MAFISADI NA UFISADI unaofanywa na baadhi ya wajumbe au wanachama wa CCM ipo siku utaanguka na wataanguka ,ni kweli ufisadi upo popote paleduniani lakini UFISADI unaodidimiza maendeleo ya nchi ni ufisadi unaofaa kupingwa na kila binaadamu kwa jinsi anavyoweza,naujadili ufisadi wa nchi masikini kama Tanzania.
CCM LEO haiwezi kuwaambia wananchi iko sawa wakati ndani yake kuna ufisadi wa kutisha mpaka unaweza mtu ukaamini nchi ya Tanzania ni kwa ajili ya watu wachache na si nchi ya waTanzania wote,NDANI YA CCM LEO HII KUNA MAFISADI WA AINA TATU
AINA YA KWANZA NI MAFISADI WANAOPINGA KUITWA MAFISADI: hawa ni wale mafisadi ambao wao wanaona kama wanaonewa lakini ukweli ni kwamba ni kweli ni mafisadi wa kutisha na ndio wanaokisumbua na kukitingisha chama chao cha CCM,hawa ni kama wakina EDWARD LOWASA,CHENGE,ROSTAM AZIZ,SUBASH JITU PATEL, TAMIL SOMAIYA,YUSUPHU MANJI,hawa ndio mafisadi wanaona wanaonewa na kundi la linalowapinga wao wakidhani linaongozwa na SAMWELI SITA,wamekosea sana kudhani hivyo,kweli akili ni nyweli kila mtu ana zake..... hawa mafisadi nitawachambua mmoja baada ya mwingine kwani nimewafuatilia kwa muda mrefu nami si mtu wa kukurupuka hata kidogo.... hata kidogo.......
AINA YA PILI NI MAFISADI WANAOWATETEA MAFISADI KWA NJIA YEYOTE ILE: sina sahaka kabisa hawa wako wengi ndani ya chama,serikalini na hata mitaani,japo mimi hao wa mitaani hawanisumbui sana ndani ya CCM wako kama kina KINGUNGE NGOMBALE MWILU,SOPHIA SIMBA,MAKONGORO MAHANGA,LAURENCE MASHA,ndani ya serikali yuko mmoja ndio kama nguvu yao wanayoiamini EDWARD HOSEA(bw takukuru)
AINA YA TATU YA MAFISADI NI WA MITAANI hawa wanaweza kuwa walishastaafu siku nyingi lakini kwa kuwa wanauswahiba na mafisadi ndio wanaotembeza habari mbali mbali huko mitaani kwamba LOWASA NA WENZIE SI MAFISADI bali wameonewa hakuna haja ya kujua sana sana hawa
MAFISADI ni kweli kama wanavyozungumzwa na vyombo vingi vya habari wananguvu ya kutisha ndani ya serikali,na sasa wanajitahidi nguvu hiyo iwepo katika chama na niwasifu kwa hilo maana wameweza kumtingisha SPEAKER WA BUNGE LA NCHI YA TANZANIA SAMWELI SITA katika mkutano mkuu wa NEC YA CCM ,kama si mtazamo wa mwenyekiti wa CCM yao,muda huu tungekuwa tunazungumza mengine ndani ya nchi ya Tanzania
kwa waTanzania wengi musiojua UFISADI wao unakadiriwa kuwa ni TRILLIONI 22 ZA KITANZANIA,SISEMI KUWA NA PESA NYINGI NI UFISADI BALI WALIVYOZIPATA NDIO KUNAPELEKEA NIWAITE MAFIDASI,kila mmoja amezipata kinyume na katiba na sheria na nchi ya Tanzania.
wadau musishangae mkisikia mkisikia wanachanga bilioni nne kwa ajili ya kutaka kummaliza mbunge fulani asichaguliwe mwakani ,kwao ni kitu kidogo sana,kwani wanajua zitarudi tu,KAMA ROSTAM KAWEZA KUMPA SOPHIA SIMBA MILLIONI 400/- kuhakikisha anashinda uchaguzi wa UWT,na ameshinda sintoshanga anapopeleka BAISIKELI 200 KYELA KWA MWAKYEMBE,500 URAMBO KWA SITA,huyu waTanzania tuliharibu wenyewe pale tulipokubali awe katika BOARD MEMBER YA FDI(forign direct investiment ya dunia) akiiwakilisha Tanzania..........sijui viongozi wa wakati huo walikuwa wanalala usingizi wa namna gani sijui...huyu UMAFYA WAKE UKO KILA MAHALI mfano ni RAIA WA NCHI KAMA VENEZUELA,UEA,CANADA,OMAN,IRAN, huko kote ana ASSET ZISIZO KUWA NA KIKOMO,leo mwakiyembe anaposema atapambana naye mpaka kufa mimi naseme namtakia kila la kheri na waTanzania tumuombe kwa MWENYEZIMUNGU AWEZE KUFANIKISHA HILO....KILA LA KHERI DAKTARI MWAKYEMBE......... mtu ambaye anaweza kupokelewa kama Rais wa nchi anapotua Dubai International airport,nafikia kusema zaidi ya rais ni jeshi la UAE linampokea namna hiyo kila anapokwenda huko,Je leo kwanini asipange mambo ndani ya nchi masikini kama TANZANIA awezavyo? huyu anaweza kumuita waziri yeyote saa yeyote atakayo kama anaita mfanya kazi wake wa ndani .....LAWRENCE MASHA HAWEZI KUBISHA katika hili, huo ni mfano mmoja tu akibisha nitaijulisha dunia ni lini wapi,saa ngapi,mwaka gani,siku,tarehe ilifanyika hilo
nataka niseme hivi LOWASA ndio mtu wa kwanza kujuana na ROSTAM NA si JAKAYA kama wengi wanavyofikiri,ndio baada ya hapo wakajenga kitu tunaita PEMBE TATU,na mahusiano ya LOWASA NA ROSTAM NI KIBIASHARA ZAIDI KULIKO SIASA,isipokuwa wanapokutana wote watatu ndio wanajenga mahusiano ya KISIASA.
WIKI IJAYO nitaeleza walijipanga vipi kuhakikisha wanaingiza nguvu zao ndani ya chama nikianzia na UCHAGUZI WA NEC YA CCM YAO YA SASA ilivyo kuwa hapo ndio waTanzania mutajua HATMA YA CCM IKO WAPI KATIK SIKU ZA BAADAE?
KAMATI YA MZEE MWINYI inaendelea na kazi tusubiri ,nitachambua humu mjengoni wanaopinga UFISADI wamejipanga namna gani kuhakikisha wanakabiliana nao kila kukicha,tuishie hapo
ALUTA CONTINOUR
MTAFITI
mtafiti@yahoo.com