Kumbe Kitunguu Saumu kinalipa hivi

Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
9,544
Points
2,000
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
9,544 2,000
KWANGO CHA MBEGU
Kupanda heka moja zinaitajika kilo 200 hadi 300

MAVUNO
Mavuno ni kati ya tani 5 hadi 6 kwa heka moja.

SOKO
Sokoni Kariakoo bei ni kati ya shilingi 4000 hadi 7000 kwa kilo kutegemea msimu ulivyo.
Kwa ujumla ni bidhaa inayohitajika sana nchini na nje ya nchi.
Mbegu zinapatikana wapi hasa?
 
I

Inno mrosso

New Member
Joined
Apr 12, 2018
Messages
3
Points
20
I

Inno mrosso

New Member
Joined Apr 12, 2018
3 20
Jamani watanzania ifike mahali tuache maneno mengi tufanye kazi....mimi kwasasa niko shambani niko nalima japo kwasasa nimejikita kwenye kilimo cha hoho ila mwaka huu nalima tangawizi pia....rai yangu kwa yeyote anayetaka kujifunza aje hapa IGAWA - MBEYA atajifunza mengi sana kuhusu kilimo cha umwagiliaji....hapa watu wanalima sana vitunguu(maji)...japo sijaona mkulima mzuri wa vitunguu swaumu....lakini pia hapa maji yapo mwaka mzima.

karibuni sana tulime kisasa....kilimo kinalipa sana...atakaye taka kuja igawa kujifunza nitampa ushirikiano wa hali ya juu with maximum care and security

M

mapenz matam

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Messages
213
Points
250
M

mapenz matam

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2012
213 250
Haya wakuu naomba mniulize sasa mnataka nini katika hiki kilimo cha vitunguu saumu. Nimeingia field nimelima na nimejionea mengi sana. Ama kweli usisikie ya watu bora uingie front mwenyewe
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Messages
40,452
Points
2,000
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2014
40,452 2,000
Haya wakuu naomba mniulize sasa mnataka nini katika hiki kilimo cha vitunguu saumu. Nimeingia field nimelima na nimejionea mengi sana. Ama kweli usisikie ya watu bora uingie front mwenyewe
Vp soko lake?ulikutana na changamoto yoyote kwenye kuuza

Ova
 
Mushi92

Mushi92

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Messages
3,927
Points
2,000
Mushi92

Mushi92

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2013
3,927 2,000
mkuu Red Giant haya mazao mawili; kitunguu saumu na tangawizi kiukweli ukimudu kupata mtaji ukalima na kuhudumia vizuri basi umasikini byebye!!
jiulize tu mbegu ya kupanda ekari1 ya tangawizi ni karibu gunia10: wakati kilo1 cha tangawizi ni sh5000 shambani!!! kadharika Kwa saumu mambo ni yaleyale ngoma ipo kwenye gharama ya mbegu!!
Maadam shamba lenye chanzo cha maji ninalo ngoja nijikongoje kupata mtaji.
Mkuu bado tangawizi ina hiyo bei yq 5000 kwa kilo?
 
M

mapenz matam

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Messages
213
Points
250
M

mapenz matam

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2012
213 250
Vp soko lake?ulikutana na changamoto yoyote kwenye kuuza

Ova
Hapana kabisaa soko liko wazi wazi mkuu na nililimia Dodoma na vikakubali kabisaa na nikavuna vizuri saana na ni vitunguu ambavyo havina shida kabisaa jamani
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Messages
40,452
Points
2,000
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2014
40,452 2,000
Hapana kabisaa soko liko wazi wazi mkuu na nililimia Dodoma na vikakubali kabisaa na nikavuna vizuri saana na ni vitunguu ambavyo havina shida kabisaa jamani
Ok safi sana,uliwauzia watu gani madalali wa sokoni au

Ova
 
pendomamtefu

pendomamtefu

Senior Member
Joined
Jul 9, 2018
Messages
185
Points
250
pendomamtefu

pendomamtefu

Senior Member
Joined Jul 9, 2018
185 250
Haya wakuu naomba mniulize sasa mnataka nini katika hiki kilimo cha vitunguu saumu. Nimeingia field nimelima na nimejionea mengi sana. Ama kweli usisikie ya watu bora uingie front mwenyewe
hello mapenzi matamu, naomba nije pm kwako nipate mawasiliano yako tafadhali
 
TopUp

TopUp

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2017
Messages
2,554
Points
2,000
TopUp

TopUp

JF-Expert Member
Joined May 19, 2017
2,554 2,000
Haya wakuu naomba mniulize sasa mnataka nini katika hiki kilimo cha vitunguu saumu. Nimeingia field nimelima na nimejionea mengi sana. Ama kweli usisikie ya watu bora uingie front mwenyewe
Vip kuhusu gharama mkuu heka mojainakost kiasi gani cha mbegu na ni sh ngapi
Jibu tafadhali
 
M

mapenz matam

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Messages
213
Points
250
M

mapenz matam

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2012
213 250
Kitunguu saumu hakina gharama kaka. Gharama kubwa ni mbegu maana ili upande mbegu za vitunguu saumu ni vitunguu vyenyewe wakuu. sasa unakuta heka moja waweza tumia debe 5 au sita (tegemea na space yako utakayoamua) kingine ni mbolea hasa ya kuku japo wakati wa kupanda pandia DAP na weka mbolea ya kuku kisha jiandae na dawa ya ukungu (RIDOMIL GOLD NI NZURI SANA)
mwishoni vikiwa karibu kukomaa weka booster aina ya SUPER NEO HIGH K ili ku boost zile bulbs huko chini.
 
blogspot

blogspot

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2017
Messages
1,149
Points
2,000
blogspot

blogspot

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2017
1,149 2,000
Jamani watanzania ifike mahali tuache maneno mengi tufanye kazi....mimi kwasasa niko shambani niko nalima japo kwasasa nimejikita kwenye kilimo cha hoho ila mwaka huu nalima tangawizi pia....rai yangu kwa yeyote anayetaka kujifunza aje hapa IGAWA - MBEYA atajifunza mengi sana kuhusu kilimo cha umwagiliaji....hapa watu wanalima sana vitunguu(maji)...japo sijaona mkulima mzuri wa vitunguu swaumu....lakini pia hapa maji yapo mwaka mzima.

karibuni sana tulime kisasa....kilimo kinalipa sana...atakaye taka kuja igawa kujifunza nitampa ushirikiano wa hali ya juu with maximum care and security
Mkuu Tuwe na afya ipo siku nitafika hapo kwa sasa bado nakimbizana hapa SUA first year ila nampango wakulima huko mbeleni 4 acre Mkononi.
 
A

antimatter

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2017
Messages
1,866
Points
2,000
A

antimatter

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2017
1,866 2,000
Hv Rufiji au Kisarawe vitunguu saumu, tangawizi yanaweza kustawi?
 
mimi.mimi

mimi.mimi

Senior Member
Joined
Jul 11, 2013
Messages
135
Points
225
mimi.mimi

mimi.mimi

Senior Member
Joined Jul 11, 2013
135 225
[h=3]KILIMO CHA VITUNGUU TWAUMU - garlic[/h]
UDONGO
Vitunguu twaumu vinahimili aina nyingi za udongo, ila vinastawi zaidi katika udongo usiotuamisha maji kabisa na wenye mbolea asili, kama mbolea si ya kutosha kwenye udongo, tumia samadi iliyokwisha oza vizuri usitoe samadi bandani na kuipeleka shambani moja kwa moja kwenye shamba la vitunguu thwaumu, labda kama utaliacha shamba bila kulimwa kwa zaidi ya miezi 6, pia unaweza kutumia mbolea za viwandani kama ammonium nitrate, ammonium sulphate, urea n.k wakati wa kupanda na kila baada ya wiki 4 – 6 mara mbili zaidi

UPANDAJI
Kipindi kizuri kwa upandaji ni kipindi ambacho hakuna joto hasa miezi ya May mpaka August kwa Tanzania, Unachukua kitunguu twaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 10 na kati ya mistari ni sentimeta 30. Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kungolewa kabisa. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu thwaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu.

UMWAGILIAJI

Kama kuna upungufu wa mvua au ni kipindi cha kiangazi basi ni vizuri ukamwagilia shamba lako, wakati mzuri wa kumwagilia vitunguu twaumu ni asubuhi na sio jioni au mchana, hii inasaidia vitunguu twaumu kujijengea uwezo wa kupambana na magonjwa, baada ya mizi miwili unaweza kupunguza umwagiliajai huku ukiangalia kwa kuchimba kidogo kama vitunguu twaumu vimezaliana vya kutosha na kuanza kukomaa, ukiona vimekomaa acha kabisa kumwagilia ili visioze

UANGALIZI
Aina nyingi za vitunguu twaumu vitakuwa kama vinatoa mbegu kwenye mmea (angalia picha chini), ingawa kuna nadharia nyingi lakini inashauriwa kukata hizi mbegu chini kabisa kwa kisu kikali na kisafi, usikate mapema mara baada ya kutokeza bali subiri mpaka mmea unapoanza kama kujikunja ndipo ukate, kwa wale wanaoacha mbegu hizi ukiamua kuzipanda kwa msimu wa kwanza zitazaa kitunguu kimoja tu cha duara lakini chenyewe ukikipanda tena kwenye mzunguko wa pili kitazaa vitunguu vingi kama kawaidaUngoleaji wa magugu na majani ni muhimu muda wote ili kuondoa kugombea rutuba, hewa na maji shambani, kwa wenye mashamba makubwa wanaweza kutumia dawa za kemikali kama ROUNDUP na nyinginezo ili kudhibiti magugu, ingawa mimi sishauri hivyo.

MAGONJWA
Magonjwa kama botrytis (kuoza shingo) blue mould na fusarium (kuoza kwa vitunguu) husababisha hasara kubwa kama hayatadhibitiwa kwa kutumia viuatilifu mara unapoona dalili, pia magonjwa kama white rot huchukua zaidi ya miaka 20 kuondoka kama yatavamia shamba lako, inashauriwa kufanya mabadiliko ya zao kila baada ya miaka mitano kwa kupanda mazao mengine yasiyo jamii moja kama vitunguu maji, unaweza kupanda maharage, mahindi, karoti na kabichi katika mzunguko huo. Pia magonjwa kama kutu ya majani husababisha na unyevu mwingi hasa kama mimea itakuwa kwenye udongo unaotuamisha maji au mimea kumwagiliwa jioni au usiku, kumbuka kumwagilia asubuhi tu Ili kudhibiti ugonjwa huu wa kutu mimea ingolewe na ichomwe au utumie viuatilifu vya kuulia fangasi wa mimea.
Asante kinachukua mda wa miez mingap mpaka kuiva shamban/ kuvunwa
 
Forum statistics

Threads 1,315,048
Members 505,132
Posts 31,846,361
Top