Kitu gani kinafanya watu wa Asia Mashariki (Wachina, Wajapan, Wakorea) kuwa na akili nyingi kushinda jamii nyingine zote duniani?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,028
12,344
Hivi ni kitu gani ambacho kinacho pelekea hawa watu kutoka mashariki mwa Asia wachina, wajapan, wakorea kuwa na akili nyingi kushinda jamii nyengine zote duniani ?

Hii ni kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, hivyo nilikuwa nauliza ni kitu gani kinacho pelekea hawa watu kutuzidi sisi wengine wote.
 
Hivi ni kitu gani ambacho kinacho pelekea hawa watu kutoka mashariki mwa Asia wachina, wajapan, wakorea kuwa na akili nyingi kushinda jamii nyengine zote duniani ?

Ukweli ni kwamba hao watu si kwamba wana uwezo wa akili kushinda jamii nyingine duniani bali wanatia nia na juhudi katika mambo wanayoyafanya...

Kiakili Wachina ni maamuma kuliko hata Waafrika, lakini linapokuja suala la determination, perseverance wanatuzidi mbali sana...

Kama hao jamaa wangelikuwa na uwezo kiakili kushinda jamii zote, basi wangekuwa vinara wa ugunduzi wa maarifa na kanuni nyingi za kisayansi lakini haipo hivyo...
 
Hivi ni kitu gani ambacho kinacho pelekea hawa watu kutoka mashariki mwa Asia wachina, wajapan, wakorea kuwa na akili nyingi kushinda jamii nyengine zote duniani ?

Hii ni kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, hivyo nilikuwa nauliza ni kitu gani kinacho pelekea hawa watu kutuzidi sisi wengine wote.
kitu cha kwanza, wanakula sana vyakula vinavyoboresha ubongo wakati wa ukuaji, sea food. pili, wanasisitiza sana watoto wao wasome na wanajali sana elimu. korea kusini kwa mfano, vifo vingi vya kujirusha gorofani vinatokana na wanafunzi ambao hawajafaulu mitihani. kitu kingine, ni kuzaa watoto wachache unaoweza kuwatunza na kuwapa mahitaji yote kuanzia chakula, shule za awali hadi vyuo vikuu, kingine ni mifumo yao ya elimu, mtu anasoma kile anachoenda kukifanya na miundombinu inawasapoti. pia, wanatumia sana suppliments. hata hapa kwetu tungekuwa hivyo watu wangetuona kuwa tuna akili nyingi.

tofauti na bongolala, tunakula ugali, viazi, magimbi, michapati, hatuli nyama ya kutosha, hatuli samaki za kutosha kwasababu hatuna pesa. familia za asia samaki kila siku wanaweza kuwepo, bongo kwa wiki unaweza kununua smaaki kidogo sana na mnagombania na watoto (badala ya kuwaaahca watoto wale). vyakula vyetu vingi havina madini ya kukuza ubongo wa watoto vizuri.
 
Siri kubwa ya hao jamaa iko kwenye mambo matatu tu.
1. Juhudi (wanapambana mnoo kufanya kila kitu kinachowahusu katika maisha yao pasipo kuchoka)
2. Nidhamu (kwenye muda, kazi, maisha ya kila siku)
3. Makuzi (wako makini mnoo kukuza watoto wao katika njia za kimaisha, kielimu na kitamaduni watakayopaswa kuja kuishi siku zote)

Jamii yoyote ile iliyojikita kwenye hiyo mitazamo mitatu itaonekana kuwa na akili na maarifa makubwa. Fanya hivyo wewe na familia yako, baada ya miaka kumi tu watu watakuja kuhadithia namna mlivyo na akili na maarifa au kufanikiwa.
 
Mchina huyu huyu anae copy na kupaste
Kama kukop na ku paste sio akili jaribu wewe bro.

Naomba ukopi tu hata kiberiti au toothpick

Bro hao jamaa ni akili sana bila mchina leo maisha ya Waafrika yangekuwa mabovu sana. Imagine ungevaa mtumba nguo 100% mpk leo

Imagine leo unacheki flat screen kwa sh. Laki 2 tu. Smartphone hadi kwa elfu 50 tu. Imagine bila mchina na ushindani wake, awepo LG, Sony na Samsung flat screen ingekuwa ndani kwa Mo tu na wenzie

Smartphone wangemiliki wateule tu dunia hii. Imagine Apple tu na Samsung na Sony ndio wangekuwa wazalisha Smartphone.

Ashukiriwe mchina sana. Leo wakandarasi hawanunui tena escavator ya CAT used kwa million 500tsh. Mchina anakupa Ligong Mpya kwa milioni 350

Ngoja niishie hapa kwanza ila wachina akili 100%
 
Kwamba sisi jamii zengine zote duniani tuliobaki hutuweki nia na juhudi ?

Huwezi linganisha juhudi za hao jamaa na za jamii nyingine...

Hao jamaa wakikomalia kitu lazima wakifanikishe, iwe kwa namna yeyote ile...

Nimeishi na kusoma mashariki ya mbali muda mrefu tu miaka ya nyuma, katika madarasa kulikuwa na jamii za Wachina, Wakorea, Wajapan, Wazungu na Waarab (haswa Wapalestina), na sisi Waafrika tulikuwa tunawakimbiza vizuri tu haswa kwenye masomo ya sayansi pamoja na elimu zetu za kumeza...
 
Siri kubwa ya hao jamaa iko kwenye mambo matatu tu.
1. Juhudi (wanapambana mnoo kufanya kila kitu kinachowahusu katika maisha yao pasipo kuchoka)
2. Nidhamu (kwenye muda, kazi, maisha ya kila siku)
3. Makuzi (wako makini mnoo kukuza watoto wao katika njia za kimaisha, kielimu na kitamaduni watakayopaswa kuja kuishi siku zote)

Jamii yoyote ile iliyojikita kwenye hiyo mitazamo mitatu itaonekana kuwa na akili na maarifa makubwa. Fanya hivyo wewe na familia yako, baada ya miaka kumi tu watu watakuja kuhadithia namna mlivyo na akili na maarifa au kufanikiwa.
umenifurahisha hapo, umeongea point nzuri, makuzi, vile unavyomkuza mtoto ndivyo anavyokuja kuwa. mfano, waarabu namna wanavyowakuza watoto wao mlengo wao wote unakuwa kwenye dini hata elimu kwao ni mbadala tu, ndio maana hawajawahi kutoa invention yeyote duniani. hata mafuta ni Mungu tuamewawekea wachote.
 
Back
Top Bottom