Kumbe kitunguu saumu kinalipa hivi

Red Giant,
Kitunguu saumu kina shughuli kwenye kulima, kwanza kuanzia mbegu, kununua vitunguu saumu ni gharama sana, bado kulihudumia shamba, unatakiwa ulimwagilie kwa miezi isiyopungua sita, mwezi wa sita ndio unavuna
 
Kama upo maeneo rafiki jaribu kulima vitalu viwili utapata majibu.thaumu hupandwa kipindi cha mvua na kiangazi,ukilima sasa hivi mpaka mweezi wa pili utapata majibu na hutokosea kwa hio nenda kanunue mbegu za aina mbalimbali utapata majibu kwa vitendo.Udongo unaokubali ni mfinyanzi na wenye rutuba,mbolea samadi na dukani(npk) zote sawa tu.Msim u ni mwezi wa 2-3 kwa mbeya na njombe wanaanza 12.lakini unaweza panda kiangazi na ukamwagilia, vitunguu vinapenda sehemu za baridi na mvua nyingi,jua la kuanikia la kutosha.Debe la vitunguu ni sh 45-60 elfu heka moja ni kilo 100.Binafsi nimefanya majaribio ya vitalu viwili kwa nusu sado ya vitunguu
Mkuu asante sanaa nitajaribu hivyo ila nilikua na wasiwasi kwa huku kwetu sisi watu wa visiwa tumezungukwa na bahari. Ila nitajaribu nashkuru sanaa kwa msaada wako
 
airwing,
Mimi nimelima hoho za njano na kijani nzuri tu kule Kigamboni, Yaleyale Puna 50km kutoka feri. Kuna udongo wenye rutuba hatari
 
Habari wakuu. Mimi ni kijana mkulima na mfanyabiashara wa kitunguu Swaumu. Nimejichimbia mkoa wa manyara kwa miaka michache sasa nikiendesha shughuli zangu baada ya kumaliza chuo. Kama unavyojua suala la ajira kidogo ni tatizo sasa kwasababu home tayari walikuwa na msingi katika hili zao nikasema hakuna jinsi ngoja nikomae lakini katika namna ya kufanya kilimo kwa njia ya kisasa na kuleta tija.


Nashukuru JF imekuwa msaada mkubwa sana kwangu kujifunza mambo mengi hasahasa nikisoma experience za wadau waliowahi kulima zao fulani hapo nyuma, Changamoto walizopitia lakini mafanikio pia waliyopata. Leo na mimi nataka ni-share kitu ninachokifanya ili wakulima na wajasariliamali kama mimi tupeane mbinu za masoko lakini pia hii naamini ni njia nzuri yakuwasiliana na watu watakaohitaji hii bidhaa iwe kwa matumizi binafsi au kwabiashara.


UTANGULIZI
Kitunguu swaumu ni zao linalotumiwa na jamii tofauti duniani (Asia, Africa pia Unataka) kote kwasababu ya sifa yake ya kutibu maradhi. Kitunguu Swaumu ni tiba nzuri ya magonjwa yafuatayo

• High blood pressure
• Matatizo ya liver
• TB
• Interstinal Worms
• Kisukari etc

Kwasababu ya faida hizi zao hili la garlic nimekuwa na uhitaji mkubwa katika miaka yote. Kwa mfano sasa hivi mimi nauza gunia la kg 100 kwa tsh 350,000/= hadi 400,000 hapa nazungumzia kama utanunua store, na msimu wa mavuno nauuza kwa tsh 250,0000 hadi 300,000 kwa gunia la kg 100. Wewe kama mfanyabiashara wa kati unaweza kuuza kwa bei ya juu zaidi kutegemea urahisi wa kusafirisha.

Hapa kama yupo mdau anayetaka hii bidhaa tuzungumze kwa kina kuhusu njia bora na nafuu za kusafirisha lakini pia kupata wateja zaidi unaweza kunitumia pm nitashukuru nikijifunza toka kwako pia.

MAANDALIZI KABLA YAKUANZA KULIMA KITUNGUU SWAUMU. WEKA KILA KITU SAWA

Kabla hujaanza kuingia shambani kuna mambo ya kadhaa yakuzingatia mapema kwasababu usipoanza na msingi mzuri utakosea na hiyo itakuwa hasara kwako. Kitu cha kwanza kabisa ni kufahamu jinsi soko linavyoenda kwa msimu husika. Hii itakusaidia kufahamu iwapo gharama utakazoingia zitaweza kurudi siku unauza garlic yako. Kuelewa masoko ni muhimu sana ndiyo maana nataka hapa JF watu serious tuwasiliane na kufanye hii mambo katika kiwango cha juu.

Sasa baada ya kuelewa mwenendo wa soko (na hii unafahamu kwa kuongea na watu tu) ni wakati wakauingia shambani na kufanya kazi yenyewe ya uzalishaji.

MAHITAJI/GHARAMA SHAMBANI.

Hapa nachukulia mfano ninalima ekari 1 . Hekari moja utavuna tani 3 .Nitauza kg 1 kwa tsh 3000 - 3500 sokoni * 3= 9,000,000 kama nitauza kg 1 kwa tsh 3000

Kama utasubiri msimu wa sikukuu yaan December, Ramadhan, pasaka utauza kwa bei juu zaidi

Hapa unaweza kuona ni namna gani garlic ina bei zuri iwapo utazalisha vizuri. Na jambo zuri ni kwamba soko ni stable. Ukiwa na mfumo mzuri wa usafirishaji basi umemaliza.

Sasa tuangalie cost utakazokutana nazo kuhudumia shamba lenye ukubwa wa ekari 1

Kukodi shamba la ekari 1 = tsh 1,000,000 hapa itategemea kama hakuna ushindani kama kuna ushindani itazidi hapo

Mbegu kwa eka 1 inahitaji kg 350- 400kg, kg 1 ya mbegu inauzwa tsh 1500 kwa kg 1 * 400 = 600,000/=
Hatua ya kwanza ni kuandaa shamba kama utalima kwa trekta ni tsh 50000 *2 = 100,000/=
Hatua ya pili ni kupanda shamba, mfano unataka bustani ziwe na urefu wa 9m x upana wa 3m utapata bustani 180 * tsh 500 = 90000/=

Kutengeneza channels ya kupandia vitunguu tsh 200 * 180 =36000/=
Kurudishia udongo kwenye hizo channels za kupandia vitunguu tsh 100*180 =18000/

Kumwagilia shamba 20000 * 16 weeks =320,000/=

Hapa unatumia mifereji kumwagilia source ya maji ni mto


MBOLEA
DAP mifuko 2 kg 50 2@7000*2= 140,000/=
Urea mifuko 2@70000 * 2= 140000/=

MADAWA
Boosters kg 3 10000 *3= 30000 kama utanunua kwa pamoja yaani starter, vegetative na finisher
Madawa ya kutu mimi natumia folicur ni dawa ya mafuta ina matokeo mazuri lita 2 kwa eka 1cm³ =tsh 80 *2000cm³ = 160,000/=

Kibarua wa kupiga dawa pumps 6 kwa eka @500*6=3000 * 6 = 18000/= yaani kila hatua utapiga dawa x 2 pia inategemea kama zao limeanza kushambuliwa na kutu itazidi hapo

KUVUNA
Kung'oa bustani 1 tsh 500@1800 * 500 = 90000/=

KUHIFADHI
Kama utaamua kuvikata na kuweka kwenye chanja
Beseni 1tsh 500 *2 = 1000 mfano bustani itatoa beseni 2, itakuwa 1000 * 180 = 180,000/=
Kama utaamua kuvifunga iliuning'inize bustani 1 tsh 300*180 = 54000/=
Jumla ya gharama zote ni tsh 3,138,000/=
9,000,000 - 3,138,000 = 5,862,000/= hii ni profit yako

Kama unataka kupata mavuno mazuri na kupunguza gharama za uzalishaji panda garlic yako pindi mvua imeanza kukatika kuanzia mwezi wa 3 mwishoni hadi wa 5 hii ni kwa kanda ya kaskazini,

Kanda ya kusini kuanzia mwezi wa 5 mwishoni hadi wa 6 mwanzoni.

Garlic inastawi vizuri sehemu zenye baridi na upepo

Mikoa kama Mbeya, Iringa, Singida, Arusha, na Manyara yanafanya vizuri sana kwenye kilimo cha hili zao

ANGALIZO:
Huo mchanganuo unatokana na uzoefu wangu katika kilimo cha hili zao, sina utaalamu wowote zaidi ya kupata uzoefu kutoka kwa wazazi wangu.

KWANINI GARLIC NI MBADALA?

Haihitaji kumwagiliwa Mara kwa Mara kama ilivyo kitunguu maji;
Utamwagilia kila baada ya siku 6-7.
Hapa nazungumzia from my experience, hili zao halihitaji maji mengi yatasababisha mizizi yake kuoza
Haihitaji utaalamu au gharama kubwa wakati wa kuandaa mbegu;
Hili zao halina mambo mengi pindi unapoandaa mbegu.
Unachofanya ni kuanika vitunguu vyako juani baada ya masaa 2-4 unaanza kupukuchua mpaka zile punje zitawanyike ila kuwa makini usitumie nguvu nyingi wakati wa kupukuchua utasababisha mbegu zitoe maganda hii hali itasababisha mbegu zako siziote shambani

3.Inachukua miezi minne kupanda hadi kuvuna;

Kwa kawaida ina chukua miezi 4 toka unapanda hadi unavuna. Baada ya hapo ni kuweka vizuri kwa ajili ya kuuza,au kuweka store ili kusubiri bei ipande ili uuze kwa bei juu na upate faida kubwa

MASOKO NA NJIA ZAKUWAFIKIA WAHITAJI.

Binafsi kwa sasa nafanya kazi na washirika wangu waliopo Dar es Salaam. Kazi yangu hapa ni kutafuta hawa watu wakushirikiana nao lakini pia kuhakikisha natuma mzigo kwa uaminifu mkubwa.

Lengo langu nikufanya kazi na watu wengi zaidi ili kupanua wigo wa biashara kwasababu nafahamu soko lipo. Natoa wito kwa yoyote anayetaka tufanye Hii business milango ipo wazi. Kikubwa ni kuwasiliana na kuelewana jinsi tunavyoweza kufanya kwa mfanikio zaidi.

Hawa watu ninaofanya nao kazi wao wanauza hapo Dar es Salaam. Hapa pia natafuta mdau atakayeelewa zaidi kuhusu soko la garlic nje ya mipaka ya nchi yetu au mikoa mingine hapa TZ tupige kazi.

CHANGAMOTO NAZOKUTANA NAZO

Kama ilivyo biashara yoyote ile changamoto hazikosekani. Binafsi napitia changamoto zifuatazo.

• Gharama kubwa kwenye usafirishaji. Kiasi kikubwa kinaenda kwenye usafirishaji. Lakini hii nadhani inaweza kupata solution kama tutaunda mtandao mzuri wa usafirishaji.
• Njia nzuri yakuji-market ili kuwafikia wateja wapya. Hapa nashukuru JF inaenda kuwa mkombozi ndiyo maana nimeandika hii thread.
• Kupata mtaji mkubwa ili kulima kwa kiwango kikubwa, au kununua mzigo mwingi na kuweka store. Hapa nakaribisha yoyote anayetaka tuongee kuhusu hili kwa kina. We can do something.
. Changamoto ya hewa, kuna msimu unakuwa na mvua chache kwahiyo maji yanakuwa hayatoshi na uhitaji ni mkubwa hii itapelekea uzalishaji kuwa mdogo

NENO LA MWISHO
Wakuu kama nilivyosema mimi ni kijana na lengo langu nikufikisha biashara yangu mbali. Nakaribisha mazungumzo kwa yoyote na nipo tayari kupiga kazi.

IMG_20191107_192419_305.jpeg
IMG_20190923_170234_4.jpeg
 

Attachments

  • FB_IMG_1571760278470~2_1572680738095.jpeg
    FB_IMG_1571760278470~2_1572680738095.jpeg
    51 KB · Views: 20
  • FB_IMG_1571760278470~2_1572680738095.jpeg
    FB_IMG_1571760278470~2_1572680738095.jpeg
    51 KB · Views: 16
  • FB_IMG_1571760278470~2.jpeg
    FB_IMG_1571760278470~2.jpeg
    64.2 KB · Views: 21
Ukiona mkulima anakwambia kilimo fulani kinalipa jua unaenda lia. Vyote vinavyolipa havitanagzwi, ukiona vinatangazwa jua utaenda anzisha na kuumia.
Nakazia hapa. Ukiona unapewa mbinu hivi jua hakuna jambo humo.
 
Ipo vizuri ,nimetamani sana kulima garlic kwa kuwa ni kweli nimeona kuna faida nzuri kabisa hata wanaobeza hapa waende wakaulize kg 1 ya garlic ni tsh ngapi ndipo wataelewa kuna faida
Changamoto kila sehemu zipo tu ila watu wanafanikiwa humohumo ndani ya changamoto hivyo siwezi kuogopa maana hata ukimwambia mtu mahindi yanaweza kukutoa kimaisha anaweza kubisha ila tuliolima mahindi tunafahamu utamu wake.

Ngoja nikucheck INBOX tuongee vizuri ,maana nimepata changamoto sana kuipata mbegu huenda wewe ukanisaidia
 
Boss mfano nikichukua vitunguu hivyo vikavu nikatoa mbegu moja moja then nikapanda vitaota au Kuna mbegu nyingine mbadala?
 
Ipo vizuri ,nimetamani sana kulima garlic kwa kuwa ni kweli nimeona kuna faida nzuri kabisa hata wanaobeza hapa waende wakaulize kg 1 ya garlic ni tsh ngapi ndipo wataelewa kuna faida
Changamoto kila sehemu zipo tu ila watu wanafanikiwa humohumo ndani ya changamoto hivyo siwezi kuogopa maana hata ukimwambia mtu mahindi yanaweza kukutoa kimaisha anaweza kubisha ila tuliolima mahindi tunafahamu utamu wake.

Ngoja nikucheck INBOX tuongee vizuri ,maana nimepata changamoto sana kuipata mbegu huenda wewe ukanisaidia
Kuna siku nilipita Lindi nikauliza kg ya hivi vitunguu ilikuwa 12000 elfu
 
Boss mfano nikichukua vitunguu hivyo vikavu nikatoa mbegu moja moja then nikapanda vitaota au Kuna mbegu nyingine mbadala?
Vitaota ila angalia kama hilo punje limeanza kuota kiini cha kijani kwa kulivunja katikati na vingine vimepulizwa dawa ili visiote
 
Back
Top Bottom