Kuna kazi nyingi katika nchi hii hazina faida kwa Taifa. Serikali ifikiri namna ya kuzikomesha au kuziboresha

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,141
Nchi ya Tanzania watu wanachapa kazi sana na watu wavivu au wenyewe wanajiita wasio na kazi wako pia.

Turudi kwenye mada.

Serikali inawaza nini juu ya kazi ambazo hazina tija kwa taifa, hazichangii pato la taifa?

Kazi ambazo zinampa ugali mfanyaji na familia yake basi.

Taifa litasonga vipi mbele ikiwa wananchi wako busy kufanya kazi zisizo na mchango kwenye pato la taifa?

• Kazi ya udalali
Hapa nchini haina mchango kwenye kukuza pato la taifa. Madalali hawalipi Kodi. Hakuna wanachozalisha.
Ni muda sasa madalali wasajiliwe na kulipishwa kodi. Ni aibu nchi kubwa kama hii kusaidiwa na kinchi kidogo kama Uswizi. Dawa ni kupanua wigo wa mlipa Kodi.

• Kazi za umachinga
Licha ya kazi hii kuwa ndiye mwajiri mkubwa hapa nchini lakini haina faida kwa Taifa. Machinga wengi au wote hawalipi Kodi licha ya kuwa wapo machinga mauzo yao kwa siku moja kufikia mpaka milioni 5. Pili machinga wengi huuza bidhaa za kichina hivyo machinga ni watumishi wa nchi ya uchina wanaofanya kazi nje ya China. Wanakuza uchumi wa nchi za watu .

• Kazi ya bodaboda
Serikali imeshindwa hata kugawa leseni za kuendeshea bodaboda angalau kwa sh. 50000. Kazi ya bodaboda haina manufaa kabisa kwa hii serikali. Bodaboda ni kama kitengo cha ukusanyaji mapato binafsi ya polisi na mgambo. Wapo watu watasema bodaboda ananunua mafuta serikali inapata kodi, lakini wanashindwa kufikiri zaidi ya hapo. Kwanza bodaboda zinajenga uchumi wa India na China maana wao ndio wanaozizalisha na kuzi export maelfu kwa maelfu kila siku kuja kuvunja migongo ya vijana wa Dunia ya 3.
 
Mkuu Kodi hizi ambazo wenzetu walioko kwenye system wanapiga? Tangu nakua nasikia tu kiongozi fulani kapiga bilioni, million kadhaa, etc na hakuna hakuna hatua wanachukulia. Hapana kwakweli Kodi inayokusanywa tu ingekuwa inafanya kazi km inavyotakiwa tungekuwa mbali sn.

Inatia uvivu sn,ndo maana ht wakwepa Kodi wengi.
 
Na pesa za misaa kila leo zinaingia
 
Kuna kazi zingine unaweza kuziona hazina tija, ila government inaziacha ziwe ili kuziba gape la wasiokuwa na ajira. Kwanza uelewe kuwa Dunia nzima hakuna nchi ambayo serikali imefanikiwa kuwapa raia wake wote kazi. Hata USA kuna jobless, hivyo inaangaliwa njia ambayo inasaidia au itasaidia kupunguza hao jobless.

Serikali ikianza mfano kuwakamua wamachinga kwenye swala la kodi, wengi watashindwa kulipa na hivyo kujikuta wanakaa mtaani bila kazi na wakati wana familia mke mtoto au watoto.

Mwisho wa siku kila mtu atataka kuwa mwizi ili apate hela ya kulisha familia yake, au kuwalipia watoto ada za shule.
 
Mkuu Kodi hizi ambazo wenzetu walioko kwenye system wanapiga???
Tangu nakua nasikia tu kiongozi fulani kapiga bilioni, million kadhaa ...etc na hakuna hakuna hatua wanachukulia..
Hapana kwakweli Kodi inayokusanywa tu ingekuwa inafanya kazi km inavyotakiwa tungekuwa mbali sn...

Inatia uvivu sn,ndo maana ht wakwepa Kodi wengi......
Sawa,Woman of God!....
 
Kuna kazi zingine unaweza kuziona hazina tija, ila government inaziacha ziwe ili kuziba gape la wasiokuwa na ajira. Kwanza uelewe kuwa Dunia nzima hakuna nchi ambayo serikali imefanikiwa kuwapa raia wake wote kazi. Hata USA kuna jobless, hivyo inaangaliwa njia ambayo inasaidia au itasaidia kupunguza hao jobless.

Serikali ikianza mfano kuwakamua wamachinga kwenye swala la kodi, wengi watashindwa kulipa na hivyo kujikuta wanakaa mtaani bila kazi na wakati wana familia mke mtoto au watoto.

Mwisho wa siku kila mtu atataka kuwa mwizi ili apate hela ya kulisha familia yake, au kuwalipia watoto ada za shule.
Jobless wa Marekani wengi ni wa kujitakia. Kama umewahi kwenda Marekani au kuwa na rafiki wa karibu raia wa Marekani utagundua hilo.
Marekani non professional job ziko nyingi na kwa siku moja hukosi Dola 100 sawa na laki mbili na 40 ya Kibongo.
240k ndio mshahara wa kampuni binafsi wa mwezi mzima bongo. Tena kampuni nyingi nilikuwa zinalipa laki na 50 kwa mwezi na hiyo kazi kuipata mpaka connect au rushwa.
Imagine kazi ya malipo ya sh. 5000 kwa siku Tanzania unaipata kwa kuhonga
 
Mkuu,hiyo bange umeivutia wapi🤔.Ofsini au chooni,au kwenye gari mkuu.
Taifa Lina hasara kuwa kubwa kuwa na watu wenye maono na mtazamo kama wa kwako mkuu.

Una chuki isiyo ya kawaida.
Hauna ubunifu wowote kwa taifa,na kama umeajiriwa basi ni hasara tupu.
Nilitegemea nikute umetaja baadhi ya mashirika na taasisi ambazo ndo zinaliingiza taifa hili katika hasara.
We kaa na hako kamshahala na uendelee kulipa madeni ya mikopo mpaka ustaafu.
Hizo nyanja ulizitaja inaonekana uelewa wako ni ziro.pole,povu ruksa.
 
Kazi ya udalali hapa nchini haina mchango kwenye kukuza pato la taifa. Madalali hawalipi Kodi. Hakuna wanachozalisha.
Ni muda sasa madalali wasajiliwe na kulipishwa kodi.
Ni aibu nchi kubwa kama hii kusaidiwa na kinchi kidogo kama Uswizi. Dawa ni kupanua wigo wa mlipa Kodi.
Hii imeisha ua hoja yako madalali wanalipa kodi! Tatizo namna ya kukagua mapato Yao ndiyo changamoto
 
Jobless wa Marekani wengi ni wa kujitakia. Kama umewahi kwenda Marekani au kuwa na rafiki wa karibu raia wa Marekani utagundua hilo.
Marekani non professional job ziko nyingi na kwa siku moja hukosi Dola 100 sawa na laki mbili na 40 ya Kibongo.
240k ndio mshahara wa kampuni binafsi wa mwezi mzima bongo. Tena kampuni nyingi nilikuwa zinalipa laki na 50 kwa mwezi na hiyo kazi kuipata mpaka connect au rushwa.
Imagine kazi ya malipo ya sh. 5000 kwa siku Tanzania unaipata kwa kuhonga
😀😀😀
 
Kuna kazi zingine unaweza kuziona hazina tija, ila government inaziacha ziwe ili kuziba gape la wasiokuwa na ajira. Kwanza uelewe kuwa Dunia nzima hakuna nchi ambayo serikali imefanikiwa kuwapa raia wake wote kazi. Hata USA kuna jobless, hivyo inaangaliwa njia ambayo inasaidia au itasaidia kupunguza hao jobless.

Serikali ikianza mfano kuwakamua wamachinga kwenye swala la kodi, wengi watashindwa kulipa na hivyo kujikuta wanakaa mtaani bila kazi na wakati wana familia mke mtoto au watoto.

Mwisho wa siku kila mtu atataka kuwa mwizi ili apate hela ya kulisha familia yake, au kuwalipia watoto ada za shule.
Hapa umemaliza utata.
 
1.) Alibaba ni dalali tu, bila alibaba itabidi ufunge safari hadi China na kutafuta duka, gharama unazookoa ni kubwa sana, hivyo dalali anazalisha huduma muhimu sana!

2.) Machinga anatoa bidhaa kwa gharama ndogo sababu hana fremu, hivyo ni muhimu kwa taifa. Ila mchakato ufanyike walipe kodi.

3.) Bodaboda ni muhimu sana, mfano delivery ya vifurushi bya DHL na vyakula kama Pizza kwa uharaka!
 
Nchi ya Tanzania watu wanachapa kazi sana na watu wavivu au wenyewe wanajiita wasio na kazi wako pia.

Turudi kwenye mada.

Serikali inawaza nini juu ya kazi ambazo hazina tija kwa taifa, hazichangii pato la taifa?

Kazi ambazo zinampa ugali mfanyaji na familia yake basi.

Taifa litasonga vipi mbele ikiwa wananchi wako busy kufanya kazi zisizo na mchango kwenye pato la taifa?

• Kazi ya udalali
Hapa nchini haina mchango kwenye kukuza pato la taifa. Madalali hawalipi Kodi. Hakuna wanachozalisha.
Ni muda sasa madalali wasajiliwe na kulipishwa kodi. Ni aibu nchi kubwa kama hii kusaidiwa na kinchi kidogo kama Uswizi. Dawa ni kupanua wigo wa mlipa Kodi.

• Kazi za umachinga
Licha ya kazi hii kuwa ndiye mwajiri mkubwa hapa nchini lakini haina faida kwa Taifa. Machinga wengi au wote hawalipi Kodi licha ya kuwa wapo machinga mauzo yao kwa siku moja kufikia mpaka milioni 5. Pili machinga wengi huuza bidhaa za kichina hivyo machinga ni watumishi wa nchi ya uchina wanaofanya kazi nje ya China. Wanakuza uchumi wa nchi za watu .

• Kazi ya bodaboda
Serikali imeshindwa hata kugawa leseni za kuendeshea bodaboda angalau kwa sh. 50000. Kazi ya bodaboda haina manufaa kabisa kwa hii serikali. Bodaboda ni kama kitengo cha ukusanyaji mapato binafsi ya polisi na mgambo. Wapo watu watasema bodaboda ananunua mafuta serikali inapata kodi, lakini wanashindwa kufikiri zaidi ya hapo. Kwanza bodaboda zinajenga uchumi wa India na China maana wao ndio wanaozizalisha na kuzi export maelfu kwa maelfu kila siku kuja kuvunja migongo ya vijana wa Dunia ya 3.
Labda kuziboresha na si kuzifuta.
Watu tunaishi kwenye social SYSTEM ambayo ina mambo ya kila aina. Provided kitu siyo crime, ukiamua ukiondoe kwa kudhani kuwa hakifai, unaweza ukajikuta ume-destabilize system nzima hadi kwenye mambo yale ambayo unayaona ni ya maana. Elimination ya jambo ambalo lipo kwenye social system limeshaota mizizi na ambalo siyo CRIME, is very dangerous; as dangerous as killing a person
However, improvement is always a key to improvement and success as well
 
Makampuni mengi makubwa yanakwepa kodi why ulaumu bodaboda na madalali. Kuna kampuni inajihusisha na usafirishaji Ina maroli kibao nliwahi fanya kazi pale. Wana katabia ka ku duplicate karatasi za tra. Unakuta gari imepiga trip 3 kwa siku let's us say dar pwani but anatumia list hiyo hiyo moja kwa maroli more than one 100 kila moja trip 2 wameduplicate ni hasara kiasi gani. Na makampuni ni mengi. My fend Mambo mengine acha yapite tu ukiyafatilia sna utaumia bichwa lako tu
 
Back
Top Bottom