ankol
JF-Expert Member
- Aug 21, 2012
- 2,113
- 3,484
Salaam wadau.
Leo ningependa kuelezea jinsi gani uchumi wa nchi unavyo/takavyoathiriwa na biashara ya bodaboda.
Biashara hii inayokua kwa kasi kila uchao imekua ni kimbilio la vijana wengi wanaotafuta maisha hasa kutokana na ukweli kua ni biashara rahisi isiyohitaji mtaji na nguvu kazi kubwa kuifanya.
Yaani ukiweza tu kuendesha you are good to go.
Biashara hii ina impact ya moja kwa moja na uchumi wa nchi kwani inawashirikisha vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa. Wanashindwa kufanya ubunifu na kuliingizia taifa kipato badala yake wamekua wakingangania vijiweni kutokana na uwingi wao wamekua wakigombaniana abiria wachache na kuambulia kichache na kuridhika na maisha.
Kiuhalisia vijana hawa wanashindwa kuwa productive kwa taifa na badala yake ni suala la muda tu athari zake zitakuja jitokeza.
Nashauri serikali i-control biashara hii ya bodaboda kwa kuweka kodi kubwa kwa wafanya biashara hizo ili kunusuru vijana wengi kukimbilia huko kabla hali haijawa mbaya.