Kumbe kitunguu saumu kinalipa hivi

Paul S.S,
Kuna clip niliona YouTube, yaani ilinifurahisha sana. Ni kijana mkenya alikua mmnoa visu, katika kuhangaika kwake siku mmoja alijarubu kupanda kitunguusaumu kwenye eneo dogo sana.

Alishangaa pale alipo vuna Yale mavuno yake, hapo hapo skapats akili na akapata ardhi robo heka, zile zile mbegu alizovuna ndio akazipanda tena, hapo ndio ikwa mwanzo wa safari yake ya utajiri, alifikisha kulima ndhani hekari 10.

Hajawahi kuota kwamba angemiliki nyuma au gari lakini sasa anao kila anachotaka.
 
Brown73,
Aisee safi sana.
Vipi hiyo Video inahadithia mafanikio yake au inaonyesha jinsi ya ulimaji wa kitunguu swaumu?
 
Aisee safi sana.
Vipi hiyo Video inahadithia mafanikio yake au inaonyesha jinsi ya ulimaji wa kitunguu swaumu?
Infact maelezo mengi inhusu mafanikio yake huyo jamaa, Na ni fundisho zuri kwa kweli, lakini kuna masomo mengi mazuri tu ya vitunguu saunu. Jaribu kuandika KILIMO CHA VITUNGUU SAUMU kwenye Google.
 
Jamani watanzania ifike mahali tuache maneno mengi tufanye kazi....mimi kwasasa niko shambani niko nalima japo kwasasa nimejikita kwenye kilimo cha hoho ila mwaka huu nalima tangawizi pia....rai yangu kwa yeyote anayetaka kujifunza aje hapa IGAWA - MBEYA atajifunza mengi sana kuhusu kilimo cha umwagiliaji....hapa watu wanalima sana vitunguu(maji)...japo sijaona mkulima mzuri wa vitunguu swaumu....lakini pia hapa maji yapo mwaka mzima.

karibuni sana tulime kisasa....kilimo kinalipa sana...atakaye taka kuja igawa kujifunza nitampa ushirikiano wa hali ya juu with maximum care and security
Nipo very interested kuja kufanya kilimo huko....je gharama zikoje kwa ekari moja ya vitunguu maji?
 
The hammer,
Hivi mkuu ukifanikiwa kulima haya mazao ya mboga mboga kama nyanya au bamia au nyanya chungu kipindi cha masika na ukahudumia hiyo miezi uliyoisema Jan to April si unaweza kupata bingo la maana?
 
Mkuu marejesho vipi kilimo cha hoho, ulifanikiwa? nami nataka kulima hoho. Ila ni beginner kabisa kwenye kilimo, naomba unipe uzoefu wako katika zao hili. Nipo maeneo ya Dar. Najipanga kutafuta shamba pembezoni mwa Dar. Ahsante
Hoho Dar Haioti. Hoho ni Iringa labda na mbeya. Mimi nilikuwa mlanguzi wa Hoho mashambani na kuuza Sokoni pale Sambusa-Kigogo..
Kukodi shamba ni 300,000 pamoja na Pump.

Mashamba ya Iringa kandokando ya mtu Ruaha mfano kama Pale Ruaha Mbuyuni ni mazuri na bei yake ni hiyo. Maji ni ya uhakika ule mto Ruaha haukaukagi, Ila jitahd kupata mbegu bora, ni heri ukatumia gharama kubwa ya mbegu ili upate Hoho bora, Hoho zina Grade. Hoho ikiwa nzuri, kubwa na Ina mng'ao ahaah mbona sokoni wataigombania Mpaka Watu watakunjana mashati.

Walanguzi/ wanunuzi wa hoho ni wengi ni wa uhakika wewe tu bidii yako kuzalisha. ila angalia na upepo wa sokoni sio ufyatue tu uje ukute soko ni 30,000 kwa gunia.

Karibu, Namba yangu ni 0746 785704 kwa msaada zaidi wa Kilimo cha Hoho.
 
Shark, Huwezi kuzalisha kitu pasipo kuwa na Mbinu ya soko. Wafugaji wengi huwa hawafuatiliagi soko Lipoje au wanawez kuuza wapi na kwanani? Wanafanya ufugaji wa kubet kwa wanunuzi watakuja tu..

2. Hawajaribu kufuatilia ushindani wa kile wanachofuga hasa katika maeneo walipo au kanda hiyo, Lakini pia kufuatilia ushindani wa soko kwa kanda hiyo upoje na ikitokea soko ilo limezidiwa atauzia wapi? Ufugaji au kilimo kinaitaji Utulize akili na Mahesabu sio tu umekurupushwa na wewe ukakurupuka, ufugaji au kilimo utajirisha kwa haraka zaidi, na "Ufilisi pia kwa haraka zaidi". Ni hesabu za kucheza na Mzani.
 
Jamani naomba mtu ambaye ameshalima kitunguu swaumu snipe ABC zake!!! Km Wapi ananunulia mbegu bora. Madawa yanayotumika, hatua za uupandaji mpk kuvunA, vitu vya kuzingatia ktk hiki kilimo, heka moja inaweza gharimu kiasi gani? Na hiyo heka inaingia mbegu kiasi gani?!!! Ntashukuru kwa Masada wenu
Wakwambie ulete ushindani sokoni..
Tumia akili, Weka bidii yako Kupata data so usubiri mtu akapikie, akuandalie, akutafunie wewe umeze..
Kama una nia Tafuta madalali wa zao hili wao watakupa ABC maana dalali wa kitunguu ni kitunguu tu, kabeji ni kabeji wale ni wazoefu wa miaka, ila shida yao mda mwngne wanatoa data za uongo ili ukalime uwaletee..
 
Jamani wakuu waliolima vitunguu thom (saumu) tusaidieni jamani na sisi tupate elimu ya kujua jinsi ya kulima. Hekari moja kilo ngapi zinahitajika kupanda.
Changamoto zake zikoje.
Udongo wa aina gani unakubali mpaka mavuno yake ahsanteni
 
puruwanji,
Mimi nilijaribu vitalu vinne kwa majaribio. Mbegu nilinunua sado moja 9 sh.10000 na ikabaki nyingi tu.

Nililima mwezi wa tisa hivyo maji ya kumwagilia ilikuwa changamoto,vilikomaa mwezi wa kwanza. Jua la kuanikia lilikuwa changamoto sana vingi vilioza.

Kitalu nilichopanda mwezi wa kumi kilikutana na mvua hivyo basi vilishambuliwa na kutu. Udongo niliolima ni mfinyanzi mwekiundu na mbolea ya samadi sikutumia ya dukani na vilistawi sana.

Kitu cha kuzingatia hautsaakiwi uwe na mambo mengi,vilevile wakati wa kupanda usitumie watu wasio makini utapata hasara kama watafukia sana au watavigeuza juu chini,hata umbali wa kitunguu na kitunguu.
 
puruwanji,
Kama upo maeneo rafiki jaribu kulima vitalu viwili utapata majibu.thaumu hupandwa kipindi cha mvua na kiangazi,ukilima sasa hivi mpaka mweezi wa pili utapata majibu na hutokosea kwa hio nenda kanunue mbegu za aina mbalimbali utapata majibu kwa vitendo.

Udongo unaokubali ni mfinyanzi na wenye rutuba,mbolea samadi na dukani(npk) zote sawa tu.Msimu ni mwezi wa 2-3 kwa Mbeya na Njombe wanaanza 12.lakini unaweza panda kiangazi na ukamwagilia, vitunguu vinapenda sehemu za baridi na mvua nyingi, jua la kuanikia la kutosha.

Debe la vitunguu ni sh 45-60 elfu heka moja ni kilo 100. Binafsi nimefanya majaribio ya vitalu viwili kwa nusu sado ya vitunguu
 
Back
Top Bottom