Kumbukizi ya Dkt. Remmy Ongala wakati wa Nyerere hakukuwa na mgao wa umeme

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,994
Kumbukizi ya Dr Remmy Ongala wakati wa Nyerere hakukuwa na mgao wa umeme.. unaniamsha unajua nimelala vipi uhuni huo.

Namuhofia tuu mbwa mmoja mfia dini FaizaFoxy ambaye kwao hakukuwa na umeme wakati wa mwalimu
Mpaka leo hatuujuwi umeme wa serikali, tunajitegemea kwa umeme wetu wenyewe tokea kabla ya Uhuru.

Unazijuwa karabai na friji za mafuta ya taa wewe? Mie nimetumia zote hizo. Sasa hivi mambo kwa sola solar tu.

AlhamduliLlah, njoo ujionee kwetu, tuna hybrid electrical generation system ambayo tunasubiri Tanesco wakifisha nyaya zao tuwauzie umeme wa ziyada katika tunafua wenyewe.

Maana naona washaweka maguzo yao ya umeme.
 
Mpaka leo hatuujuwi umeme wa serikali, tunajitegemea kwa umeme wetu wenyewe tokea kabla ya Uhuru.

Unazijuwa kaharabi na friji za mafuta ya taa wewe? Mie nimetumia zote hizo. Sasa hivi mambo kwa sola solar tu.

AlhamduliLlah, njoo ujionee kwetu, tuna hybrid electrical generation system ambayo tunasubiri Tanesco wakifisha nyaya zao tuwauzie umeme wa ziyada katika tunafua wenyewe.

Maana naona washaweka maguzo yao ya umeme.
Ninakuja
 
mwisho wa nyimbo nimemuona yule trafiki maaarufu.... MAYENU
Da siku zimeenda ndugu yangu. Huyu traffic namkumbuma sana pale ubungo. Alikuwa burudani tosha. Aliwatoa watu stress za kazi Kwa style yake ya uongozaji magari...
sijui yuko wapi sasa huyu mayeni. Nchi ilikuwa Na Furaha Na matumainu ingawaje matatizo yalikuwa mengi...
 
Kumbukizi ya Dr Remmy Ongala wakati wa Nyerere hakukuwa na mgao wa umeme.. unaniamsha unajua nimelala vipi uhuni huo.
Unalinganisha vipi umeme wa wakati wa Nyerere na hivi sasa? Wakati wake alisema kuwa na friji au television ni luxury, kuendesha gari mwisho saa nane mchana siku za jumapili, foleni kila kitu unachohitaji.
 
Huo ni uongo uliofunzwa... wakati wa mwalimu watu walikuwa na television na walitazama television ya Zanzibar kabla ya TVT. Ila watu wengi hawakumudu kununua television Ndio ukweli. Hiyo ya foleni sidhani hata kama ilisumbua zaidi ya miaka miwili hapana... maisha ya mwalimu wakati wote watu walikuwa na furaha sana.

Mijinga miviongozi iliyofuata.. kweli kwa wingi huu tutumie kidatu na mtera alivyovijenga Mwalimu?

Heri jiwe aliona huu ni ubazazi akalazimisha ujenzi wa bwawa la mwalimu nyerere
 
Mahitaji ya nyakati ,Sasa hivi tunaishi miaka 30 nyuma!
 
Unalinganisha vipi umeme wa wakati wa Nyerere na hivi sasa? Wakati wake alisema kuwa na friji au television ni luxury, kuendesha gari mwisho saa nane mchana siku za jumapili, foleni kila kitu unachohitaji.
Hawa wa Sasa ingekuwa enzi za Nyerere ndio kwanza tusingeujua hata umeme wenyewe. Vita ya Ukraine tu ikawa kisingizio vitu vikapanda Bei sembuse.....
 
Huo ni uongo uliofunzwa... wakati wa mwalimu watu walikuwa na television na walitazama television ya Zanzibar kabla ya TVT. Ila watu wengi hawakumudu kununua television Ndio ukweli. Hiyo ya foleni sidhani hata kama ilisumbua zaidi ya miaka miwili hapana... maisha ya mwalimu wakati wote watu walikuwa na furaha sana.

Mijinga miviongozi iliyofuata.. kweli kwa wingi huu tutumie kidatu na mtera alivyovijenga Mwalimu?

Heri jiwe aliona huu ni ubazazi akalazimisha ujenzi wa bwawa la mwalimu nyerere
nadhani wewe ulizaliwa miaka ya tisini ndiyo unasema uongo uliofunzwa. Sisi wenzako tulisota kwenye mifoleni ya kila aina ya mahitaji ya nyumbani. Ati watu wengi hawakumudu kununua tv - basi huo ndiyo uongo wako uliojiaminisha, kwani hakukuwa na wafanya biashara na wafanya kazi wa serikali na makampuni?

Ati maisha ya mwalimu wakati wote watu walikuwa na furaha sana - furaha ya umasikini uliokithiri au furaha ya kulazimishwa kuimba zidumu fikra zake sahihi? Ingekuwa hayo pangekuwa na jaribio la mapinduzi?
 
Back
Top Bottom