Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

kama nyie mnaamini maneno ya mwalimu pia alisema 'upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm'
mimi nashangaa hawa kina Dr.salim,Mwandosya and the likes wanachosubiri nini mpaka sasa??

wanaogopa ngawira babangu! WAKIHAMA CCM WATAKUWA MGENI WA NANI? WAKATI WAFANYABIASHARA WOTE NA WANACHI WANakuabudu ukiwa kwenye ufisadi ? kwani chadema wana benki kuu mahali pa kuchota mabilioni bwelele? sasa nani ahame ccm afe njaa?
 
huwa mnakosea kuhusu msemo wa mwalimu kuwa bila ccm madhubuti ccm itayumba. mwalimu alikuwa na mazoea ya kuzungumza kufuatana na nyakati. kwa wakati ule ilikuwa ni kweli kwa kuwa bila ccm manake ingekuwa ni mrema na nccr mageuzi. lakini mwalimu angekuwepo leo angesema kitu kingine kabisa, yaani bado mnaamini bila ccm ya akina jk, lowas, chenge, rostam, makamba, na wengine nchi itayumba?
pia tunapokariri misemo ya mwalimu tusichukue vipande vipande, kwa pale dodoma kuna bango kubwa sana pale kuu street limewekwa na kampuni moja ya kifisadi inayoitwa OITDOOR LENYE MAANDISHI MAKUBWA BILA CCM MADHUBUTI TAIFA LITAYUMBA. mbona hawajaandika kuhusu msemo maarufu wa mwalimu kuwa ccm si mama yake na kuwa angeweza kuachana nacho wakati wowote?

...Mkuu tupe hint ya hiyo bold quoted text.... nasikia jamaa (zadok) amehamia bondeni baada ya uchaguzi kuisha... nashangaa kama naye hakuwepo ktk wawekezaji wa EPA..... hebu tupe utamu mkuu ktk hilo
 
Unajua hivi sasa CCM haipo waliobaki ni wababaishaji tu,hawajui wanalolifanya ,kila mmoja anasukuma kivyakevyake ,kwa kweli hawajui walitendalo sera na dira vyote vimechawanyika ,kila kiongozi anajijenga kwa mwenzake,kila mmoja anataka aonekane yeye anamlinda mwenzake na hii yote ni kuogopana kwa hizi sifa za viongozi wao zilivyoibuka ,hawa sasa wanaongozana wenyewe kwa wenyewe hawajali ya mwananchi wa kawaida wapo katika kulinda maslahi yao binafsi na hatima yao,ili likitokea la kutokea kila mmoja awe ameshajijenga kwa mwengine ndio ukaona hata kuchukuliana hatua inakuwa ni tatizo kubwa sana ,ila natarajia atakuja kutokea kichwa mchungu miongoni mwao awatolee uvivu wenzake ,Mkapa alijaribu lakini mwishowe akajiunga nao ,Muungwana amejaribu lakini ameonekana kufeli pengine watatu atakae kuja atafanikiwa kuwakusanya akina Mkapa na Muungwana na kuwasweka jela moja kwa moja na hapo ndio itakuwa mwisho wa huyu ni mwenzetu na sapoti ya wenye nchi itampa kifua mbele kuona hakuna ila yeye ndie aliewaweza wahafidhina wezi wa mali ya Taifa la Tanzania na Pemba.
 
kwani CCM ndo fisadi?CCM haitakufa maana kuna wasafi pia!
Huwezi kumkumbatia mwenye mivi na wewe ukatoka na kuonekana msafi ,unajua hata ukisafiri basi abiria wengine wakikuona na pasipoti ya Tanzania utaona wanavutavuta na kukusanya mikobakoba yao karibu na kukutizama kwa jicho la pembeni huku wakikonyezana ,wanatuona nasi ni mafisadi na tunauzoefu wa mkonomkono.Wandugu hawa mafisadi athari yao si ndogo ni hatari kweli.
 
kwani CCM ndo fisadi?CCM haitakufa maana kuna wasafi pia!
kama wapo si wawaondoe mafisadi. Unakumbuka mafisadi wameisha sema ndani ya CCM kuwa wao ni watu wazito? Sasa wazito tena kuna wengine? CCM walisha sema CCM ina wenyewe na wenyewe ni .............
 
kama wapo si wawaondoe mafisadi. Unakumbuka mafisadi wameisha sema ndani ya CCM kuwa wao ni watu wazito? Sasa wazito tena kuna wengine? CCM walisha sema CCM ina wenyewe na wenyewe ni .............

Wenyewe ni wana CCM!ufisadi ni tabia ya mtu na siyo chama!Wewe tulia Dawa ya mafisadi ipo jikoni!pia dawa ya mafisadi tunayo sisi wenyewe maana sisi ndo wapiga kura!
 
Huwezi kumkumbatia mwenye mivi na wewe ukatoka na kuonekana msafi ,unajua hata ukisafiri basi abiria wengine wakikuona na pasipoti ya Tanzania utaona wanavutavuta na kukusanya mikobakoba yao karibu na kukutizama kwa jicho la pembeni huku wakikonyezana ,wanatuona nasi ni mafisadi na tunauzoefu wa mkonomkono.Wandugu hawa mafisadi athari yao si ndogo ni hatari kweli.

jamani ufisadi ni mtu!sio ufisadi wa mtu ukuaffect wewe!sasa mtu aatakaefikiri na wewe ni fisadi eti tu kwa sababu ni mtanzania na nchini kwako kuna mafisadi!Huyo mtu atakuwa hatendi haki.
 
Wenyewe ni wana CCM!ufisadi ni tabia ya mtu na siyo chama!Wewe tulia Dawa ya mafisadi ipo jikoni!pia dawa ya mafisadi tunayo sisi wenyewe maana sisi ndo wapiga kura!

Mkuu kura yako ndani ya chama ni moja tu.

Ufisadi umekuwa ndani ya chama siyo leo ni miaka, sidhani kama wana CCM wana uwezo huo, kama spika wa bunge anayetoka ktk chama aliambiwa kuwa anyamaze make anaongea na watu wakubwa, unafikiri kuna mwana CCm wa kuongea zaidi?

kinachotakiwa Mkuu Hollo tuko pamoja hapa anzisha CCM B isiyokuwa ya mafisadi vinginevyo utakwenda Musoma, utakwenda dodoma nk, upepo utakuwa ule ule, mtabadilisha vikao kwenda bagamoyo ndo utakuwa mwisho.

Cha muhimu kama unataka kuwaletea watanzania maendeo keep sera lakini badili jina hiyo CCM haita weza kumkomboa mtanzania kabisa. kinacho iua CCM ni kubadilisha mwelekeo wa kumkomboa mtanzania na kuwa chama cha biashara. kwa kufanya hivyo CCM imejichafuka vya kutosha. kilichobakia ni waanzirishi wahakikishe inakufa na isifufuke tena kwa sababu imekiuka miiko ya walioianzisha.
 
karume lazima ang'olewe, jk itabidi ajiuzulu, sitta lazima atang'olewa....sasa hivi ccm ! wow................tuendeleeni kupoteza muda ili kijiwe kisiwe cha baridi !
 
Hivi kweli unafikiri CCM itakufa?ama kweli ndoto za mchana!

Mkuu unajua usipokuwa na mawazo kuwa CCM itakufa basi utakuwa umepitwa na wakati. nani achukue CCM mafisadi au? kuna mtu yuko tayari kupoteza au unafikiri migogoro iliyopo sasa inatoka wapi? kanu imekufa lakzima CCm kwa sababu ilianzishwa na watu lazima ife tu. CCM sasa hivi ni kampuni ya kuwalinda majambazi na kama haitawafukuza majambazi lazima ife tu.
 
Huwezi kumkumbatia mwenye mivi na wewe ukatoka na kuonekana msafi ,unajua hata ukisafiri basi abiria wengine wakikuona na pasipoti ya Tanzania utaona wanavutavuta na kukusanya mikobakoba yao karibu na kukutizama kwa jicho la pembeni huku wakikonyezana ,wanatuona nasi ni mafisadi na tunauzoefu wa mkonomkono.Wandugu hawa mafisadi athari yao si ndogo ni hatari kweli.

Acha kujenga hoja za kijinga kwamba tunaposafiri kwa kutumia passport za nchi yetu basi tunashukiwa na kila mtu kuwa watanzania wote ni mafisadi.Kama huna hoja kaa kimya sio kuzusha uongo usiokuwa na msingi.Labda unalenga kuwapotosha wale wasiokuwa na uzoefu wa kusafiri.Watu tunasafiri sana tena kwenda mataifa makubwa,hatujakumbana na upuuzi huo,leo wewe unataka kutufanya wote mazezeta hapa,wacha kabisa ujinga wako huo.
Nchi yetuTanzania pamoja na ufisadi uliojitokeza hivi karibuni,haijafikia kiwango cha kutisha kwa ufisadi kulinganisha na mataifa yanayotambulika duniani kwa ufisadi kiasi cha kwamba basi mtu akiona passport yetu macho yamtoke kama ilivyo kwa baadhi ya nchi.Nakubaliana nawe kuwa athari za ufisadi ni kubwa na ni lazima tuunganishe nguvu zetu kwa kuupiga vita na kuulani kwa nguvu zote,lakini si kwa namna unavyotaka kutushawishi kwa kujenga hoja za vijiweni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom