Kuna Mchezo Unachezwa!

Mzee Mwanakijiji,

Lakini yawezekana sisi wananchi ndio hatujui mchezo wa mgonjwa alolazwa ICU akitetemeka kwa hofu ya kufa tukidhani anapandisha mashetani na dhikiri. tatizo kubwa ni kutoelewa WATU na MAZINGIRA maanake kuna watu waliondoka Muhimbili, O'bay na Lugalo wakaenda Loliondo kwa imani tu kwamba kikombe cha babu kitawaponyesha kuliko tiba ya hospital. Tumewaona wazee na wakubwa wote wakienda huko wengine tukajiuliza kulikoni?... wengine tukafunga safari nasi kwa mkumbo ule ule maadam kenda Lowassa basi lazima kuna tiba, kumbe mwenzetu ndio yuko ktk mkakati wa kuvuta wachezaji ili ngoma yake ipate kunoga...

Sasa, maadam imani ya tiba toka Hospital imekwisha na uchawi ama uganga sasa hivi ndio umeshika maamuzi ya wahitaji wengi, tutaendelea kucheza ngoma za kichawi na yeyote anayepinga ngoma za mizimu atafanyiwa kafara...(kina Mwakyembe). Na kibaya zaidi tumeshindwa kujiuliza kwa nini watu wengi hawaendi tena Hospital badala yake wanachezeshwa ngoma za kiasili? - UWEZO! ni asilimi 20 tu ya wananchi wote wanaweza kugharamia tiba ya Hospital zetu, sasa mtu kwenda Loliondo sii kwa sababu anapenda ama kuamini isipokuwa unafuu wake ndio umempa imani mpya...Watu wengi hawailewi katiba mpya italeta ama ina ubora gani kwa sababu hawajawahi kucheza ngoma nyingineyo..

Katiba Mpya haitapatikana kwa matakwa yenu..Hili sio Disco mnakocheza kwa santuri, CD na Video zenye ujuzin wa kubadilisha kila muziki, bali ngoma ya kienyeji ambayo haina vimbwenga vya keyboard mnavyotaka vijana wa generation hii. Sasa aidha mcheze ngoma yao, mvae njuga na madogoli mtaweza kuielewa ngoma yao, laa sivyo tafuteni uwanja mwingine..CCM will never, and I mean never let the Constitution inayowalinda na waliyoizoea ibadilishwe na kuwa ngoma za vijana wa Madisco. Bado mizee tumeshika hatamu na ngoma za kienyeji zitaendelea kupigwa na kama mnataka mabadiliko lazima yawe ktk ngoma za asili..Sisi wazee tutaweza vipi kucheza ngoma yenu vijana? - aaaaah!
 
unazungumzia wale wenzetu wanaoshinikiza maandamano? Hivi kweli yatakuwepo? Kweli haka katiba kadogo sana. Hakatoshi kumponyesha mgonjwa. Labda pia kautaalam nako ni kadogo. Labda tukifika India tiba itakuwa advance zaidi, na mgonjwa atapona
 
M
Sasa, maadam imani ya tiba toka Hospital imekwisha na uchawi ama uganga sasa hivi ndio umeshika maamuzi ya wahitaji wengi, tutaendelea kucheza ngoma za kichawi na yeyote anayepinga ngoma za mizimu atafanyiwa kafara...(kina Mwakyembe). Na kibaya zaidi tumeshindwa kujiuliza kwa nini watu wengi hawaendi tena Hospital badala yake wanachezeshwa ngoma za kiasili? - UWEZO! ni asilimi 20 tu ya wananchi wote wanaweza kugharamia tiba ya Hospital zetu, sasa mtu kwenda Loliondo sii kwa sababu anapenda ama kuamini isipokuwa unafuu wake ndio umempa imani mpya...Watu wengi hawailewi katiba mpya italeta ama ina ubora gani kwa sababu hawajawahi kucheza ngoma nyingineyo..

Katiba Mpya haitapatikana kwa matakwa yenu..Hili sio Disco mnakocheza kwa santuri, CD na Video zenye ujuzin wa kubadilisha kila muziki, bali ngoma ya kienyeji ambayo haina vimbwenga vya keyboard mnavyotaka vijana wa generation hii. Sasa aidha mcheze ngoma yao, mvae njuga na madogoli mtaweza kuielewa ngoma yao, laa sivyo tafuteni uwanja mwingine..CCM will never, and I mean never let the Constitution inayowalinda na waliyoizoea ibadilishwe na kuwa ngoma za vijana wa Madisco. Bado mizee tumeshika hatamu na ngoma za kienyeji zitaendelea kupigwa na kama mnataka mabadiliko lazima yawe ktk ngoma za asili..Sisi wazee tutaweza vipi kucheza ngoma yenu vijana? - aaaaah!

Ni kweli kabisa maana kama haya ya chachacha yanatushinda labda tujaribu haya mambo ya gombe sogo na segelesegele!
 
yes, deus kibamba amealikwa kucheza na sasa anacheza mchezo huo(angalia channel ten deus akicheza kwa kumsifia jk, muda si mrefu chadema, nccr nao wataingia kwenye rumba na mchezo utakwisha, mwishoni mwa siku wote watapewa medali yaani katiba ya jk na wachezaji wake na wala si katiba ya watz
 
Mchezo ni huu, Edo tayari a viable pres. candidate wa CCM 2015 tena mchezo mtamu maana ccm wenyewe watampitisha, umagamba mtajua wenyewe na search anakubalika kweli kichama, na campaign ishawaka moto, na my ubongo unaniambia atashinda sanaaa, 90 mins bado ila jamaa kasha wapiga mabao wapinzani wake woote, watching.....

Kuna mchezo unachezwa na wapo wanaopenda kucheza mchezo huo. Mchezo unaochezwa na wenye kucheza hucheza. Mchezo huo huchezwa na wale wenye kuupenda mchezo huo. Ukikaa pembeni wanakushangaa kwa nini hutaki kucheza na ukiingia kucheza utakavyo watakuuliza 'mbona huchezi kama sisi'?

Ukiwaambia mchezo wenu haufuati kanuni wala mlio wa muziki watakuambia haijalishi wewe cheza tu alimradi uonekane unacheza.

Kuna mchezo unachezwa na wapo wanaopenda kucheza mchezo huo. Ukialikwa kucheza utacheza au utabakia kutazama? Au utajaribu kutaka mchezo ubadilishwe ili wengi waufurahie kwa kufuata kanuni, na mirindimo yenye kuendana na uzuri wa mchezo wenyewe?

Ndugu zangu, kuna mchezo unachezwa, na wapo wenye kupenda kucheza mchezo huo!

MMM
 
LOL!!
You've made my weekend!!
 
shida ya mchezo wenyewe wakati wa kupumzika wachezao wanakula nyama ya binadamu! Watakualika uingie mchezoni.Utaona wenzako waliokuwa wakiangalia mmojammoja wanainuka na kuanza kucheza. Wakicheza tofauti wanaulizwa kwa ukali au vitisho,KWANINI HUCHEZI KAMA SISI? Wananyongea na kukubali kucheza. Utajikuta uko peke yako ama huna hakika kama wengine walioanza kucheza bado wako upande wako ama la!
 
Naam mchezo ni mtamu sana hasa unapokuwa na busara [wisdom] lakini ni mchungu sana unapokosa busara.Wachezeshwaji uchezeshwa pale wanapoalikwa kucheza mchezo wakapewa jezi wakakubali kuingia bila kujua kanuni za mchezo.Ukiwa mchezaji makini [Mwenye busara] ukaomba kujua kanuni za mchezo,watakwambia kanuni zipo utazijua kiwanjani we ingia hakuna shida.Ole wako ukakakosa busara hivyo kichwa kichwa ukaingia bila kujua kanuni za mchezo, ghafla ukataka kumlekebisha Refa kwa kosa [foul] unaliona zaili kuwa ni kosa ndani ya mchezo.Refa wa mchezo achelewi kuwambia marunsman wake kuwa mwangalieni mchezaji huyu ni mjanja wa kukosoa kuwa hatuchezeshi vizuri wakati watazamaji [Audiences] walioko jukwaani tunawasikia wanasema REFA PETA TU [Yaani Refa endeleza Mchezo].

Kwa kuwa Mwasisi wa Mchezo alianzisha mchezo wa kiwanja cha Watanzastadium,akiwa hana sheria sahihi za kanuni za kuwafaa wachezaji akiamini kuwa atashirikiana na wachezaji kutunga sheria sahihi kulingana na uwanja na mahitaji ya washangiliaji wa mchezo.Lakini chonde Refa wa kwanza uchezeshaji wa mchezo wake ulikuwa ni wa damu kutokana na mapenzi ya dhati ya kuupenda mchezo kama watizamaji wa mchezo huo walivyoupenda wakati akiuchezesha japo baadhi waliona anachezesha kishamba, lakini kumbe kwa ushamba wake huo ndiye aliyekuwa na ,mapenzi dhahili ya kusimamia burudani ya Watanzastadium.

Leo hii wachezaji watatu wamebahatika nao kuwa ni sehemu ya Marefa wa wachezaji wa kiwanja cha burudani cha Watanzastadium,mambo yamekuwa si mambo wamenogewa na kuchezesha kwa stairi ya zamani ya hiari wakati wameingia kama marefa wa kulipwa,Marefa leo sio tena ni marefa wa hiari bali ni marefa wa kulipwa [Professionalism].Hakika wachezaji wamekaribisha kucheza lakini mwiko kuomba kanuni,na kama uwezi kucheza nenda kakae nyumbani,na kama ukikaa jukwaani tena kuanzia sasa ukae kimya vinginevyo ukipiga kelele za kusema refa refa mbona unachezesha kimafyongo,Refa atakufuata uko uko jukwaani na kukuramba kadi ya njano [Yellow Card] sana sana akichukia sana anakuramba kadi nyekundu [Red Card] na kuagiza wasimamizi wa ulinzi wa Watanzastadium kukutoa nje ya uwanja na ndio mwisho wako kuhudhulia mchezo wa watanzastadium kama mchezaji au mshangiliaji.

Kupitia kuingia kwa teknolojia kama vile computer na television mashabiki na baadhi ya wachezaji wa mchezo wanaona na pia kuanza kujifunza mbinu mpya na za kisasa za kucheza na kushangilia kwa aina mpya yenye ubora wa mchezo na pia wenye faida nzuri kwa pande zote tatu yani wachezaji, wachezeshaji [Refa na runsmans wake] na hatimae watazamaji au mashabiki wa mchezo husika.

Hakika Mchezo umenoga lakini refa wa sasa na baadhi ya wachezaji wao bado wanaamini kuendelea kucheza kwa style na mfumo ule ule wao wanaoamini kuwa ni sahihi kumbe,mashabiki na baadhi ya wachezaji wameshajifunza aina mpya ya burudani ya uchezaji na ushangiliaji hivyo wakati wowote uwanjani hapo mchezo unaweza vunjika na mechi hiyo inaweza kuleta kizaazaa.

Hakika Mechi hiyo yaweza kuzaa WIMBO mtamu kuimbwa na timu mbili uwanjani ama "SIMBA IMARA SIMBA IMARA, YANGA YANGA MAKOPO" au "YANGA IMARA YANGA IMARA, SIMBA MAKOPO SIMBA MAKOPO."

Haya tena kidedea au ?
 
mh! huo mchezo ni wa mpira wa miguu na wanaocheza ni vipofu na pia ni viziwi hivyo hawajui goli liko upande gani? na wala hawasikii filimbi ikilia na inaonekana refa ni kiwete hivyo hawezi kuwafukuzia wachezaji na kuiona faulo vizuri na pia namuonea huruma maana kuumaliza huo mpira ni kazi.
 
Yaaa, ni kwelikuna nmchezo unachezwa; wachezaji wanacheza kwa STEPU ILI WASIOCHEZA WASIJUE KAMA MCHEZO UNACHEZWA, lakini tunawaona wanacheza, na stepu zao hatujui kama ni za kweli kwani hata mdundo hatuuskii-tutabadili vp stepu MMU/? wakati hatujui hata mchezo unaochezwa/? cmon maan; najua cjui kwa nn unaongea hv, kama lengo lako ni kutujuza kuwa mchezo unachezwa kwa stepu zisizochezeka....kwa nn tena na wewe unacheza kama walle jamaa wanaocheza/?:spy::spy:
 
shida nyingine ya huu mchezo huwezi kutoka kwa kuamua mwenyewe kiwanjani! Ni mapumziko tu ambapo kukata kiu mnakunywa damu ya binadamu! Hata kama hukupenda mchezo wenyewe,unashurutishwa kucheza tu!
 
Aisee!nimeipenda sana hii..siku nyingi nilikuwa sijacheza mchezo wa kuifikirisha medula.
 
huu mchezo unachezwa na Wababe na wenye Hela kama Sumo na Golf, we mnyonge na maskini kaa pembeni.
 
Chakacha, kirumba, gombesugu, mdundiko, hata achezae kwa kuimba kwaya au iwe ni rusha roho. Utaingia mtazamaji ukaanzishe mirindimo yako pasi na kualikwa? hata huo mchezo ukiwa ni mdako inabidi ukaribishwe.

Wa Mwambao hunena "matezo n' gharama".
 
Kuna mchezo unachezwa na wapo wanaopenda kucheza mchezo huo. Mchezo unaochezwa na wenye kucheza hucheza. Mchezo huo huchezwa na wale wenye kuupenda mchezo huo. Ukikaa pembeni wanakushangaa kwa nini hutaki kucheza na ukiingia kucheza utakavyo watakuuliza 'mbona huchezi kama sisi'?

Ukiwaambia mchezo wenu haufuati kanuni wala mlio wa muziki watakuambia haijalishi wewe cheza tu alimradi uonekane unacheza.

Kuna mchezo unachezwa na wapo wanaopenda kucheza mchezo huo. Ukialikwa kucheza utacheza au utabakia kutazama? Au utajaribu kutaka mchezo ubadilishwe ili wengi waufurahie kwa kufuata kanuni, na mirindimo yenye kuendana na uzuri wa mchezo wenyewe?

Ndugu zangu, kuna mchezo unachezwa, na wapo wenye kupenda kucheza mchezo huo!

MMM

Sie watazamaji hatuna wasiwasi ilimradi kati ya timu zinazoucheza huo mchezo yupo mwamuzi. Tena mwamuzi asiekuwa na upendeleo maana uamuzi atakao ufanya ni kwa maslahi ya wote!
 
Back
Top Bottom