Utofauti kati ya Elimu na Akili

Kuwite94

Member
Oct 10, 2016
16
117
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.

Kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni walichofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.

Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.

Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.

Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakaweka utaratibu wa mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Kama huamini jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?

So mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, ni msaada kwa jamii kuliko mtu mwenye elimu lakini akakosa akili. Mark Zukerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.

Yeye ndiye mmiliki wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona "kawaida" darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao. Kama sio FB basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa wamezidiwa ujanja na "kijana" mwenye Akili.

Usijidharau kwa uchache wa madarasa ulionayo, unaweza kuwa na akili nyingi kuliko mwenye degree 4.

Kumbuka Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Jiulize ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree au PhD unayojivunia, kichwa chako kinabaki na nini?

Kama kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa "AKILI".
FB_IMG_1701289130047.jpg
 
- Akili ni uwezo wa kuchakata maarifa/ elimu.

- Elimu ni mapokeo au content zinazounda akili.

- Huwezi kutenganisha akili na elimu. Mtoto anapozaliwa anakua hana akili wala elimu, anaanza kupata akili pale anapoanza kuingiza maarifa/Elimu (both formal and informal)
 
Asikudanganye mtu, shule ni muhimu sana. Mark Zuckerberg went to Harvard. Don't ever forget that.

Ili mtu apate sifa za kitaaluma kuingia Harvard siyo lelemama; lazima shule hasa ipande akilini.

Isaac Newton to Cambridge.

Albert Einstein obtained his mathematics and physics teaching diploma from Swiss Federal Polytechnic institute in Zurich in 1900 and his PhD from the University of Zurich in 1905)

The problem is not school, but what is taught in school.

Can you name the best intellectuals and renown scientists in the recent past who never attended school?
 
Asikudanganye mtu, shule ni muhimu sana. Mark Zuckerberg went to Harvard. Don't ever forget that.

Isaac Newton to Cambridge.

The problem is not school, but what is taught in school.

Can you name the best intellectuals and renown scientists in the recent past who never attended school?
Best thread ever.
 
Inategemea na Elimu MTU anayopata Kwa nchi zetu Kama Tanzania Elimu ya chuo kikuu ni Kama darasa la Saba haina content za kumfanya mtu kuwa smart

Unafundishwa na lecturer anayeghairisha kipindi ili akatazame mpira Wa simba na yanga.

Akili ni bora kuliko Elimu Ila huwezi kuwa na akili bila kuwa na maarifa sahihi
 
Mtu anaweza kuwa na akili.na asiwe na elimu.Akili ni uwezo wa kuchakata taarifa na kuja na maamuzi sahihi...Elimu ni maarifa yanayokuwa induced...formally , informally, kwa kujua au kutokujua...
 
Akili ni Kama mwili usipoipa maarifa sahihi haifanyi kazi
Mtu anaweza kuwa na akili.na asiwe na elimu.Akili ni uwezo wa kuchakata taarifa na kuja na maamuzi sahihi...Elimu ni maarifa yanayokuwa induced...formally , informally, kwa kujua au kutokujua...
 
UKIONDOA DIPLOMA, DEGREE AU PHD ULIYONAYO, KICHWA CHAKO KINABAKI NA NINI?

Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.

Kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni walichofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.

Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.

Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.

Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakaweka utaratibu wa mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Kama huamini jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?

So mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, ni msaada kwa jamii kuliko mtu mwenye elimu lakini akakosa akili. Mark Zukerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.

Yeye ndiye mmiliki wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona "kawaida" darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao. Kama sio FB basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa wamezidiwa ujanja na "kijana" mwenye Akili.

Usijidharau kwa uchache wa madarasa ulionayo, unaweza kuwa na akili nyingi kuliko mwenye degree 4.

Kumbuka Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Jiulize ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree au PhD unayojivunia, kichwa chako kinabaki na nini?

Kama kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa "AKILI".View attachment 2829874
Albert hakuwa mwanasaikolojia ya akili. Alitoa maoni yake kama mtu meingine bila kkuzingatia afiti zinasemaje.
Elon Musk hutoa maoni ya kuwa digrii sio kigezo cha kufanikiwa na kuelewa mambo au ujuzi, watu wanaompinga humuuliza kwa nini kaweka kigezo cha digriii na PhD ili uajiriwe kwenye kampuni zake wakati kuna watu wengi duniani walio na digrii na wanavipaji.
Bloom anefanya tafiti kuhusu kujifunza na akapendekeza "NLOOM TAXONOMY" na baadae wanasayansi wakaleta " MODIFIED BOOM TAXONOMY" .
Albert hsna tafiti uouote ina sapoti statement yake. Ukumbukebhata theory zake xinapingwa na wanasayansi wenzake sio wote wanakubaliana nae.
Elimu knowledge, skill and altitude.
Intellect is menral capacity.
Intelligence is ability to learn

Nyerere alisema the purpose of education os to sharpen your mindbor intellect or space of mind.
Kuna vango moja labukutani lilianfika.
Thenputpose of educetion is to repkace an empty mind with annopen one!.
I direct oppose your arguments.
Your arguments are totaly "VAGUE".
Kwa nini ?
Huwezi kutenganisha akili na elimu. Vinaenda pamoja.
Hakuna mwanadamu anaweza kutenganisha elimu kwenye akili.
Akili ni kama sumaku, ina nasa kila kitu.
Akili ni uwezo wa kujifunza , kukumbuka, na kutumia.
Bwana Bloom alisisitiza sana namna ya kuzijenga hizo nyanja na namna ya kuzipima.
Wataalamu wa elimu wanasema kuna elimu rasmi na isiyo rasmi.
Kujifunza kuongea lugha ya mama ni elimu isio rasmi. Wewe kutokuwa na digriii, diploma, cheti haimaanishi huna elimu, bali una elimu isiyorasmi.
Hakuna mtu mwenye elimu asiekuwa na akili. Akili ni kigezo cha kupata elimu.
Akili zinachangia sana kupata elomu.
 
Mijdala inayobangua bongo si maarufu sana kwa kupata wachangiaji hapa JF kwa kipindi hiki.
Inawezekana elimu na akili ya kufikiri haipewi kipaumbele, wengi hatupendi kuumiza bongo, akili zimepungua au vyote kwa pamoja. Tegemea mwitikio mdogo ktk hii mada
 
Back
Top Bottom