Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…

Unamuongelea Lissu ambae baada ya madhila ameikimbia Nchi? Mbowe nae yupo kama hayupo amedhulumiwa mabilion ya pesa zake lakini aliufyata amekuja kusema juzi wakati Magufuli ameshafariki dunia

Hata huyo Mayalla hoja za kichokonozi alikuwa anatoa lakini zile nondo kali alipumzika kidogo
Kuwa na akili kidogo, Mbowe hana bunduki wala silaha yoyote, silaha yake ni mdomo. OVer
 
Asije tu akakurupuka kuwaachia kiholela watuhumiwa kweli kwa kupenyezewa rupia,wananchi hatutokubali kamwe,na mazingira ya rushwa pia lazima yaangaliwe ktk kuwatoa hao watuhumiwa
 
Kwani wewe mbele ya habinda Seth sio mnyonge?mbele ya papa msofe sio mnyonge?hawawezi wakakuweka ndani bila hata kosa na ukaozea jera.Hawawezi wakaja kujenga kwenye kiwanja chako na na hati unayo wala usiwafanye kitu?sasa kwanini usiwe mnyonge
Mnyonge ni wew na familia yako na watu wenye mawazo kama hako, mimi siyo mnyonge na siwezi kuja kuwa mnyonge kamwe. But no offense intended.
 
View attachment 1825109

Wanabodi,
Naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", nikiangazia suala zima za utoaji haki nchini, ambapo makala hii ni muendelezo wa ushauri kwa DPP, ulioanza wiki iliyopita.

Wanasheria wana vimisemo vyao vingi vingi vya kisheria, vingi viko kwenye lugha ya Kilatini, na kutafsiriwa kwa Kiingereza kisha Kiswahili, mmoja wa msemo maarufu sana kuhusu haki, unasema "Justice must not only be done, must be seen to be done", kumaanisha "Haki sio tuu ni lazima itendeke, bali pia ionekane inatendeka". Kwa muda wa mwezi mmoja sasa, wiki nne mfululizo, nimekuwa nikiandika makala za "Kilio cha Haki" nikijiekeza ofisi ya DPP, hatimaye sasa kuna kitu kinatendwa na kinaonekana.

Unapoandika makala kulalamikia jambo fulani, na kutoa ushauri wa nini kifanyike, halafu ikatokea hicho ulichashauri kikafanyika, kama ulivyoshauri, hatua ya kwanza ni kutoa pongezi, kwa hicho kilichofanyika, hivyo makala ya leo, naianza kwa kumpongeza DPP, ametenda!. Kumbe Kutenda haki kunawezekana, hongera sana DPP mpya kwa kuianza kazi yako vizuri, sasa sio tuu haki inatendeka, bali pia inaonekana kutendeka, hivyo kazi hii nzuri na iendelee, na sio kusubiri tena hadi Mama aseme!.

Sasa naendelea na ule ushauri wa DPP, wiki iliyopita niliishia number 6, leo naendelea.
  1. Kuna watuhumiwa wako mahabusu kwa makosa yanayodhaminika, bali DPP ameiamuru mahakama kuzuia dhamana zao. Hapa kuna mambo 3.Moja ni masuala ya weledi, haki na uwajibikaji wakati wa kutekeleza mamlaka kwa mujibu wa kifungu hiki. Mbili ni uhalali wa kifungu hiki kikatiba ambacho kwa kweli hakitoi uwajibikaji kabisa ndio maana kilifutwa kwenye CPA baada ya mahakama kujiridhisha kifungu hiki kinakwenda kinyume cha katiba, kisheria, mahakama ikiishatoa amri, sharia fulani au kifungu fulani kiko kinyume cha katiba, na kifungu hicho kifute, kifungu hicho kinakuwa “null and void ab initio”, yaani hakukuwahi kuwepo,
  2. Lakini kwenye kufutwa kwa kifungu hiki, kuna kitu cha ajabu kimetokea, wakati kifungu hiki kimefutwa na mahakama kwa kuwa kinyume cha katiba kwenye CPA, kifungu hicho bado kipo kwenye EOCCA!. Hili ni jambo la ajabu sana!. Hapa naiomba Mahakama inatamka kifungu fulani kinakwenda kinyume cha katiba, na kuamuru kifutwe, kifungu hicho kifutwe kwenye sheria nyingine zote.
  3. Sasa tunaishi kwenye ulimwengu wa kidigitali, Tanzania na sisi tutumie nafuu za kidigitali, kwa kuanzisha “digital custody “ mahabusu za kidigitali na “digital cells”, jela za kidigitali, mtuhumiwa anazuiliwa nyumbani kwake, hata kutumikia kifungo akiwa nyumbani kwakwe kwa kufungiwa kifaa maalum cha GPS (tracking device), inayofungwa kwa lakiri ya kidigitali, na kuwa kuzuiwa nyumbani kwake, nyumba hiyo inafungwa kamera, maalum, (IP Camera) kama zile kamera za CCTV, hivyo polisi/magereza wanaona nyendo zote za mtuhumiwa, akivuka tuu ile IP camera, inapiga alarm, mtuhumiwa anakuwa amekiuka masharti hivyo kustahili kuzuiliwa mahabusu. Utaratibu huu unaruhusu mke anapata haki zake za ndoa, watoto wanapata mapenzi ya baba, na baba kuendelea na shughuli za kuingiza kipato cha kuendesha familia.
  4. Mahabusu ni mtuhumiwa tuu, anahesabika hana hatia hadi athibitishwe na mahakama, lakini mahabusu wetu, wanahesabiwa kama wafungwa, wananyimwa haki zao , mfano watuhumiwa wengi tuu ambao sio hatarishi wamefiwa na ndugu zao, wazazi wao, wapendwa wao au jamaa zao, bila kupewa haki ya kushiriki mazishi yao, akiwemo mwanafani mwenzetu Erick Kabendera, ambaye mama yake alitoa kilio chake mahali kuwa uhai wake unamtegemea mwanae. Mama huyo alipoteza maisha kwa sababu ya mwanae kushikiliwa mahabusu, na mwanae hakuruhusiwa kumzika. Sisi watu wa karma, tulitoa angalizo la karma ya huyu mama, wanaojua karma ilikuja kufanya nini, wanajua!. Mahabusu wa wenzetu, hata wana ndoa, wanaruhusiwa kupata haki zao, hata wawapo mahabusu au vifungoni,
  5. Mhabusu zetu ni mahali mahali hatarishi, na kutokana na umasikini wetu, hatuna magereza ya mahabusu (remand prison) na jela ya wahalifu, Mahabusu wetu, wanashikiliwa jela kama wafungwa. Wapo baadhi ya mahabusu wanafanyiwa vitendo vibaya au viovu wakiwa mahabusu na wapo ambao wamepata matatizo ya kiafya permanently kwa kurundikana mahabusu bila huduma za msingi ambapo wangeweza kujihudumia wenyewe wawapo nje. DPP/serikali inapata faida gani kuswekwa watu rumande na kuzuia dhamana?!.
  6. Japo hapa natetea haki za watuhumiwa , pia naomba pia kuzingatia haki za wahanga wa uhalifu. Katika ulimwengu wa uhalifu kuna watu wabaya kupita kipimo. Just imagine unakuta mtu mzima umembaka mtoto wa miaka 2 na kumharibu vibaya sehemu zake za siri na pengine akamwambukiza HIV, mauaji ya kutisha , vitendo vya vikundi vya kihalifu kama panya road na mapanga yao wanapokuingilia na kukucharanga mapanga bila huruma na kumbaka binti yako au mkeo mbele yako na visa vingine vingi. Hao ni ma “psychopath” wanastahi kukaa mahabusu kwasabu ni watu hatarishi, wasipate dhamana kwa vile wamepoteza sifa za haki yao kuwa huru.
  7. Ule utaratibu wa notification kwa makosa ya usalama barabarani, na kulipa faini za papo kwa papo, utumike pia kwenye vituo vya polisi, mwizi wa kuku akiri kuiba kuku, akubali kumlipa aliyemuibia na kulipa faini, kesi hiyo inaishia hapo hapo kituoni wala haina haja ya kufikishwa mahakamani.
  8. Majaji wetu, kwa ajili ya kusikiliza maombi ya dhamana, nao wanapaswa kufanya kazi kama vituo vya polisi, mahospitali na dharura nyingine kwa saa 24. Kama ilivyo kwa madaktari wa zamu anapigiwa simu kukitokea dharura, kuwe na majaji wazamu saa 24/7. Nimeshuhudia hii Afrika Kusini, kila mtuhumiwa anapelekwa kwa hakimu wakati wowote hadi usiku wa manane, kama vile madaktari au vituo vya polisi.
  9. Mwisho, Mheshimiwa sana, DPP wetu mpya, hongera kwa uteuzi wako mpya, Watanzania tunamatumaini makubwa sana na Rais wetu Mama Samia katika nia yake ya dhati kutaka Watanzania watendewe haki, na Mama Samia, amekuaminia wewe kuongoza na ofisi hii muhimu sana, ya DPP, timiza wajibu wako kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, kama ulivyoanza, Taifa litaponywa, kwa haki sio tuu kwa haki kutendeka, bali pia kwa haki kuonekana imetendeka.
Mungu Ibariki Tanzania.

Baada ya kumalizana na DPP, ungana nami wiki ijayo tukianzana na Jaji Mkuu na Mfumo mzima wa Mahakama katika utoaji haki. .

Paskali.
Rejea za Mfululizo huu wa makala za DPP
View attachment 1825142
View attachment 1825139
View attachment 1825143
Nitapingana na wote wanaokutakia upate TEUZI..! Maana wanataka madini kama haya tusiyapate tena. Uzoefu unaonesha teuzi zinawapoteza watu mf. Bashe
 
View attachment 1825109

Wanabodi,

Wanasheria wana vimisemo vyao vingi vingi vya kisheria, vingi viko kwenye lugha ya Kilatini, na kutafsiriwa kwa Kiingereza kisha Kiswahili, mmoja wa msemo maarufu sana kuhusu haki, unasema "Justice must not only be done, must be seen to be done", kumaanisha "Haki sio tuu ni lazima itendeke, bali pia ionekane inatendeka".

Paskali.]
Leo ndio leo, jee haki itatendeka na kuonekana imetendeka ama...
Let's wait and see,
Ushauri wangu ni lets hope for the best kuwa ama DPP ataibuka na Nolle, ama Mahakama itatamka "there is no case to answer" but also let's get prepared for the worst mtu wetu akakutwa kweli ni gaidi hivyo ana kesi ya kujibu!.
Tusubirie...
P
 
View attachment 1825109

Paskali.
Rejea za Mfululizo huu wa makala za DPP
View attachment 1825142
View attachment 1825139
View attachment 1825143
Hili jambo, tumelipigia Sana kelele, tumepandisha ma thread na mathreads, makala na makala hatimaye Leo kimefanyika kitu.

wa kilichofanyika leo, Ile Nolle ya Mbowe, hongera Sana DPP, utabarikiwa, aliyekutuma atabarikiwa, Tanzania tutabarikiwa. Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana na haki ikaonekana imetendeka.

Mungu ibariki Tanzania,
Pasco
 
Paskali walibana wee wAmeachia!!
 
Umweke mtu mahabusu kwa miezi 8 bila ushahidi madhubuti kumbe anajua wazi akijisikia tu anamwachia!! Ukatili kiasi gani huu?
 
View attachment 1825109

Wanabodi,
Naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", nikiangazia suala zima za utoaji haki nchini, ambapo makala hii ni muendelezo wa ushauri kwa DPP, ulioanza wiki iliyopita.

Wanasheria wana vimisemo vyao vingi vingi vya kisheria, vingi viko kwenye lugha ya Kilatini, na kutafsiriwa kwa Kiingereza kisha Kiswahili, mmoja wa msemo maarufu sana kuhusu haki, unasema "Justice must not only be done, must be seen to be done", kumaanisha "Haki sio tuu ni lazima itendeke, bali pia ionekane inatendeka". Kwa muda wa mwezi mmoja sasa, wiki nne mfululizo, nimekuwa nikiandika makala za "Kilio cha Haki" nikijiekeza ofisi ya DPP, hatimaye sasa kuna kitu kinatendwa na kinaonekana.

Unapoandika makala kulalamikia jambo fulani, na kutoa ushauri wa nini kifanyike, halafu ikatokea hicho ulichashauri kikafanyika, kama ulivyoshauri, hatua ya kwanza ni kutoa pongezi, kwa hicho kilichofanyika, hivyo makala ya leo, naianza kwa kumpongeza DPP, ametenda!. Kumbe Kutenda haki kunawezekana, hongera sana DPP mpya kwa kuianza kazi yako vizuri, sasa sio tuu haki inatendeka, bali pia inaonekana kutendeka, hivyo kazi hii nzuri na iendelee, na sio kusubiri tena hadi Mama aseme!.

Sasa naendelea na ule ushauri wa DPP, wiki iliyopita niliishia number 6, leo naendelea.
  1. Kuna watuhumiwa wako mahabusu kwa makosa yanayodhaminika, bali DPP ameiamuru mahakama kuzuia dhamana zao. Hapa kuna mambo 3.Moja ni masuala ya weledi, haki na uwajibikaji wakati wa kutekeleza mamlaka kwa mujibu wa kifungu hiki. Mbili ni uhalali wa kifungu hiki kikatiba ambacho kwa kweli hakitoi uwajibikaji kabisa ndio maana kilifutwa kwenye CPA baada ya mahakama kujiridhisha kifungu hiki kinakwenda kinyume cha katiba, kisheria, mahakama ikiishatoa amri, sharia fulani au kifungu fulani kiko kinyume cha katiba, na kifungu hicho kifute, kifungu hicho kinakuwa “null and void ab initio”, yaani hakukuwahi kuwepo,
  2. Lakini kwenye kufutwa kwa kifungu hiki, kuna kitu cha ajabu kimetokea, wakati kifungu hiki kimefutwa na mahakama kwa kuwa kinyume cha katiba kwenye CPA, kifungu hicho bado kipo kwenye EOCCA!. Hili ni jambo la ajabu sana!. Hapa naiomba Mahakama inatamka kifungu fulani kinakwenda kinyume cha katiba, na kuamuru kifutwe, kifungu hicho kifutwe kwenye sheria nyingine zote.
  3. Sasa tunaishi kwenye ulimwengu wa kidigitali, Tanzania na sisi tutumie nafuu za kidigitali, kwa kuanzisha “digital custody “ mahabusu za kidigitali na “digital cells”, jela za kidigitali, mtuhumiwa anazuiliwa nyumbani kwake, hata kutumikia kifungo akiwa nyumbani kwakwe kwa kufungiwa kifaa maalum cha GPS (tracking device), inayofungwa kwa lakiri ya kidigitali, na kuwa kuzuiwa nyumbani kwake, nyumba hiyo inafungwa kamera, maalum, (IP Camera) kama zile kamera za CCTV, hivyo polisi/magereza wanaona nyendo zote za mtuhumiwa, akivuka tuu ile IP camera, inapiga alarm, mtuhumiwa anakuwa amekiuka masharti hivyo kustahili kuzuiliwa mahabusu. Utaratibu huu unaruhusu mke anapata haki zake za ndoa, watoto wanapata mapenzi ya baba, na baba kuendelea na shughuli za kuingiza kipato cha kuendesha familia.
  4. Mahabusu ni mtuhumiwa tuu, anahesabika hana hatia hadi athibitishwe na mahakama, lakini mahabusu wetu, wanahesabiwa kama wafungwa, wananyimwa haki zao , mfano watuhumiwa wengi tuu ambao sio hatarishi wamefiwa na ndugu zao, wazazi wao, wapendwa wao au jamaa zao, bila kupewa haki ya kushiriki mazishi yao, akiwemo mwanafani mwenzetu Erick Kabendera, ambaye mama yake alitoa kilio chake mahali kuwa uhai wake unamtegemea mwanae. Mama huyo alipoteza maisha kwa sababu ya mwanae kushikiliwa mahabusu, na mwanae hakuruhusiwa kumzika. Sisi watu wa karma, tulitoa angalizo la karma ya huyu mama, wanaojua karma ilikuja kufanya nini, wanajua!. Mahabusu wa wenzetu, hata wana ndoa, wanaruhusiwa kupata haki zao, hata wawapo mahabusu au vifungoni,
  5. Mhabusu zetu ni mahali mahali hatarishi, na kutokana na umasikini wetu, hatuna magereza ya mahabusu (remand prison) na jela ya wahalifu, Mahabusu wetu, wanashikiliwa jela kama wafungwa. Wapo baadhi ya mahabusu wanafanyiwa vitendo vibaya au viovu wakiwa mahabusu na wapo ambao wamepata matatizo ya kiafya permanently kwa kurundikana mahabusu bila huduma za msingi ambapo wangeweza kujihudumia wenyewe wawapo nje. DPP/serikali inapata faida gani kuswekwa watu rumande na kuzuia dhamana?!.
  6. Japo hapa natetea haki za watuhumiwa , pia naomba pia kuzingatia haki za wahanga wa uhalifu. Katika ulimwengu wa uhalifu kuna watu wabaya kupita kipimo. Just imagine unakuta mtu mzima umembaka mtoto wa miaka 2 na kumharibu vibaya sehemu zake za siri na pengine akamwambukiza HIV, mauaji ya kutisha , vitendo vya vikundi vya kihalifu kama panya road na mapanga yao wanapokuingilia na kukucharanga mapanga bila huruma na kumbaka binti yako au mkeo mbele yako na visa vingine vingi. Hao ni ma “psychopath” wanastahi kukaa mahabusu kwasabu ni watu hatarishi, wasipate dhamana kwa vile wamepoteza sifa za haki yao kuwa huru.
  7. Ule utaratibu wa notification kwa makosa ya usalama barabarani, na kulipa faini za papo kwa papo, utumike pia kwenye vituo vya polisi, mwizi wa kuku akiri kuiba kuku, akubali kumlipa aliyemuibia na kulipa faini, kesi hiyo inaishia hapo hapo kituoni wala haina haja ya kufikishwa mahakamani.
  8. Majaji wetu, kwa ajili ya kusikiliza maombi ya dhamana, nao wanapaswa kufanya kazi kama vituo vya polisi, mahospitali na dharura nyingine kwa saa 24. Kama ilivyo kwa madaktari wa zamu anapigiwa simu kukitokea dharura, kuwe na majaji wazamu saa 24/7. Nimeshuhudia hii Afrika Kusini, kila mtuhumiwa anapelekwa kwa hakimu wakati wowote hadi usiku wa manane, kama vile madaktari au vituo vya polisi.
  9. Mwisho, Mheshimiwa sana, DPP wetu mpya, hongera kwa uteuzi wako mpya, Watanzania tunamatumaini makubwa sana na Rais wetu Mama Samia katika nia yake ya dhati kutaka Watanzania watendewe haki, na Mama Samia, amekuaminia wewe kuongoza na ofisi hii muhimu sana, ya DPP, timiza wajibu wako kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, kama ulivyoanza, Taifa litaponywa, kwa haki sio tuu kwa haki kutendeka, bali pia kwa haki kuonekana imetendeka.
Mungu Ibariki Tanzania.

Baada ya kumalizana na DPP, ungana nami wiki ijayo tukianzana na Jaji Mkuu na Mfumo mzima wa Mahakama katika utoaji haki. .

Paskali.
Rejea za Mfululizo huu wa makala za DPP
View attachment 1825142
View attachment 1825139
View attachment 1825143
Moja ya watu waliokwenye wimbi la mawazo ni jaji Tiganga ambaye alikuwa kwenye ndoto za kupanda cheo kupitia kesi ya mbowe kama mwenzake alivyopata mseleleko kucheza dili na maccm kunahitaji umakini hawaeleweki wao punda afe mzigo ufike!!
1646128894798.jpg
 
View attachment 1825109

Wanabodi,
Naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", nikiangazia suala zima za utoaji haki nchini, ambapo makala hii ni muendelezo wa ushauri kwa DPP, ulioanza wiki iliyopita.

Wanasheria wana vimisemo vyao vingi vingi vya kisheria, vingi viko kwenye lugha ya Kilatini, na kutafsiriwa kwa Kiingereza kisha Kiswahili, mmoja wa msemo maarufu sana kuhusu haki, unasema "Justice must not only be done, must be seen to be done", kumaanisha "Haki sio tuu ni lazima itendeke, bali pia ionekane inatendeka". Kwa muda wa mwezi mmoja sasa, wiki nne mfululizo, nimekuwa nikiandika makala za "Kilio cha Haki" nikijiekeza ofisi ya DPP, hatimaye sasa kuna kitu kinatendwa na kinaonekana.

Unapoandika makala kulalamikia jambo fulani, na kutoa ushauri wa nini kifanyike, halafu ikatokea hicho ulichashauri kikafanyika, kama ulivyoshauri, hatua ya kwanza ni kutoa pongezi, kwa hicho kilichofanyika, hivyo makala ya leo, naianza kwa kumpongeza DPP, ametenda!. Kumbe Kutenda haki kunawezekana, hongera sana DPP mpya kwa kuianza kazi yako vizuri, sasa sio tuu haki inatendeka, bali pia inaonekana kutendeka, hivyo kazi hii nzuri na iendelee, na sio kusubiri tena hadi Mama aseme!.
Hii ndio Taarifa mpya ya leo ya Gazeti la Raia Mwema , Kwamba kutokana na kuvuja kwa Taarifa nyingi kuhusu unyama uliotendwa kwenye kilichoitwa Plea Bargain , iliyosimamiwa kikamilifu na DPP wa wakati ule aliyeitwa Biswalo Mganga Wadau wamemkumbusha Mh Rais kuhusu Makando kando ya Mtu huyo na kumuomba Amng'oe haraka.

Ngoja tusubiri majibu ya barua hiyo .

Chanzo : Raia Mwema
Watu wanasubirì hadi madudu yafukunyuliwe ndipo waseme!, sisi tulioyaona yakifanyika, tulipigia kelele na haikusaidia kitu!, sijui kama hiyo barua itasaidia kitu maana post aliyopo sasa has a security of tenure, anaweza kuteuliwa tuu, hawezi kutenguliwa!, na post iliyotangulia ya DPP ina kinga ya kutohojiwa na yeyote au kushitakiwa!.
Huku ni kutwanga tuu maji kwenye kinu!.
P
 
2. Heshimi Haki za binadamu ambazo zimeainishwa kwenye Katiba. Kuna uvunjifu wa haki za binadamu mdogo mdogo
Kwenye eneo hili la haki za binaadamu, Mama Samia, apewe kongole sana, huyu ni mpenda haki, muwaza haki, msema haki, mtenda haki.
Ameonyesha kwa kauli na matendo!.
Mifano iko mingi tuu ya kumwaga hapa nakupa mifano mitano tuu!, ukitaka 10, nakupa, ukitaka 20 nakupa
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
Kwenye eneo la haki, so far Rais Samia ameisha onyesha kwa kauli na matendo, is the best of the best... ila sasa kwa kwa kadri siku zinavyokwenda, naona kama na yeye anaanza... itaendelea!, nitamalizia ...

Watu wengi tu majalada yetu yamekwama kwenda Mahakamani kisa Office ya DPP inachagua pande badala ya haki mradi tu una pesa za kumtuliza DPP!!!! Kuna Jamaa Kaka na file langu la Jinai pale Dodoma kwa DPP huu Mwaka wa pili,na ananipiga sound tu eti tunalifanyia kazi kumbe wamesha malizana na mtuhumiwa kwa mlungulaa na mi wameniacha kwenye mataaa!!
 
Lakini poa tu Karma itafanya kazi yake!!!
 
1. Huyu DPP miaka yote walikuwa wapi?
2. Leo ndio wameona watu wanaonewa?
Bora angekaa kimya kama ambavyo wamekuwa kimya sie huwa tunalia kwa Mola wetu ambae ndie hakimu wa haki.
 
TOKA MAKTABA :

6 February 2020

Mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli, rais wa TLS atoa nondo kali:

Mfumo wa sheria za jinai ulioko sasa nchini Tanzania , hauna tofauti na sheria za kikoloni, zilizotumika kutia hofu wananchi ili watii amri za kikoloni bila kuhoji.

Kauli hiyo imetolewa na Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo tarehe 6 Februari 2020, jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini.

Dk. Rugemeleza Nshala ameishauri serikali ya Rais John Magufuli kufanya mabadiliko ya sheria katika mfumo Haki Jinai, ili kuondoa sheria kandamizi zinazonyima watuhumiwa dhamana.

18 September 2021
Dr. Rugemeleza A.K Nshala, rais mstaafu wa Tanganyika Law Society TLS amesema mfumo wa Jinai Haki ( Criminal Justice System) wa nchini Tanzania unahitaji mabadiliko makubwa kwa kufumuliwa na uundwe upya ili kulinda haki za raia na watu .

Azungumzia mazito kuhusu

  • Nolle prosequi / kufutiwa mashtaka bila kuelezwa sababu za msingi zaidi ya ofisi ya DPP kusema imeamua kutoendelea na mashtaka
  • Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP
  • Makubaliano kati ya raia na kitu kinachotisha kikubwa yaani raia asiishitaki serikali akiachiwa pia asidai fidia
  • Marekebisho ya sheria yanahitajika ili mahakama iweze kusikiliza haki ya dhamana na ikiwa inafaa mahakama ipewe mamlaka ya kumuachia mtuhumiwa wakati Polisi na waendesha mashtaka wakiwa wanaendelea kusaka ushahidi
  • Watuhumiwa wengi wanaozea ndani ya mahabusu gerezani kwa muda mrefu wakati inadaiwa vyombo vinaendelea na upelelezi
  • Mtuhumiwa siyo mhalifu mpaka hapo atakapo pata haki yake kwa kuhukumiwa na Mahakama.
  • Hii ya mtuhumiwa kuhukumiwa na Polisi, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka au kiongozi yeyote ni uvunjifu wa haki za raia na katiba.
  • Wenye jukumu la kurekebisha mfumo huu Jinai Haki, ni serikali iliyopo madarakani kwa kutumia wataalamu wake na bahati kuna wasomi bobezi waliopo ofisini , ni kama Mwanasheria Mkuu Jaji Dr. Feleshi, Waziri wa Sheria Prof. Palamagamba na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Wadau wengine kama TLS, Kituo cha Haki za Binadamu, Vyombo vya Habari na wananchi ni kupaza sauti na kupigia kelele mfumo huu mbovu wa Haki Jinai uliopo sasa hivi.
  • Polisi hawawezi kulaumiwa, wao Polisi hawana jukumu lolote bali kupiga saluti na kutekeleza amri na sheria hii mbovu inayoendesha Mfumo Haki Jamii ( Criminal Justice System) kama wanavyoelekezwa na viongozi wanaowaongoza jeshini na wanasiasa serikalini.
  • Watanzania tuamke toka dhamira zetu zilizo mfu, tupiganie haki hii wote kabisa bila kujali vyeo vyetu, vyama vya kisiasa, itikadi n.k

Rugemeleza Nshala, holds Doctor of Juridical Studies (S.J.D) from the Ivy league Harvard Law School. He holds a Bachelors of Laws Degree (LL.B) from the University of Dar es Salaam, Tanzania (his home country), which he obtained in 1993; the Masters of Laws Degree (LL.M) from Harvard Law School and Masters of Environmental Management (MEM) from Yale School of Forestry and Environmental Studies that he obtained in 1997 and 2007, respectively. Source : Harvard African Development Conference

Haki Jinai / Criminal Justice System

SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA MFUMO WA HAKI JINAI​

Imewekwa: Wednesday 15, June 2022

SERIKALI YAJIPANGA KUBORESHA MFUMO WA HAKI JINAI
View attachment 2471512
Serikali imejipanga kuboresha Mfumo wa Haki Jinai nchini kwa kubaini changamoto na kupendekeza maboresho katika mnyororo mzima wa haki jinai. Hayo yamebainishwa katika Kikao kazi kilichoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Wadau wa Haki jinai nchini. Kikao kazi hicho cha siku tano kimefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu leo tarehe 13 Juni, 2022 Jijini Dodoma.

Dkt. Kazungu amewataka Wadau wa haki jinai kujadili changamoto zinazoukabili mnyororo mzima wa haki jinai na kupendekeza namna bora ya kuboresha mfumo huo ili kujenga mfumo madhubuti wa sheria unaoaminika na jamii katika utoaji haki.

Maoni yatakayotolewa katika kikao kazi hiki yatatumika kuboresha Andiko la Mapendekezo ya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai Nchini kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 hadi 2026/27.

Aidha, Dkt. Kazungu amesema mabadiliko ya mfumo wa haki jinai yamekuja wakati muafaka kwani hayo yamekuwa moja ya maono ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro tangu alipoteuliwa kuongoza Wizara hiyo

Source : https://www.sheria.go.tz/news/serikali-yajipanga-kuboresha-mfumo-wa-haki-jinai

Mkuu bagamoyo, asante kwa hii post, kwa ruhusa yako, naomba kuitumia kama mbolea kuboreshea baadhi ya mabandiko yangu ya kilio cha haki.

Natanguliza shukrani.

Paskali
 
Back
Top Bottom