Ni Asubuhi tulivu ya siku ya Alhamisi.

Kiongozi mkuu wa Upinzani Freeman Mbowe anatarajiwa kuletwa mahakamani Kisutu Leo katika Kesi ya Ugaidi
Kesi zote za Kigaidi Duniani huendeshwa kwa umakini mkubwa, na ulinzi huwa unaimarishwa. Hakuna mihemko katika hili

Hili suala ni vyema NYUMBU wakalielewa, hapa ni hoja za Kisheria tu, maandamano, mabango huwa hayamnusuru mtuhumiwa wa Ufadhili wa Ugaidi au Gaidi mtekelezaji.

Gaidi hawezi kutetewa Kigaidi, hutetewa Kisheria.
 
Hivi unamkumbuka mdude alijigamba vipi baada ya kusamehewa? Kiongozi gani anakubali maneno ya kejeli kama hayo. Midomo inawaponza
Kama hamtaki kukosolewa, hata kama unaona ni kwa maneno ya kejeli, achieni madaraka, au mtakufa kwa magonjwa ya stress!
 
Hata nyie kubali vipigo acha kulalamika kama visimbe
Nani amelalamika? Wewe Una uvumilivu gani, sukumagang? Maneno tu unalialia eti kejeli, kama kibao kikikugeukia ujikute Wewe ndo unapaswa kukubali vipigo, utavumiliaje?!
 
Namnukuu mwanakijiji mmoja kutoka ukerewe

"John Pambalu asingekubali kufanya Kazi na mwenyekiti muhujumu uchumi na Gaidi"

Mwisho wa kunukuu.

My take
Malipo ya uzalendo na kupigania haki ni kupewa kesi za uhujum uchumi na ugaidi.

Tunapo sema mbowe ni Gaid tusishangae utalii na uwekezaji kushuka maana Tanzania tuna hifadhi magaidi........Hizi siasa za kuitana magaidi zipigwe na wote wapenda amani...
 
Ni Asubuhi tulivu ya siku ya Alhamisi.

Kiongozi mkuu wa Upinzani Freeman Mbowe anatarajiwa kuletwa mahakamani Kisutu Leo katika Kesi ya Ugaidi.

Kesi hii inavuta kila mpenda haki na mwanademokrasia kutokana na ukweli Mbowe amebambikizwa kesi hii ili kumnyamazisha kutokana na Kampeni aliyoasisi ya Kudai Katiba Mpya...
Ushauri.
1. Naomba kwa unyenyekevu mkubwa na moyo wa uzalendo haki tendeka.
2. Mh. Rais wa JMT SSH ulishakemea ubambikizaji wa kesi kwa wananchi hivyo basi tunakusihi usimamie na kuyaishi ya maneno yako.
3. Mtaani ukitembea wananchi wanaanza kuwa na mioyo migumu. Wanaanza kubaini makosa yanayo fanyika na kuhoji. Taratibu wanakomaa.
4. Leo haya yanafanyika kwa faida ya nani? Marehemu Samwel Sitta alisema "mwanasiasa lazima mawe na ngozi ngumu"!
5. Turuhusu siasa za ushindani na hapo ndipo mambo yatanyooka, hata wewe utafanya kazi bila bughudha huku ukiwa na watetezi wa kweli nyuma yako.
6. Nyufa kwenye nyumba zinaendelea kushuka kwenye msingi.
 
Hivi unamkumbuka mdude alijigamba vipi baada ya kusamehewa? Kiongozi gani anakubali maneno ya kejeli kama hayo. Midomo inawaponza
Mdude alisamehewa ama alishinda kesi? Vijana wa CCM ni majuha sana.
 
Wapenda amani kote nchini na wazalendo wa nchi popote pale walipo kamwe tusikubali hawa wahuni wachache wanao jifanya wanadai haki kwa kuvunja sheria watuharibie Amani ya nchi yetu.
tuchukue hatua za kuwafichua na kuwa ripoti popote pale walipo.
sio wafuasi wote wa chadema wanafurahia uhuni huu bali wapo wahuni wachache wenye chembe chembe za Ugaidi/uhalifu/ujanbazi/wizi ndio wanafanya vitendo hivi vya kihuni ili wapate sababu.
 
Mchumia tumbo mamboleo. Ubinafsi ndio moyo wake, haki ya wengine kwake sio ya msingi. Jambo la msingi yeye ashibe hata kama wengine wanaumizwa vipi.!
 
Back
Top Bottom