Upungufu wa Gesi na maji ndio chanzo mgao wa umeme

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, imeweka wazi kuwa sababu ya mgao wa umeme nchini umesababishwa na upungufu wa maji na gesi.

“Sababu za uzalishaji wa umeme kuwa mdogo ni pamoja na upungufu wa maji kwenye mabwawa tegemezi yakiwemo Mtera, Kidatu na Kihansi; uchakavu wa mitambo ya kuzalishia umeme na miundombinu ya kusafirishia umeme, na upungufu wa gesi ya kuzalishia umeme. Aidha, athari za upungufu huo wa umeme ni maeneo mengi ya nchi kuingia katika mgao wa umeme.” – Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini

Kwa upande mwengine Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amesema katika kipindi kifupi, zaidi ya mashine umba (transifoma) 87 zimeibwa katika mkoa wa Pwani na Dar es Salaam na hivyo kupelekea tatizo la umeme.

Nini maoni yako?

Written by Mjanja M1 ✍️
 
rekebisheni izo kasoro na sio kuleta siasa kwenye ishu muhimu kama ya umeme.
 
Kwa upande mwengine Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amesema katika kipindi kifupi, zaidi ya mashine umba (transifoma) 87 zimeibwa katika mkoa wa Pwani na Dar es Salaam na hivyo kupelekea tatizo la umeme.
Aisee,hii Kali.
 
toka maktaba

Capture.PNG
 
Generator zote hizo zinaibiwa kwa mikoa miwili tu!!!
Halafu upungufu wa maji kivipi wakati mvua zimenyesha hadi kuleta mafuriko?Au kwamba maji yalikwepa kuingia kwenye mabwawa.

Sasa mwisho wa siku mnafanya nini?
The dying country!
 
hawa TANESCO hata hawaeleweki.....sijui wanatuonaje?
Inakuwaje waliweza kubuni miradi mipya ya umeme isiyo na tija yoyote kipindi hiki kama huko Bukoba sijui na iringa nk iliyo gharibu mabilioni ya pesa .... badala ya kutoa kipaumbele cha kukarabati miundo mbinu???
Lakini pia tunahitaji technologia mpya...haya mamita yamepitwa na wakati....tunataka mtu akinunua umeme kwa simu uingie kwenye mita...

Nafikiri TANESCO inaweza kubinafsishwa kwa 49% ambapo bado mwenye hisa nyingi atakuwa Serikali .
Kwa kufanya hivyo wateja watapata huduma nzuri na kwa bei rafiki na Kodi ya serikali ingeongezeka.
Private sector hakuna longolongo kwani wana amini kuwa; matatizo ya ndani sio kisingizio cha kuchelewesha huduma; kwani hayamuhusu mteja aliyelipia huduma....
Naamini kabisa hili dubwana lina muumiza sana Mama Kichwa hivyo ni suala la muda tu.....
 
Generator zote hizo zinaibiwa kwa mikoa miwili tu!!!
Halafu upungufu wa maji kivipi wakati mvua zimenyesha hadi kuleta mafuriko?Au kwamba maji yalikwepa kuingia kwenye mabwawa.

Sasa mwisho wa siku mnafanya nini?
The dying country!
KWa sasa mafuriko yamezidi hivyo mitambo ya kutengeneza umeme imesimamishwa kwa mda kukwepa uharibifu usio wa lazima.
Endeleeni kuwa wavumilivu😁
 
Back
Top Bottom