Kuna aina mpya ya kutengwa kwa njia ya kidijitali kwenye magroup, ni kitu nilichogundua kinawumiza wengi

Kuna aina mpya ya kutengwa kwa njia ya kidijitali kwenye magroup, ni kitu nilichogundua kinawumiza wengi

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,447
Kuna hali ambayo imeanza kuonekana ya kawaida, lakini ndani yake kuna maumivu ya kimya. Mnajuana mitaani, mnacheka pamoja, mnafanya biashara au kazi sehemu moja, mnaabudu pamoja kanisani au msikitini, au hata ni ndugu, jamaa na marafiki halafu kuna “group” linaanzishwa, lakini wewe huingizwi.

Hii siyo tu kusahaulika. Mara nyingi ni aina ya kutengwa kimakusudi kimya kimya, bila kelele, lakini chenye athari kubwa kisaikolojia. Unajikuta uko karibu na watu, lakini haupo “ndani” yao. Unaona mawasiliano yanaendelea, maamuzi yanafanyika, mipango inapangwa, lakini wewe uko nje ya mzunguko.

Hii ni aina mpya ya bullying ya kidijitali. Sio maneno makali wala ugomvi wa wazi, bali ni kunyimwa nafasi ya kuwa sehemu ya kundi. Na kwa akili ya binadamu, kutengwa huku hugusa moja kwa moja hitaji la msingi la kuhusika (belonging). Unaanza kujiuliza: Kuna nini kwangu? Kwa nini sihusishwi?

Katika baadhi ya nchi hasa Marekani kwenye shule, hii tayari inatambulika kama bullying, kuwaacha wanafunzi nje ya magroup ya darasa au kozi fulani, kuwaonea kisaikolojia bila kuwapiga.
 
Wala hamna noma as long as huko kunitenga kwao hakuniondolei madusko yangu mfukoni wala kupunguza salio kwenye akaunti zangu za benki.!!!

Mbona freshi.
 
Back
Top Bottom