Swali kwa vigogo wa AMECEA: Jinsi ni kitu gani, sio kitu gani na nani mwenye mamlaka ya kusanifu fasili ya kitu hicho?

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
KUELEKEA UKOLONUZI NA USTAARABISHAJI WA KICHWA CHA MWAFRIKA: JINSI NI KITU GANI, SIO KITU GANI NA NANI MWENYE MAMLAKA YA KUSANIFU FASILI YA KITU HICHO?

bipotential gonads.png

Mchoro wenye kuonyesha gonadi za kiume, gonadi za kike na chimbuko lake--yaani gonadi zisizofungamana na jinsi yoyote.

UTANGULIZI

Mhariri wa gazeti la Kiongozi, linalomilikiwa na Kanisa Katoliki la Tanzania, ambalo ni mwanachama wa AMECEA, amepokea na kutumia makala ya mwandishi aliyemtambulisha kama Raphael Kamuli.

Nimeambiwa na msiri wangu kuwa Kamuli ni kigogo katika Shirika la Pro-life Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

Makala ya Kamuli ina kichwa cha maneno “Wajibu wa kisheria na kijamii kulingana na jinsi” na inapatikana kwenye jukwaa hili la JamiiForums.

Makala hiyo imechapishwa katika gazeti la Kiongozi, toleo Na. 32, la tarehe 09-15 Agosti 2019, kwenye ukurasa wa 12 (ISSN 0856-2563).

Dhamira kuu ya mwandishi ni kutetea hoja yenye pointi saba zifuatazo:


  1. Kwamba, “[viungo vya] jinsi ni alama [asilia] yenye kuonesha tofauti kati ya mwanamke na mwanamume na ni kitu cha kudumu” milele;
  2. kwamba, tofauti zinazojionyesha katika maumbile ya “[viungo vya] jinsi” ni chimbuko la tofauti katika majukumu ya kijinsia;
  3. kwamba, “wajibu wa msingi kwa binadamu kulingana na viungo vya [jinsi] ni kuzaliana,” kulea watoto na kuendeleza ukoo wa mababu na mabibi; na
  4. kwamba, “jinsia ni wajibu wa kijamii wa binadamu kulingana na [tofauti zinazojionyesha katika viungo vya] jinsi,”
  5. kwamba, kila tukio la mapenzi ya jinsi moja linapaswa kuhesabiwa kuwa haramu kimaadili na kisheria kwa kuwa ni tendo lililo "kinyume cha utaratibu na mpangilio wa maumbile" ya kijinsi,
  6. kwamba, "haki batili ya kuchagua mwelekeo wa kimapenzi imebeba mtazamo wa [tabia za] kimagharibu."
  7. Na kwamba, kwa hiyo, "ni sahihi kwa sheria za Tanzania kuharamisha mwelekeo wa kimapenzi ambao unahusisha mapenzi ya jinsi moja."
Naandika kukosoa hitimisho lililofikiwa na mwandishi wa makala na kuungwa mkono na mhariri wa gazeti la Kiongozi.

Nakusudia kuonyesha kwamba, sio kila mapenzi ya jinsi moja yanapaswa kuwa haramu kimaadili na kisheria, na kwamba sio kila ndoa ya jinsi moja inapaswa kuwa haramu kimaadili na kisheria.

Nionavyo mimi, msingi wa makosa ya mhariri na mwandishi ni kushindwa kwao kutambua na kukubali ukweli ufuatao:

  1. Kwamba, kuna jinsi tatu, yaani wanaume, wanawake na mahunta, kwa maana ya jinsi ya kiume, jinsi ya kike na jinsi ya kihunta.
  2. Kwamba, kuna mapenzi ya watu wawili wenye jinsi tofauti na mapenzi ya watu wawili wenye jinsi moja;
  3. Kwamba, hadi sasa hakuna nchi hapa duniani inayounga mkono mapenzi ya jinsi moja kati ya wanaume wawili au wanawake wawili.
  4. Kwamba, mpaka sasa, mijadala yote duniani inayoongelea "mapenzi ya jinsi moja" na "ndoa za jinsi moja" ni mijadala inayohusu "jinsi moja ya kihunta," na sio juu ya "jinsi moja ya kiume" wala juu ya "jinsi moja ya kike."
  5. Kwamba, kuna mapenzi ya jinsi moja ya aina tatu, yaani: mapenzi kati ya wanaume wawili, wanawake wawili na mahunta wawili.
  6. Kwamba, "mwelekeo wa kimapenzi" sio kitu kinachoweza kuchaguliwa kama ambavyo mtu anaweza kuchagua kula embe na kubagua kula chungwa.
  7. Kwamba, "mwelekeo wa kimapenzi" ni sifa ya kimaumbile ambayo ni sehemu ya ujinsi wa mtu.
  8. Kwamba, chimbuko la "mwelekeo wa kimapenzi" ni ninasaba, homoni ndani ya mwili wa mimba, homoni katika mwili wa mwanamke mjamzito (yaani mazingira ya ndani ya tumbo la uzazi) na malezi ya mtoto mara tu baada ya kuzaliwa (yaani mazingira nje ya tumbo la uzazi).
  9. Na kwamba, kwa hiyo, misahafu ya kidini yenye asili yake huko Magharibi na Mashariki inaposema kuwa hapo mwanzo Mungu aliwaumba mwanamke na mwanamuke pekee (Mwanzo 2:24 & Mathayo 19:4) haisemi ukweli wote unaojulikana leo kulingana na misahafu ya kisayansi.
Katika aya zifutazo nitaonyesha ukweli huu katika upeo usioacha shaka la kimaarifa.

UFAFANUZI KUHUSU UREFU NA UPANA WA TATIZO

Mwandishi wa makala inayojadiliwa hapa pamoja na mhariri wa gazeti la Kiongozi hawako peke yao. Kuna vigogo wengi wa Kanisa na kiserikali, ndani na nje ya Tanzania, wenye mawazo kama yao kwa zaidi ya karne kadhaa sasa. Nitatumia mifano michache.

Kwa hapa Tanzania, makala ya mwandishi Florence Majani, wa gazeti la Mwananchi, “Nyanda Mtanzania mwenye utata wa jinsi,” kama ilivyochapishwa katika toleo la 28 Machi 2017, ni ushahidi mmojawapo. Jamii imemnyanyapaa Sana Nyanda.

Ushahidi mwingine wa hapa kwetu ni ule wa mtoto mwenye jinsi mbili aliyeripotiwa kupitia gazeti la HabariLeo, toleo la Desemba 2017. Pale hospitali ya Muhimbili alifanyiwa uchunguzi na upasuaji ili ageuzwe mwanamke au mwanamime na sio vinginevyo.

Pia, mwaka 2010, huko Shinyanga, kuliripotiwa mfungwa aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela. Huyu “aliwachanganya” maafisa gereza baada ya kukutwa ana jinsi zote mbili. Gereza hilo halikuwa na utaratibu wa kuwahudumia wafungwa wa aina hiyo.

Na hivi karibuni kauli ya Padre Dr. Charles Kitima inahusika. Majuzi, pale Rais Magufuli alipowakaribisha viongozi wa dini Ikulu, Padre kitima alisikia akisema yafuatayo: kwamba "sisi viongozi wa dini zote tunaunga mkono fundisho la ndoa ya mwanamke na mwanamume na kupinga ndoa ambazo sio za mwanamke na mwanamume."

Kwa mujibu wa kauli hii, ni wazi kuwa Baraza la Maaskofu Katoliki la Tanzania (TEC) na washirika wao hawatambui uwepo wa jinsi ya kihunta.


Tatizo la aina hii haliko Tanzania pekee. Huko Afrika Kusini kuna mtu aitwaye Padre Sally Gross, mwenye kisa cha kusisimua.

Padre Sally alizaliwa Afrika Kusini mwaka 1953, akatambuliwa na wazazi kama mtoto wa kiume, na kubatizwa kama mkatoliki mwaka 1976. Alihamia Botwana, Israeli, na hatimaye kutulia Uingereza mwaka 1981 alipojiunga na masomo ya kipadre kwenye shirika la Mapadre Wadominikani.

Alipadirishwa mwaka 1987, akapata shahada ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Oxford na kupata nafasi ya kufundisha chuoni hapo.

Katika maisha yake yote hayo alikuwa anajua fika utata wa jenitalia zake. Hivyo, mwaka 1990 akaamua kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu. Hatimaye, mwakia 1993 akiwa na umri wa miaka 40, ndipo akaambiwa na madaktari kwamba yeye, sio mwanamke wala mwanaume, bali ni “hunta” au “huntha,” yaani “intersexual.”

Hunta ni neno la Kiswahili linalomaanisha mtu ambaye sio mwanaume kamili wala mwanamke kamili. Huyu ni mtu mwenye mseto wa baadhi ya sifa za kike na baadhi ya sifa za kiume ama katika ngazi ya seli, ngazi ya gonadi, ngazi ya jenitalia, au ngazi ya homoni, au katika ngazi zote hizi. Hunta ni mtu mwenye jinsi mseto, yaani jike-dume.

Kwa sababu hizi, Padre Sally Gross alishauriwa kufanyiwa upasuaji wa plastiki kusudi awekewe jenitalia za kiume. Lakini alikataa kwa hoja kwamba hicho kitakuwa sio kitendo adilifu.

Hatimaye, Padre Sally Gross alipatiwa paspoti na cheti cha kuzaliwa chenye jina la kike, kwa hoja kwamba, wakati alipozaliwa wauguzi walikosea kuandika jinsi yake. Akachagua jina jipa ya la Sally Gross (jina jipya la kike) badala ya Selwyn Gross (jina la zamani la kiume).

Na mwaka 1994 Padre Sally Gross ulivuliwa upadre kwa sababu ya hoja kwamba, wanawake kama yeye hawana haki ya kuwa mapadre ndani ya Kanisa Katoliki.

Akafukuzwa kutoka kwenye boma la mapadre. ‘Padre’ Sally Gross sasa akaamua kuhamia tena Afrika ya Kusini alikozaliwa, na kuanza maisha mapya. Alifariki mwaka 2014 nchini Afrika ya Kusini.

Kabla ya kifo chake, Padre Sally Gross tayari alikuwa ameandika sana kuhusu misukosuko aliyoipata. Aliambiwa na makuhani wenzake kwamba, kwa vile Mwanzo 1:27 inasema kwamba Mungu aliumba mwanaume na mwanamke pekee, sifa muhimu ya kuitwa binadamu ni ama kuwa mwanamke au mwanaume, lakini sio vinginevyo.

Kwa hiyo, Padre Sally Gross akaelezwa kwamba, kwa mujibu wa kigezo hicho, yeye hakuwa binadamu. Na akaambiwa kwamba, kwa kuwa ubatizo unawahusu binadamu, basi hata ubatizo wake ulikuwa batili, kwa kuwa yeye sio binadamu. Akafutiwa ubatizo na kuzuiwa kukomunika kwa sababu hiyo. (Sally Gross, “Intersexuality and Scripture”, Theology and Sexuality 11 (1999) 65-74).

Misukosuko yote hii ilimkumba Padre Sally Gross katika kipindi cha utawala wa Papa Yohanne Paulo II (1978-2005). Miongoni mwa urithi tulioachiwa na Papa Paulo II ni kitabu chake kinachoongelea ujinsi wote wa binadamu kwa kutumia misamiati inayotambua uwepo wa jinsi ya kiume na jinsi ya kike pekee, bila kuacha mwanya wa kuwepo kwa kitu kingine chochote katikati ya pande hizi mbili.

Kitabu hicho kinaitwa: “Man and Woman He Created Them: A Theology of the Body (Boston: Pauline Books & Media, 2006).” Pamoja na umahiri na uzoefu wake wa kiteolojia, kifalsafa, kichungaji, na kitafiti, ni yule Papa Yohanne Paulo II aliyetangazwa mtakatifu hivi karibuni, ambaye alifuta upadre wa Padre Sally Gross mwaka 1994.

Kwa ufupi, historia ya Padre Sally Gross inaonyesha vizuri changamoto za unyanyasaji wa kijinsi unaowakumba mahunta—watu wenye jinsi mbili—sehemu mbalimbali duniani na Tanzania ikiwemo.

Kwa haya machache, inatosha kusema kuwa kwa miaka 400 sasa, sayansi imekuwa ikifanya kazi kama kimiminika ambacho kinayeyusha punje za mawazo ya kishirikina na kiteolojia yanayopingana na uhalisia wa mambo.

Hata hivyo, bado mawazo ya kishirikina na kiteolojia yasiyokubaliana na uhalisia wa mambo yanabebwa na viongozi wa kijamii weny e dhamana kubwa. Kwa nini? Kwa kuwa wao ni wengi, wana jukwaa kubwa la usikivu, na hivyo kanuni tata isemayo kwamba "kisemwacho mara nyingi na watu wengi ni ukweli" inachukua nafasi yake.

Lakini, kimantiki tunasema "plausibility does not always imply validity."

Yaani, "kuungwa mkono na watu wengi sio kigezo cha ukweli mara zote." Hivyo basi, kwa vile sasa tunaujua ukweli wa kisayansi kuhusu ujinsi wa binadamu, hatuwezi kunyamaza.

MASWALI MAKUU YA KITAFITI

Kwa hiyo kuna haja ya kutafiti na kujibu kwa dhati kabisa maswali kadhaa ili kuweka msingi wa kufuta ulaghai uliofanywa kupitia gazeti la Kiongozi, pamoja na machapisho mengine ya kidini. Maswali hayo ni haya hapa:

  1. Jinsi ni kitu gani?
  2. Jinsi sio kitu gani?
  3. Jinsi ni neno linalorejea kategoria asilia au kategoria ya kitamaduni?
  4. Kama neno “jinsi” linarejea kategoria ya kitamaduni nani mwenye mamlaka ya kusanifu fasili hiyo?
  5. Kama neno “jinsi” linarejea kategoria asilia tafiti za kisayansi zinasema ni kitu gani?
  6. Ni kwa vipi mtoto huzaliwa na jinsi ya kike, jinsi ya kiume au jinsi ya kihunta?
  7. Chimbuko la mwelekeo wa kimapenzi kama vile uandrofilia, ugainefilia na uambifilia ni kitu gani?
  8. Na je, mitaala yetu ya masomo ya bayolojia na uraia inawapa maarifa gani wanafunzi wetu kuhusu jinsi ya binadamu?

MBINU YA UTAFITI

Natumia mbinu ya kupitia fasihi andishi zenye kumbukumbu za utafiti wa kisayansi juu ya chimbuko la jinsi za binadamu na idadi yake. Pia narejea visa vya watu wenye jinsi tata akiwemo padre aliyekuwa na jinsi mbili ili kuonyesha misukosuko inayowakabili watu wa aina yake.

MFUMO WA NADHARIA ELEKEZI

Misamiati iliyotumika mapaka hapa inaashiria wazi kuwa kuna nadharia kadhaa ambazo lazima zitumike kutoa mwanga sahiki wa kimaarifa katika utafiti huu.

Nadharia ya kwanza elekezi ni "embryological theory" yenye kueleza jinsi mtoto anavyoanza tumboni mwa mama yake, kukua, na mpaka akazaliwa.

Nadharia ya pili elekezi ni "genetic theory" ambayo inaeleza ni kwa namna gani watoto huzaliwa wakiwa wanafanana na wazazi wao wa kike, kiume au wote wawili.

Tafiti za kijenetiki, kama zilivyofanywa na Padre GREGOR MENDEL (1822-1884) zilizohitimishwa mwaka 1865. Huyu ni mwanasayansi aliyefanikiwa kuwachochea wanasayansi mpaka wakagundua namna urithi wa kibayolojia kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto unavyofanyika.

Sasa tunafahamu kwamba, urithi huo hufanyika kupitia kemikali inayobeba taarifa za kinasaba zikiwa zimetunzwa katika vidonge vidogo vidoogo viitwavyo DNA (deoxybo-nucleic-acid). Vidonge kadhaa vya DNA vinapounganika hutengeneza pingili iitwazo jeni. Na jeni kadhaa zinapounganika hutengeneza kromozomu.

Tangu mwaka 1956 wanasayansi wamethibitisha kwamba kila seli ya binadamu inazo kromozomu 46 zilizopangiliwa katika jozi 23. Kati yake, jozi moja (1) ikiwa imebeba kromozomu zinazoratibu michakato ya kijinsia mwilini, wakati jozi baki 22 zikiwa zimebeba kromozomu zinaongoza michakato mingine inayoendelea katika mwili wa binadamu.

Kupitia utafiti wake, mendel alibainisha kanuni kubwa mbili za urithi wa kibayolojia kati ya wazazi na watoto. Kanuni hizi zinaongelea mduara wa kuzaliana kwa njia ya ngono (sexual reproduction cycle). Kwa mujibu wa Mendel, kanuni moja inaitwa “law of segregation,” wakati kanuni ya pili inaitwa “law of independent assortment.

Kwa ufupi, kanuni hizi inasema mambo makuu yafuatayo: Mosi, zinasema kwamba, kila sifa inayorithiwa na mtoto kutoka kwa wazazi wake inahusisha jozi moja ya jeni.

Pili, zinasema kwamba, kwa ajili ya maandalizi ya kuzaliana, jeni zilizo katika jozi hiyo, huachana na kutengeneza gameti mbili za uzazi kupitia mchakato unaoitwa meyosisi, ambapo jeni za kike huingia katika yai na jeni za kiume huingia katika spermatozoa.

Tatu, zinasema kwamba, kufuatia tendo la ngono linalofanyika kwa kuunganisha jenitalia ya kiume na jenitalia ya kike, gameti hizi huweza kuungana wakati wa urutubisho wa yai kwa msaada wa spematozoa.

Na nne, kanuni hizi zinasema kwamba, kwa sababu hii, kila sifa inayorithiwa na mtoto kutoka kwa wazazi inahusisha jozi moja ya jeni, jeni ya kwanza ikiwa imetoka kwa baba na jeni ya pili ikiwa imetoka kwa mama yake.

Taarifa ya utafiti wa Mendel ilikuwa na jina, “Experiments in Plant Hybridisation (1865),” na ilichapishwa katika majarida wa wakati huo kwa kutumia lugha ya kwao.

Aidha, huu ni utafiti juu ya mahusiano yaliyopo kati ya vianzilishi na vitokelezi, mahusiano yaliyopo kati ya sababu na matokeo, au mahusiano yaliyopo kati ya chanzo na hatma, ambapo matokeo ni "jinsi" na chanzo chake ndio kinatafutwa. Kwa hiyo kunahitajika nadharia ya kifalsafa inayoongelea utokanishaji (etiology).

Kuna nadharia kuu tano za aina hiyo. Yaani,
Regularity theory of causation, Probability theory of causation, Counterfactual theory of causation, Process theory of causation, na Intervention theory of causation.

Kwa ajili ya mapitio haya, "Probability theory of causation" itatumika kuchambua matokeo ya tafiti mbalimbali zilizomo katika misahafu ya kisayansi.

Kwa mujibu wa metafizikia ya sababu na matokeo (metaphysics of causality au etiology) kwa mtazamo wa mahesabu ya yamkini (probability), kama yalivyojadiliwa na Hume (1975), Eells (1991) na Gallow (2017) kanuni za kietiolojia zifuatazo zahusika:

Kwamba:


"Given a causally positive background K, an event C is a cause of an event E, if and only if: the probability of E given the occurrence of C is greater than the probability of E given the non-occurrence of C [P(E/C)>P(E/C')], meaning that, P(E/C)-P(E/C')>0."

MATOKEO YA UTAFITI

Kwa kutumia ugunduzi wa Padre Mendel, mpaka miaka ya 1990 tayari wafuasi wa Mendel, walikuwa wamethibitisha kwamba, kazi ya kusimikwa na kuhuishwa kwa jinsi ya mtoto aliye tumboni (sex determination and differentiation) hufanywa na vinasaba hivi ndani ya wiki saba za kwanza tangu siku ya kutungwa kwa mimba. Kwa mujibu wa utafiti wao, mchakato huu unapitia katika hatua kuu tano.

Hatua ya kwanza ni kusimika jinsi ya mtoto katika ngazi ya seli (chromosome sex/genetic sex) kwa kuhakikisha kwamba, baada ya tendo la ngono, mchakato wa urutubishaji unazalisha, ama mimba yenye kromozomu 46 zenye fomati ya ‘XX’ (46XX), au mimba yenye kromozomu 46 zenye fomati ya XY (46XY).

Mimba yenye kromozomu 46 zenye fomati ya ‘XX’ ni mimba yenye muudo wa jenetiki unaoonyesha jinsi ya kike (46XX KE).

Na mimba yenye kromozomu 46 zenye fomati ya ‘XY’ ni mimba yenye muudo wa jenetiki unaoonyesha jinsi ya kiume (46XY ME).

Katika hatua hii ya kwanza, kimimba kinakuwa na mfumo wa uzazi wenye sehemu tatu zifuatazo: gonadi mbili zisiofungamana na jinsi yoyote, au tuseme gonadi mtambuka (bipotential ginads); mifereji ya muleria na mifereji ya wolfi (mellerian ducts, wolfian ducts), kama picha inavyoonyesha hapo juu. Kulingana na mazingira ya wakati husika, gonadi mtambuka na mifereji yake huweza kugeuka jenitalia za kiume au jenitalia za kike, kama tutakavyoona punde.
Hatua ya pili, hujitokeza katika wiki ya saba ya mimba, na inahusu kusimikwa kwa jinsi ya mtoto katika ngazi ya gonadi (gonadal sex). Katika hatua hii, gonadi mtambuka mbili (bipotential ginads), ama hugeuka ovari au hugeuka korodani.

Gonadi mtambuka zikigeuka ovari, inapatikana mimba ya mtoto mwanamke. Na gonadi mtambuka zikigeuka korodani, inapatikana mimba ya mtoto mwanamume. Mambo haya hutokea katika mimba yenye umri wa siku hamsini au zaidi.

Hatua hii husimamiwa na jeni kadhaa. Lakini, jeni muhimu kwa leo ni ile ambayo hapa itapewa jina la “jeni inayotofautisha jinsi” (sex determining region Y gene—SRY gene). Kwa ufupi, “jeni inayotofautisha jinsi” ni pingili inayopatikana katika ncha mojawapo ya kromozomu ya Y, ambayo ni kromozomu ya kiume.

Na kama jina lake linavyoonyesha, “jeni inayotofautisha jinsi” inayo kazi kubwa moja: kuzalisha kemikali inayobadilisha gonadi mtambuka mbili (bipotential gonads) na kuzigeuza korodani . Kemikali hiyo, kwa hapa itaitwa “protini inayootesha korodani” (testicle determining factor—TDF).

Kupatikana kwa vitu hivi viwili katika kromozomu ya Y, huzilazimisha gonadi mtambuka mbili (bipotential gonads) zilizo katika mimba iliyo na mfumo wa jenetiki wenye fomati ya ‘XY’ kugeuka korodani , na hivyo, kupatikana kwa mimba ya kiume. Hili ni tukio katika wiki ya saba ya uhai wa mimba.

Na kwa upande mwingine, “jeni inayotofautisha jinsi” na “protini inayootesha korodani” havipatikani katika kromozomu ya X, ambayo ni kromozomu ya kike. Kukosekana kwa vitu hivi viwili katika kromozomu ya X, huziruhusu gonadi mtambuka mbili (bipotential gonads) zilizo katika mimba iliyo na mfumo wa jenetiki wenye fomati ya ‘XX’ kugeuka ovari, na hivyo, kupatikana kwa mimba ya kike. Tusisahau kuwa, hili ni tukio katika wiki ya saba ya uhai wa mimba.

Hivyo, mtoto akizaliwa ni mwanaume kamili anakuwa na mfumo wa jenetiki wenye fomati ya ‘XY’ ulioambatana na “uchanya” katika “jeni inayotofautisha jinsi.” Yaani, anakuwa na jinsi ya kijenetiki yenye fomati ya “46XY ME, SRY+.

Kwa upande mwingine, mtoto akizaliwa ni mwanamke kamili anakuwa na mfumo wa jenetiki wenye fomati ya ‘XX’ ulioambatana na ukosefu wa “jeni inayotofautisha jinsi.” Yaani, anakuwa na jinsi ya kijenetiki yenye fomati ya “46XX KE, SRY-.

Hatua ya tatu ni kudhihirisha jinsi ya mimba katika ngazi ya jenitalia na viungo kadhaa vya mwili, na hivyo kumpa mofolojia/mwonekano maalum (genital sex/phenotypic sex). Hatua hii husimamiwa na homoni za kiume kama vile testosterone zinazozalishwa kwenye korodani ya mimba na homoni za kike kama vile estrojeni zinazozalishwa kwenye ovari ya mimba.

Kwa upande wa jenitalia, kuna jenitalia za nje na jenitalia za ndani. Na kwa upandne wa mimba ya kike hutokea jenitalia za nje zifuatazo: uke wa nje (vulva) wenye masikio mawili makubwa, masikio mawili madogo, kisimi, mlango wa uzazi na mlango wa mkojo. Aidha, mwanamke hupata jenitalia za ndani zifuatazo: vagina, uterasi, mifereji miwili ya falopia na ovari.

Kwa upande wa mimba ya kiume, hutokea jenitalia za nje zifuatazo: uume na korodani mbili zilizoshuka kwenye mifuko yake. Aidha, mwanaume hupata jenitalia za ndani zifuatazo: tezi dume, epididimisi, seminovesko, na vasidiferensi.

Hatua ya nne ni kudhihirisha jinsi ya mtoto mkubwa katika ngazi ya jenitalia na viungo kadhaa vya mwili, na hivyo kumpa mofolojia/mwonekano maalum (genital sex/phenotypic sex) katika umri wa kubalehe. Aidha, hatua hii husimamiwa na homoni za kiume kama vile testosterone zinazozalishwa kwenye korodani ya mimba na homoni za kike kama vile estrojeni zinazozalishwa kwenye ovari ya mtoto.

Kwa kawaida, hatua ya kwanza, ya pili, na tatu hapo juu, huzalisha sifa za kijinsi za awamu ya kwanza (primary sex characteristics). Hizi ni sifa za kijinsi ambazo mtoto huzaliwa nazo baada ya kukaa tumboni mwa mama yake kwa miezi tisa.

Baada ya mtoto kuzaliwa, kukua na kufikia umri wa kubalehe hupata sifa mpya za kijinsi, ziitwazo sifa za kijinsi za awamu ya pili (secondary sex characteristics). Hizi pia hubadili mofolojia/mwonekano ya mtoto.

Kwa mvulana, sifa hizi ni pamoja na kuota ndevu, kupata sauti nzito, kuota kikoromeo, kupanuka kifua, na kukakamaa ngozi na misuli. Na kwa msichana, sifa hizi ni pamoja na kuota matiti, kupata sauti nyembamba, kupanuka nyonga, na kulainika ngozi na misuli.

Na hatua ya tano inahusu jinsi ya mtu katika ngazi ya kisaikolojia (psychological sex/brain sex). Hapa tunajiuliza mtu anasema yaye ni mwanamke au mwanaume. Katika hatua hii, hisia alizo nazo mtu ubongoni zinategemea jinsi yake katika ngazi ya jenetiki, gonadi, na mwonekano.

Kwa ujumla, jinsi ya mtu katika ngazi ya jenetiki inasukuma jinsi yake katika ngazi ya gonadi, jinsi ya mtu katika ngazi ya gonadi inasukuma jinsi yake katika ngazi ya mofolojia yenye msingi wake katika homoni, na jinsi ya mtu katika ngazi ya mofolojia inasukuma jinsi yake katika ngazi ya kisaikolojia.

Kwa ufafanuzi zaidi wa hatua hizi, tazama kitabu cha Friedrich Vogel na Arno G. Motulsky, kiitwacho, “Human Genetics: Problems and Approaches 3rd Ed. (Berlin/ Heidelberg: Springer-Verlag, 1996).”

Na sasa tuongee kidogo kuhusu chimbuko la watu wenye jinsi mbili. Mpaka sasa tumejadili ukuaji wa kijinsi bila kugusia changamoto za jinsi tata (Disorders of Sexual Development—DSD). Mfano mzuri hapa ni watu wenye jinsi mbili, ambao ndio mada kuu ya mjadala wetu.

Hapo awali tuliona kwamba, mtoto akizaliwa ni mwanaume kamili anakuwa na mfumo wa jenetiki wenye fomati ya ‘XY’ ulioambatana na uwepo wa “jeni inayotofautisha jinsi.” Yaani, anakuwa na jinsi ya kijenetiki yenye fomati ya “46XY ME, SRY+.

Kwa upande mwingine, tulsema kuwa, kama mtoto akizaliwa ni mwanamke kamili anakuwa na mfumo wa jenetiki wenye fomati ya ‘XX’ ulioambatana na ukosefu wa “jeni inayotofautisha jinsi.” Yaani, anakuwa na jinsi ya kijenetiki yenye fomati ya “46XX KE, SRY-.

Lakini kwa bahati mbaya, ikitokea kwamba, mimba yenye mfumo wa jenetiki wenye fomati ya ‘XY’ ikaambatana na kromozomu ya Y iliyomeguka kwa kiwango cha kupoteza kipande cha “jeni inayotofautisha jinsi,” madhara makubwa ya kijenetiki hutokea kwa mimba.

Kwanza, mimba hii haitapata “protini inayootesha korodani” ili mtoto aweze kuzaliwa wa kiume.

Badala yake, pamoja na kwamba mimba inao mfumo wa jenetiki wenye fomati ya ‘XY,’ ambayo ni fomati ya kiume katika ngazi ya kromozomu, mimba hii itaotesha ovari kana kwamba mimba hiyo inao mfumo wa jenetiki wenye fomati ya ‘XX,’ ambayo ni fomati ya kike.

Hatimaye, atazaliwa mtoto mwenye jinsi ya kiume katika ngazi ya seli, wakati anayo jinsi ya kike katika ngazi ya gonadi.

Atakuwa ni "mlemavu" wa kijinsia mwenye mfumo wa jenetiki ulio na fomati ya “46XY KE, SRY-.

Ovari zake zitazalisha homoni za kike, na atakuwa na mofolojia ya kike, wakati ndani anazo seli zenye fomati ya kiume (genotypitical male, phenotypical female).

Mabadiliko haya yanaitwa mapinduzi ya kijinsi kutoka uanaume kwenda uanauke (male-to-female sex reversal).

Hivi ndivyo, mwanamume mwenye sura ya kike, kama vile Caster Semenya, mwanariadha wa Afrika Kusini, anavyokuja duniani. Nisitize kwamba, huyu ni binadamu kamili kwa kuwa anazo kromozomu 46 kama zetu, anayo akili na utashi pia.

Kwa bahati mbaya tena, ikitokea kwamba, mimba yenye mfumo wa jenetiki wenye fomati ya ‘XX’ ikaambatana na kromozomu ya X iliyookota kipande cha “jeni inayotofautisha jinsi,” baada ya kuwa kimemeguka na kudondoka kutoka katika kromozomu ya Y, madhara makubwa ya kijenetiki hutokea kwa mimba pia.

Kwanza, mimba hii hupata “protini inayootesha korodani” na kusababisha mtoto kuzaliwa wa kiume.

Kwa sababu hii, pamoja na kwamba mimba inao mfumo wa jenetiki wenye fomati ya ‘XX,’ ambayo ni fomati ya kike katika ngazi ya kromozomu, mimba hii itaotesha korodani kana kwamba mimba hiyo inao mfumo wa jenetiki wenye fomati ya ‘XY,’ ambayo ni fomati ya kiume.

Hatimaye, atazaliwa mtoto mwenye jinsi ya kike katika ngazi ya seli, wakati anayo jinsi ya kiume katika ngazi ya gonadi. Atakuwa ni "mlemavu" wa kijinsia mwenye mfumo wa jenetiki ulio na fomati ya “46XX ME, SRY+.

Korodani zake zitazalisha homoni za kiume, na atakuwa na mofolojia ya kiume, wakati ndani anazo seli zenye fomati ya kike (genotypitical female, phenotypical male).

Mabadiliko haya yanaitwa mapinduzi ya kijinsi kutoka uanauke kwenda uanaume (female-to-male sex reversal).

Kwa mujibu wa sayansi, hivi ndivyo mwanamke mwenye sura ya kiume, anavyoweza kuja duniani.

Kwa ujumla, mahunta wanagawanyika katika makudi makuu manne. Muhtasari ufuatao unaonyesha makundi hayo, kwa kubainisha sifa kuu za kila kundi (tafsiri itafanyika baadaye):

According to the book authored by Robert Crooks and Karlar Baur, entitled “Our Sexuality, 12th edition (Belmonte, USA: Wadsworth; 2014, Table 5.3 on p.121),” there are more than 70 atypical conditions of the sex chromosomes or hermaphroditism. The authors argue that, based on their causes, hermaphrodites can be divided into four main categories, namely:

  • True gonadal hermaphrodites;
  • 46,XX hermaphrodites;
  • 46,XY hermaphrodites;
  • Complex hermaphrodites which involve other disorders of sexual development beyond simple 46,XX and 46,XY, and which may include: 45,XO hermaphrodites, 47,XXY hermaphrodites, and 47,XXX hermaphrodites
A. True Gonadal Hermaphroditism

An individual with true gonadal hermaphroditism has both ovarian and testicular tissue, either in the same gonad (referred to as an ovotestis) or in one ovary and one testis. Some affected individuals have XX chromosomes, others have XY chromosomes, and others have a combination of both. Likewise, the external genitalia can vary in form, from male, or female, to ambiguous.

The cause of this type of hermaphroditism is not clear. Some animal studies have suggested a link to exposure to agricultural pesticides, although this has yet to be established in human studies.

B. Syndrome: Androgen insensitivity syndrome

  • Chromosomal Sex: 46,XY
  • Gonadal Sex: Undescended testes
  • Reproductive Internal Structures: Lacks a normal set of either male or female internal structures
  • External Genitals: Normal female genitals and a shallow vagina
  • Fertility: Sterile
  • Secondary Sex Characteristics: At puberty, breast development and other signs of normal female sexual maturation appear, but menstruation does not occur.
  • Gender Identity: Female
C. Syndrome: Fetally androgenized females
  • Chromosomal Sex: 46,XX
  • Gonadal Sex: Ovaries
  • Reproductive Internal Structures: Normal female
  • External Genitals: ambiguous (typically more male than female)
  • Fertility: Fertile
  • Secondary Sex Characteristics: Normal female (individuals with adrenal malfunction must be treated with cortisone to avoid masculinization).
  • Gender Identity: Usually female, but significant level of dissatisfaction with female gender identity; oriented toward traditional male activities
D. Syndrome: Dihydrotestosterone (DHT) deficient males
  • Chromosomal Sex: 46,XY
  • Gonadal Sex: Undescended testes at birth; testes descend at puberty
  • Reproductive Internal Structures: Vas deferens, seminal vesicles, and ejaculatory ducts but no prostate; partially formed vagina
  • External Genitals: ambiguous at birth (more female than male); at puberty, genitals are masculinized.
  • Fertility: Sterile
  • Secondary Sex Characteristics: Female before puberty; become masculinized at puberty.
  • Gender Identity: Female prior to puberty; majority assume traditional male identity at puberty.
E. Syndrome: Turner’s syndrome
  • Chromosomal Sex: 45,XO
  • Gonadal Sex: Fibrous streaks of ovarian tissue
  • Reproductive Internal Structures: Uterus and fallopian tubes
  • External Genitals: Normal female
  • Fertility: Sterile
  • Secondary Sex Characteristics: Undeveloped; no breasts
  • Gender Identity: Female
F. Syndrome: Klinefelter’s syndrome
  • Chromosomal Sex: 47,XXY
  • Gonadal Sex: Small testes
  • Reproductive Internal Structures: Normal male
  • External Genitals: Undersized penis and testes
  • Fertility: Sterile
  • Secondary Sex Characteristics: Some feminization of secondary sex characteristics; may have breast development and rounded body contours.
  • Gender Identity: Usually male, although higher than usual incidence of gender identity confusion

MAJADILIANO NA HITIMISHO

Majadiliano

Nilianza utafiti huu kwa ajili ya kujibu maswali yafuatayo:

  1. Jinsi ni kitu gani?
  2. Jinsi sio kitu gani?
  3. Jinsi ni neno linalorejea kategoria asilia au kategoria ya kitamaduni?
  4. Kama neno “jinsi” linarejea kategoria ya kitamaduni nani mwenye mamlaka ya kusanifu fasili hiyo?
  5. Kama neno “jinsi” linarejea kategoria asilia tafiti za kisayansi zinasema ni kitu gani?
  6. Ni kwa vipi mtoto huzaliwa na jinsi ya kike, jinsi ya kiume au jinsi ya kihunta?
  7. Na je, chimbuko la mwelekeo wa kimapenzi kama vile uandrofilia, ugainefilia na uambifilia ni kitu gani?
Kutokana na yaliyojadiliwa hapo juu, majibu yafuatayo yanafuata kimantiki kulingana na ushahidi uliowasilishwa:
  1. Jinsi ni neno linalorejea, sio kategoria ya kitamaduni, bali kategoria asilia. Hivyo, kunahitajika mashuhuda zaidi ya mmoja ili kuthibitisha kinachoongelewa.
  2. Kwa kuwa neno “jinsi” linarejea kategoria asilia, basi ni jukumu la mwanasayansi kutwambia "jinsi ni kitu gani na sio kitu gani."
  3. Kwa kuwa neno “jinsi” linarejea kategoria asilia tunapaswa kurejea tafiti za kisayansi ili kuona zinasema jinsi ni kitu gani na sio kitu gani.
  4. Tafiti za kisayansi zinasema kuwa jinsi ni kundi la watu wanaofanana maumbile yanayotambulishwa na parameta/vigezo vikuu vitano, yaani, jenitalia, gonadi, homoni, kromozomu, na saikolojia au tuseme mwelekeo wa kimapenzi
  5. Tafiti za kisayansi zinasema kuwa Jinsi haitambulishwi na jenitalia pekee, au gonadi pekee, au homoni pekee, au kromozomu pekee, mwelekeo wa kimapenzi pekee. Bali inatambulishwa na jenitalia, gonadi, homoni, kromozomu, na mwelekeo wa kimapenzi kwa pamoja.
  6. Mtoto huzaliwa na jinsi ya kike, jinsi ya kiume au jinsi ya kihunta, sio kwa sababu za kishirikina au mapepo, bali kwa sababu za michakato ya kiembriyolojia inayoongozwa na vinasaba, homoni na parameta zingine kadhaa kama ilivyojadiliwa hapo juu.
  7. Kwa asilimia kubwa, chimbuko la mwelekeo wa kimapenzi kama vile uandrofilia, ugainefilia na uambifilia ni vinasaba vilivyo katika mwili wa mtoto au au homoni zilizo katika mwili wa mtoto kabla ya kuzaliwa au homoni zilizo katika mazingira ya mtoto kabla hajazaliwa au vyote kwa pamoja. Lakini, kromozomu zinayo nafasi kubwa zaidi. Mtazamo huu unatokana na udadavuzi wa kimantiki unaoanzia kwenye matokea na kurejea kwenye chanzo (effect to cause argumentation). Ni hivi: Kwa kuwa watu wengi wenye kromozomu za XX wanakuwa na mwelekeo wa kimapenzi wa uandrofilia; kwa kuwa watu wengi wenye kromozomu za XY wanakuwa na mwelekeo wa kimapenzi wa ugainefilia, na kwa kuwa watu wengi wenye mseto wa kromozomu za XY na XX wanakuwa na mwelekeo wa kimapenzi wa uambifilia, basi inafuata kimantiki kwamba, kwa asilimia kubwa, mwelekeo wa kimapenzi ni zao la vinasaba vinavyobebwa na kromozomu fulani mwilini.
Hivyo basi, sasa tunaweza kueleza vizuri dosari zilizomo katika makala ya Kamuli ambayo inajadiliwa hapa.

Kwa ujumla, napendekeza kwamba, hoja ya Raphael Kamuli inazo dosari nyingi za kimuundo, kimaudhui na kisemantiki.

Kwa hapa nataka kujielekeza katika dosari kuu tano zinahusiana na mgongano kati ya taasisi za kijamii zenye jukumu la kujenga imani ya jamii, yaani, taasisi ya sayansi, taasisi ya dini na taasisi ya upashanaji habari.

DOSARI YA KWANZA ni kwamba, makala inafanya ulaghai kwa njia ya kusema ukweli nusu nusu juu ya ujinsi wa binadamu, yaani “deception by omission.”

Ni kama vile mwandishi wa Makala na mhariri wa gazeti la Kiongozi hawana habari yoyote kuhusu chimbuko la jinsi za kibinadamu na kanuni za bayolojia zinazoongoza mchakato wa majilio ya jinsi za watoto tangu siku za kwanza tumboni mwa mama zao.

Naongelea mchakato wa “sex determination and differentiation into males, females and intersexuals.

Kwa mujibu wa maarifa ya sayansi mamboleo, ni wazi kwamba kuna jinsi tatu, na sio mbili kama mwandishi wa makala na mhariri wa gazeti la kiongozi wanavyotaka jamii kuamini.

Jinsi hizo ni jinsi ya kiume, jinsi ya kike na jinsi ya hunta. Hii ya mwisho ni jinsi ya ujike-dume. Kwa ufafanuzi zaidi tazama Kiambatanisho Part A na Kiambatanisho Part B.

DOSARI YA PILI pia inahusiana na ulaghai kwa njia ya kusema ukweli nusu nusu juu ya maelekeo ya kimapenzi.

Kanuni za sayansi ya bayolojia sasa zinatufundisha kuwa, kuna maelekeo ya kimapenzi ya aina nne, yaani:

  1. mwelekeo wa kuvutiwa na mwanamume, yaani uandrofilia (androphilia);
  2. mwelekeo wa kuvutiwa na mwanamke, yaani ugainefilia (gynephilia); na
  3. mwelekeo wa kuvutiwa na wanawake na wanaume, yaani uambifilia (ambiphilia), na
  4. mwelekeo wa kutovutiwa na wanawake wal wanaume, yaani uhanithi (impotence/frigidity).

Hivyo, kwa kuzingatia mwelekeo wa kimapenzi pamoja na viungo vya kijinsi alivyo nazo mhusika, wanadamu wote wanagawanyika katika makundi mengi kama vile:
  1. wanaume androfilia (androphilic males),
  2. wanaume gainefilia (gynephilic males),
  3. wanawake androfilia (androphilic females),
  4. wanawake gainefilia (genyphilic females),
  5. wanaume ambifilia (ambifilic males),
  6. wanawake ambifilia (ambiphilic females),
  7. wanaume mahanithi (impotent males), na
  8. wanawake mahanithi (frigid females).

Mwanamume gainefilia pamoja na mwanamke androfilia wanaitwa watu wenye mwelekeo wa kimapenzi unaomsukumu mhusika kutaka kujamiiana na mwenza wa jinsi tofauti. Unajulikana kama mweleko wa kiheterofilia (heterophilic sexual orientation).

Mwanamume androfilia anaitwa mtu wenye mwelekeo wa kimapenzi unaomsukumu kutaka kujamiiana na mwenza wa jinsi ya kiume. Unajulikana kama mwelekeo wa ushoga (gay sexual orientation).

Mwanamke gainefilia anaitwa mtu wenye mwelekeo wa kimapenzi unaomsukumu kutaka kujamiiana na mwenza wa jinsi ya kike. Unajulikana kama mwelekeo wa usagaji (lesbian sexual orientation).

Kwa pamoja, mwelekeo wa ushoga pamoja na mwelekeo wa usagaji ni maelekeo ya kimapenzi yanayojulikana kwa pamoja kama maeleko ya uhomofilia (homophilic sexual orientations).

Watu wenye viungo vya jinsi ya kiume na viungo vya jinsi ya kike kwa mpigo, yaani mahunta, au “intersexuals” kwa Kiingereza, mara nyingi, huwa na maelekeo ya kuvutiwa na wanawake na wanaume kwa mpigo. Yaani, wanao mwelekeo wa uambifilia (ambiphilic sexual orientation).

Mchchoro ufuatao unafafanua zaidi mausiano kati ya maelekeo ya kimapenzi na jinsi ya mhusika kwa kuzingatia vigezo baki.

Tafiti za kisayansi zinaonyesha kuwa, watu wanaozaliwa na maelekeo ya uhomofilia na uambifilia ni wastani wa asilimia 10 duniani kote.

Kwa hiyo, sio sahihi kusema kwamba, mweleko wa uhomofilia na mwelekeo wa uambifilia sio maelekeo sahihi eti kwa sababu ni maelekeo yaliyo kinyume cha utaratibu na mpangilio wa maumbile ya binadamu wengi.

Lazima kutambua kuwa hapa kuna tofauti katika maumbile ya wanadamu wengi walio na mwelekeo wa uheterofilia na maumbile ya wanadamu wachache walio na ama mwelekeo wa uhomofilia au mwelekeo wa uambifilia.

Kukataa ukweli huu ni sawa na kukataa ukweli kwamba dunia inalizunguka jua.

DOSARI YA TATU ni kwamba, mwandishi na mhariri hawaonekani kuelewa kwamba neno “jinsi,” kama likichukuliwa kama kiwakilishi cha kategoria asilia (natural kind), jambo ambalo mwandishi wa makala na mhariri wa gazeti la Kiongozi wanalikubali, ni neno lenye maana zaidi ya moja. Kuna jinsi zifuatazo:

  1. jinsi ya kijenitalia (phenotypic/genital sex),
  2. jinsi ya kijenetiki (genetic/chromosomal sex),
  3. jinsi ya kihomoni (hormonal sex),
  4. jinsi ya gonadi (gonadal sex), na
  5. jinsi ya kisaikolojia (psychological sex), yaani mwelekeo wa kimapenzi, au "sexual orientation" kwa Kiingereza.

Kwa ufafanuzi zaidi tazama kitabu cha Sharon E. Sytsma, Ethics and Intersex (Netherlands: Springer, 2006).

DOSARI YA NNE ni kwamba, bila uhalali wowote, mwandishi wa makala na mhariri wa gazeti la Kiongozi wamekweza kanuni za kimila zilizo kaika sheria za Bunge na Katiba ya nchi dhidi ya kanuni za kimaumbile.

Wanaonekana kuelewa mchakato wa kutengeneza fasili za maneno yanayorejea kategoria asilia (natural kinds) kama vile maji, aside, uhai na jinsi.

Pia Wanaonekana kuelewa mchakato wa kutengeneza fasili za maneno yanayorejea kategoria ya kitamaduni (cultural kinds) kama vile mseja, kiti, mila, desturi, sheria za bunge, na jinsia, kwa upande mwingine.

Hata hivyo, hawaonekani kuelewa kwamba, "cultural kinds" ni zao la "natural kinds" na kwamba kinyume chake sio kweli.

Kwa ajili ya kueleza jambo hili, hapa yafaa kudokeza mambo kadhaa kuhusu dhana ya utamaduni.

Kimsingi, utamaduni wa jamii husika ni imani inayogawanyika katika vipengele vikuu vitatu. Kuna imani kuhusu maumbile, imani kuhusu tunu na imani kuhusu kanuni za kimila. Yaani, “descriptive beliefs, evaluative beliefs and normative beliefs.”

Imani kuhusu maumbile huwawezesha wanajamii kutambua kile wanachokiona kuwa ni kanuni za maumbile na hivyo kung’amua kile wanachokiona kuwa ni maumbile ya kweli na kuelewa kile wanachokiona kuwa ni maumbile yasiyo kweli.

Utambuzi huu, mang’amuzi haya na uelewa huu vinaweza visiendane na uhalisia wa mambo katika ulimwengu ulio nje ya vichwa vya waumini wa utamaduni husika.

Imani kuhusu tunu za jamii huwawezesha wanajamii kutofautisha kati ya malengo bora na malengo hafifu, malengo ya mpito na malengo ya kudumu.

Na imani kuhusu kanuni za kimila huwawezesha wanajamii kutofautisha kati ya matendo halali na matendo haramu, matendo adilifu na matendo ya kihalifu.

Kanuni za kimila zinajumkuisha desturi, maadili, katiba na sheria za Bunge la nchi husika. Na kwa ujumla, tunu na kanuni za kimila ni zao la imani kuhusu maumbile. Ndio kusema kwamba, mabadiliko katika imani kuhusu maumbile husababisha mabadiliko katika kanuni za kimila na tinu katika jamii husika.

Kwa mfano, jamii iliyokuwa inaamini kuwa kila tendo la ngono huchangia katika mimba ambayo hatimaye hutungwa inapaswa kubadili mawazo yake kuhusu nafasi ya tendo la ngono katika maisha ya watu pale sayansi inapothibitisha kwamba katika siku 30 za mwezi uwezekano wa kutokea kwa mimba ni 7/30.

Mwandishi wa makala na mhariri wa gazeti la Kiongozi hawaonekani kuwa na habari kuhusu ukweli huu: Kwamba, kanuni za maumbile zinayo nguvu ya veto dhidi ya tunu na kanuni za kimila.

Kwa hiyo, ukweli kwamba Katiba na sheria za nchi, ambavyo ni mazao ya mikono ya binadamu, havitambui uwepo wa mahunta, sio msingi wa kudumu kwa ajili ya kuonyesha kwamba, binadamu mahunta hawapo na kwamba mapenzi ya jinsi moja miongoni mwao hayapaswi kuruhusiwa kisheria.

Na DOSARI YA TANO ni matumizi ya misamiati yenye maana inayoyumba bila mwandishi kueleza maana iliyokusudiwa (equivocation).

Katika mazingira ya mjadala huu, Maneno "mapenzi ya jinsi moja" yanaweza kumaanisha mapenzi Kati ya wanaume wawili, wanawake wawili, mahunta wawili, mwanamume na hunta, au mwanamke na hunta.

Kila jozi iliyotajwa inavyo vionjo vya kierotiki kulingana na maumbile yake ya kijinsi.

Hivyo kutaka tabia za makundi Haya yote ziratibiwe kwa mujibu wa kapu moja la kanuni za maadili asilia ni sawa na kuchanganya maembe, mananasi, viazi, mihogo na machungwa katika kapu moja kwa kudhani kimakosa kuwa yote Ni matunda.

Majumuisho

Hivyo, kutokana na matokeo ya utafiti pamoja na majadiliano yaliyofanyika hapo juu, tunaweza kufanya majumuisho yafuatayo:

  1. Watu ambao ni wanawake mwanzo mwisho kuanzia seli hadi sura, wana mfumo wa jenetiki ulio na fomati ya “46XX KE, SRY-.
  2. Watu ambao ni wanaume mwanzo mwisho kuanzia seli hadi sura, wana mfumo wa jenetiki ulio na fomati ya “46XY ME, SRY+.
  3. Kuna watu wenye jinsi mbili, wakiwa na seli za kike lakini sura ya kiume, kwa maana kuwa, wana mfumo wa jenetiki ulio na fomati ya “46XX ME, SRY+.
  4. Kuna watu wenye jinsi mbili, wakiwa na seli za kiume lakini sura ya kike, kwa maana kuwa, wana mfumo wa jenetiki ulio na fomati ya “46XY KE, SRY-.
  5. Kuna jinsi tatu za binadamu, yaani jinsi ya wanaume, jinsi ya wanawake na jinsi ya mahunta. Hawa mahunta ni wanadamu wenye jinsi ya kiume na jinsi ya kike kwa mpigo.
  6. Maneno "mapenzi ya jinsi moja" yanaweza kumaanisha mapenzi kati ya watu wawili wenye jinsi ya kiume, mapenzi kati ya watu wawili wenye jinsi ya kike, au mapenzi kati ya watu wawili wenye jinsi ya hunta.
  7. Mahunta wawili, wenye jenitalia zote zinazofanya kazi sawasawa, wakifanya mapenzi haiwezekani kusema kwamba mwanamume ni huyu au mwanamke ni yule.
  8. Kwa mahunta, mapenzi ya jinsi moja ni jambo la kawaida na lisiloepukika. Na inawezekana wapenzi wa aina hii wakatiana na kujazana ujauzito kiasi kwamba baba wa mtoto X ni mama wa mtoto Y. Huo ndio ukweli wa agano jipya la kisayansi unaopindua ukweli wa agano la kale la misahafu. Hauepukiki.
  9. Watu wenye jinsi ya hunta wanaweza kufunga ndoa ya jinsi moja, kwa maana ya jinsi ya hunta, na hii itaitwa ndoa ya jinsi moja. Na ndoa ya aina hii ni halali kimaadili, na inapaswa kuwa halali kisheria na kikatiba.
  10. Kwa sehemu kubwa, welekeo wa kimapenzi ni zao la vinasaba vinavyobebwa na kromozomu fulani mwilini. Homoni katika mwili wa mimba na homoni katika mwili wa mama zinachangia katika kuamua mwelekeo wa kimapenzi. Na kwa nadra sana mazingira ya malezi ya mtoto baada ya kuzaliwa yanaweza kuchangia kwa sehemu ndogo. Tafiti zipo kuthibitisha mitazamo hii.

Hivyo, ni hitimisho langu kwamba, sisi kama Taifa na kama wakazi wa Bara la Afrika, tunapaswa kubaini, kukuza na kuhami haki zote za wanawake, wanaume na mahunta ndani na nje ya makanisa bila kukwazwa na kigugumizi kilichowalima ngwala kina Papa Yohanne Paul II, mpaka wakamtesa vikali Padre Sally Gross kwa sababu za kiteolojia na kimapokeo.

MAPENDEKEZO KWA VIGOGO WA KANISA, SERIKALI NA MEDIA

Mwisho, napendekeza mambo kadhaa kwa viongozi wa dini, serikali na jamii pana.

Mosi, ni kuhusu mhariri wa gazeti la Kiongozi na wahariri baki hapa Tanzania na Afrika. Wote wanapaswa kutenga muda wao na kusoma kitabu huria cha "Our Sexuality" (kwa sababu ya ukubwa kimembatanishwa hapa katika sehemu mbili--Our Sexuality Part A na Our SexualityPart B) kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wao pale wanapohariri kazi zinazojadili jinsi ya binadamu.

Wanapaswa kuachana na kasumba ya ukoloni wa misahafu ya kidini inayosema kwamba kuna jinsi mbili pekee, yaani wanaume na wanawake. Ukweli wa kisayansi unaonyesha kwamba kuna jinsi tatu, yaani wanaume, wanawake na mahunta.

Pili, ni kuhusu Kitengo cha Taifa cha Takwimu. Wanapaswa kuandaa madodoso yao ya sensa ya watu katika namna ambayo inaiwezesha serikali kuwatambua wanaume, wanawake na mahunta wote waliko nchini Tanzania, ili kila kundi liweze kuhudumiwa kwa mujibu wa takwimu sahihi.

Tatu, ni kuhusu sheria zetu. Bunge linapaswa kurekebisha sheria za takwimu, vizazi na vifo, na sheria zote husika ili ziweze kutambua kisheria jinsia ya mahunta. Kenya tayari wako mbioni kufanya marekebisho haya. Sisi hatuna sababu ya kusubiri.

Nne, viongozi wa Makanisa, na hasa Kanisa Katoliki, wanapaswa kuachana na propaganda ya kupotosha hadhira kwa kuibua hoja inayohusu kile wanachokiita "vuguvugu la ushoga" ili kuzuia mjadala muhimu juu ya ujinsi wa binadamu kwa kuzingatia mtazamo wa ternary sexuality na sio mtazamo wa binary sexuality. Mahunta sio mashoga wala wasagaji. Mahunta ni jinsi ya kibinadamu inayojitegemea.

Tano, viongozi wetu wa kijamii, na hasa viongozi wa dini wanapaswa kuachana na propaganda zisemazo kwamba tabia za mashoga, wasagaji na mahunta ni zao la "utamaduni wa Magharibi." Ukweli wa kisayansi uliojadiliwa hapo juu umeweka bayana chimbuko la tabia za watu hawa. Tunapaswa kuukubali ukweli huu na kujifunza kuishi nao.

Sita, taasisi za kijamii zenye dhamana ya kujenga imani ya jamii (social doctrine) katika mataifa ya Afrika zikumbuke mara zote kuwa Misahafu na Mapokeo ya Kikristo, Kiarabu, Kigriki na Kirumi inayo nafasi katika maisha ya Waafrika. Hata hivyo, wasisahau kuwa hivi ni vyanzo vya maarifa vyenye mapengo yanayoweza na yanayopaswa kuzibwa kwa msaada wa maarifa yapatikanayo katika misahafu ya sayansi asilia, sayansi za jamii na sayansi fomalia (formal sciences). Sayansi fomalia ni sayasni zenye mahadhi ya hisabati.

Saba, kuna umuhimu na uharaka wa Wizara ya Elimu kuboresha mitaala ya biology na civics ili sasa iongelee ternary sexuality badala ya binary sexuality. Aidha, kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), Wizara ihakikishe kuwa vitabu vya kiada na ziada viandaliwe haraka kwa ajili ya kuziba pengo hili la maarifa miongoni mwa jumuiya ya wanafunzi wetu walioko shuleni na vyuoni. Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima inapaswa kufuata mkondo huo pia.

Na nane ni kuwa, pamoja na kwamba, andiko hili limeelekezwa kwa Vigogo wa AMECEA, yaani, The Association of Member Episcopal Conferences of Eastern Africa (inayohusisha nchi za Ethiopia, Eritrea, Kenya, Malawi, Tanzania, Zambia, Sudan, Uganda, Somalia, Na Djibouti), bado hoja yake inapaswa kufanyiwa kazi na Vigogo wa Mashirikisho baki ya Kikristo, yaani:

  • Association of Episcopal Conferences Of Central Africa (ACEAC), Yaani Burundi, Rwanda, na DRC;
  • Association of Episcopal Conferences of Central Africa Region (ACERAC), Yaani Afrika Ya Kati, Drc, Gabon, Chad, Cameroun, Na Guinea Ya Ikweta.
  • Inter-Regional Meeting Of The Bishops Of Southern Africa (IMBISA), Yaani São Tomé, Mozambique, Lesotho, Namibia, Afrika Kusini, Na Zimbabwe.
  • Regional Episcopal Conferences of North Africa (CERN), Yaani Algeria, Libya, Morocco, Tunisia, Na Sahara Magharibi.
  • Regional Episcopal Conferences Of West Africa (RECOWA/CERAO), Yaani Liberia, Nigeria, Niger, Guinée-Bissau, Ivory Cost, Guinea, Benin, Mali, Togo, Ghana, Gambia, Na Sierra Leone.
  • Symposium of Episcopal Conferences of Africa and Madagascar (SECAM)
Huu ni wakati wa kufanya ukolonuzi wa kichwa cha Mwafrika (decolonisation of the African mind) dhidi ya kasumba hasi zilizopenyezwa katika bara hili wakati wa enzi za umisionari na ukoloni wa Wazungu na Waarabu.

Mama Amon,
Sumbawanga.

 

Attachments

  • Our Sexuality - Book--Part A--Pages 1-319.pdf
    18.9 MB · Views: 9
  • Our Sexuality - Book--Part B--Pages 320-708.pdf
    15.9 MB · Views: 8
Lakini ikiwa kusudi la Mungu katika uumbaji ni kuujaza ulimwengu. Na hili ni.kwa wanyama na mimea.

Na Mungu mwenyewe akamwambia mwanadamu kuwa nenda ukatawale vyote.

Basi sina shaka kabisa na uamuzi wa MUNGU kuzuia kwa uweza na nguvu zake kwamba mwanadamu asiweze kuzaliana na viumbe wengine. Na.kwann alilifanya hili kuwa gumu hadi wanasayansi wakasema tofauti katika specie husababisha specie moja kuto kuwa na uwezo wa kuzaliana na specie nyingine.

Nina uhakika kabisa binadamu angekuwa kiumbe wa kwanza kabisa Kucross breed hata na tembo ili tu kumprove Mungu kuwa wrong.

Ndio mana Mungu àlisema "sitabishana na mwanadamu kwasabbu na yy ni nyama".
 
Mleta mada umeandika makala ndefu kutetea ushoga na usagaji lakini chama Cha madaktari bingwa wa marekani walishatoa tamko kuwa ushoga na usagaji Ni tabia ya mtu anayoiendekeza mwenyewe haina Cha kisingizio Cha kuzaliwa hivyo au Nini.Mfano mdogo masista nyege wanazo za kutosha Mbona wanazidhibiti.Mapadre pia Wana nyege nyingi tu wanadhibiti.Hiyo mishoga na misagaji ni tabia zao tu za kijinga
 
Mleta mada umeandika makala ndefu kutetea ushoga na usagaji lakini chama Cha madaktari bingwa wa marekani walishatoa tamko kuwa ushoga na usagaji Ni tabia ya mtu anayoiendekeza mwenyewe haina Cha kisingizio Cha kuzaliwa hivyo au Nini.Mfano mdogo masista nyege wanazo za kutosha Mbona wanazidhibiti.Mapadre pia Wana nyege nyingi tu wanadhibiti.Hiyo mishoga na misagaji ni tabia zao tu za kijinga

Sio madai ya kweli kusema kuwa chama cha madaktari bingwa wanadai hayo uliyoyasema.

Wao wanatambua uwepo wa wanaume, wanawake, mahunta, mashoga na wasagaji kwa mujibu wa maumbile yao.

Rejea hapa American Psychological Association on LGBTI and sexual orientation.Kwa ufupi utaona pamphlet yenye maneno yafuatayo:


"Since 1975, the American Psychological Association has called on psychologists to take the lead in removing the stigma of mental illness that has long been associated with lesbian, gay and bisexual orientations. The discipline of psychology is concerned with the well-being of people and groups and therefore with threats to that well-being. The prejudice and discrimination that people who identify as lesbian, gay or bisexual regularly experience have been shown to have negative psychological effects. This pamphlet is designed to provide accurate information for those who want to better understand sexual orientation and the impact of prejudice and discrimination on those who identify as lesbian, gay or bisexual."

Pia, sababu za kuhalalisha utetezi wa kuwepo kwa wananaume, wanawake na mahunta ni zile zile--maumbile.

Uelewa mdogo tu wa embryology na genetics unathibitisha hivyo.

Aidha, zingatia kuwa hoja nzito zinahitaji makala ndefu. Half-cooked arguments are for kindergerten and primary school kids.

Jielekeze kwenye hoja kwa kutumia ushahidi unaotokana na utafiti mbadala.

Ama sivyo, baki mtazamaji.

No research no right to speak.
 
Wewe nyege hazidhibitiwi hata siku moja hilo ni swala la kimaumbile hao jamaa uliowataja mapadii na masistaaa wanafanya ngono balaaa
Mleta mada umeandika makala ndefu kutetea ushoga na usagaji lakini chama Cha madaktari bingwa wa marekani walishatoa tamko kuwa ushoga na usagaji Ni tabia ya mtu anayoiendekeza mwenyewe haina Cha kisingizio Cha kuzaliwa hivyo au Nini.Mfano mdogo masista nyege wanazo za kutosha Mbona wanazidhibiti.Mapadre pia Wana nyege nyingi tu wanadhibiti.Hiyo mishoga na misagaji ni tabia zao tu za kijinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duu, lengo la jinsia ni propagation, hivyo mahusiano yeyote ambayo inherently by default hayaleti propagation ni a waste of energy and resources, hivyo ni haramu.
 
Back
Top Bottom