Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

So huyu jamaa Makala anataka wanyamazia huu wizi eti kisa na wao waliiba? Anataka kutuambia kuwa hawakumpeleka keko kuendeleza kuendeleza utamaduni wao wa kulindana. Sasa anapoongea wanataka kumnyamazisha.


Wezi wakubwa hawa Vigogo na K@#%$ zao, Msitufanye Mabwege........
 
2009-04-19 21:35:40
Na Restuta James

Mbunge wa Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe, ametoa changamoto kwa wazee wa Chama Cha Mapinduzi kukishinikiza chama hicho kiwafukuze wanachama wake wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi badala ya kuwakebehi wanaoongoza mapambano hayo kwa kuwaita wanatafuta umaarufu wa kisiasa na umaarufu wa mtu binafsi.

Mpendazoe aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, alipozungumza na gazeti hili na kutoa maoni yake juu ya tamko la wazee hao, vita dhidi ya ufisadi na rushwa.

Bila kuwataja, alisema wanachama wa CCM wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi ni sawa na misumari ndani ya chama na hivyo wazee wanapaswa kukishinikiza chama kiwaondoe kwenye nyadhifa walizonazo.

Nilitegemea wazee wetu katika kumuunga mkono Mwenyekiti wetu wa chama, Rais Jakaya Kikwete, katika vita dhidi ya ufisadi wangetoa tamko kwamba chama kiwaondoe kwenye nyadhifa wale wote wanaokichafua kwa kuthibitika kuhusika na ufisadi mbalimbali, kwani kuwaacha na nyadhifa wanakuwa ni sawa na mzigo wa misumari kwa chama, alisema.

Alisema sio sahihi kuwaita wanaopambana na rushwa kuwa wanatafuta umaarufu wa kisiasa au umaarufu binafsi ilihali vitendo hivyo vinaongeza ufa kati ya walionacho na wasionacho.

Alitoa mfano kwamba ubadhirifu uliofanywa na watu wachace kupitia kampuni za Meremeta, Richmond na nyinginezo unakadiriwa kufikia Sh. trilioni 1.25, ambazo kama zingetumiwa kwa manufaa ya taifa zingeweza kujenga barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 500 au madarasa 7, 500.

Sio sahihi wazee hawa kuona watu wanaopambana na ufisadi wanatafuta umaarufu ilani ya CCM na katiba ya nchi yetu vinatamka bayana kabisa kwamba kila mwananchi anapaswa kushiriki katika ulinzi wa rasilimali za taifa letu, tunapaswa kuwaunga mkono wale wote wenye nia ya dhati ya kulinda mali za taifa kwa manufaa ya Watanzania wote, alisema.

Kuhusu Jumuiya za CCM kutangaza kumuunga mkono Rais Kikwete na kuwataka wanaotaka kugombea urais mwaka ujao wahame CCM, alisema nia hiyo si sahihi kutangazwa sasa kwa sababu kufanya hivyo ni kuwanyima wananchi haki ya kumchagua mgombea watakayempenda.

Alisema suala la nani awe mgombea urais lipo mikononi mwa wanachama baada ya mgombea kutangaza nia yake ya kutaka kuwa Rais wa nchi hivyo, kufanya maandamano sasa ya kumuunga mkono mgombea fulani ni sawa na kuwashinikiza wanachama wa chama hicho wakubaliane na matakwa ya viongozi wao.

Yanayoanza kutokea ni dalili za mizengwe, nawakumbusha wanachama wenzangu wasubiri muda ufike na wazingatie taratibu za kumpata mgombea na wakumbuke pia kuwa kila mwanachama mwenye sifa anayohaki ya kupiga na kupigiwa kura alisema.

Amewataka wanachama wenzake kuacha chokochoko zisizo na msingi na badala yake wapambane na changamoto nzito zinazolikabili taifa kwa sasa.

Mpendazoe amelipongeza Bunge, Rais Kikwete na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi kwa kuongoza vita dhidi ya ufisadi na kuwataka wasikate tamaa.

Kadhalika, amewapongeza wabunge wa CCM wanaopambana na ufisadi akiwemo Anne Kilango Malecela, Same mashariki (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, Kyela (CCM), Lucas Selelii, Nzega (CCM) na Aloyce Kimaro, Vunjo (CCM).

Mapema wiki iliyopita Wenyeviti wastaafu wa mikoa wa (CCM) wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi, walionya watu wasitumie vita ya ufisadi kama mtaji wa kisiasa na kujipatia umaarufu.

* SOURCE: Nipashe
My Take: Yeye ndo atakuwa wa KWANZA kung'olewa. na hii ni kutokana na siasa za CCM
 
Mpendazoe analilia mno naye! Huenda asirudi bungeni 2010
 
Mpendazoe analilia mno naye! Huenda asirudi bungeni 2010

..si ndiye huyu aliyesema MAFISADI wanataka kumtoa jimboni?? cha msingi kama kazi yake ni njema atapita hata kwa chama kingine ila nakubaliana na hoja yake ya msingi lakini ajue kuwa upepo ukimgeukia watamshukia kama mwewe angani...
 
asitubabaishe bwana kama hapendi ufisadi na atoke huko, si kila siku wanaambiwa hataweza kuwa wasafi wakati wanaoga maji ya tope?
 
Dawa atoke ahamie Chadema au CUF au TLP wananchi waliomchagua ndio wenye nguvu zaidi kuliko CCM ,CCM ni kutumia mapolisi na siku hizi wale polisi wanaotumika huishia jela mambo yanapogeuka ,sijui kama mlimsikia mkuu wa Majeshi ya Thailand alipoulizwa mbona huendi kulinda mambo yanaharibika ,aliruka na kusema hayo hayaingilii kwani upepo ukitulia yatamgeukia na wale wote maswahiba watamruka na kumuona alitumia nguvu zisizostahili na kumuwacha akielekezwa jela au kuhukumiwa kifo huku wengine wale aliokusudia kuwalinda wakiendelea kuponda raha ,It was a powerfull statement to the government na ilikubalika na kuwacha wanasiasa waonyeshane nguvu wenyewe kwa wenyewe maana nchi haijavamiwa na majeshi ya kigeni ,huku akiendelea kunywa soda yake.
 
....Lakini sasa, mawazo yangu nataka kuyaelekeza katika kuundwa kwa nguvu thabiti ya kuiondoa CCM madarakani kuanzia kwenye Bunge 2010 na urais ifikapo 2015, tukiweza kuyafanya yote 2010 itakuwa bora zaidi!
Labda itawezekana siku moja!
 
Nakweli ndugu CCM imejaa mafi na kuanuka 😡 Tumechoka kabisa na CCM kwa sababu awana nafuu kabisa kwa wananchi kabisa. When you look at them, they have no time to fight for our rights but rather colluded with the so called Indians due to corruption.

The 5 PAPAS mentioned are the so called supporting CCM in their elections therefore, they cannot speak. We should congratulate Mr. Reginald Mengi for the courage for mentioning them and there many more in the pipeline. Mr. Mengi anafanya mengi kutosaidia sisi walala hoi wa Tanzania na ni Mtanzania mwenzetu hata kama biidi zake zinawenekana haya hawa Wahindi wanafanya nini kwetu ??? Dawa zao iko zikoni inachemka ??? Na huyo Rastam anakiburi kwa sababu anakula na CCM wenzake na haza Mkapa ndio amewampa kiburi asubiri aone kitema ukuni MSHENJI. Nani anaweka kwenda Iraq kwa Mbunge ??? Yeye si ni M-Iraqi anafanya nini Tanzania?

Hata kama ni Mtanzania.. WaTanzania ni weusi sio rangi ya FANTA. AKOME KABISA kumsemea Mengi laa si hivyo ataona Wa Tanzania walisi katika njia zake.
 
Maneno yako Mzee Mwanakijiji ni mazito; nimetafuta jina la kukubatiza sijalipata.

Naamini mambo manne ni muhimu ili huu utabiri wako utimie.

Kwanza, watu wapigike sana kimaisha na waweze kuhusisha kikamilifu madhira wanayoyapata na utawala wa CCM. Pili, wananchi walio wengi watakapogundua kuwa CCM ni gari lililokwisha kufa na halikarabatiki hata aje dereva awaye yule, awe Mwinyi, Mkapa, Kikwete, na yeyote yule hii gari haiendi. Tatu, wananchi walio wengi waamini kwamba wana uwezo wa kuitoa CCM madarakani kwa kutumia kura zao. Nne, wananchi wakiangalia pembeni waone chama na viongozi mbadala cha kuwapa hizo kura zao. Yaani, waione gari mpya na dereva aliye mwerevu wa kuiendesha.

Mimi nafikiri wananchi walio wengi tayari wameshapigika sana na maisha na kwamba matumaini waliyopewa na Kikwete yameshayeyuka. Ila sidhani kwamba wananchi walio wengi wameweza kuoanisha sawasawa katika kupigika huko kimaisha na utawala wa CCM. Naamini pia kuwa wananchi walio wengi pia bado wanafikiri kwamba tatizo la CCM ni dereva na sio gari. Yaani, wanafikiri ukibadilisha dereva hamna neno. Hadi pale watakapoelewa kuwa CCM ni gari lililokwisha kufa, halikarabatiki hata aje fundi na dereva wa namna gani hawezi! Naamini kuwa wananchi sasa wanaamini kwamba wanaweza kubadilisha uongozi kwa kura zao. Vinginevyo, upinzani usingepata hao wabunmge wachache waliowapata.

Kuhusu vyama na viongozi mbadala (gari jipya na dereva mwerevu)-Japokuwa mwanga umeanza kupenyeza, nafikiri hapa ndio bado kuna kazi kidogo. Tatizo moja kubwa sana lililopo ni kukosekean kwa umoja wa vyama vya siasa. Watanzania wanapenda sana umoja. Kwa hivyo kwa hili la kuwa kila chama kinajiona bora kuliko chama kingine na kijiendeshea mambo yake chenyewe, ni kikwazo kikubwa kwa vyama vya upinzani kupenyeza katika nyoyo za watanzania. Ndio maana makala yako Mzee Mwanakijiji imenikuna hasa ulipogusia muungano wa vyama vya siasa. Nakwambie siku vyama vya upinzani vikiungana, utakuwa ndio mwanzo wa mwisho wa CCM. Lakini nisisitize hapa kuwa sio muungano, bali muungano miongoni mwa vyama vilivyo makini kwani tunajua kuna vyama vingine ni matawi ya haohao CCM.

Mimi ninashawishika sasa kuliko kipindi kingine chochote juu ya nguvu ya ushawishi tulio nayo katika forum hii. Kwa hivyo, nawaombeni ndugu zangu tuanze rasmi kuwapa shinikizo viongozi wa vyama vya siasa wa upinzani waanze mazungumzo ya kuunganisha vyama vyao. Kwa kuanzia ningeomba tuanze na vyama hivi: CHADEMA, CUF, NCCR, TLP na UDP. Ninaamini vyama hivi vikiungana, itakuwa ni nguvu kubwa na itakuwa ndio mwisho wa shutuma za udini na ukabila zinazotusumbua CHADEMA na CUF.

Tunaweza kuanza kwa kuandika barua ambayo wale tunao amini katika muungano tutaisaini. Barua hiyo iwe ni barua rasmi kutoka kwa watanzania wanaoishi nje na iende kwa viongozi wakuu wote wa vyama vya siasa vya upinzani.

Naomba kuwasilisha

Good thinking and response
 
Watanzania jinsi walivyo, huu unabii labda Yesu arudi ndio utawezekana.
 
CCM is the giant of its own kind in the political arena of our country. Niliposoma hii thread nikakumbuka msemo wa kiswahili unaosema asiyejua kufa, achungulie kaburi!! Nikapata hamasa kuchungulia tu hivi kwenye makabuli ya ma giant waliokufa kwasababu ya failures mbalimbali amelala nani!

Suprisingly nilioweza kuwatambua mapema walikuwa World Com, Enron, Lehman Brothers etc etc
Nikajiuliza ilikuwaje haya madubwana yakajikuta yamekwenda mapema kwenye mapumziko ya amani. Moja nililoligundua ni kudharau uhalisi wa mambo ulivyo, utapeli na complacency iliyokithiri ya kudhani kwamba haiwezekani giant kufa hata siku moja. Ingawa yapo mengi mengine yaliyosababisha haya madubwana kulala mapema kwenye makaburi ya waliofeli.

Siasa za leo za TZ zinataka mabadiliko ya kweli tena ya haraka. Chelewa chelewa utakuta mwana si wako. Taratibu tumeanza kufumbuka macho. Inawezekana kabisa my next visit to the graveyard of giants would find CCM close to Worldcom or Enron etc!! Who knows!!
 
CCM is the giant of its own kind in the political arena of our country. Niliposoma hii thread nikakumbuka msemo wa kiswahili unaosema asiyejua kufa, achungulie kaburi!! Nikapata hamasa kuchungulia tu hivi kwenye makabuli ya ma giant waliokufa kwasababu ya failures mbalimbali amelala nani!

Suprisingly nilioweza kuwatambua mapema walikuwa World Com, Enron, Lehman Brothers etc etc
Nikajiuliza ilikuwaje haya madubwana yakajikuta yamekwenda mapema kwenye mapumziko ya amani. Moja nililoligundua ni kudharau uhalisi wa mambo ulivyo, utapeli na complacency iliyokithiri ya kudhani kwamba haiwezekani giant kufa hata siku moja. Ingawa yapo mengi mengine yaliyosababisha haya madubwana kulala mapema kwenye makaburi ya waliofeli.

Siasa za leo za TZ zinataka mabadiliko ya kweli tena ya haraka. Chelewa chelewa utakuta mwana si wako. Taratibu tumeanza kufumbuka macho. Inawezekana kabisa my next visit to the graveyard of giants would find CCM close to Worldcom or Enron etc!! Who knows!!

Tunaomba Mungu kwa nguvu zote hilo litimie mapema! kwa hakika huu ndo mzizi wa ufisadi wote Tanzanaia na kutufanya tuwe MATONYA wakati Mungu katupa utajiri wa kupindukia!
 
ila kwa wasioijua sisiemu watadhani huu ndo mwisho wake, la hasha huu ndio mwanzo wa utungu tu, lolote linawezekana.
 
kuna wimbo rais mstaafu wa Kenya Mh. D. A. Moi, alikuwa akiwaimbisha Wakenya katika mikutano yake ya hadhara ya KANU, akiimba hivi " bila ya KANU", watu wanaitikia "hakuna mishahara, hakuna maji safi, hakuna maendeleo, hakuna... hakuna...hakuna..."
Leo wapi, wafanyakazi wanalipwa mishahara, kinachofanyika kinafanyika na KANU ni chama cha wanaotafuta ushirika kwa wengine kupata tonge zao tu. khalas!
Inawezekana kabisa na si miaka mingi tokea leo tukaimba nyimbo nyengine badala ya zile za nambari wani eeeeeee!! nambari wani ni....."
 
CCM kufa? Hapana. CCM ni nyoka kwa hiyo itabadili magamba yake. Angalia historia yake tangu TANU mpaka leo. Huwa inabadilisha magamba tu kwa maana ya sura ya viongozi wake na sera zake. Viongozi wake wa sasa karibu asilimia 25 ifikapo mwaka 2025 hawatakuwepo na baadhi yako kama akina Kikwete, Lowasa, Rostam na wanaofanana na hao watakuwa vikongwe kama alivyo Kingunge na mzee Kawawa leo. Hawatakuwa na impact haata kidogo. Ninaamini hata wewe Mwanakijiji na wengi wenu mnaochangia kwenye JF na mimi included tutakuwa ama tumechooka au tumeishaenda mbele ya HAKI.

Mimi suala hili naliangalia kwa jicho tofauti. Alimuradi wewe Mwana Kijiji unazungumzia utabiri. Mimi ninachokiona leo ni kile ambacho ndani ya Biblia na hata Mtume Muhamad (SAW) pia aliwahi kukisema. Nalo ni kuwa enzi hizi za ufisadi ndiyo realities of today. Whether CCM iko au haiko. CUF, CHADEMA. Viongozi wao wote ni kizazi cha ufisadi na wanachogombea ni kupata fursa ya kuila hii nchi kiufusadi. I am not a prophet of doom. No soma maandiko. Leo hii nchini Tanzania tupo enzi za Nuhu. Wapo watu tena wengi sana ambao wamejichimbia katika anasa na ufisadi ambao hata uwaambie vipi roho zao ziliisha kufa.

Inatisha kuwa waovu hao wamejaa miongoni mwa viongozi wa serikali na vyama vya siasa, NGOs, makanisani, misikitini, ndani ya familia zetu. Kwa kweli tuko zile enzi ambazo Paulo alimwambia Timotheo katika 2 Timotheo 3 1-9 ambazo ni:

  • nyakati za taabu.
  • Watu wana ubinafsi. Kila mtu anafikiria kumiliki kila kitu yeye tu.
  • Watu wana tamaa ya fedha. EPA, RADAR, DOWANS, TICTS n.k
  • Watu wana majivuno. Tazama kauli za wabunge wetu na baadhi ya wachungaji wetu wa kiroho; mashekhe. Angalia vita ndani ya BAKWATA.
  • Watu ni wenye kujiona (dharau)
  • Watu wanamtukana Mungu. Miradi kama ya DECI
  • Watu hawatii wazazi wao
  • Watu hawana shukrani
  • Watu ni waovu. Angalia jinsi jamii inavyowasifia wezi na mafisadi. Tazama magereza yalivyojaa.
  • Watu hawana upendo moyoni
  • Watu hawana huruma. Angalia wananchi wa Mbagala walioathirika na mabomu. Hiyo misaada badala ya kupelekwa kawo mtaona itakavywanufaisha watendaji wa serikali. Posho, mikutano n.k
  • Watu wachongezi (masengenyo, kusingizia). Angalia malumbano ya Mengi dhidi ya akina Rostam and vice versa.
  • Watu walafi
  • Watu wakali.
  • Watu wanachukia chochote kilicho chema
  • Watu ni wahaini
  • Watu ni wakaidi
  • Watu wamejaa kiburi
  • Watu wanapenda anasa kuliko Mungu
  • Wengine wanajifanya wameokoka na kumcha Mungu lakini hawakiri nguvu ya Mungu
  • Baadhi ya wachungaji badala ya kuwasaidia wanawake ambao huwaendea ili kusaidiwa kwa Neno na kujifunza wanazini nao

Haya ni mambo ambayo yaliishatabiriwa na yapo na sisi. Tunachotakiwa ni kufanya kama alivyofanya Nuhu. Kuendelea kumcha Mungu na kuongozwa na Roho wake Mtakatifu ili tusije tukaangamia. Miili yetu tuisalimishe kwa Roho Mtakatifu ili isije ikatuangamiza. Tuepuke kuingia kwenye mojawapo ya kundi hilo. Otherwise woe to us.
 
CCM kufa? Hapana. Itakachofanya ni kujivua magamba yake kwa sababu CCM ni kizazi cha nyoka. Na vyama vyote vya siasa ni vya uzao huo. Wanaokufa ni viongozi wake basi. JK ataondoka 2015. Baada ya hapo kizazi chake watabakia wachache bungeni. Ikifika 2025 wote watakuwa hawana impact. Wakiwa hai basi watakuwa vikongwe kama walivyo akina Kinguge na Kawawa leo. Nina hakika wewe MM na wengie wetu tunaochangia mada hii ndani ya JF mwaka huo hata meno yatakuwa tunayo ya badnia na wengine watakuwa wametangulia mbele ya haki.Sawa unzungumzia utabiri. Na mimi nakubali. Unajua nyakati hizi zilitabiriwa na Biblia na hata Muhamad (SAW). Si CCM wala si CUF wala CHADEMA ambao viongozi wake ni safi. Hawa wanagombea fursa ya kuendeleza ufisadi. Kwa hiyo jawabu siyo CCM kufa. Imetokea tu hizi ni enzi za ufisadi na hivyo ndivyo ilivyotabiriwa.Leo hii nchini Tanzania tupo enzi za Nuhu. Wapo watu tena wengi sana ambao wamejichimbia katika anasa na ufisadi ambao hata uwaambie vipi roho zao ziliisha kufa. Inatisha kuwa waovu hao wamejaa miongoni mwa viongozi wa serikali na vyama vya siasa, NGOs, makanisani, misikitini, ndani ya familia zetu. Kwa kweli tuko zile enzi ambazo Paulo alimwambia Timotheo katika 2 Timotheo 3 1-9 ambazo ni:• nyakati za taabu. Angalia hali ya uchumi na umasikini miongoni mwa watanzania wengi na utajiri uliokithiri mikononi mwa watu wachache. • Watu wana ubinafsi. Kila mtu anajipigania mwenyewe. Hakuna upendo wa dhati hata kati ya mke na mume wala watoto na wazazi na ndugu hata wa tumbo moja. Kila mtu kivyake vyake tu.• Watu wana tamaa ya fedha mno. Migogoro ya DECI, Upatu na watu kurushana na kutapeliana imkekuwa nim jambo la kawaida.• Watu wana majivuno. Angalia kiburi walicho nacho watanzania wengi?• Watu ni wenye kujiona (dharau). Wanawake kwa waume.• Watu wanamtukana Mungu. Hawamuogopi Mungu ndiyo maana madhambi yamezidi. Angali kashfa za ngono kila uchao. Watu wazima na watoto wadogo. Ushoga, Usagaji n.k Kila guest house inayojengwa inalenga kukidhi shughuli ya ngono.• Watu hawatii wazazi wao• Watu hawana shukrani• Watu ni waovu• Watu hawana upendo moyoni• Watu hawana huruma. Angalia vibaka wanavyouawa. Polisi inavyodhulumu wananchi. Serikali yenyewe inavyodanganya wananchi na kuwaibia haisemeki.• Watu wachongezi (masengenyo, kusingizia)• Watu walafi• Watu wakali• Watu wanachukia chochote kilicho chema. Kilicho haramu kinaonekana halali na kushabikiwa na kushangiliwa na wengi.• Watu ni wahaini• Watu ni wakaidi. Hakuna anayetii utawala wa sheria. Ni nchi isiozingatia sheria• Watu wamejaa kiburi. Watanzania wengi ni wabishi na wajuaji.• Watu wanapenda anasa kuliko Mungu. Angalia miradi mingi ni ya starehe na burudani nchi hii. Kila kijana anataka kuwa msanii. Lugha na hata msamiati unaozungumzwa mpaka na hata viongozi ni wa kihuni.• Wengine wanajifanya wameokoka na kumcha Mungu lakini hawakiri nguvu ya Mungu• Baadhi ya wachungaji badala ya kuwasaidia wanawake ambao huwaendea ili kusaidiwa kwa Neno na kujifunza wanazini nao Haya ni mambo ambayo yaliishatabiriwa na yapo na sisi. Tunachotakiwa ni kufanya kama alivyofanya Nuhu. Kuendelea kumcha Mungu na kuongozwa na Roho wake Mtakatifu ili tusije tukaangamia. Miili yetu tuisalimishe kwa Roho Mtakatifu ili isije ikatuangamiza. Tuepuke kuingia kwenye mojawapo ya kundi hilo.
 
Tatizo sio CCM. Tatizo ni kushindwa kwetu kuiwajibisha.

CCM kuondoka sio suluhisho kwani kitakuja chama tawala kingine na kuvurunda kama CCM.

Suluhisho tujifunze kuwajibisha chama na serikali.

Nasisitiza: TATIZO SIO CCM
 
Back
Top Bottom