Kumbe Kitunguu Saumu kinalipa hivi

Red Giant

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Messages
11,865
Points
2,000
Red Giant

Red Giant

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2012
11,865 2,000
Nasikia gunia la kitunguu saumu la debe tano linauzwa 500,000!

Hiki kitunguu hakina mbegu hivyo unapanda vile vipande vyake. wanasema ekari moja inaweza kupanda gunia 16 hadi 28 za kilo mia kutegemeana na spacing. hivyo utapanda vya Tsh 8m-14m. kinaweza kuzaa mara 5 hadi 8 ya gunia ulizopanda.

Wengi wanasema ni wastani wa gunia 75 kwa ekari. ambazo zinakupa milioni 37.5. inasemekana sehemu yenye kitunguu maji na saumu hustawi.

Naomba wakulima wenye uzoefu huko babati mje mtupe uzoefu wa shambani.
 
Asante

Asante

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2009
Messages
2,072
Points
2,000
Asante

Asante

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2009
2,072 2,000
[h=3]KILIMO CHA VITUNGUU TWAUMU - garlic[/h]
UDONGO
Vitunguu twaumu vinahimili aina nyingi za udongo, ila vinastawi zaidi katika udongo usiotuamisha maji kabisa na wenye mbolea asili, kama mbolea si ya kutosha kwenye udongo, tumia samadi iliyokwisha oza vizuri usitoe samadi bandani na kuipeleka shambani moja kwa moja kwenye shamba la vitunguu thwaumu, labda kama utaliacha shamba bila kulimwa kwa zaidi ya miezi 6, pia unaweza kutumia mbolea za viwandani kama ammonium nitrate, ammonium sulphate, urea n.k wakati wa kupanda na kila baada ya wiki 4 – 6 mara mbili zaidi

UPANDAJI
Kipindi kizuri kwa upandaji ni kipindi ambacho hakuna joto hasa miezi ya May mpaka August kwa Tanzania, Unachukua kitunguu twaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 10 na kati ya mistari ni sentimeta 30. Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kungolewa kabisa. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu thwaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu.


UMWAGILIAJI

Kama kuna upungufu wa mvua au ni kipindi cha kiangazi basi ni vizuri ukamwagilia shamba lako, wakati mzuri wa kumwagilia vitunguu twaumu ni asubuhi na sio jioni au mchana, hii inasaidia vitunguu twaumu kujijengea uwezo wa kupambana na magonjwa, baada ya mizi miwili unaweza kupunguza umwagiliajai huku ukiangalia kwa kuchimba kidogo kama vitunguu twaumu vimezaliana vya kutosha na kuanza kukomaa, ukiona vimekomaa acha kabisa kumwagilia ili visioze

UANGALIZI
Aina nyingi za vitunguu twaumu vitakuwa kama vinatoa mbegu kwenye mmea (angalia picha chini), ingawa kuna nadharia nyingi lakini inashauriwa kukata hizi mbegu chini kabisa kwa kisu kikali na kisafi, usikate mapema mara baada ya kutokeza bali subiri mpaka mmea unapoanza kama kujikunja ndipo ukate, kwa wale wanaoacha mbegu hizi ukiamua kuzipanda kwa msimu wa kwanza zitazaa kitunguu kimoja tu cha duara lakini chenyewe ukikipanda tena kwenye mzunguko wa pili kitazaa vitunguu vingi kama kawaidaUngoleaji wa magugu na majani ni muhimu muda wote ili kuondoa kugombea rutuba, hewa na maji shambani, kwa wenye mashamba makubwa wanaweza kutumia dawa za kemikali kama ROUNDUP na nyinginezo ili kudhibiti magugu, ingawa mimi sishauri hivyo.

MAGONJWA
Magonjwa kama botrytis (kuoza shingo) blue mould na fusarium (kuoza kwa vitunguu) husababisha hasara kubwa kama hayatadhibitiwa kwa kutumia viuatilifu mara unapoona dalili, pia magonjwa kama white rot huchukua zaidi ya miaka 20 kuondoka kama yatavamia shamba lako, inashauriwa kufanya mabadiliko ya zao kila baada ya miaka mitano kwa kupanda mazao mengine yasiyo jamii moja kama vitunguu maji, unaweza kupanda maharage, mahindi, karoti na kabichi katika mzunguko huo. Pia magonjwa kama kutu ya majani husababisha na unyevu mwingi hasa kama mimea itakuwa kwenye udongo unaotuamisha maji au mimea kumwagiliwa jioni au usiku, kumbuka kumwagilia asubuhi tu Ili kudhibiti ugonjwa huu wa kutu mimea ingolewe na ichomwe au utumie viuatilifu vya kuulia fangasi wa mimea.
 
Red Giant

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Messages
11,865
Points
2,000
Red Giant

Red Giant

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2012
11,865 2,000
Asante shukrani mkuu. kuna pdf nataka kuiweka. kama unafahamu naomba unielekeze.
 
Last edited by a moderator:
Red Giant

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Messages
11,865
Points
2,000
Red Giant

Red Giant

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2012
11,865 2,000
Ni kweli inalipa, japo sina hakika na 500,000, bei niliyoisikia mimi ni ya tsh 300,000.
Niliwahi jaribu kulima mkuu, nililima eka moja huko babati sehemu moja inaitwa kiru, changamoto kubwa ni maji mkuu
vipi gharama ya vitunguu vya kupanda ilikuwaje?
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
45,862
Points
2,000
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
45,862 2,000
Gharama ni kubwa mkuu, debe moja la mbegu 80,000
Kama ushawah kulima tunaomba utupe taarifa zaid ili tujue tukianza kulima tutakutana na changamoto zipi.

1. Eka 1 inachukua debe ngapi?

2. Msimu wa kupanda ni upi?

3. Maeneo yanayolimwa ni yapi?

4. Nikilima sehem yenye vyanzo vya maji vya uhakika?

5. Eka 1 unavuna gunia ngapi?

6. Vinachukua miezi mingap shambani?

7. Utaratibu wa kupanda unakuwaje?
 
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
3,758
Points
2,000
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2010
3,758 2,000
mkuu Red Giant haya mazao mawili; kitunguu saumu na tangawizi kiukweli ukimudu kupata mtaji ukalima na kuhudumia vizuri basi umasikini byebye!!
jiulize tu mbegu ya kupanda ekari1 ya tangawizi ni karibu gunia10: wakati kilo1 cha tangawizi ni sh5000 shambani!!! kadharika Kwa saumu mambo ni yaleyale ngoma ipo kwenye gharama ya mbegu!!
Maadam shamba lenye chanzo cha maji ninalo ngoja nijikongoje kupata mtaji.
 
Last edited by a moderator:
Asante

Asante

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2009
Messages
2,072
Points
2,000
Asante

Asante

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2009
2,072 2,000
Ni kweli inalipa, japo sina hakika na 500,000, bei niliyoisikia mimi ni ya tsh 300,000.
Niliwahi jaribu kulima mkuu, nililima eka moja huko babati sehemu moja inaitwa kiru, changamoto kubwa ni maji mkuu
Bei ya 500,000/= ni bei anayopata muuzaji wa rejareja sokoni kariakoo kwa gunia la kilo 100
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
45,862
Points
2,000
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
45,862 2,000
mkuu Red Giant haya mazao mawili; kitunguu saumu na tangawizi kiukweli ukimudu kupata mtaji ukalima na kuhudumia vizuri basi umasikini byebye!!
jiulize tu mbegu ya kupanda ekari1 ya tangawizi ni karibu gunia10: wakati kilo1 cha tangawizi ni sh5000 shambani!!! kadharika Kwa saumu mambo ni yaleyale ngoma ipo kwenye gharama ya mbegu!!
Maadam shamba lenye chanzo cha maji ninalo ngoja nijikongoje kupata mtaji.
Nadhani shida ni jinsi ya kuendesha shamba. Bei ya mbegu sio ishu as long as umeamua kulima na hela itarudi tu.

Kama una jua chochote jazia nyama mkuu
 
Last edited by a moderator:
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
3,758
Points
2,000
Kisima

Kisima

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2010
3,758 2,000
Kuna watu hapa jukwaani wao ni kila kukicha ni kuchukua data tuuuu wajawahi kabisa kuingia kwenye field zaidi ya kuuliza ABCD za fursa mbalimbali zinazopambanuliwa hapa jukwaani. Mmoja wao ni huyu bwana Bulldog ni kero tupu aseee mpaka kero, ebu fanya utupie material things hapa jukwaani.... otherwise unaboa mkuu!!
q
 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,315,048
Members 505,132
Posts 31,846,361
Top