Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

CCM haiwezi kufa ila viongozi wezi na mafisadi ndiyo watakufa,CCM ni chama ambacho kimezaa watoto wengi,waharibifu na walio bora.wanopenda kumpinga mama yao wakati kakosea

1.Maalim seif alishwahi kuwa CCM,aliondoka ila CCM baod ipo
2.Padri slaa alikuwa CCM akaondoka
 
CCM haiwezi kufa ila viongozi wezi na mafisadi ndiyo watakufa,CCM ni chama ambacho kimezaa watoto wengi,waharibifu na walio bora.wanopenda kumpinga mama yao wakati kakosea

1.Maalim seif alishwahi kuwa CCM,aliondoka ila CCM baod ipo
2.Padri slaa alikuwa CCM akaondoka

hapo namba 2 - mkewe kabaki ccm na ni diwani ! hongera mama slaa !
 
wengine wanaganga tu njaa, wanakula wengine wao wako huku...

nasema tena jamani ccm itakufaa!!!!!!!!!
 
ooh haifi, itatawala milele, sijui ita...!

mbona iko icu saa hizi, dokta kashasema wakiondoa mashine tu, ndo mwisho - serikali inaweza hata sasa kutangaza kuwa imekufa.

Poleni sana waganga njaa wetu.
 
ooh haifi, itatawala milele, sijui ita...!

mbona iko icu saa hizi, dokta kashasema wakiondoa mashine tu, ndo mwisho - serikali inaweza hata sasa kutangaza kuwa imekufa.

Poleni sana waganga njaa wetu.

naona pia mawazo yako yapo ICU !
 
Heeee Jamani Wana JF, Hili la CCM kufa au kutokufa. Sisi pia tunaweza kuwa wanaccm na tukatumia Jina lake kubwa kuwin hii nchi na kuwahakikishia mafisadi hawana lao tena. Si unajua kuwa Company yenye jina ndio nzuri. Kuisafisha CCM ni garama ndogo sana kuliko kuanzisha chama kingine. Tunahitajika vijana tuingie CCM tuwachachavye hawa mafisadi kwani ukitaka kumuua nyuni usimsubiri atoke kichankani kwake mfuate hukohuko. Huenda ukamkuta amelala. Vijana amkeni, okoeni taifa lenu.
 
Waambie hao wapinzani ipole.
CCM haifi na wala haiendi kokote kule.
CCM itatawala milele zote Tanzania - na that's a fact!


Mkuu,umeshawahi kuwa na maradhiya kichwa siku za karibuni?
Pole sana ndugu yangu,kazania matibabu
 
Waambie hao wapinzani ipole.
CCM haifi na wala haiendi kokote kule.
CCM itatawala milele zote Tanzania - na that's a fact!

kwa haya yanayotokea ya viongozi waandamizi wa CCM kubambwa wanawanga usiku wa manane, kweli tunahitaji kupiga ramli kama wao wanavyopenda ushirikina ili kujua kama chama choa kinakufa au la?
 
kwa haya yanayotokea ya viongozi waandamizi wa CCM kubambwa wanawanga usiku wa manane, kweli tunahitaji kupiga ramli kama wao wanavyopenda ushirikina ili kujua kama chama choa kinakufa au la?

wewe unaota kweli, yaani ccm na mapesa yote hayo nani ataitoa madarakani? wakimuona Rostam tu wapinzani wote chali, na hapo manji hajatokea. Hao wawili wakizidiwa basi Sinclair mwenyewe anajitokeza kuziba kiraka kabisa.

Mwaka 2010 wananchi wote Tanzania watapewa vitenge, kofia na tisheti na bila kusahau chumvi ya kuweka kwenye maji ya kunywa na wote wanapigia chama kubwa kura.

Weka mayai yako kwenye kapu la ccm na usipoteze muda huko kwingine rafiki yangu. ccm iko hapa na wapinzani ndio watayeyuka wenyewe kama vile walivyoanza kuyeyuka hapa JF.
 
wewe unaota kweli, yaani ccm na mapesa yote hayo nani ataitoa madarakani? wakimuona Rostam tu wapinzani wote chali, na hapo manji hajatokea. Hao wawili wakizidiwa basi Sinclair mwenyewe anajitokeza kuziba kiraka kabisa.

Mwaka 2010 wananchi wote Tanzania watapewa vitenge, kofia na tisheti na bila kusahau chumvi ya kuweka kwenye maji ya kunywa na wote wanapigia chama kubwa kura.

Weka mayai yako kwenye kapu la ccm na usipoteze muda huko kwingine rafiki yangu. ccm iko hapa na wapinzani ndio watayeyuka wenyewe kama vile walivyoanza kuyeyuka hapa JF.

Kuna chama kilichokuwa na nguvu duniani kama cha kikomunisti cha Urusi,leo hii kiko wapi? wewe ndiyo unaota!
 
kILA KITU HUWA KINAKUA KUKOMAA ,KUZEEKA NA HATIMAYE KUFA .

CCM PIA INAPITIA HATUA ZOTE HIZO NA SASA KIPO HATUA YA MWISHO.
 
kILA KITU HUWA KINAKUA KUKOMAA ,KUZEEKA NA HATIMAYE KUFA .

CCM PIA INAPITIA HATUA ZOTE HIZO NA SASA KIPO HATUA YA MWISHO.

katika birthday kuna kitu huwa tunakikwepa,kila ukisheherekea kuzaliwa kwako ujue wakati huohuo unasheherekea kukaribia kufa kwako! miaka 31 ya CCM inatosha kuipeleka "kuzimu" na siyo ahera baada ya kifo chake!!
 
Ninachojua mimi ni kuwa kila mfumo,huzaliwa,hukua,hukomaa na kisha hufa,iwe CCM? ni lazima ife siku moja,hata kama si kesho basi keshokutwa.
 
Ninachojua mimi ni kuwa kila mfumo,huzaliwa,hukua,hukomaa na kisha hufa,iwe CCM? ni lazima ife siku moja,hata kama si kesho basi keshokutwa.
CCM haita kufa jamani watu watakufa na kuiacha!CCM ina mapembe itawachoma kwenye mbavu na mtaiacha hai kabisa!
 
Waswahili husema dua la kuku halimpati mwewe CCM haitakufa na kwa ni kife kwa ajili ya chuki zako CCM siyo fisadi mafisadi ni watu siyo chama

kwani CCM ni nini kama siyo watu? siyo kila mwenye kadi ndiyo CCM bali wafanya maamuzi ndiyo CCM. kwa mfano tulipopeleka jeshi Comoro siyo watanzania wote waliamua kupeleka jeshi Cmoro, bali Rais ambaye kimantiki ndiye Tanzania!

unapossema CCM siyo fisadi bali watu ndiyo fisadi unamaanisha kwamba CCM siyo chama cha watu bali ni chama cha "mahayawani?kama Kikwete Fisadi au anakumbatia mafisadi, Makamba awe fisadi,Chenge fisadi,Kingunge fisadi,Mkapa fisadi.... bado tuu CCM siyo chama Fisadi?
 
kwani CCM ndo fisadi?CCM haitakufa maana kuna wasafi pia!

CCM ni watu na watu walioko CCM ndio mafisadi. na kama CCM kuna waliosafi kwanini wasiisafishe CCM, kwanini wakubali kukaa na mafisadi ndani?? au unataka kutuambia wewe unapenda kukaa na majambazi na huoni kama kuna tatizo?/?
 
Tishio jipya CCM

na Martin Malera, Dodoma



KIKAO cha Bunge la Bajeti kiliendelea mjini Dodoma jana huku upepo wa kisiasa ukionekana dhahiri kuendelea kukigawa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika makundi ambayo sasa yanatoa mwelekeo wa kihasama kuliko wa kishindani.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima kwa siku nzima jana na kufuatilia kauli zilizotolewa na baadhi ya wabunge, zinaonyesha kwamba semina ya mwishoni mwa wiki iliyojumuisha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na wabunge wanaotokana na chama hicho tawala, imethibitika kuzaliwa na kushamiri upya kwa makundi.

Aidha, semina hiyo kwa upande mwingine, imethibitisha kwamba vidonda vilivyotokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 ndani ya chama hicho havijapona na bado vinakitafuna chama hicho.

Mmoja wa watu waliohudhuria kikao hicho ameieleza Tanzania Daima kwamba kauli aliyoitoa ndani ya semina hiyo Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, akisema kuna ‘watu bado wana ndoto za urais’ unaweza ukawa ushahidi kwamba makundi yamegeuka kuwa ugonjwa sugu.

Dalili za kuendelea kushamiri kwa makundi hayo zimethibitishwa na kile kinachodaiwa kutokea ndani ya Bunge jana kati ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Surukamba (CCM) na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango.

Taarifa ambazo Tanzania Daima ilizipata kutoka bungeni jana na zikathibitishwa na Serukamba mwenyewe, zinaeleza kuwa Kilango alimfuata Serukamba katika kiti alichokaa na akamuonya kuhusu matamshi aliyoyatoa wakati wa semina ya mwishoni mwa wiki kabla ya kumtaka ajiandae kwa kisasi.

‘‘Ni kweli leo asubuhi Mama Kilango kanifuata katika kiti changu na kunitisha kutokana na kile nilichosema ndani ya semina jana na akasema eti alikuwa akikusudia kulipiza kisasi, sijui ni kisasi cha namna gani amepanga kulipiza,” alisema Serukamba.

Kwa mujibu wa Serukamba, mbunge huyo mwenzake wa CCM alitoa matamshi hayo wakati wabunge wengine wawili, Ritha Mlaki (CCM-Kawe) na Nazir Karamagi (CCM-Karagwe) wakisikia.

Alipoulizwa ni kitu gani hasa alikuwa amekisema wakati wa semina hiyo ya CCM, Serukamba alisema anaamini pengine ni kauli aliyoitoa kwa makada wenzake wa chama hicho kuacha kuwatuhumu watu katika kashfa pasipo kuwa na uhakika wa kutosha kuhusu kile wanachotuhumu.

Serukamba alikiri kutoa mfano wa matamshi yaliyopata kusemwa ndani ya Bunge na Kilango wakati wa mjadala wa ufisadi kuwa mfano wa tuhuma ambazo zilitolewa pasipo kuwapo kwa ushahidi.

Alipoulizwa ni hatua gani alikuwa akikusudia kuchukua kutokana na kauli hizo, Serukamba alisema alikuwa ameshaamua kumtaarifu Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuhusu suala hilo, pia alikuwa akitarajia kulifikisha mbele ya vikao vya CCM.

Hata hivyo, mwandishi wa Tanzania Daima aliyepo bungeni Dodoma alipomtafuta Kilango bungeni jana mchana na kumkosa, na baadaye kuwasiliana naye kwa simu, mbunge huyo aliahidi kulizungumzia suala hili jioni ya jana, atakapokuwa amerejea bungeni. Hata hivyo hakuweza kuonana naye jana.

Kwa upande wake, Mlaki ambaye ilielezwa na Serukamba kuwa alikuwa karibu kabisa wakati Kilango akitoa matamshi hayo, hakuwa tayari kusema lolote alipofuatwa na mwandishi na kuulizwa iwapo alikuwa amesikia lolote.

Suala hili linatokea wakati huu, wakati ikieleweka bayana kwamba, Kilango amekuwa mstari wa mbele na waziwazi akipambana na ufisadi ndani ya CCM na serikali, wakati Serukamba amekuwa mmoja wa watu ambao siku zote wamekuwa wakipinga kuhusu ufisadi kugeuzwa ajenda ya kisiasa.

Ndani na nje ya vikao rasmi, Serukamba amekaririwa mara kadhaa akieleza kukerwa na namna wabunge wenzake wa chama hicho tawala, akiwamo Kilango, wanavyoufanya ufisadi kuwa ni ajenda ya kumalizana wenyewe kwa wenyewe CCM.

Mbali ya hilo, katika hatua nyingine, taarifa za kuwapo kwa mbunge mmoja wa CCM aliyedaiwa kutupa vitu vya kishirikina ndani ya Bunge mwishoni mwa wiki iliyopita, ziliendelea kuzua mjadala hata baada ya chama hicho tawala kutoa taarifa ya ufafanuzi juzi.

Habari za uhakika kutoka miongoni mwa makada wa chama hicho tawala zinaeleza kuwa, suala hili nalo sasa linaonekana kuchukua mkondo ule ule wa ugomvi wa kimakundi, ambao unakitafuna chama hicho tawala.

Katika hatua ya kushangaza, ofisa mmoja wa juu wa Ikulu jana aliwasiliana na Tanzania Daima na akaitaka kulichukulia kwa uangalifu mkubwa suala hilo ambalo alidai limekuzwa kwa sababu na malengo ya kisiasa.

Mbali ya hilo, ofisa huyo wa Ikulu ambaye hakutaka kuandikwa gazetini, alisema mtuhumiwa mkuu katika sakata hilo ambaye bado jina lake halijatajwa rasmi, alikuwa ameshajiandaa kueleza ukweli kuhusu tuhuma hizo nzito zinazoelekezwa kwake, ambazo iwapo zitathibitika, basi anaweza kutiwa hatiani kwa kosa la jinai chini ya Sheria dhidi ya uchawi ya mwaka 1971, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Wakati hilo likitokea, jana hiyo hiyo Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alilazimika kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu taarifa hizo za watu wanaodaiwa kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge na kufanya mambo yanayodhaniwa kuwa ni ya kishirikina.

Akizungumza bungeni jana, Sitta alisema kuwa mbunge mmoja na ofisa mmoja wa Bunge wanaohisiwa kuweka vitu vya ushirikina ndani ya ukumbi wa Bunge, walifanya tukio hilo majira ya saa 2:10 usiku, wakati wabunge wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walipokuwa kwenye kikao chao.

Alisema ingawa ofisi yake kwa bahati mbaya ilikuwa ikitoa majibu tofauti, asingeweza kupuuzia taarifa ya kuwapo ushirikina ndani ya Bunge, kwani alihisi wahusika waliweka aina ya sumu ya kisasa.

Sitta alisema mara ya kwanza alizipata taarifa hizo Juni 12, siku ya Alhamisi iliyosomwa hotuba ya bajeti kutoka kwa Kaimu Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila.

“Naunganisha na tukio hilo, baadaye siku hiyo hiyo, Mbunge wa Lupa, Mheshimiwa Victor Mwambalaswa, aliniandikia kikaratasi kunijulisha kuwa ameondoka kumsaidia Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe kumpeleka hospitali baada ya kuugua ghafla bungeni.

“Nilihisi inawezekana wahusika walitupa kitu aina ya sumu ya kisasa, nikaona nisipuuzie. Bahati mbaya sana katika majibu, ofisi yangu ilitoa majibu tofauti,” alisema Sitta.

Alisema siku ya Jumamosi, maofisa usalama walifanya ukaguzi wa kitaalamu na kubaini kuwa ukumbi wa Bunge uko salama na kuwataka wabunge kuondoa wasiwasi uliokuwapo awali wa kuwapo aina ya vitu vya kishirikina.

Alisema kwa sasa, maofisa wa usalama wamechukua picha za kamera hiyo zilizopigwa kwa saa 72, sawa na siku tatu kabla ya siku ya tukio, na kuziweka kwenye CD, ili kuangalia kwa makini tukio hilo, ambalo juzi liliwafanya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, mbele ya Mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete, kutofautiana kimawazo.

“Kwa sasa tuchukulie taarifa hiyo kama ni uvumi tu, hadi hapo uchunguzi utakapokamilika,” alisema Sitta.
 
Kuna habari kuwa kuna wabunge wanajiandaa kuihama CCM kwa mkupuo wa pamoja au mmoja mmoja ,kitu ambacho kipo kwenye mashauriano.
Habari zimezidi kutonya kuwa wabunge hao ambao wameamua kulinda maslahi na malengo yaliowapeleka hapo Bungeni badala ya kukaa na kuwalinda watu wasio kuwa na uchungu wa Inchi hii ,wana imani kubwa kuwa WaTanzania walio wengi watawaunga mkono katika kitendo hicho ambacho wamekiita ni cha Kishujaa na utii kwa wananchi na pia wana imani kuwa wananchi waliowachagua kuwapeleka Bungeni watawachagua tena hata wakiwa ni wagombeaq binafsi kwa vile msimamo wao ni kulinda maslahi ya wananchi na kutowaonea haya wezi wa fedha ya Nchi hii na mali zake.
Wabunge hao wamezidi kuipa msonyo CCM kuwa ni Chama kinachoendeshwa kidikiteta na zaidi wengine kujiona wao ni wa Mjini na wanaweza kufanya lolote bila ya huruma kwa wananchi,na kuwafanya wabunge wawe na hali ngumu kurudi kuomba kura tena pale ufikapo msimu wa harakati za kujinadi ili wachaguliwe tena.
Wakizidi kutoa mchapo kuwa CCM kumejaa vigogo ambao wanatumia fedha nyingi kwa kulinda maslahi binafsi na kusahau kama wao wapo hapo kwa ajili ya maslahi ya Taifa na wananchi wake ,ndio ukaona jinsi wanavyoiba fedha ya umma bila ya huruma ..mmoja wao aliongezea.
Wabunge hao ambao wengi wao huwa wanaonekana wakimya ndani ya bunge wamezidi kutonya kuwa safari hii CCM magome watafahamu kuwa mizizi ndio muhimu kwa mti.
 
Back
Top Bottom