Kumbe kitunguu saumu kinalipa hivi

ndugu gwiji huku igawa mashamba ya kukodisha yanapatikana heka moja ni laki mbili kwa mwaka
Okay
Na kama unaweza kunisaidia zaid
Je mazao gani hasa mnalima?na je mmezamia kilimo vha umwagiliaji au chq msimu/ mnasubiria mvua?
 
365,
Verry brilliant mkuu
Nimependa sana hilo wazo
But kama kweli unayaka kupiga pesa lima against msimu yaana lima kwa umwagiliaji
 
Kaka interest yangu ni tangawizi. Nipo Makambako ipo siku nitakuja hapo Igawa. Napenda kilimo sana. Mashamba yangu yapo Mambi Igurusi
Kwa mwenye somo la tangawizi tafadhali alishushe kwa thread yake
 
Mkuu naomba usinichoke kwa maswali yangu
Wanna knw ulikosea wp tofauti na unachokisema
Nyanya ulilima miez gani?
Kwanza uchaguzi wa mbegu bora ni muhimu sana,kwenye vitunguu niliuziwa mbegu fake.

Then kwa kilimo cha mazao yanayooza, kabla ya kulima jaribu kufanya survey ya maeneo yanayo-supply mazao hayo kama wamelima kwa kiasi gani. Mimi nilipata hasara kutokana na msimu niliolima nyanya watu wengi sana walilima zao hilo kiasi kwamba mtu anataka debe moja kwa 1500 tena kwa mkopo.

So,sio kama ina msimu maalum ya kulima nyanya ila wewe ukishakabidhiwa shamba ndo utaamua unalima vitunguu,nyanya,hoho,mahindi au viazi.

Mfano kulima vitunguu kuanzia mwezi January ni gharama na wengi hawalimi miezi hiyo kiasi kwamba April na mwezi May mwanzoni bei kwa gunia la kilo 100 inafika 150,000/= hadi 200,000/= but ikifika mwezi March wengi wanapanda na kivuna mwezi June na kupelekea bei kuwa Tsh.30,000/= hadi 50,000/=.

Kwa hiyo unaona kabisa bei inashushwa na wingi wa bidhaa. Hivyo ukifanya timing nzuri unapiga faida kubwa sana ila ukibugi ndo madhara unayapata hasa kwa nyanya ambayo huwa inaharibika kwa kuoza isipochumwa mapema.

Hope umenipata kidogo!
 
Mi ningekushauri kulima against msimu ili kupata faida kubwa
Kwa ushauri na experience za watu humu utafanikiwa mkuu
Kilimo kinalipa sana
Yap! Ni kweli ila sometime huku nilipo challenge ya maji ni kubwa sana,so ndo maana nataka niangalie Morogoro
 
Asante sana kwa ushauri. Nitafanya majaribio kwanza. Nitapanda kasehemu kadogo nione inakuwaje. Nitapanda katika ka green house kadogo.
 
Jamani watanzania ifike mahali tuache maneno mengi tufanye kazi....mimi kwasasa niko shambani niko nalima japo kwasasa nimejikita kwenye kilimo cha hoho ila mwaka huu nalima tangawizi pia....rai yangu kwa yeyote anayetaka kujifunza aje hapa IGAWA - MBEYA atajifunza mengi sana kuhusu kilimo cha umwagiliaji....hapa watu wanalima sana vitunguu(maji)...japo sijaona mkulima mzuri wa vitunguu swaumu....lakini pia hapa maji yapo mwaka mzima.

karibuni sana tulime kisasa....kilimo kinalipa sana...atakaye taka kuja igawa kujifunza nitampa ushirikiano wa hali ya juu with maximum care and security

Kiongozi naomba kuja kujifunza ninasoko kubwa la mazao kwa mawasiliano zaidi ntmgenesis@yahoo.com ili tupeane contacts.
 
  • Thanks
Reactions: 365
Haya mazao mawili; kitunguu saumu na tangawizi kiukweli ukimudu kupata mtaji ukalima na kuhudumia vizuri basi umasikini byebye!!

Jiulize tu mbegu ya kupanda ekari1 ya tangawizi ni karibu gunia10: wakati kilo1 cha tangawizi ni sh5000 shambani!!! kadharika Kwa saumu mambo ni yaleyale ngoma ipo kwenye gharama ya mbegu!!

Maadam shamba lenye chanzo cha maji ninalo ngoja nijikongoje kupata mtaji.

Inachosha sana tangawiz kama mgomba vile, kutoka kupanda mpka kuvuna karibu miez tisa.
 
Back
Top Bottom