
Stategy nyingine ni ile ya "if you can't beat them, join them", ili ujijenge upya na kuja ku fight them from within. Hii ni strategy ya compromise, "if you can get what you want, take what you get" ili safari iendelee na sio kuisusa safari jumla, wakati wenzako wanaendelea, mwisho wa siku, watakaofanikisha safari, ni wale tuu waliofika mwisho wa safari no matter how rough the road was!.