Kumbe kitunguu saumu kinalipa hivi

nasikia gunia la kitunguu saumu la debe tano linauzwa 500,000!

hiki kitunguu hakina mbegu hivyo unapanda vile vipande vyake. wanasema ekari moja inaweza kupanda gunia 16 hadi 28 za kilo mia kutegemeana na spacing. hivyo utapanda vya Tsh 8m-14m. kinaweza kuzaa mara 5 hadi 8 ya gunia ulizopanda.

wengi wanasema ni wastani wa gunia 75 kwa ekari. ambazo zinakupa milioni 37.5. inasemekana sehemu yenye kitunguu maji na saumu hustawi. naomba wakulima wenye uzoefu huko babati mje mtupe uzoefu wa shambani.


asante kwa kushare
 
Jamani Watanzania ifike mahali tuache maneno mengi tufanye kazi. Mimi kwa sasa niko shambani niko nalima japo kwa sasa nimejikita kwenye kilimo cha hoho ila mwaka huu nalima tangawizi pia. Rai yangu kwa yeyote anayetaka kujifunza aje hapa IGAWA - MBEYA atajifunza mengi sana kuhusu kilimo cha umwagiliaji. Hapa watu wanalima sana vitunguu (maji) japo sijaona mkulima mzuri wa vitunguu swaumu, lakini pia hapa maji yapo mwaka mzima.

Karibuni sana tulime kisasa. Kilimo kinalipa sana, atakayetaka kuja Igawa kujifunza nitampa ushirikiano wa hali ya juu with maximum care and security.
 
Jamani watanzania ifike mahali tuache maneno mengi tufanye kazi....mimi kwasasa niko shambani niko nalima japo kwasasa nimejikita kwenye kilimo cha hoho ila mwaka huu nalima tangawizi pia....rai yangu kwa yeyote anayetaka kujifunza aje hapa IGAWA - MBEYA atajifunza mengi sana kuhusu kilimo cha umwagiliaji....hapa watu wanalima sana vitunguu(maji)...japo sijaona mkulima mzuri wa vitunguu swaumu....lakini pia hapa maji yapo mwaka mzima.

karibuni sana tulime kisasa....kilimo kinalipa sana...atakaye taka kuja igawa kujifunza nitampa ushirikiano wa hali ya juu with maximum care and security
kweli kabisa mkuu. hoho return yake ikoje kwa ekari? ukitaka kujifunza ndizi kwa umwagiliaji nitembelee hapo Igurusi.
 
kweli kabisa mkuu. hoho return yake ikoje kwa ekari? ukitaka kujifunza ndizi kwa umwagiliaji nitembelee hapo Igurusi.
Red giant hoho inalipa sana endapo utaweza kutunza shamba vizuri ukavuna kwa muda wa miezi 10...heka moja lazima zifike 10m.

halafu nitashuka hapo igulusi nipate hiyo elimu kilimo cha ndizi kwa umwagiliaji....
 
igurusi ni morogoro?
kitunguu saumu moro kitastawi?
mbegu au miche nanunua wapi?
Igurusi ipo mMarali Mbeya. kitunguu swaumu kinahitaji baridi baridi. labda mwezi wa sita kinaweza stawi maeneo ya juu. mbegu unanunua vizima na kupanda vipande vyake. China ndiyo nchi inaongoza kwa kulima vitunguu swaumu. So kama una mtaji mkubwa na muda naamini huko itakuwa cheap kufuata mbegu. Cheki na hiyo pdf ya wa south nimeattach hapo juu, ina mawili matatu.
 
Red giant hoho inalipa sana endapo utaweza kutunza shamba vizuri ukavuna kwa muda wa miezi 10...heka moja lazima zifike 10m.

halafu nitashuka hapo igulusi nipate hiyo elimu kilimo cha ndizi kwa umwagiliaji....
input kwa one acre inaweza fika Tsh ngapi?
 
kama ni fresh farmer inaweza kua 2M..ila kama ni mkulima tayari ni one milion inatosha....sababu vitu kama waterpumb..mabomba ya dawa...na zana nyingine utakuanazo
shukrani kwa taarifa mkuu. mwaka huu inabidi nilime.naona huwa haungii sana humu, naomba uni pm namba yako nami ntakupm yangu.
 
Back
Top Bottom