Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

Hawa jamaa mwisho wa siku wanaingia zizi moja tu
 
Hawa jamaa mwisho wa siku wanaingia zizi moja tu


Ni kweli. Nilikaa kwenye mazungumzo ya faragha watu wachache na kiongozi mmoja mkuu wa ki-taifa (PM) wa zamani. Alitoa maoni mengi na moja ni kuwa JMK pamoja na kuwa na nia nzuri na nchi lakini nchi inamshinda na itaendelea kumshinda kutokana na uswahiba wake na wajanja wachache (na akawataja majina watu kama sita hivi). Ajabu ni kuwa mwezi mmoja baadaye huyu huyu bwana akiwa kwenye NEC Butiama, hakusema lo lote la kumsaidia JMK na nchi zaidi ya kusema kuwa kuna haja ya CCM kuwa na mshikamano na mtazamo mmoja. Go figure!
 
Hivi sasa ni takriban miaka 40 imepita tangu nchi yetu ipate uhuru kutoka kwa Waingereza. Miaka 40 si michache kwa nchi yenye viongozi wenye upeo wa kuona mbali na kuwa na mikakati ya kuwakomboa wananchi wake kutoka kwenye lindi la umaskini. Hata hivyo, jambo la kusikitisha ni kuwa cha kinachojiita cha mapinduzi kimeshindwa kabisa kuwaongoza watanzania na kuwaletea maendeleo. Hili ni jambo la aibu sana. Awali, watu wengi walikuwa wanajiuliza inakuwaje nchi hii iwe kwenye orodha ya vinchi maskini Duniani wakati imejaliwa na Mwenyezi Mungu kila aina ya rasilimali kuanzia madini, wanyama na kubwa zaidi ardhi?!?!?!? Jambo la kutia moyo ni kwamba angalau sasa watanzania tumebaini kuwa kumbe mojawapo ya vikwazo vikubwa vya maendeleo ya nchi yetu ni UFISADI unaofanywa na viongozi waandamizi wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi. Misingi mizuri ya kiuchumi kuanzia sekta ya kilimo hadi viwanda vidogovidogo na vikubwa imebomolewa na viongozi hao hao waandamizi wa Serikali. Kwa maneno mengine, pamoja na sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wetu watanzania, kama nchi, umaskini wa Tanzania umechangiwa kwa kiasi kikubwa na Chama kinachojiita cha Mapinduzi. Kwa maoni yangu, watanzania kuzungumzia maendeleo chini ya CCM ni kuota ndoto za mchana.

Hayati Mwl. Nyerere aliwahi kusema kwamba CCM anaipenda lakini si zaidi ya Tanzania. Maneno hayo aliyatamka wakati fulani akielezea uchafu uliokuwa ukifanywa na viongozi wa Serikali pasipo kukemewa na Chama. Mwalimu Nyerere alionesha masikitiko makubwa kwa jinsi chama kilivyokuwa kimepoteza mwelekeo na kuacha misingi yake muhimu. Leo hii chama cha CCM kipo kwenye hali mbaya zaidi ya wakati ule mwalimu alipokuwa akitoa maoni yake. Watanzania sasa Mungu amewafumbua macho na kubaini kuwa hiki si Chama Cha Mapinduzi bali ni Chama Cha Majambazi (Mafisadi) wanaodidimiza hali ya maisha yao kiuchumi na hata kisiasa na kijamii. Kila mwaka wa uchaguzi ukifika, watanzania tunadanganywa kwa kauli za kututia moyo; kauli za kutufanya tuvute subira. Lakini kikishinda uchaguzi basi hali inakuwa mbaya zaidi na zaidi. Fikiria, mbwembwe za Kikwete na mtandao wake. Eti sijui "maisha bora kwa kila mtanzania", mara ooohh, "tumaini lililorejea", n.k. Wote huu ni udanganyifu mkubwa na usanii wa kupindukia. Maisha ya watanzania yameendelea kudidimia siku hadi siku wakati wao wakiendelea "kutanua". Kila kukicha tunasikia Rais wetu yupo Marekani, Uingereza, Japan, n.k. Muda anaokaa Rais nchini mwake kushughulikia wapiga kura wake ni mfupi kuliko anaotembelea nchi za wenzie zenye "maziwa na asali". Yeye anadhani wenzie walijenga nchi zao kwa kutembeza bakuli kama anavyofanya yeye. Hayati Mwalimu Nyerere alisema na nanukuu "kazi ndiyo msingi wa maendeleo. Nchi maskini haiwezi kuendelea kwa msingi wa fedha. Nchi maskini haiwezi kujitawala kama inategemea misaada kutoka nchi za nje", mwisho wa kunukuu. Viongozi wetu wakiongozwa na Kikwete wanajidanganya na kupoteza muda mwingi “kutembeza bakuli” badala ya kutulia nchini mwao wakishirikiana na wananchi kufanya kazi kwa bidii na kujiletea maendeleo. Wanadhani maendeleo yataletwa na mabilioni ya akina MCC kumbe hata tukijaziwa fedha nyingi kiasi gani pasipo kufanya kazi kwa bidii na maarifa ni bure tu.

Ndiyo maana nasema CCM imepoteza mwelekeo na hivyo haina jipya la kuwasaidia watanzania kuachana na umaskini. Chama kimekuwa kama gari kuukuu; lisilotengenezeka, ambalo kutolitumia ni faida zaidi kuliko kulitumia. Njia pekee ni kulitelekeza na kuangalia uwezekano wa kuwa na gari jingine imara linaloweza kutufikisha kwenye nchi ya “maziwa na asali”. Watanzania tusiogope kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini. Tunaweza kuongozwa na chama chochote cha siasa. Wenzetu Wakenya, Wamalawi, Wazambia, Waghana, n.k., mbona wameonesha njia!!?? Kwa nini tusikiadabishe hiki Chama Cha Mafisadi kwa kuchagua chama kingine.

Gosbert, G
Niandikie: gosbertgoodluck@yahoo.com
 
Dhana hii ina umuhimu na maana zaidi leo kuliko wakati mwingine wowote ule katika maisha yetu watanzania. Ni ama tukubali kuiua CCM au tukubali CCM ituue sisi,kupanga ni kuchagua!
 
karume lazima ang'olewe, jk itabidi ajiuzulu, sitta lazima atang'olewa....sasa hivi ccm ! wow................tuendeleeni kupoteza muda ili kijiwe kisiwe cha baridi !

Makada wamekosa ubunifu, wameambiwa wahakikishe kila wakati wanaadika humu, lakini ukweli ni kwamba hawajui what is next!!!

CCM ni chama cha watanzania wote including wanachama wa vyama vingine, na ndiyo maana wakati wote wanaikosoa na hayo ndiyo mafundisho makubwa ya CCM.

Tuendelee kuburudika KM?
 
Msikimbie vivuli vyetu wakuu, yaani sizitaki mbichi hizi, sour grapes bwana kaaazi kweli kweeeeli,

tatizo Hussein Mwinyi na Nape sio mafisadi, ni watoto wa lowassa tu ndio mafisadi, Ridhiwani si tumeambiwa hapa kuwa ni safi au?

Haya wakuu mambo yote Columbus, nitakuwepo ninakuja kummwaga ma-Rap kibao si unajua enzi zile nilipokuwa DJ huko ma-NY, sasa nataka kuja huko kukumbushia haya wakuu tukutane huko hakuna siasa, ni kula kuku tu wallahi ninakuja kuwaga ma-Rap mtindo wa LL Coool J, Mazee Big Daddy Cane, Heavy D, Doug Fresh yaani itakuwa kutoka Radioooo ya station ya FMES, yaani vitu Jinglig baby na Raw, mazee Geeque I hope you are coming tooo, waalllahi asiyekuwa na mwana abebe jiwe, mazee Nyani vipi mkulu wangu are you on, au?

Wakuu are we on au?


Ovyoooooooooooooooooooooooooooooooooooo! majisifa tu, wote tungebanika starehe zetu humu nani wa kumtetea mkulima wa kijijini
 
kwani CCM ndo fisadi?CCM haitakufa maana kuna wasafi pia!

Hollo, baadhi ya hao wasafi wanatetea mafisadi na ndiyo maana watu wanaona mwelekeo huo hauipeleki sisiemu mahali pazuri. Kama wewe ni mkereketwa mzuri wa sisiemu basi ungefurahi kuona wakosoaji wanasema nini ili kirekebishwe na hatimaye kuwa na sisiemu safi. Watu wenye akili nzuri wanapenda hivyo.

Lakini kwa sababu ya unafiki na kutaka kuficha maovu yanayofanywa na baadhi ya wanachama wa sisiemu sioni nuru inayong'ara bali giza tu. Wakati sisiemu inazaliwa mimi nilikuwa mmojawapo wa vijana chipukuzi. Na tulikuwa tunaimba: "sisiemu ndiyo baba na ndiyo mama" - kwa maana kwamba malezi yaliyotarajiwa kuletwa na sisiemu yalikuwa sawa na malezi ya mzazi kwa watoto wake.

Nia ilikuwa ni kuleta mapinduzi katika maisha ya Watanzania - yaani, kuleta "maisha bora". Leo yote hayo hamna na kama bado yanasemwa ni unafiki tu.

Tunaona rasilimali za nchi zinatafunwa bila huruma na haya na wakubwa na masiha ya wananchi yanazidi kuwa magumu zaidi na zaidi. Hapa hakuna mapinduzi wala maisha bora bali RETROGRESSION!
 
kwani CCM ndo fisadi?CCM haitakufa maana kuna wasafi pia!
aliyemsafi ndani ya CCM ajitokeze awe wa kwanza kuwarushia mawe kina Chenge na mafisadi wote!!! hakuna msafi ndani ya CCM na hilo liko wazi
 
kwani CCM ndo fisadi?CCM haitakufa maana kuna wasafi pia!
samaki mmoja akioza MTOE miongoni mwa wenzake,mavi ya kale hayanuki!!!!!!!!!!!!KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!nyinyi ndio wale mliokosa vyeo mnatapatapa,waswahili walisema mfa maji heshi kutapatapa,ndani ya ccm ninaamini wapo wasafi MUDA ukifika mtawajua tu wajameni watu wako kwenye mazoezi sasa,wachafu wote watatoka kwani watakosa pa kuegemea, ni kweli ndugu yangu anavyosema wasafi wapo!!!
 
Ni wazo mwanana,lakini na sindano ya ganzi hii watanzania tuliyopigwa,nina wasiwasi kama wazo hilo linatekelezeka.
 
samaki mmoja akioza MTOE miongoni mwa wenzake,mavi ya kale hayanuki!!!!!!!!!!!!KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!nyinyi ndio wale mliokosa vyeo mnatapatapa,waswahili walisema mfa maji heshi kutapatapa,ndani ya ccm ninaamini wapo wasafi MUDA ukifika mtawajua tu wajameni watu wako kwenye mazoezi sasa,wachafu wote watatoka kwani watakosa pa kuegemea, ni kweli ndugu yangu anavyosema wasafi wapo!!!

chukua muda kufikiri kabla hujaruhusu vidole vyako kuandika. kuna watu humu ndani ni Maprofesa ambao hawajuani hata na huyo mgawa vyeo(Rostam Azizi) kwa humu wenye hasira na kunyimwa vyeo hawamo,ukiwataka nenda Pale mtaa wa Lumumba au Muulize makamba atakuonyesha walipo.
 
.....CHA MUHIMU KWA MTIZAMO WANGU NI...VIONGOZI BORA!! maana hata kama siasa itakuwa safi namna gani, viongozi wenye mikono michafu wataichafua tu!! kama hakuna kabisa viongozi wasafi hapa kwetu, basi shime tuwakamate waliopo tuwasafishe hadi watakate watake wasitake hata kama kwa masasa wa chuma ama dodoki! si wameomba kuwa viongozi, na mashrti ya uongozi lazime wawe wasafi!!!!!
 
chukua muda kufikiri kabla hujaruhusu vidole vyako kuandika. kuna watu humu ndani ni Maprofesa ambao hawajuani hata na huyo mgawa vyeo(Rostam Azizi) kwa humu wenye hasira na kunyimwa vyeo hawamo,ukiwataka nenda Pale mtaa wa Lumumba au Muulize makamba atakuonyesha walipo.

Coolgirl uko sawasawa kabisa na huo ndiyo uhuru wako ulionao wa kujieleza kwa yale unayoyaamini ni sawa.

Baadhi ya watu ni mashabiki tu wasiojua ni nini kitafuata baada ya hapa. Ugomvi uliokuwepo kati ya Mbowe na Rostam umegeuzwa ni ugomvi wa CHADEMA na CCM. Ni heri mngeufanya ni ugomvi wa Tanzania Daima na Rai hapo kidogo ningewaelewa.
Endeleeni na upofu wenu bila ya kujiuliza 'what is next?'
 
Endeleeni na upofu wenu bila ya kujiuliza 'what is next?

Acha matusi haya mkuu, sio lazima urushe haya maneno ya low class ili kueleweka, hapa JF hakuna vipofu, serikali haiwezi kufunga forum yenye vipofu!

Waziri Mkuu Lowassa hwezi kuja hapa JF kujibu vipofu, hoja hujbiwa kwa hoja, sio matusi!
 
Ovyoooooooooooooooooooooooooooooooooooo! majisifa tu, wote tungebanika starehe zetu humu nani wa kumtetea mkulima wa kijijini

Siwezi kukusaidia matatizo yako, kwamba umekulia kijijini sio kosa langu na wala sio kosa kukulia kijijini, ila ni wasi wasi wako tu, maana angalau simtapeli mtu na maneno yangu hayo ya starehe au?

Hakukatazi mtu hapa kutuambia jinsi ulivyokuwa DJ huko Mwakaleli!mtumzima Oooooooohvyo
 
Acha matusi haya mkuu, sio lazima urushe haya maneno ya low class ili kueleweka, hapa JF hakuna vipofu, serikali haiwezi kufunga forum yenye vipofu!

Waziri Mkuu Lowassa hwezi kuja hapa JF kujibu vipofu, hoja hujbiwa kwa hoja, sio matusi!

Coolgirl uko sawasawa kabisa na huo ndiyo uhuru wako ulionao wa kujieleza kwa yale unayoyaamini ni sawa.

Baadhi ya watu ni mashabiki tu wasiojua ni nini kitafuata baada ya hapa. Ugomvi uliokuwepo kati ya Mbowe na Rostam umegeuzwa ni ugomvi wa CHADEMA na CCM. Ni heri mngeufanya ni ugomvi wa Tanzania Daima na Rai hapo kidogo ningewaelewa.
Endeleeni na upofu wenu bila ya kujiuliza 'what is next?'
 
CCM haita kufa jamani watu watakufa na kuiacha!CCM ina mapembe itawachoma kwenye mbavu na mtaiacha hai kabisa!

ccm ni lazima ife ili izaliwe upya...Watakaoiuwa(REVOLUTION) ni wananchi wote bila kujali vyama...Wananchi wasigawanywe kwa sasa...Huu ni wakati wa kudai chetu ndani ya ccm halafu tuje pamoja tu unde chama cha watanzania...Chama chenye kuyajali maslahi ya wananchi wake wajinga na masikini...Hayo mapembe ni lazima yakatwe kwasasa..Tunahitaji chama chenye upendo kisichokuwa na washirikina na wauwaji...Nchi inaenda wapi?
Taifa liko mikononi mwa wananchi na si ccm yenye mapembe na yenye kuwachoma wananchi kila kukicha NA KUWAUWA!
 
Kigogo alia makundi CCM

Tuesday, 07 April 2009 16:17

Na Gladness Mboma

Majira

KATIBU wa Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Amos Makalla amesema makundi mengi yanayojengwa ndani ya chama hicho ni ya tangu mwaka 2000 hadi 2005 ambayo kwa sasa yamegeuzwa kuwa miradi.

Bw. Makalla alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati za utekelezaji za jumuiya hiyo Mkoa wa Pwani mara baada ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya chama hicho.

"Inashangaza sana mpaka sasa watu wanaendeleza makundi na visasi ya uchaguzi mkuu wa tangu mwaka 2000 hadi 2005 na hayo makundi ndiyo yanayorudisha nyuma chama na si kitu kingine.

"Ukitaka kuwa mwanasiasa mzuri unatakiwa kupunguza maadui na kuongeza marafiki. Ni lazima tuwe kitu kimoja, makundi hayajengi bali yanabomoa," alisema.

Alisema makundi hayo yamekuwa yakichukua ajenda ya kupambana na rushwa na ile ya ufisadi ambayo ni ya CCM, huku wengine wakiwa wamesahau madhambi yao.

Bw. Makalla alisema alishangazwa na kauli ya Waziri Mstaafu Bw. Hassy Kitine aliyoitoa hivi karibuni kwa vyombo vya habari kwamba Serikali inaendeshwa kwa makundi na Idara ya Usalama wa Taifa inapwaya.

"Bw. Kitine akumbuke kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliojisahahu huku akijua ana madhambi makubwa ambayo leo angekuwa ameozea gerezani kwa kashfa ambayo iliwahi kumkumba ya matibabu ya mkewe. Je, anakumbuka?

"Kitine asitufanye Watanzania wasahaulifu. Je, anaweza kuwa miongozi mwa watu wasafi? Ieleweke ajenda ya kupambana na rushwa na ufisadi ni ya CCM kama chama na si kikundi cha watu wachache," alidai.


Alisema wapo wana-CCM ambao sasa wameamua kuibuka na kuikosoa Serikali wakati wangekuwa vijijini au magerezani kwa kashfa ambazo ziliwahi kuwakumba enzi za uongozi wao.

Wakati huo huo, Bw. Makalla amedai Rais Jakaya Kikwete ataendelea kuwa Rais 2010, kwani wapinzani hawajawa tayari kwa urais bali wanataka kuokoteza mitaa, vitongoji mwaka huu na mwakani wanajipanga kwa ubunge na udiwani na si urais.

Aliwataka wana-CCM kuhakikisha wanashinda kwa kishindo uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu ili uchaguzi mkuu mwakani wapinzani waambulie patupu.

Aliwataka viongozi kutofanya mikutano ya ndani na badala yake wafanye mikutano mikubwa ya hadhara na kuzungumza na umma kile ambacho Serikali imefanya.
 
Hivi wana Jf huyu jamaa anaejidai kada,kigogo anasahau kuwa anapomnyoshea mkono Kitine kuwa ni mchafu,amesahau kuwa yeye ni mchafu zaidi?Amos anafahamika kwa kula Rushwa,itakumbukwa kuwa mpaka leo subash patel ndie anaempatia Fedha na Mabati anayogawa kila kukicha Mvomero.

Itakumbukwa kuwa kama Mradi wa UVCCM ungelifatiliwa huyu jamaa ndie aliehusika kuuza Jengo lile anavomuuliza KITINE kuwa watanzania si wasahaulifu,afahamu kuwa hata yeye anaboliti ambalo litakuwa linamtafuna mpaka uzeeni kwake afadhali kitine ameisha zeeka.

Amos anafahamika jinsi anavogushi risiti,na malipo hapo ccm huku akitumia umbumbu wa kina makamba kujitajirisha,asionglee usafi yeye ni mmoja wa watu wachafu ambao wanajificha katika udhaifu wa kikwete kupenda kusifiwa na kusahau maovu yao,pale ccm huyu jamaa ni picha RA ndie muweka hazina,ktk waadilifu,wasafi,wanaotka kutuamisha na yeye ni mmoja wakati hana usafi wowote.
 
Back
Top Bottom