Ujumbe kwa DPP juu ya kumfutia Kesi ya Jina Pauline Gekul

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mosi, hili shauri limefunguliwa chini ya Kifungu 128(2) cha CPA na mshtaki binafsi (private prosecutor), ambapo utaratibu huu sheria inamtaka Hakimu kwanza AJIRIDHISHE kuna ushahidi wa kutosha kabla ya kuanzisha mashtaka. Hakimu alifanya hivyo na akakubali kuanzishwa kwa mashtaka kwa sababu aliona kuna ushahidi mbele yake.

Pili, kama kusingekuwa na ushahidi, kifungu cha 129 cha CPA kinampa Hakimu MAMLAKA ya kufuta kesi pale atakapojiridhisha kuwa MALALAMIKO & USHAHIDI ulioletwa mbele yake haufichui kosa dhidi ya mtuhumiwa, na Hakimu hutakiwa kuandika sababu ya kufuta kesi na mtuhumiwa huachiwa huru.

Kwakuwa Hakimu alikubali kuanzisha mashtaka, maana yake ALIJIRIDHISHA pasipo shaka kwamba kuna ushahidi wa kutosha. Vinginevyo angetupilia mbali hii kesi kupitia kifungu tajwa hapo juu; s129.

Jambo jingine katika hili, japo DPP ana mamlaka ya kufuta kesi kwa NOLLE PROSEQUI, kwa mtazamo wangu katika kesi hii DPP AMEZUIA haki kutendeka. Labda angeacha tusikilize ushahidi wa pande zote kwanza kabla ya kuondoa kesi. Au hata ushahidi wa pande moja kama ilivyokuwa kwenye "kesi ya Mbowe".

Ndio, sheria inampa DPP MAMLAKA ya kuondoa kesi pasipo kutoa sababu, lakini pia sheria HAIJAMKATAZA kutoa sababu (hili la msingi kuzingatiwa). Ushauri wangu, kwa kuzingatia maslahi ya umma, uwekwe utaratibu wa DPP kueleza sababu za kufuta kesi katika kesi zenye MASLAHI KWA UMMA au kesi yoyote yenye kufuatiliwa kwa ukaribu na kundi kubwa ndani ya Jamii. Hii itaondoa SINTOFAHAMU.

Jambo lingine, DPP anasema anasubiri ushahidi! Lakini, tayari alituambia amepokea jalada la mashtaka toka Polisi. Kama ushahidi hautoshi angesema!

UTARATIBU WA KUFUNGUA MASHTAKA KUPITIA DPP.

Hatua ya awali Jeshi la Polisi hufanya uchunguzi ikiwemo kuhoji pande zote mbili; mlalamikaji & mlalamikiwa. Polisi ikijiridhisha kuna chembe ya JINAI ndio huandaa jalada la mashtaka na kuliwasilisha kwa DPP ili mashtaka yafunguliwe mahakamani. Kama ofisi ya DPP ilipokea jalada husika, maana yake polisi ilijiridhisha na ilileta ushahidi. Afisa mpelelezi hatakiwi kuleta jalada kwa DPP kama hana ushahidi.

Swali 1: ni ushahidi gani DPP anausubiri wakati katika sura ya kimazingira ya kesi inaonekana kuna ushahidi tayari toka upande wa Wakili wa MALALAMIKO & toka jeshi la polisi?

Swali 2: kwanini DPP hakushirikisha upande wa mlalamikaji kabla ya kufuta kesi?

Upande wa mlalamikaji una haki hiyo kwa sababu ndio ulioanzisha kesi hii. Walau DPP angeshauriana nao kwanza. Huenda upande wa mlalamikaji wana ushahidi wa kutosha.

Mwisho, kwakuwa NOLLE PROSEQUI sio hukumu, nategemea kesi hii kurudi mahakamani ili haki itendeke kwa pande zote mbili.

#BabaMwita
 
Sawa tatamoke sawabho moita!

Namimi jana nilikuwa nataka kuanzisha humi uzi kuulizia mwendelezo wa hii kesi ya Pauline Gikuri, kusema kweli Serikali ya CCM imapaswa kuliangalia hili maana linatia doa moja kwa moja ni jinsi gani hili taifa lisivyothamini wasiokuwa nacho,

Na hii inaleta taswira kwamba Tanzania mtu mwenye hela yuko juu ya sheria, naomba Team ya waandishi wa habari watafute upande wa familia ya yule kijana ili tujue ni kipi walichoambiwa juu ya lile sakata lao
 
Mosi, hili shauri limefunguliwa chini ya Kifungu 128(2) cha CPA na mshtaki binafsi (private prosecutor), ambapo utaratibu huu sheria inamtaka Hakimu kwanza AJIRIDHISHE kuna ushahidi wa kutosha kabla ya kuanzisha mashtaka. Hakimu alifanya hivyo na akakubali kuanzishwa kwa mashtaka kwa sababu aliona kuna ushahidi mbele yake.

Pili, kama kusingekuwa na ushahidi, kifungu cha 129 cha CPA kinampa Hakimu MAMLAKA ya kufuta kesi pale atakapojiridhisha kuwa MALALAMIKO & USHAHIDI ulioletwa mbele yake haufichui kosa dhidi ya mtuhumiwa, na Hakimu hutakiwa kuandika sababu ya kufuta kesi na mtuhumiwa huachiwa huru.

Kwakuwa Hakimu alikubali kuanzisha mashtaka, maana yake ALIJIRIDHISHA pasipo shaka kwamba kuna ushahidi wa kutosha. Vinginevyo angetupilia mbali hii kesi kupitia kifungu tajwa hapo juu; s129.

Jambo jingine katika hili, japo DPP ana mamlaka ya kufuta kesi kwa NOLLE PROSEQUI, kwa mtazamo wangu katika kesi hii DPP AMEZUIA haki kutendeka. Labda angeacha tusikilize ushahidi wa pande zote kwanza kabla ya kuondoa kesi. Au hata ushahidi wa pande moja kama ilivyokuwa kwenye "kesi ya Mbowe".

Ndio, sheria inampa DPP MAMLAKA ya kuondoa kesi pasipo kutoa sababu, lakini pia sheria HAIJAMKATAZA kutoa sababu (hili la msingi kuzingatiwa). Ushauri wangu, kwa kuzingatia maslahi ya umma, uwekwe utaratibu wa DPP kueleza sababu za kufuta kesi katika kesi zenye MASLAHI KWA UMMA au kesi yoyote yenye kufuatiliwa kwa ukaribu na kundi kubwa ndani ya Jamii. Hii itaondoa SINTOFAHAMU.

Jambo lingine, DPP anasema anasubiri ushahidi! Lakini, tayari alituambia amepokea jalada la mashtaka toka Polisi. Kama ushahidi hautoshi angesema!

UTARATIBU WA KUFUNGUA MASHTAKA KUPITIA DPP.

Hatua ya awali Jeshi la Polisi hufanya uchunguzi ikiwemo kuhoji pande zote mbili; mlalamikaji & mlalamikiwa. Polisi ikijiridhisha kuna chembe ya JINAI ndio huandaa jalada la mashtaka na kuliwasilisha kwa DPP ili mashtaka yafunguliwe mahakamani. Kama ofisi ya DPP ilipokea jalada husika, maana yake polisi ilijiridhisha na ilileta ushahidi. Afisa mpelelezi hatakiwi kuleta jalada kwa DPP kama hana ushahidi.

Swali 1: ni ushahidi gani DPP anausubiri wakati katika sura ya kimazingira ya kesi inaonekana kuna ushahidi tayari toka upande wa Wakili wa MALALAMIKO & toka jeshi la polisi?

Swali 2: kwanini DPP hakushirikisha upande wa mlalamikaji kabla ya kufuta kesi?

Upande wa mlalamikaji una haki hiyo kwa sababu ndio ulioanzisha kesi hii. Walau DPP angeshauriana nao kwanza. Huenda upande wa mlalamikaji wana ushahidi wa kutosha.

Mwisho, kwakuwa NOLLE PROSEQUI sio hukumu, nategemea kesi hii kurudi mahakamani ili haki itendeke kwa pande zote mbili.

#BabaMwita
Nchi hii tatizo wanaccm wanajiona wapo juu ya Sheria au viongozi wanajiona hii Nchi ni yao wao na Babu zao ......IPO SIKU.....
 
Back
Top Bottom