Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,571
Kwa Maslahi ya Taifa, Hongera DPP Mpya.jpg

Wanabodi,
Naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", nikiangazia suala zima za utoaji haki nchini, ambapo makala hii ni muendelezo wa ushauri kwa DPP, ulioanza wiki iliyopita.

Wanasheria wana vimisemo vyao vingi vingi vya kisheria, vingi viko kwenye lugha ya Kilatini, na kutafsiriwa kwa Kiingereza kisha Kiswahili, mmoja wa msemo maarufu sana kuhusu haki, unasema "Justice must not only be done, must be seen to be done", kumaanisha "Haki sio tuu ni lazima itendeke, bali pia ionekane inatendeka". Kwa muda wa mwezi mmoja sasa, wiki nne mfululizo, nimekuwa nikiandika makala za "Kilio cha Haki" nikijiekeza ofisi ya DPP, hatimaye sasa kuna kitu kinatendwa na kinaonekana.

Unapoandika makala kulalamikia jambo fulani, na kutoa ushauri wa nini kifanyike, halafu ikatokea hicho ulichashauri kikafanyika, kama ulivyoshauri, hatua ya kwanza ni kutoa pongezi, kwa hicho kilichofanyika, hivyo makala ya leo, naianza kwa kumpongeza DPP, ametenda!. Kumbe Kutenda haki kunawezekana, hongera sana DPP mpya kwa kuianza kazi yako vizuri, sasa sio tuu haki inatendeka, bali pia inaonekana kutendeka, hivyo kazi hii nzuri na iendelee, na sio kusubiri tena hadi Mama aseme!.

Sasa naendelea na ule ushauri wa DPP, wiki iliyopita niliishia number 6, leo naendelea.
  1. Kuna watuhumiwa wako mahabusu kwa makosa yanayodhaminika, bali DPP ameiamuru mahakama kuzuia dhamana zao. Hapa kuna mambo 3.Moja ni masuala ya weledi, haki na uwajibikaji wakati wa kutekeleza mamlaka kwa mujibu wa kifungu hiki. Mbili ni uhalali wa kifungu hiki kikatiba ambacho kwa kweli hakitoi uwajibikaji kabisa ndio maana kilifutwa kwenye CPA baada ya mahakama kujiridhisha kifungu hiki kinakwenda kinyume cha katiba, kisheria, mahakama ikiishatoa amri, sharia fulani au kifungu fulani kiko kinyume cha katiba, na kifungu hicho kifute, kifungu hicho kinakuwa “null and void ab initio”, yaani hakukuwahi kuwepo,
  2. Lakini kwenye kufutwa kwa kifungu hiki, kuna kitu cha ajabu kimetokea, wakati kifungu hiki kimefutwa na mahakama kwa kuwa kinyume cha katiba kwenye CPA, kifungu hicho bado kipo kwenye EOCCA!. Hili ni jambo la ajabu sana!. Hapa naiomba Mahakama inatamka kifungu fulani kinakwenda kinyume cha katiba, na kuamuru kifutwe, kifungu hicho kifutwe kwenye sheria nyingine zote.
  3. Sasa tunaishi kwenye ulimwengu wa kidigitali, Tanzania na sisi tutumie nafuu za kidigitali, kwa kuanzisha “digital custody “ mahabusu za kidigitali na “digital cells”, jela za kidigitali, mtuhumiwa anazuiliwa nyumbani kwake, hata kutumikia kifungo akiwa nyumbani kwakwe kwa kufungiwa kifaa maalum cha GPS (tracking device), inayofungwa kwa lakiri ya kidigitali, na kuwa kuzuiwa nyumbani kwake, nyumba hiyo inafungwa kamera, maalum, (IP Camera) kama zile kamera za CCTV, hivyo polisi/magereza wanaona nyendo zote za mtuhumiwa, akivuka tuu ile IP camera, inapiga alarm, mtuhumiwa anakuwa amekiuka masharti hivyo kustahili kuzuiliwa mahabusu. Utaratibu huu unaruhusu mke anapata haki zake za ndoa, watoto wanapata mapenzi ya baba, na baba kuendelea na shughuli za kuingiza kipato cha kuendesha familia.
  4. Mahabusu ni mtuhumiwa tuu, anahesabika hana hatia hadi athibitishwe na mahakama, lakini mahabusu wetu, wanahesabiwa kama wafungwa, wananyimwa haki zao , mfano watuhumiwa wengi tuu ambao sio hatarishi wamefiwa na ndugu zao, wazazi wao, wapendwa wao au jamaa zao, bila kupewa haki ya kushiriki mazishi yao, akiwemo mwanafani mwenzetu Erick Kabendera, ambaye mama yake alitoa kilio chake mahali kuwa uhai wake unamtegemea mwanae. Mama huyo alipoteza maisha kwa sababu ya mwanae kushikiliwa mahabusu, na mwanae hakuruhusiwa kumzika. Sisi watu wa karma, tulitoa angalizo la karma ya huyu mama, wanaojua karma ilikuja kufanya nini, wanajua!. Mahabusu wa wenzetu, hata wana ndoa, wanaruhusiwa kupata haki zao, hata wawapo mahabusu au vifungoni,
  5. Mhabusu zetu ni mahali mahali hatarishi, na kutokana na umasikini wetu, hatuna magereza ya mahabusu (remand prison) na jela ya wahalifu, Mahabusu wetu, wanashikiliwa jela kama wafungwa. Wapo baadhi ya mahabusu wanafanyiwa vitendo vibaya au viovu wakiwa mahabusu na wapo ambao wamepata matatizo ya kiafya permanently kwa kurundikana mahabusu bila huduma za msingi ambapo wangeweza kujihudumia wenyewe wawapo nje. DPP/serikali inapata faida gani kuswekwa watu rumande na kuzuia dhamana?!.
  6. Japo hapa natetea haki za watuhumiwa , pia naomba pia kuzingatia haki za wahanga wa uhalifu. Katika ulimwengu wa uhalifu kuna watu wabaya kupita kipimo. Just imagine unakuta mtu mzima umembaka mtoto wa miaka 2 na kumharibu vibaya sehemu zake za siri na pengine akamwambukiza HIV, mauaji ya kutisha , vitendo vya vikundi vya kihalifu kama panya road na mapanga yao wanapokuingilia na kukucharanga mapanga bila huruma na kumbaka binti yako au mkeo mbele yako na visa vingine vingi. Hao ni ma “psychopath” wanastahi kukaa mahabusu kwasabu ni watu hatarishi, wasipate dhamana kwa vile wamepoteza sifa za haki yao kuwa huru.
  7. Ule utaratibu wa notification kwa makosa ya usalama barabarani, na kulipa faini za papo kwa papo, utumike pia kwenye vituo vya polisi, mwizi wa kuku akiri kuiba kuku, akubali kumlipa aliyemuibia na kulipa faini, kesi hiyo inaishia hapo hapo kituoni wala haina haja ya kufikishwa mahakamani.
  8. Majaji wetu, kwa ajili ya kusikiliza maombi ya dhamana, nao wanapaswa kufanya kazi kama vituo vya polisi, mahospitali na dharura nyingine kwa saa 24. Kama ilivyo kwa madaktari wa zamu anapigiwa simu kukitokea dharura, kuwe na majaji wazamu saa 24/7. Nimeshuhudia hii Afrika Kusini, kila mtuhumiwa anapelekwa kwa hakimu wakati wowote hadi usiku wa manane, kama vile madaktari au vituo vya polisi.
  9. Mwisho, Mheshimiwa sana, DPP wetu mpya, hongera kwa uteuzi wako mpya, Watanzania tunamatumaini makubwa sana na Rais wetu Mama Samia katika nia yake ya dhati kutaka Watanzania watendewe haki, na Mama Samia, amekuaminia wewe kuongoza na ofisi hii muhimu sana, ya DPP, timiza wajibu wako kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, kama ulivyoanza, Taifa litaponywa, kwa haki sio tuu kwa haki kutendeka, bali pia kwa haki kuonekana imetendeka.
Mungu Ibariki Tanzania.

Baada ya kumalizana na DPP, ungana nami wiki ijayo tukianzana na Jaji Mkuu na Mfumo mzima wa Mahakama katika utoaji haki. .

Paskali.
Rejea za Mfululizo huu wa makala za DPP
1624252735094.png

1624252688874.png

1624252805784.png

Update
Hatimaye usaidizi huu, unakwenda kufanyika, kupitia kipindi cha TV kwenye kituo cha Channel Ten, kila siku za Jumapili Saa 3:00 usiku na marudio kila Jumatano saa 9:30 Alasiri.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=IXfA8sZkNPxpaeZn
Usikose kuangalia!.
P
 
Viongozi wa CCM wamepitwa na wakati na ndio maana bado wanaendeleza mifumo ya kikoloni katika kuendesha nchi.

Wanapata exposure lakini hawabadiliki!
Pls mkuu usipinge kwa kuonekana kila kitu unapinga,give credits pale panapositahili,President Samia she is doing very well so far,amefungulia voices nyingi ambazo zilikuwa silenced,uhuru wa haki umeanza na hawezi kubadilisha kila kitu overnight na elewa bado anakabiliwa na wasiotaka mabadiliko ndani ya CCM, Mr.Mayala umetoa moja ya mada nzuri na nimeipenda(ingawa mambo mengi tunatofautiana na ni haki yetu)now tunahitaji TAASISI imara zenye maamuzi ya kujitegemea.
 
Pascal Mayalla wewe ni brilliant sana. Mtu akuchukie akupende..you know your stuff. To that nasema hongera sana!

Lakini zikija mada ambazo zinamtaka mtu asimame upande fulani (unpopular positions) ahesabiwe, you simply run AWOL. Mimi nadhani at your age and level, be who you are. Say it as it is. Tulitegemea watu kama nyinyi ndo akina Jenerali wa kesho. watu wanaoweza kuchambua mambo kwa kina bila kujipendekeza kwa yeyote.

But it is unfortunate kwamba hata wewe, sometimes unaweka taaluma yako pembeni kutetea waliochafuka vya kutosha. the past five yours have revealed your true colors. Again, maybe siko fair kukulaumu maana, wengi tulikuwa kama wewe. WE were terrified na wasiojulikana. It was really terrifying.

Tujitahidi tujenge kizazi cha vijana wasio waoga. Vijana wathubutu. Pascal, wewe level yako siyo hata ya kuwazia kuwa DC au DED..you are way past that level bro. Don't sell yourself cheap (ingawa najua mwisho wa siku wote tunahitaji kula na kulipa bills). But please.....protect your credibility at any cost! You are better and you deserve better.

Hizi kazi za U-DC waachie akina Lijualikali and the likes...maana ni kazi ambazo hazihitaji creativity ya aina yoyote zaidi ya kuvaa suti isiyo na collar :)

Wasalaam,
 
Pls mkuu usipinge kwa kuonekana kila kitu unapinga,give credits pale panapositahili,President Samia she is doing very well so far,amefungulia voices nyingi ambazo zilikuwa silenced,uhuru wa haki umeanza na hawezi kubadilisha kila kitu overnight na elewa bado anakabiliwa na wasiotaka mabadiliko ndani ya ccm,Mr.Mayala umetoa moja ya mada nzuri na nimeipenda(ingawa mambo mengi tunatofautiana na ni haki yetu)now tunahitaji TAASISI imara zenye maamuzi ya kujitegemea.
Nakubaliana na wewe 100%
 
Well said.
 
View attachment 1825109

Wanabodi,
Naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", nikiangazia suala zima za utoaji haki nchini, ambapo makala hii ni muendelezo wa ushauri kwa DPP, ulioanza wiki iliyopita.

Wanasheria wana vimisemo vyao vingi vingi vya kisheria, vingi viko kwenye lugha ya Kilatini, na kutafsiriwa kwa Kiingereza kisha Kiswahili, mmoja wa msemo maarufu sana kuhusu haki, unasema "Justice must not only be done, must be seen to be done", kumaanisha "Haki sio tuu ni lazima itendeke, bali pia ionekane inatendeka". Kwa muda wa mwezi mmoja sasa, wiki nne mfululizo, nimekuwa nikiandika makala za "Kilio cha Haki" nikijiekeza ofisi ya DPP, hatimaye sasa kuna kitu kinatendwa na kinaonekana.

Unapoandika makala kulalamikia jambo fulani, na kutoa ushauri wa nini kifanyike, halafu ikatokea hicho ulichashauri kikafanyika, kama ulivyoshauri, hatua ya kwanza ni kutoa pongezi, kwa hicho kilichofanyika, hivyo makala ya leo, naianza kwa kumpongeza DPP, ametenda!. Kumbe Kutenda haki kunawezekana, hongera sana DPP mpya kwa kuianza kazi yako vizuri, sasa sio tuu haki inatendeka, bali pia inaonekana kutendeka, hivyo kazi hii nzuri na iendelee, na sio kusubiri tena hadi Mama aseme!.

Sasa naendelea na ule ushauri wa DPP, wiki iliyopita niliishia number 6, leo naendelea.
  1. Kuna watuhumiwa wako mahabusu kwa makosa yanayodhaminika, bali DPP ameiamuru mahakama kuzuia dhamana zao. Hapa kuna mambo 3.Moja ni masuala ya weledi, haki na uwajibikaji wakati wa kutekeleza mamlaka kwa mujibu wa kifungu hiki. Mbili ni uhalali wa kifungu hiki kikatiba ambacho kwa kweli hakitoi uwajibikaji kabisa ndio maana kilifutwa kwenye CPA baada ya mahakama kujiridhisha kifungu hiki kinakwenda kinyume cha katiba, kisheria, mahakama ikiishatoa amri, sharia fulani au kifungu fulani kiko kinyume cha katiba, na kifungu hicho kifute, kifungu hicho kinakuwa “null and void ab initio”, yaani hakukuwahi kuwepo,
  2. Lakini kwenye kufutwa kwa kifungu hiki, kuna kitu cha ajabu kimetokea, wakati kifungu hiki kimefutwa na mahakama kwa kuwa kinyume cha katiba kwenye CPA, kifungu hicho bado kipo kwenye EOCCA!. Hili ni jambo la ajabu sana!. Hapa naiomba Mahakama inatamka kifungu fulani kinakwenda kinyume cha katiba, na kuamuru kifutwe, kifungu hicho kifutwe kwenye sheria nyingine zote.
  3. Sasa tunaishi kwenye ulimwengu wa kidigitali, Tanzania na sisi tutumie nafuu za kidigitali, kwa kuanzisha “digital custody “ mahabusu za kidigitali na “digital cells”, jela za kidigitali, mtuhumiwa anazuiliwa nyumbani kwake, hata kutumikia kifungo akiwa nyumbani kwakwe kwa kufungiwa kifaa maalum cha GPS (tracking device), inayofungwa kwa lakiri ya kidigitali, na kuwa kuzuiwa nyumbani kwake, nyumba hiyo inafungwa kamera, maalum, (IP Camera) kama zile kamera za CCTV, hivyo polisi/magereza wanaona nyendo zote za mtuhumiwa, akivuka tuu ile IP camera, inapiga alarm, mtuhumiwa anakuwa amekiuka masharti hivyo kustahili kuzuiliwa mahabusu. Utaratibu huu unaruhusu mke anapata haki zake za ndoa, watoto wanapata mapenzi ya baba, na baba kuendelea na shughuli za kuingiza kipato cha kuendesha familia.
  4. Mahabusu ni mtuhumiwa tuu, anahesabika hana hatia hadi athibitishwe na mahakama, lakini mahabusu wetu, wanahesabiwa kama wafungwa, wananyimwa haki zao , mfano watuhumiwa wengi tuu ambao sio hatarishi wamefiwa na ndugu zao, wazazi wao, wapendwa wao au jamaa zao, bila kupewa haki ya kushiriki mazishi yao, akiwemo mwanafani mwenzetu Erick Kabendera, ambaye mama yake alitoa kilio chake mahali kuwa uhai wake unamtegemea mwanae. Mama huyo alipoteza maisha kwa sababu ya mwanae kushikiliwa mahabusu, na mwanae hakuruhusiwa kumzika. Sisi watu wa karma, tulitoa angalizo la karma ya huyu mama, wanaojua karma ilikuja kufanya nini, wanajua!. Mahabusu wa wenzetu, hata wana ndoa, wanaruhusiwa kupata haki zao, hata wawapo mahabusu au vifungoni,
  5. Mhabusu zetu ni mahali mahali hatarishi, na kutokana na umasikini wetu, hatuna magereza ya mahabusu (remand prison) na jela ya wahalifu, Mahabusu wetu, wanashikiliwa jela kama wafungwa. Wapo baadhi ya mahabusu wanafanyiwa vitendo vibaya au viovu wakiwa mahabusu na wapo ambao wamepata matatizo ya kiafya permanently kwa kurundikana mahabusu bila huduma za msingi ambapo wangeweza kujihudumia wenyewe wawapo nje. DPP/serikali inapata faida gani kuswekwa watu rumande na kuzuia dhamana?!.
  6. Japo hapa natetea haki za watuhumiwa , pia naomba pia kuzingatia haki za wahanga wa uhalifu. Katika ulimwengu wa uhalifu kuna watu wabaya kupita kipimo. Just imagine unakuta mtu mzima umembaka mtoto wa miaka 2 na kumharibu vibaya sehemu zake za siri na pengine akamwambukiza HIV, mauaji ya kutisha , vitendo vya vikundi vya kihalifu kama panya road na mapanga yao wanapokuingilia na kukucharanga mapanga bila huruma na kumbaka binti yako au mkeo mbele yako na visa vingine vingi. Hao ni ma “psychopath” wanastahi kukaa mahabusu kwasabu ni watu hatarishi, wasipate dhamana kwa vile wamepoteza sifa za haki yao kuwa huru.
  7. Ule utaratibu wa notification kwa makosa ya usalama barabarani, na kulipa faini za papo kwa papo, utumike pia kwenye vituo vya polisi, mwizi wa kuku akiri kuiba kuku, akubali kumlipa aliyemuibia na kulipa faini, kesi hiyo inaishia hapo hapo kituoni wala haina haja ya kufikishwa mahakamani.
  8. Majaji wetu, kwa ajili ya kusikiliza maombi ya dhamana, nao wanapaswa kufanya kazi kama vituo vya polisi, mahospitali na dharura nyingine kwa saa 24. Kama ilivyo kwa madaktari wa zamu anapigiwa simu kukitokea dharura, kuwe na majaji wazamu saa 24/7. Nimeshuhudia hii Afrika Kusini, kila mtuhumiwa anapelekwa kwa hakimu wakati wowote hadi usiku wa manane, kama vile madaktari au vituo vya polisi.
  9. Mwisho, Mheshimiwa sana, DPP wetu mpya, hongera kwa uteuzi wako mpya, Watanzania tunamatumaini makubwa sana na Rais wetu Mama Samia katika nia yake ya dhati kutaka Watanzania watendewe haki, na Mama Samia, amekuaminia wewe kuongoza na ofisi hii muhimu sana, ya DPP, timiza wajibu wako kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, kama ulivyoanza, Taifa litaponywa, kwa haki sio tuu kwa haki kutendeka, bali pia kwa haki kuonekana imetendeka.
Mungu Ibariki Tanzania.

Baada ya kumalizana na DPP, ungana nami wiki ijayo tukianzana na Jaji Mkuu na Mfumo mzima wa Mahakama katika utoaji haki. .

Paskali.
Rejea za Mfululizo huu wa makala za DPP
View attachment 1825142
View attachment 1825139
View attachment 1825143

Pascal kama Pascal💪
 
Bwana Mayala huchoki kunishangaza, nikidhani umefika mwisho kunde bado una mpya. DPP ni ofisi, siyo mtu, inatawaliwa na sheria. Kwa ufahamisho wako (naona hujui) kesi za ugaidi huwa hazina ushahidi, mashahidi wameuwa au wamejiua. Dawa ni kuwashikilia as long as possible, ili jamii iwe salama kwa muda huo.

Umesahau ubalozi wa Marekani ulipolipuliwa mwaka ule? Kulikuwa na Watanzania kutoka Pemba, hawakushitakiwa Bumbwini. Kesi yao haijasikilizwa na hadi leo wako gereza la Guantanamo. Bin Laden hakushitakiwa kwao Sudan, aliuliwa Pakistan na special forces za Barak Obama.

Mfano mwingine wa kesi kuchelewa ni kesi za ndoa. Ukienda kumshitaki mkeo kwa Askofu ili upate talaka, utaambiwa njoo kesho njoo kesho, Askofu anatumai na kukuombea hoping you will cool down in good time.

Fundisho ni kwamba Rais Kikwete na Rais Shein waliowafunga (Waislamu wenzao) si watu wabaya, DPP wakati huo nadhani sasa ni Jaji wa Mahakama, waliamua hivyo. Akaja Magu, hivyo hivyo. Kaja Samia, miaka 9 inatosha kwa mtu kucool down. Usisahau pia kuna Mapadri walipigwa acid na makanisa kuchomwa moto. Kuna Wamachinga na Wachagga kutoka Bara maduka yao ya hardware Darajani yalienzuliwa. Wote hawo nao wana hasira zao, nao after 9 years wamecool down.

It is not as simple as you make it, nor funny.
 
View attachment 1825109

Wanabodi,
Naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", nikiangazia suala zima za utoaji haki nchini, ambapo makala hii ni muendelezo wa ushauri kwa DPP, ulioanza wiki iliyopita...
Good,itakuwa ajabu Kama Mh. Rais asikuteue nafasi yoyote hata ya u-DED, mkuu upo vizuri sana, japo sometimes unazingua,aswa kipindi kile Cha Ngosha
 
Back
Top Bottom