Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

Asalaam aley khum ndugu Watanzania, ni siku ya kwanza ya mwaka 2010 hii
inatuonesha kuwa tayari tumeumaliza mwaka wa 48 tangu nchi yetu ipate
uhuru, tuanaingia mwaka wa 49. Pamoja na hayo taifa la Tanzania
limepitia vipindi mbali mbali vya wananchi wake kutawali na kundi moja
la chama kimoja cha CCM tangu kuwaondoa watawala
w...a Kizungu ambao japo waliiendesha nchi kwa faida yao lakini pia
Watawaliwa walikuwa na afadhali ya ukame mahitaji, ndiyo
kilikuwa ni kipindi mtu anajaliwa kwa utu wake ukilinganisha na kipindi
walipoondolewa na nchi kumilikiwa na kundi walijiita wana wa CCM ambao
hawa waliingia katika uongozi kwa maslahi yao zaidi na maslahi ya chama
chao cha CCM na si kwa ajili ya taifa na wananchi kwa ujumla.

Utawala
wa Ulikuwa ukiongozwa na Mtu aliyejiita Mwalimu JULIUS KAMBARAGE
NYERERE chini ya serikali ya CCM Utawala ambao haukuwapenda sana
wazalendo hata kufika hatua ya kutaifisha mali zao kwa kuwabambikia
majina ya wahujumu uchumi, na wale walionekana kuwa wasomi zaidi ama
kulipenda sana taifa lao basi walifikia hatua ya 'kutaifishwa' uhai wao
ama Kulazimishwa kuishi chini kukubari kila jambo yaani 'ndiyo mzee ama
tawile'Kutokana na tabia ya CCM kutopenda usawa kwa kudumisha utu, basi
mtu
yeyote aliyeonekana kupinga alilazimishwa kufa kwa ridhaa yake au
kuuliwa, nasema kuuliwa kwa sababu ikiwa mtu amesema ukweli hupoteza
uhai katika Mazingira ambayo mtu yeyote mwenye uchungu na taifa hawezi
kuridhishwa nayo, ambapo hata serikali hainekani kustuka ama kutaka
kufanya uchunguzi wa nini kimefanyika.Siogopi kusema haya kwa
sababu demoklasia yangu inaniruhusu kusema ingawaje mara nyingi
ukweli huwafanya watu wafe ama wauliwe.

HATA BWANA YESU alikufa kwa
sababu ya kuibeba kweli na kuileta duniani wale waliopenda uovu walipanga
njama za kumwua wakisaidiana uongozi wa serikali ya Kiroma chini ya mtu
aliyejiita Pilato.Lipi lililo jepesi ukiifia kweli ama uishi kwa
kuutukunza uuaji, ushenzi,ukandamizaji, udharirishaji na utawala wa
kimabavu? Ama kuna kuwatunza viongozi vipofu na kuwafanya watoto wao
wanywe Chai ya maziwa na boflo, harafu wa kwetu wanywe chai kavu na
yenyewe kwa bahati mbaya? Hili haliwezeka kwangu mimi ni heri kuiifia
kweli ile ninayoijua,Hebu twende taratibu tukianza na Mazingira
ya kifo cha mzee wetu Edward Moringe Sokoine, kuna mtu mwingine Mzee
Korimba, kuna Imran Kombe, kuna akina Kigoma Ali Malima, si hao tu nani
anajua mazingira ya kifo cha mzee Omar Alli Juma ni vifo vyenye
mazingira ya utata, lakini serikali ya Chama cha Mapinduzi imenyaza
kimya haitwambii chochote si wengine hatujui hapana we know every thing
evil done by CCM katika kulinda na kutetea ushenzi na udikiteta wake
madarakani.

Ni nani anajua Abeid Amani Karume alipigwa risasi na
kundi la vita gani na kutoka wapi tangu Nyerere hata sasa bado kuna
uozo mkubwa unaofanywa na CCM kwa watanzania wanyonge ambao wameishia
kuburuzwa hovyo na washenzi wachache tu kwa maslahi ya vizazi vyao.
Hivi leo tuiambie serikali ya Tanzania chini ya chama cha mapinduzi
ituandalie ripoti ya matukio mbali mbali itatuambie hivi karibuni
tumeshuhudia mabomu yakilipuliwa kwa makusudi Mbagala hakuna hata la
kuuridhisha umma kwa maelezo Umefika wakati wa kuambiana ukweli bila
hata ya kuogopana wala kuoneana aibu kama kuuana heri, kuangalia ndugu
jamaa zetu wakipoteza maisha kwa ujinga tu, haiwezekani, viongozi na watanzania
wengi wanaujua ukweli hawataki kuweka kwa kuogopa kufishwa, nani kakwambia mtu ataishi
miaka yoote hapa duniani?

Maana ni heri yule aogopaye kumkosea Mwenyezi
Mungu kuliko kumwogopa mwanadamu tu, kwani mwanadamu ni nani mbele za Mungu nasema
tena na tena kama kufa tutakufa woote lakini kweli lazima tuitenge na
giza kwa msaada wa Mungu, haiwezekani kabisa lazima maana imeandikwa
'msiwaogope hao wawezao kuua mwili wasiweze kuiua na roho, bali
mwogopeni yule awezaye kuua mwili na roho pia' yaani Mungu tu.

Na lile
lililofanywa gizani litawekwa peupe. Na vibaraka wengi wa CCM ni waota
ndoto za mizimu, usishangae ajitokeza mtu muaguzi na utabili wake wa
kipepo na kuwakatisha tamaa wengine kwa kuandaa mazingira ya wazi wazi
ya kuua mtu muhimu atakaye tokea kuipinga CCM katika uchaguzi ujao,
hizo ni tantata lila za uongo tu, na uzushi tu ili baadae wakiua mtu
tuanze kusema aaa! alitabiri Shekh Yahya, bila aibu vingozi wenye
mikataba na CCM ya muda mrefu wanaanza kuwashauri watanzania kuto
wapuza wasoma nyota na wafuasi wa mapepo na mashetani ya uuaji,Safari
hii ni zamu yake Hakuna kiongozi yeyote wala Mgombea yeyote atakaye
jitokeza kuipinga CCM akafariki, Sasa ni wakati wa kufa mwenyewe Shekh
Yahya na kundi lake la uuwaji.

MUNGU IBARIKI TANZANIA BARIKI WATU WAKE itaendelea.........
 
mmh.. haya makubwa sasa! Karibu miaka mitatu kamili tangu makala hii itoke!
Ndio. Mwanakijiji hali ya CCM sasa hivi ni mbaya sana kuliko wakati ukiandika makala hii. Nadhani huu kweli ni Unabii na sio utabiri kama ule wa yule jamaa wa pale Magomeni.
 
Japo hii makala ni muda mrefu imeandikwa lakini itaendelea kusimama mpaka haya yaliyoandikwa yatimie. Naamini itakuwa ngumu kubadilisha kila kitu kwa wakati mmoja lakini hao wataoingia madarakani ambao TUNAOMBA WASIWE NA HATA CHEMBE YA CCM kazi yao ya kwanza iwe kutengeneza mazingira. Kama alivyoelezea sheba. Then from there mambo yanaweza kufanyika na matunda yakaonekana.

Mimi naomba huu utabiri utimie mapema zaidi.

Mfano tunasema KATIBA ina mapungufu, Kuna issue ya ZANZIBAR, kuna sheria za ajabu ajabu inabidi ziondolewe, kuna
 
Amen.
Utatimia muda si mrefu
Haya ni baadhi ya maeneo ambayo, tukubali tusikubali, Mwanakijiji ni miongoni mwa few extra ordinary tulionao humu JF.
The clock is ticking.... tick...tick....tick....
 
Haya ni baadhi ya maeneo ambayo, tukubali tusikubali, Mwanakijiji ni miongoni mwa few extra ordinary tulionao humu JF.
The clock is ticking.... tick...tick....tick....

Sure.
Nakubaliana na ww Pasco, kwani hata Roma nayo ilikuwa ni ngome kubwa lakini ilianguka. Hali kadhalika dalili za sisiemu kuanguka zinaonekana, hasa ikizingztiwa susla la kutoaminiana wao kwa wao.
Historia itahukumu
 
Hata Congo (wakati ule ikiitwa Zair), walikuwa na uchaguzi na Mobutu aligombea na hadi wakaanza kumfanyia kampeni.

CCM nayo huwa inagombea URAIS, ila sijui ni kwa asilimia ngapi ni kweli na ipi ni kuhonga na kuiba kura ili kupata Tsunami. Poleni watu wa Zanzibar maana wenzetu yameshawakuta ya waziwazi kwa kupindishwa matokeo. Ohh, Mobutu yuko wapi siku hizi?

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=w2nFDyMhSp4&feature=related"]YouTube- Candidat Na Biso Mobutu - Luambo Makiadi & le T.P .O.K. Jazz 1984[/ame]
 
we are getting there.. you know what.. watu wengi wanasahau unabii wenyewe ulikuwa unahusu nini hasa.. Niliandika hivi hapo juu:

Alipoulizwa kuhusu kujiondoa CCM, mwalimu alijibu "CCM siyo Mama yangu". Maneno hayo ya Mwalimu yamebakia mawazoni mwangu (na bila shaka ya wengine pia) kama unabii na kama wosia. Hii leo kuna baadhi ya viongozi wa Chama tawala ambao wanasisitiza maneno ya Mwalimu ya "Bila CCM madhubuti Tanzania Itayumba" na kusahau kabisa maneno hayo ya onyo kali kuwa hata kama mtu ana mapenzi kiasi gani na CCM, iko siku anaweza kukiacha na kujitahidi kukivunja! Ni rahisi kukiacha CCM kuliko kumuacha Mama mzazi!

Ni maneno hayo hayo ambayo Mpendazoe ameyarudia na mtayaona yakirudiwa na wengi wakuu watakaotoka CCM... Unabii haufanyi haraka wala hauchelewi.. hutimia kwa wakati..
 
CCM ikianguka, are we sure that the alternative party will be capable of running an effective government? Hilo ndio swali la msingi ndugu Mwanakijiji.
 
CCM ikianguka, are we sure that the alternative party will be capable of running an effective government? Hilo ndio swali la msingi ndugu Mwanakijiji.

Wewe nawe!
Hivi tuna effective government? Hujasikia juu ya autopilot?
 
CCM ikianguka, are we sure that the alternative party will be capable of running an effective government? Hilo ndio swali la msingi ndugu Mwanakijiji.

Mkuu Selemani,

Swala siyo kuwa na effective government, mimi ninacholilia siku zote ni kuwa na Bunge ambalo litakuwa balanced kiasi kwamba linaweza kuwa effective katika kuisimamia serikali ipasavyo. Kama CCM ikipasuka na kukawa na Bunge ambalo haliko-dominated na chama kimoja, ndipo tutaweza kuanza serikali effective na siyo serikali ambayo inaweza hata kulidharau Bunge. Bunge la sasa halina nguvu, linaongozwa kwa kanuni, katiba na imani ya CCM, kwa hiyo whoever anayeonekana kuipinga serikali Bungeni anaonekana ni msaliti wa chama na ndiyo maana wametanguliza mbele maslahi ya CCM ambayo yametawaliwa na maslahi binafsi.

CCM imetawaliwa na maslahi binafsi kwa kuwa JK kawekwa na mafisadi na viongozi walio wengi ndani ya CCM ni mafisadi na hivyo CCM haiwezi kuacha kulinda maslahi ya mafisadi, same applies kwa serikali kwa kuwa iliwekwa na hao hao mafisadi.

Ukombozi wa kweli wa Tanzania utaanzia Bungeni kwa kuwa na wapinzani wengi, bila kujali wanatoka chama gani. Huko ndiko ambako wabunge wetu wanaweza kudai katiba mpya itakayofuta sheria mbaya na kuweka mazingira mazuri ya kugombea, na kuifanya serikali iwe effective. Effective government ni pamoja na kuwa watendaji ambao ni wawajibikaji kwa wananchi na siyo kwa Rais aliyewateua ama kwa Chama kilichowaweka madarakani.
 
Wewe nawe!
Hivi tuna effective government? Hujasikia juu ya autopilot?
Hatuna effective government. Na sijasikia kuhusu autopilot--lakini CCJ, CUF, au Chadema are they better just because they are alternative? Koz I strongly feel like a reformed CCM is better than hawa wazushi wengine.
 
Jamani eeeh nyerere yuleyule aliyesema ccm siyo mama yake ndiye alimpigia dr benjamin william mkapa debe na yaliyofuata ama legacy ni historia.mimi na wewe ndiyo wa kuitoa ccm madarakani .ok?namnukuu karl marx:all hitherto written history is a history of class struggles!pi historia nyingine kama ya guinea-bissau .kenya,namibia.angola,mosambiki na kwingineko imeandikwa kwa herufi z matone ya damu.mnachesea historia bwasheee?mangi meli ameandikiwa historia baada ya kunyongwa pale kolila ok?histora ni vitendo tena vya hatari.haya weeeee!
 
Halafu huwezi ukawaambia wale wadudu wanaoitwa maggot kwenye elimu viumbe eti wafanye reformaio.watakula wapi bwashee wakati uozo ndiyo natural system ya kuwapatia ulaji?tuache kuamini kirahisirahisi namna hiyo wajameni!
 
Hatuna effective government. Na sijasikia kuhusu autopilot--lakini CCJ, CUF, au Chadema are they better just because they are alternative? Koz I strongly feel like a reformed CCM is better than hawa wazushi wengine.

A reformed CCM? This, I'd like to see how it happens in my beloved TZ though I've no illussions at all about political parties (all). I only believe in a well informed, serious and courageous electorate to keep politicians in check and get them to deliver.
 
Utafiti nilioufanya unabashiri kwamba CCM watabakia na 40% ya viti vya Bunge, lakini "uncoordinated, unofficial alliance" ya upinzani itachukua 60%, majority ikienda CHADEMA.

Yakija kuwa kweli msiseme mimi MNAJIMU au MCHAWI!

Ni utafiti tu!

./Mwana wa Haki
 
Nauungana na Kitila Mkumbo, ili kuondoa uozo na UFISADI ULIOSHINDIKANA NCHINI TANZANIA NI LAZIMA VYAMA VYA UPINZANI VIACHE UBINAFSI VIUNGANE VIWE NA NGUVU MOJA ILI KUMUUONDOA HUYU FISADI CCM. Chadema, CUF hawataweza hata siku moja kumtoa CCM, ili wamtoa ni lazima waungane wapate nguvu halafu sisi watanzania woteeeeee hata sisi tulio wanachama wa CCM tutakuwa nyuma yao.

Siyo kila mwana CCM mtaani anafuhishwa na UFISADI wa CCM hapana. Bahati mabaya sana haijatokea Chama chenye nguvu na cha kuaminika.
Dawa ya kupata chama chenye nguvu ni KUUNGANA TUUU!!!!!!! VYAMA VYA UPINZANI UNGANENI WOTEEEEEEE TUMTOE CCM. Labda mwaka 2010 mumechelewa, haijalishi kabla ya mwaka 2015 lazima muungane ili RAISI WA 2015 ASITOKE CCM, NA MAFISADI WOTEEEEEE WATAPIGWA RISASI 2016, NA NYUMBA ZA SERIKALI ZOTEEEEEEE ZITARUDI SERIKALINI NA BARABARA ZITAJENGWA, SHULE ZA AKINA KAYUMBA ZITABORESHWAAA, MAJI SAFI YA KUNYWA YATAPATIKANA, KODI ZITAPUNGWA ZA WAFANYAKAZI, NA WAFANYA BIASHARA WATALIPA KODI INAVYOPASWA, BILL ZA MAJI, UMEME ZITALIPWAAAAAA.
NCHI YETU NZURI YA TANZANIA NA WATU WAKE WATANEEMEEKA.

WIZI UTAPUNGUWA KAMA SIYO KUISHA.

TUMECHOSHWA NA RUSHWA ZA KILA SEHEMU KOTINI RUSHWA, POLISI RUSHWA, HOSIPITALINI RUSHWA, KILA KUKICHA RUSHWA, RUSHWA, RUSHWA,

VYAMA VYA UPINZANI UNGANENI TUWE MFANO MZURI AFRIKA. AFRIKA OYEEEEEE, TANZANIA OYEEEEEE, INAWEZEKANA BILA CCM
 
Sheria ilikuwa inazuia muungano technically maana inabidi msajili chama upya na taratibu zote zinaanza upya. Lakini nasikia msajili wa vyama "ameshinikiza" mabadiliko ya sheria ili vyama viruhusiwe kuungana bila kulazimika kusajili hicho chama upya. Alituaidi katika mkutano wa CHADEMA wa Septemba pale PTA kuwa mswada utakuwa tayari na utapelekwa katika bunge la mwezi wa pili.

Nafikiri sisi wapinzani hatujatia pressure ya kutosha kubadilisha hii sheria.

Mwanakijiji karibu CCJ ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom