Endapo wapinzani wataishia kuwa waandamanaji, na wapiga kelele lakini wakishindwa kuungana na kutuonesha kuwa wako makini na mafanikio ya nchi yetu, basi CCM itaendelea kupeta kila kukija uchaguzi! Wapinzani wasililie huruma ya CCM ili wabadilishe Katiba au kuwajengea mazingira mazuri ya kushindana nao! Wapinzani wachukua hatima yao mikononi mwao wao wenyewe! Wawaambie Watanzania kuwa lengo lao mwaka 2010 ni kulichukua Bunge la Tanzania kwani limeendelea kuwa kicheko na dhihaka katika utawala wetu wa Demokrasia! Bunge lenye kutoa azimio la kulaani filamu ya mapanki kabla hawajaiona, na likakaa kimya kwenye mikataba ya madini na nishati bila kutoa azimio la kulaani mikataba hiyo, wabunge wa bunge hilo waondolewe kwa kura! Bunge ambalo linatumia siku 60 kuzungumzia maneno ya watu wawili na kushindwa kutumia siku moja kuzungumzia suala la rada, Richmond, IPTL, ATC n.k hilo ni bunge uchwara!! Bunge lenye spika anayeangalia matumizi ya maneno "kukaza" na "kutia" badala ya kuangalia matumizi ya shilingi Bilioni 80 ya vitu tusivyovihitaji Bunge hilo ni karibu ya Bunge la serikali ya nchi ya Wagagagigikoko! Kama kweli wanataka kuwapa Watanzania matumaini viongozi wote wa upinzani ifikapo 2010 wagombee Ubunge wakiwa wamuengana na kuhamasisha Watanzania wawachague wanachama wao! Kama Watanzania watataka Kikwete apewe nafasi nyingine hilo lao, lakini Bunge lisiende CCM!
Wapinzani wakiweza kunyakuwa wingi katika Bunge la Muungano, basi mwanzo wa CCM kuporomoka utakuwa umefika! Wakiweza kuwashawishi Watanzania baada ya wao kuungana kuwa wanamaanisha wanachosema basi CCM itaanza kutikisika! Watakapochaguliwa Wabunge na wakaanza kusimamia na kupitisha sheria ambazo zina manufaa kwa wananchi watamlazimisha Rais azikubali au atumie uwezo wake wa turufu. Na akifanya hivyo kwenye miswada fulani mara kadhaa avunje Bunge na uchaguzi mpya utafanyika! Huo utakuwa ni mwisho wa Kikwete, huo utakuwa ni mwisho wa CCM!
Mkuu MKJ,
Niliisoma hii habari siku nying kule kijijini kwako, lakini leo naiona ikiwa kama vile inazidi kunikosha! I am not emotional, but today I have droped some tears.........
May God Bless us all to bring up change that we desparately need
Mungu ibariki Tanzania. Wape ujasiri NEC wa kutopendelea chama tawala. Mpe ujasiri Davis Mwamunyange aache uswahiba na JK, bali awe tayari kuzuia ghasia ambazo CCM imejiandaa kufanya ili kuchakachua matokeo. Mpe maono Said mwema kwamba nchi hii ni ya wote, asithubutu kutumia jeshi lake kutishia watu ili kushinikiza matokeo. CCM imeangunka kabla ya Oct 31. JK anajua hili. ila hatakubali, na hapo ndipo penye shida......