Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

there is something substantial that is happening within the ruling party. If carried to its logical conclusion it'll signal the end of CCM as political force in the country and will usher a new era in political and public discourse int the country. Although I believe that there is a marginal possibility that a few MPs might jump ship either to start their own political party or to reinforce current ones, the probability of that happening is still remote.

However, there are a number of things which if they were to occur we will witness a clear and unambigous withdrawal from CCM within the very short period. I can even boldly declare that if "these things" were to happen Tanzani will have mini general election before the end of the year. That however depends on "If they indeed do happen"....

what are these things you might ask... well nikiweka hadharani watajua najua.
 
wasitoke, wabaki huko huko wapambane na ccm wenzao. manake wakitoka na watu walivyokuwa wanapenda chama hata ukifanywa uchaguzi mdogo utashuhudia miujiza ya kuchaguliwa tena ccm kwenye majimbo hayo
 
Kuna habari kuwa kuna wabunge wanajiandaa kuihama CCM kwa mkupuo wa pamoja au mmoja mmoja ,kitu ambacho kipo kwenye mashauriano.
Habari zimezidi kutonya kuwa wabunge hao ambao wameamua kulinda maslahi na malengo yaliowapeleka hapo Bungeni badala ya kukaa na kuwalinda watu wasio kuwa na uchungu wa Inchi hii ,wana imani kubwa kuwa WaTanzania walio wengi watawaunga mkono katika kitendo hicho ambacho wamekiita ni cha Kishujaa na utii kwa wananchi na pia wana imani kuwa wananchi waliowachagua kuwapeleka Bungeni watawachagua tena hata wakiwa ni wagombeaq binafsi kwa vile msimamo wao ni kulinda maslahi ya wananchi na kutowaonea haya wezi wa fedha ya Nchi hii na mali zake.
Wabunge hao wamezidi kuipa msonyo CCM kuwa ni Chama kinachoendeshwa kidikiteta na zaidi wengine kujiona wao ni wa Mjini na wanaweza kufanya lolote bila ya huruma kwa wananchi,na kuwafanya wabunge wawe na hali ngumu kurudi kuomba kura tena pale ufikapo msimu wa harakati za kujinadi ili wachaguliwe tena.
Wakizidi kutoa mchapo kuwa CCM kumejaa vigogo ambao wanatumia fedha nyingi kwa kulinda maslahi binafsi na kusahau kama wao wapo hapo kwa ajili ya maslahi ya Taifa na wananchi wake ,ndio ukaona jinsi wanavyoiba fedha ya umma bila ya huruma ..mmoja wao aliongezea.
Wabunge hao ambao wengi wao huwa wanaonekana wakimya ndani ya bunge wamezidi kutonya kuwa safari hii CCM magome watafahamu kuwa mizizi ndio muhimu kwa mti.

...hata wahame na kuhama na kuhama bado hawana credibility ya kugombea tena, miaka yote au mihula yooote walikuwa wapi mpaka akina slaa wawashe moto ndipo wastuke kuvuta shuka wakati mapambazuko yanawadia??? Kuna watanzania wengi ambao ni waaminifu na tukiwatuma bungeni hawatafukuzia akili zao ktk kuongezewa posho bali wataiwajibisha serikali itende matakwa ya watu kwa manufaa ya watu.

Hii kuhama ni kutapatapa na mjue ndugu zangu, ninavyokijua chama changu (ccm) kilivyojaa wanafiki ambao wanaweza hata kutoa chozi (la pembe) kuhusu hali zetu halafu watu hao wanaweza kutumwa upinzani wakaidhoofishe kisha watarudi chama tawala kwa shangwe..... Kumbukeni mwanasiasa wa kweli si yule ambaye anawaza atachaguliwa vipi ili awepo ktk nafasi za uongozi, bali ni yule ambaye ana uwezo wa kuongoza ila hana hamu ya kuongoza.

Tusidanganyike na yanayojiri bungeni this period tukasema wabunge wameamka, naomna nikukumbushe kidogo kuhusu majuzi hapa ambapo kambi ya upinzani waligundua uongo ktk hotuba ya waziri wa fedha na mkanganyiko wa mahesabu na wakaspeak out, lakini wabunge machachari wa chama ngangari waliendelea kuipongeza na kuyatukuza mapungufu yale as ushujaa wa kuukubali ukweli..... Endapo waziri ataleta taarifa ya uongo bungeni maana yake ni kuwa serikali inalidanganya bunge na matokeo yake tumedanganywa sisi woooote. Huu upuuzi wa kusema fulani atahama huku kwenda kule ni aina ya ulafi wa madaraka, tanzania ipo itakuwepo bila hata wao.

Nawaasa vyama shindani wasikubali kupokea viongozi wanaohama kutoka chama tawala wanakuja na shombo la hukooo.... walikokuwepo awali.

NAOMBA KUWASILISHA
 
wasitoke, wabaki huko huko wapambane na ccm wenzao. manake wakitoka na watu walivyokuwa wanapenda chama hata ukifanywa uchaguzi mdogo utashuhudia miujiza ya kuchaguliwa tena ccm kwenye majimbo hayo

Japo napenda sana watoke ili nchi iwe na uwiano mzuri kisiasa, nadhani kwa siasa zetu za "maji taka" naamini Gaijin unaweza ukawa sahihi sana kwani wanaweza kutoka wakabaki mafisadi watupu na Watanzania kule vijijini hadi leo wanajua CCM ya Nyerere ipo na watawapa kura na hapo ndipo patakua hapatoshi. Kwa sasa wawabane wao ndio wakimbie CCM. Mmi siipendi wala siichukii CCM... Wala sipendi wala kuchukia chama chochote, Lakini naipenda nchi yangu na wana CCM na wapinzani watakubaliana na mimi kwamba nashirikiana na yeyote wa upande wowote anayepigania maslahi ya Taifa. Na sifanyi SIRI kwa wanaonifahamu. Sasa basi wakati ukifika na wakatoka wabunge wa CCM tunaowaamini tuwaunge mkono kwa nguvu zetu zote kupambana na mafisadi, lakini kama wakitoka mafisadi na kujiunga na upinzani ama kama wagombea binafsi tupambane nao hata kama watavaa ngozi za kondoo. Hapa nina maana kwamba SUALA SI CHAMA SUALA NI MASLAHI YA TAIFA... Ndio maana hapa utaona kuna wabunge wa CCM wanaungwa mkono na wapinzani na wana CCM wenzao na wako wabunge wa upinzani wanaungwa mkono hata na wana CCM. Tupambane tusichoke na tusikubali kupotoshwa na kama mada hii ina lengo la kuwachonganisha wapambanaji na chama chao pia tuwadhibiti kwa kusaidia kupambana na hizo propaganda. Jambo la msingi kwa sasa ni kwamba wapinzani wana nafasi nzuri sana ya kujijenga maana CCM kama chama kinazidi kuboronga kila kukicha hasa kwa kuwa na Katibu Mkuu kama Makamba na viongozi wa mikoa kama kina Mula wa Mbeya na wale viongozi wa Mwanza, Shinyanga na Arusha walioandaa mapokezi ya Lowassa na Chenge. CCM yenye watu kama kijana mwenzetu Peter Serukamba, anayejaribu kukwepa ajenda muhimu ya UFISADI eti watu wajadili maendeleo. YAPI HUKU WEZI WANATANUA??!!!
 
wasitoke, wabaki huko huko wapambane na ccm wenzao. manake wakitoka na watu walivyokuwa wanapenda chama hata ukifanywa uchaguzi mdogo utashuhudia miujiza ya kuchaguliwa tena ccm kwenye majimbo hayo

Umenena Mkuu. kama wanataka kupambana na kuleta mabadiliko, ni rahisi kuyfanya hivyo wakiwa ndani ya CCM. Wakitoka nje tu, hawatakuwa na nguvu ya kupambana nao. Hivyo kama wanataka kuopambana ni vema wabakie na kuanzisha mikakati ya kuleta mabadiliko from within
 
Kuna wakati ambapo mistari huchorwa ardhini na kutengana kunabakia kuwa ndio njia pekee ya kuleta mabadiliko na kufikia malengo fulani.
 
Hawa wabunge wahame au wasihame sio bottom line, bottom line ingekuwa kusimamia maslahi ya wananchi waliowatuma popote pale walipo hata kama ni huko huko CCM
 
we need katiba ya wananchi na si katiba ya vyama vya siasa...
we need food for our bellies
we need education for our netional development forth
we need true separation of powers
we need strong representatives not mere ceremonial
I believe tanzanians needs me (youth)
 
Youu CCM MPS you ahve seen the right then stand up for your right and tetea maslai ya nchi na siyo ya chama
 
Tatizo, kichwa cha thread hakisemi udaku. Kinadanganya!

Kweli JF tumeingiliwa, yaani kweli mtu mmoja mjinga mjinga anaandika na kujijibu mwenyewe kama mtoto mdogo na sisi wengine tunaupanda mkenge?

Yaaani mkuu hicho ndicho hasa kilichokupeleka huko Dodoma? Ooh my Gosh! Hivi hili taifa tumelaaniwa na nani? Hivi ni accomplishment zipi mtu anazipata na this kind of nonesense?

Eti hivi ndio tunalisaidia taifa kweli?
 
Kweli JF tumeingiliwa, yaani kweli mtu mmoja mjinga mjinga anaandika na kujijibu mwenyewe kama mtoto mdogo na sisi wengine tunaupanda mkenge?

Yaaani mkuu hicho ndicho hasa kilichokupeleka huko Dodoma? Ooh my Gosh! Hivi hili taifa tumelaaniwa na nani? Hivi ni accomplishment zipi mtu anazipata na this kind of nonesense?

Eti hivi ndio tunalisaidia taifa kweli?

Sikuona hii kumbe mimi ni Kuhani pia au Mwiba? Mambo ya msiba ndugu yangu.
 
Watu wengine tunahitaji ku-grow up angalau kidogo! Ni ushauri wa bure tu! Look let say hii topic imeanzishwa na Mwiba ambaye sio wewe, sasa haya yamekukuta vipi? Why mention Kuhani kwa nini sio Azimio jipya? Unaona watu wanavyojisikisha wenyewe!

Aibuu!
 
Haha, good observation. Kweli kuwa CCM unatakiwa kuwa strong, kwa sababu inabidi ukubali kukalia kimya wizi na dhuluma, ukiwa weak huwezi kuvumilia hayo kama Mrema inakubidi ukimbie. Ukiona mtu kutoka upinzani anakimbilia CCM jua huyo anataka kitu. Tambwe, Kaborou, Lamwai etc etc na mara nyingi wamekuwa wamepewa kinono fulani au kubanwa mbavu na kuamua kuwatosa wananchi na kujiunga nao.
Ukumbuke kuwa CCM si chama cha wezi, lakini ndani ya CCM kuna genge la wezi, ambao wanawatumia wanachama na wanakitumia chama kama njia ya kuwaibia watanzania. Kama Slaa, Lipumba, Mbowe etc etc wangekuwa CCM, wangeambiwa kuzungumzia mambo ya ufisadi sio msimamo wa Chama kwa hiyo Richomond, EPA, Import support etc etc sasa hivi yasingesikika. Tusingesikia hata kama Chenge anavijisenti Jersey na tusingesikia kama mjuu wa miaka minne wa mramba ana sh Bilioni nne.
Kama kweli wewe ni mwanaCCM wa kweli na ni mtanzania mzalendo halisi, unaweza kukubaliana nami. Intra party opposition, inter party opposition sio jambo baya. Hii ni wrong perception lazima tuache siasa za mzee Kingunge!

mbowe na lipumba sikuwataja katuka post yangu.......! hapo umemtaja SLAA tu......!
siku moja SLAA atakuwa CCM cadre...!
 
Haingii akilini kwamba CCM itavunjika sasa, lakini yawezavunjika wakati mwingine wowote !!! Kwa hakika ndani ya chama hakuna chama chenye demokrasia ndani ya chama kama CCM.

Haya ni maoni yangu tu!
 
Haingii akilini kwamba CCM itavunjika sasa, lakini yawezavunjika wakati mwingine wowote !!! Kwa hakika ndani ya chama hakuna chama chenye demokrasia ndani ya chama kama CCM.

Haya ni maoni yangu tu!
CCM haivunjiki ila itasambaratika ,kila mmoja atamwona mwenziwe adui kama ilivyokwisha anza ,sasa usitegemee kutokea matatizo ya kunyang'anyana tonge ,halafu ukategemea kama kutakuwa na salama ni lazima mgawanyiko utokee ndio kutakuwepo na salama lakini kama wataishi pamoja basi kuna hatari ya kunyunyiziana unga kwenye viti vyao ,natumai utakuwa uminielewa ,hapa walipofikia basi hakuna kuaminiana tena,hata soda sasa ,wanaogopa kukaribishana ,na kila mtu hataki mwengine ajue amefikia wapi.
 
Usafi wa Lowassa, uchafu wa CCM

ban.maswali.jpg
Ansbert Ngurumo

STAILI ambayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetumia kujisafisha inavutia, inashangaza, inachekesha na kutafakarisha kidogo. Ni staili inayozua maswali yasiyo na majibu au yenye majibu yasiyoridhisha.
Lililo dhahiri ni kwamba, kwa kitendo cha kujisafisha, kwa kutumia kikao cha Halmashauri Kuu (NEC), CCM imekiri kile ilichokuwa inakikataa kwa muda mrefu - kwamba imechafuka.
Lakini staili yake ya kujisafisha inatufanya tuhoji upya: Uchafu ni nini? Umeingiaje CCM? Umeingizwa na akina nani? Umeingia lini? Na unaondolewaje? Labda CCM wangejiuliza maswali haya na kuyatafutia majibu ya kina, wangepiga hatua kidogo.
Majibu ya maswali haya yanatosha kuandika kitabu ambacho kitaandikwa siku moja na kuwa marejeo ya vizazi vijavyo kuhusu historia ya ukombozi wa nchi hii kutoka mikononi mwa wakoloni weusi waliojipa haki ya kutafuna matunda ya uhuru wa Watanzania bila ridhaa yao.
Ikumbukwe kwamba zilipoibuliwa tuhuma dhidi ya CCM, hadi baadhi ya watani wake kisiasa wakakiita Chama Cha Majambazi; Chukua Chako Mapema; Chama Cha Majangili; Chama Cha Mafisadi na kadhalika. Viongozi wakuu wa wanachama walipinga, waling’aka, kuwakebehi na hata wakawatisha waliotoa tuhuma hizo.
Katika hali ya kutapatapa na kukata tamaa, na kama ilivyo kawaida ya CCM kufanya propaganda katika masuala ya msingi, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alitamka hadharani kwamba tuhuma dhidi ya CCM ni kelele za mlango zisizoweza kumzuia yeye (akajiita mwenye nyumba) kulala! Wiki hii ni yeye aliyeongoza kikao cha NEC kujaribu kujisafisha, kwa staili aliyochagua yeye na viongozi wenzake. Viongozi wenzake, naye akiwamo, pamoja na wastaafu, wamefunikwa na kashfa nzito mno kichwani hadi miguuni.
Hawaonekani! Hata waliotishia kwenda mahakamani baada ya kuhusishwa na ufisadi wameshindwa kwenda kwa sababu dhamiri zao zinawaeleza ukweli kwamba hizi si kelele za mlango, bali sauti za wanyonge, wenye mali ya nchi hii, ambao hatimaye wamegundua mnyonyaji wao ni nani.
Watuhumiwa hawa wanaogopa yasifumuke mengine wakiwa kule mahakamani. Na licha ya ushahidi wote uliopatikana hata bila kwenda mahakamani, vyombo vya dola vimeshindwa kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa.
Polisi wetu wameamua (bila shaka kwa maagizo ya kisiasa) kufanya kazi ya kisiasa. Wanakimbizana na vibaka na wezi wakuu mitaani; wanawabambikia kesi wananchi maskini wanaotafuta kwa jasho. Wakati mwingine wanawanyonga ili kuwanyang’anya walicho nacho.
Wanashindwa kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wanaotuhimiwa kwa wizi mkubwa unaofilisi hata maisha binafsi ya polisi wenyewe. Maana kama watuhumiwa walishindwa kwenda wenyewe mahakamani kuwashitaki waliowatuhumu, Jeshi la Polisi lingetusaidia kwa kuwakamata watuhumiwa ili haki itendeke.
Kimsingi, hata wanasiasa makini wanaotaka kujisafisha matope ya ufisadi, walio na dhamiri ya kuonyesha kwamba hapa kuna ari mpya, wangepaswa kuchukua hatua za kisheria ili kujisafisha au kuwasafisha watuhumiwa au kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria.
Huo ndiyo ungekuwa usafi wa CCM na serikali yake. Hapo ndipo rais angeanzia kuisafisha na kuwasafisha wenzake. Angechanganya hatua hiyo na zile fursa kadhaa zilizojitokeza, akabadilisha sura na mfumo wa utawala; akaondoa wachafu na kuweka wasafi; akafukuza wazembe na kuingiza wachapakazi.
Angepata pa kuanzia upya; na tungemsikiliza. Mara zote alizobahatika kufanya mabadiliko madogo na makubwa katika Baraza la Mawaziri zilikuwa fursa muhimu za kutuonyesha nia yake ya kusafisha serikali na CCM. Alishindwa kuzitumia.
Akawahamisha mawaziri kutoka wizara moja hadi nyingine; akawapunguza wachache wasio na tuhuma nyingi; akawabakiza wale wanaotuhumiwa kila siku. Ni sawa na mtu anayefagia nyumba yake halafu akakusanya uchafu wote akaulundika chumbani anakolala; kisha akawatangazia wana familia na majirani kwamba nyumba yake ni safi.
Harufu ya uchafu inayowakera hao, inamburudisha yeye, maana yeye na wao wana tafsiri tofauti ya usafi na uchafu. Tusisahau kuwa kabla aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu, rais alikuwa ameunda Tume ya Profesa Rwekaza Mukandala kumsaidia kuwachunguza mawaziri wake na kumpa ushauri juu ya nani mbovu, nani ana nafuu, nani aondolewe na nani abaki.
Kwa bahati mbaya, hakuunda tume kabla ya kuwateua, ili kubaini ubovu wao. Lakini wengi wa wateule wake ni wale ambao yeye na wao wamekuwa pamoja serikalini kwa zaidi ya miaka 17. Haiwezekani kwamba hakuwajua. Wala hakuhitaji ushauri wa tume.
Wananchi wenyewe walionyesha wasiwasi juu ya baadhi yao. Iweje wananchi wajue udhaifu wa mawaziri, yule aliyewateua, tena mwenye vyombo vya kiutawala vya kumsaidia kuwajua, ajidai kwamba hawajui hadi aletewe taarifa na tume ya ‘kisomi’! Ajabu ni kwamba, hata tume ilipoleta majibu, hakuyatumia. Akawateua wale wale, tena wengine wakamkejeli kwenye vyombo vya habari. Andrew Chenge ni mfano hai. Alipoteuliwa kuongoza Wizara ya Miundombinu, wanahabari wakamhoji kwanini amerudi akasema “muulize rais aliyeniteua. Ndiye anajua sababu.” Chenge alikuwa sahihi.
Na hata baadaye alipoondoka kwa kashfa za kuficha nje mabilioni ya shilingi ambazo hazijajulikana alivyozipata, alitoa kauli nyingine kwamba ameondoka ili kumwondolea ugumu rais. Maana yake, kama si kwa ajili ya rais, Chenge asingeondoka.
Lakini maana kubwa zaidi inayopatikana kwenye kauli yake ni kwamba kama asingeondoka, rais asingemfukuza! Kauli kama hii ilitolewa pia na Lowassa alipojiuzulu uwaziri mkuu, akasema amefanya hivyo si kwa kuwa ana mkono kwenye Kampuni ya Richmond, bali kwa kuwa alitaka kulinda heshima ya chama na serikali.
Baadhi yetu tuliandika kumsahihisha Lowassa, tukasema alijiuzulu kulinda heshima ya rais kwa kuwa wote walikuwa washiriki wakuu katika mradi wa Richmond. Kuna jambo lilitokea wakati ule ambalo lipo hadi sasa. Ile heshima ya chama na serikali haikurejea.
Kwa hiyo, kujiuzulu kwa Lowassa hakukusaidia kurejesha heshima ya serikali na CCM. Na sababu mojawapo iliyosababisha heshima hiyo isirejee ni kwamba mafisadi wale wale wameendelea kuwa viongozi wa CCM na serikali.
Wao walitaka tuamini kwamba fisadi ni Lowassa; akiondoka serikali inakuwa safi. Wapi! Sasa NEC ya CCM imekaa na kumsafisha rasmi Lowassa kwa kusisitiza kauli yake ya awali.
Maana yake ni kwamba CCM na serikali hii ya Kikwete inamhitaji sana Lowassa. Na imegundua kwamba inahitaji kumlinda. Inajua, kwamba tunavyojua, kwamba alipokuwa waziri mkuu, Lowassa hakutenda jambo lolote zito kwa uamuzi wake pekee.
Yote aliyatenda kwa idhini na ushauri wa rais. Ndiyo maana yalipomtokea yaliyosababisha ajiuzulu, rais alikuwa wa kwanza kumtetea, akasema amepatwa na ajali ya kisiasa; kwa kuwa Lowassa ni kiongozi mchapakazi, mwadilifu na mzalendo wa kweli.
Aliyasema hayo huku akijua kuwa umma wa Watanzania unamzomea Lowassa na kumwona fisadi wa kutupwa, maana katika sakata hili la Richmond, jina la Lowassa limetajwa mno kuliko hata la wamiliki halisi wa Richmond.
Hili ndilo ambalo CCM imejaribu kupambana nalo. Na kitendo cha NEC kumsafisha Lowassa sasa, ni uthibitisho kwamba CCM imesisitiza kauli ya Rais Kikwete juu ya ‘uadilifu na uzalendo’ wa Lowassa. CCM na Serikali ya Kikwete inamuogopa Lowassa. Na haikuanza leo.
Lakini woga huu uliongezeka pale walipoona Lowassa anawekewa zulia jekundu kwao Monduli! Woga ulizidi walipoanza kusikia akijitetea hadharani. Wakajua wasipofanya kitu, atalipuka na kulipua mambo. Wakaamua kumlipua yeye kwa njia mbili.
Kwanza, wakawa wanamtumia wajumbe wa kumpa pole na kumfariji kwa yaliyompata. Pili, walipogundua bado ana kinyongo na kwa hulka yake atazidi kusema mengine wasiyotaka aseme - maana alishaamua kujitetea asife kibudu - wakaingiza nguvu ya dola. Wakamuonya. Akaufyata! Hadi leo najiuliza. Kuna kitu gani serikali inaogopa kwa Lowassa? Kitu gani waliogopa asiseme? Na hapa walipofikia, inawezekana hatasema tena; maana wamemsafisha. Wamemziba mdomo.
Lakini usafi huu wa Lowassa una maana gani pana? Wamemsafisha Lowassa kumlinda mwingine. Na ulinzi huu ndiyo sababu ya NEC kuwatisha wabunge na kuwawekea ‘gundi’ mdomoni wasijadili masuala ya ufisadi wa EPA bungeni.
Huu ni uchafu ambao wakubwa hawataki kuondokana nao. Uchafu huu ndiyo asili ya nyadhifa zao. Uchafu huu ndiyo ulaji wao. Ukizungumzwa kwa uwazi, ukaanikwa, hakuna mmoja wao atakayebaki. Hakuna atakayemfukuza mwingine. Na ndiyo maana wamekuwa wakilindana na kuogopana hata mambo yanapokuwa yameharibika waziwazi.
Na ndiyo maana wengine tunatilia shaka hizi harakati za CCM na serikali kujisafisha kwa kuwatoa kafara wachache na kuwakumbatia wengi. Wanataka kutumia ‘usafi’ wa Lowassa kuisafisha CCM na serikali. Lakini wanashindwa kuchukua hatua za dhati kwa mafisadi wa EPA.
Hakuna atakayewaelewa. Hata Richmond (sasa Dowans) bado inaendelea kulipwa mamilioni wasiyostahili (sh 152,000,000 kila siku). Matendo haya ya NEC huku serikali ikishindwa kuchukua hatua dhidi ya mafisadi, ni sawa na CCM kujisafisha kwa kunawa matope. Sote tunajua matokeo yake.
Inavutia kufuatilia mchakato wa namna hii; inashangaza CCM wasivyojua maswali ya msingi yanayowakabili; inachekesha kwamba watawala wameamua kufanya maigizo mbele yetu; na inatafakarisha kwamba vita dhidi ya ufisadi inahitaji watawala mbadala na vyombo mbadala. Si hawa tulio nao.

ansbertn@yahoo.com
www.ngurumo.blogspot.com
+447853850425
 
Ufisadi waimega CCM

na Mwandishi Wetu, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya watu

MAPAMBANO makali ya chini kwa chini kati ya wanaharakati wa vita dhidi ya ufisadi na watuhumiwa wakubwa wa vita hivyo, yameibuka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na miongoni mwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano.

Matukio ya hivi karibuni ndani ya CCM na Bunge yanaonyesha kwamba, hali imeanza kuwaelemea viongozi na wabunge kadhaa wa chama hicho tawala, ambao kwa miezi kadhaa sasa wamekuwa wakionekana kuwa wanaharakati wanaoongoza mapambano hayo dhidi ya ufisadi.

Moja ya matukio hayo ni kauli ya mwishoni mwa wiki aliyoitoa Spika wa Bunge, Samuel Sitta mjini hapa wakati wa semina ya Huduma ya Kikristo ya MANA inayoongozwa na Mwalimu Christopher Mwakasege.

Sitta katika kauli yake hiyo nzito, alikaririwa akisema kwamba kumekuwapo na mapambano makali kati ya watetezi wa haki na wale ambao ni mafisadi ndani ya Bunge, hali ambayo kwa kiwango kikubwa inaifanya taasisi hiyo ipite katika kipindi kigumu ambacho kinapaswa kukabiliwa kwa njia ya maombi.

‘‘Baadhi ya wale wanaosimamia haki wanashambuliwa, lakini tutashinda,” alisema Sitta akionyesha dhahiri kuwapo kwa ufa mkubwa wa wazi ndani ya Bunge.

Mbali ya hilo, madai yaliyotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM) mwanzoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM) akisema alikuwa ametishia kulipiza kisasi dhidi yake, yanatajwa kuwa kiashiria cha wazi cha mapambano ndani ya chama hicho tawala, yote yakitokana na mzizi wa ufisadi.

Wafuatiliaji wa siasa za ndani ya CCM wanasema Serukamba, mbunge kijana, amekuwa akitajwa kuwa karibu kikazi na kimsimamo na makada wenzake kadhaa ndani ya chama hicho tawala kama aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambao kwa miezi kadhaa sasa wamekuwa wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali.

Aidha katika hili, Kilango, mke wa Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Malecela, amekuwa akijipambanua waziwazi kuwa mstari wa mbele kukabiliana na mafisadi waliohusika katika kashfa kama zile za Richmond na EPA, msimamo unaoelezwa kuwa umemjengea mahasimu wengi miongoni mwa wabunge na wanachama wenzake wa chama hicho tawala.

Tukio la mwisho katika mlolongo wa mapambano hayo ambalo linaweza kuthibitisha maneno ya Sitta na hali halisi ya mambo ndani ya Bunge na pengine miongoni mwa wanaCCM ni kauli iliyotolewa bungeni jana na Mbunge wa Buchosa, Samuel Chitalilo (CCM) ambaye katika hatua isiyotarajiwa, alisimama na akatumia muda mrefu kuelezwa kukerwa kwake na tuhuma za ufisadi zinazowaelemea rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya mkataba wa Richmond, Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge.

Msimamo huo wa Chitalilo unakuja siku chache tu baada ya kuibuka kwa malumbano ya hoja kuhusu suala hilo hilo la ufisadi, ambayo yalitokana na hoja ya Anna Abdallah, ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alimpiga vijembe vya waziwazi, Kilango.

Chitalilo ambaye alikuwa akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, alianza kwa kumtetea Mkapa, ambaye pamoja na mambo mengine anatuhumiwa kuanzisha kampuni akiwa rais na kuitumia kampuni hiyo, kwa ushirikiano na aliyekuwa Waziri wake wa Nishati, Daniel Yona kununua mradi mkubwa wa makaa ya mawe wa Kiwira kwa bei ya chini.

Chitalilo alisema yeye anashangazwa sana kwamba hicho kinachoitwa mabomu dhidi ya kiongozi huyo, ni mambo ambayo yamekuwa yakijirudiarudia kila siku, kwani watu wamekuwa wakitaja mara kwa mara kuhusu Kampuni ya ANBEM inayomilikiwa na rais huyo mstaafu.

“Mkapa anatukanwa na wakati mwingine anatukanwa hata na wabunge wa CCM… jamani tuachane na haya mambo, tutetee majimbo yetu na serikali yetu. Tunataka kuligeuza Bunge kuwa sehemu ya umbea,” alisema mbunge huyo huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge.

Chitalilo, pia alimtaja Lowassa na kusema kuwa kiongozi huyo alilazimika kujiuzulu katika kashfa ya Richmond kutokana na kuwajibika kisiasa.

“Hata kama mimi ningekuwa Waziri Mkuu halafu nikapatwa na mambo kama yale ningejiuzulu tu… Lowassa ameamua kuacha (Uwaziri Mkuu), lakini kosa lake lipo wapi?” alihoji mbunge huyo.

Katika hatua ambayo ilionyesha kukerwa na taarifa za akaunti za baadhi ya wanasiasa kutajwa na kuanikwa katika vyombo vya habari, mbunge huyo pia aliitaka serikali kuzifunga benki zenye tabia ya kuvujisha siri za wateja.

Baada ya hoja hiyo, Chitalilo alimuingiza Chenge katika orodha yake na kuuliza: “Hivi Chenge alisakamwa, kwani alivunja nyumba ya nani na kuiba?” Akasema kuwa iwapo Chenge angekuwa amevunja nyumba na kuiba, hata yeye asingemtetea, lakini haoni kosa alilolifanya kiongozi huyo hadi kupatwa na yaliyomkuta.

“Bunge sasa linataka kuwa la waganga… leo Chenge mchawi… kesho Spika mchawi… atakuwa mchawi…,” alisema Chitalilo kabla hajakatishwa na Spika Sitta ambaye alimtaka arejee katika hoja iliyokuwa inajadiliwa.

“Mheshimwia Mbunge rudi katika hoja iliyopo mezani, hao wanaosema wana haki ya kutoa maoni yao kama ambavyo na wewe ulivyo na haki ya kusema, tujadili haya yaliyopo mbele yetu,” alisema Sitta.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya CCM na bungeni zinaeleza kwamba, hoja hiyo ya Chitalilo kama ilivyokuwa kwa ya Anna Abdallah hazikuja bungeni kwa bahati mbaya bali ni kielelezo cha wazi cha kuibuka kwa mapambano makali ndani ya chama hicho tawala kuhusu ufisadi na wale wanaotuhumiwa kuhusika.

Kiongozi mmoja wa juu wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki alisema kuibuka kwa kasi ya ajabu kwa malumbano hayo, kunatokana na kuwapo kwa utata mkubwa kuhusu msimamo wa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho tawala, Rais Jakaya Kikwete kuhusu vita hiyo ukiwa haujawekwa bayana.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwanyoshea kidole viongozi wenzake kadhaa anaowahusisha kuwa ni mafisadi, alisema kuwa, hali ya kuzorota kwa mambo ilianza kujionyesha siku kadhaa kabla ya kufanyika kwa semina ya uongozi ya chama hicho mjini Dodoma, iliyowajumuisha wabunge wanaotokana na CCM na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, hali ya mambo ilivyokuwa kabla, wakati na baada ya kikao hicho ambacho kilitawaliwa na hoja nzito dhidi ya ufisadi na hatima yake kwa chama hicho, ilionyesha kuanza rasmi kwa mapambano ambayo awali yalionekana yameanza kumalizika.

Mbali ya hilo, mwanaCCM huyo alisema kauli ya Kikwete wakati wa semina hiyo akieleza kuhusu kuwapo kwa watu ambao wanaonekana kuendelea kuutaka urais wa mwaka 2005, ilionyesha kuwa kwake na hofu ya kuendelea kushamiri kwa makundi, na pengine ikaonyesha kuwa kwake katika upande ambao awali alionekana kutokuwapo.

‘‘Kikao kile kilitufungua macho baadhi yetu. Kwanza katika hatua ya kushangaza mwenzetu mmoja ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu anayetuhumiwa kwa ufisadi, alitoa maelezo marefu ya kumtetea na kumsafisha Mkapa, jambo lililotufanya baadhi yetu kubakia midomo wazi,” alisema mjumbe huyo.

‘‘Si hilo tu, Mwenyekiti (Kikwete) anaonekana kubadili mwelekeo, na sasa ni kama vile naye yuko upande wa marafiki zake wa siku nyingi ambao wanapita katika tanuri la moto. Ni wazi hajatoa tamko la wazi ingawa kuna wasiwasi kuwa ametukimbia,” alisema.

Kiongozi huyo aliendelea kueleza kuwa, muda mfupi baadaye, katika hatua iliyozidi kuzusha maswali ambayo hadi sasa hayajapata majibu, alisimama aliyepata kuwa Waziri Mkuu, Lowassa ambaye kwa mara ya kwanza alianza kueleza masikitiko yake ya namna alivyohusishwa katika sakata zima la Richmond, na akasema juhudi alizofanya kuhakikisha kuwa mkataba kati ya Tanesco na Richmond unavunjwa bila ya mafanikio yoyote.

Kwa mujibu wa kada huyo, uamuzi wa wanaCCM hao wawili marafiki, mmoja kumtetea Mkapa na mwingine kujitetea yeye mwenyewe, ulisababisha baadhi yao kuanza kuchukua tahadhari kubwa kwani walianza kuona kuwapo kwa dalili za wazi za kuanza kulipizana kisasi.

‘‘Kauli za watu hawa zilitushtua. Baadhi yetu tuliwasiliana kwa haraka na tukaanza kujipanga kukabiliana na kishindo chochote ambacho kingeweza kutokea. Tulipomuangalia mwenyekiti (Kikwete) na kumuona akionyesha kutoshtushwa na kauli za wanaCCM hao wawili na wengine kadhaa walioungana nao mkono baadaye, mara moja tulianza kuhisi hatari mbele yetu,” alisema mwanaCCM huyo.

Hata hivyo, Tanzania Daima ilipowasiliana na mbunge mmoja kijana wa CCM ambaye naye alitajwa kuwa miongoni mwa watu wanaounda kundi linalotetea mafisadi, alikiri kuwapo kwa utetezi huo wa Lowassa na mjumbe mwingine wa Kamati Kuu aliyemtetea kwa nguvu kubwa Mkapa.

‘‘Mimi ninachoweza kukuambia ni kweli kwamba Lowassa alitoa maelezo marefu na ya msingi, akielezea mlolongo mzima wa sakata la Richmond, na kwa kweli kwa mara ya kwanza naamini kila mmoja aliyekuwapo pale ndani alikubali kuwa Edward alikuwa ameonewa, na Kamati (Teule ya Bunge) ya Mwakyembe ilipiga porojo za kisiasa kuchafua watu,” alisema mbunge huyo ambaye hata hivyo hakuwa tayari kuandikwa jina lake gazetini.

Mbunge huyo alilieleza gazeti hili pia kwamba, alishangaa katika kikao hicho kuona watu waliokuwa mstari wa mbele kuwanyoshea vidole wenzao kwa ufisadi wakiwa kimya kabisa wakati wote wa semina, huku wengine wakikwepa kuhudhuria mkutano huo kwa kutoa sababu tofauti.

‘‘Hawa akina Sitta (Samuel) jeuri yao iko ndani ya Bunge, wakifika katika vikao vya chama wanafunga midomo. Sitta hakuzungumza chochote ndani ya Bunge na mpambe wake Kilango alikimbia kabisa kikao cha CCM,” alisema mbunge huyo kwa kujiamini.

Mmoja wa watuhumiwa wakubwa wa ufisadi aliyezungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki iliyopita kwa sharti la mazungumzo hayo kubakia siri, alisema wamedhamiria kupambana kufa na kupona ili kuhakikisha wanasafisha majina yao ambayo alisema yamechafuliwa kwa kuzushiwa ufisadi.

‘‘Nadhani tunayo haki ya kujibu, hatuwezi kukaa kimya wakati hawa jamaa wamejipanga kutumaliza... nachoweza kusema ni kwamba CCM ya Kikwete ‘is too soft’, kwani naamini watu kama akina Kilango (Anne) walipaswa kufukuzwa katika chama kwa kutuzushia. Wewe hukuona jinsi Anna Abdallah alivyomshughulikia?” alisema mwanaCCM huyo ambaye anatajwa kuwa mmoja wa marafiki wa muda mrefu wa Kikwete.

Alipoulizwa ni njia gani watakazotumia ili kuhakikisha wanafanikiwa kuwashinda wapinzani wao hao, mwanaCCM huyo alisema: ‘‘Tutatumia vyombo hivi hivi vya habari wanavyovitumia kutuchafua. Tutajibu kila tuhuma, tumechoka kushambuliwa kwa kuzushiwa.”
 
Sasa naliona wazi kama haya ni ya kweli, basi ni suala la muda nadhani JK inawezekana amekubali rasmi kuwa katika kundi la MAFISADI. Ongeleni JK, wananchi wako tutasimama imala kuhakikisha mafisadi wanakamatwa tu na sheria inachukua mkondo wake.

Nafikiri wakati wa Plan B uliotabiliwa toka mwanzo unaweza kuonekana wazi.
 
Back
Top Bottom