Kipondo havi kwa shemeji....

mkuu naona familiya yenu hampo pamoja'yaani hakuna upendo wa kweli'huyo dada laabda anaishi na huyo bingwa kwa sababu za kiuchumi'ningekuwa mimi ningeondoka na dada kurudi home
 
afu na mtoa mada nae, talaka haidaiwi chumbani! huyo bidada si aondoke talaka itamfuata huko aliko? mi nakasirika kweli mwanamke kushindwa kujitambua!

mkwe hapo ndipo ninapozidi kukulove...
Toka lini talaka ikabembelezwa jamani!
Kuna mdada naye alikuwa anakula vichapo vya kutosha kila wakisuluhisha jamaa hasikii, bidada akavua pete la ndoa akalitupilia mbali. Akamwambia kama pete ndio identity ya ndoa basi pete yako hiyooo.
 
Kuna dada etu kaolewa dom lakini tangu kaolewa miaka 3 iliyopita amekuwa akichezea kichapo sana tokakwa mumewe ambaye ni mlevi na mkorofi sana ameshamvunja mkono dada mara mbili kwa kipigo..nipo dom kwa mapumziko na nilienda kumtembelea dadangu ambae ana p.o.p mkono wakushoto kwa kipigo cha mumewe nilipo muuliza ni kwa nini iwe hivo na ndugu wanasemaje akasema ndugu washachoka kuamua mana wakati mwingine nao huambulia vitisho kama si kipigo toka kwa njemba hiyo...mbaya zaidi jamaa amegoma hata kutoa talaka...sasa wakati tukizungumza na dada mara shem kaingia na kuanza na kejeli na dharau zake kwangu eti tunamfatilia sana na maisha yake n mke wake mara ooh ntaoa uko mzima nilipomwambia ajiheshimu ndo kama kapata sababu nilikua nakunywa chai akachukua ile chai na kunimwagia na maneoo kibao ya kashfa dada kuona vile akaingilia kati maskini kunitetea dah! Alisukumwa na kukanyagwa vibaya aisee nilipata hasira mbaya nilichomfanya huyo jamaa sasa hivi yupo moi nilivunja mguu na mkono....sasa kimbembe kimekuja ndugu wa huyo ***** na wangu kuna bifu kubwa na kibaya zaidi baadhi ya ndugu upande wangu wanaunga mkono upande wa pili eti kwa nini naingilia ndoa za watu...kesi iko polisi na kesho kuna kikao hapa hom kizito....hebu nambieni waungwana nisimamie wapi' na je nilichokifanya ni kosa?

Kama unachoeleza ni kweli kilitokea naona huyo shemeji yako alipitiliza mipaka ya kuheshimiana. Kitendo cha kukutupia maneno ya kashfa, kukumwagia chai mbele ya dada yako na kisha kuanza kumshambulia dada yako mbele yako kilipitiliza mipaka ya uungwana na hakivumiliki. Kwa mtazamo wangu ulichofanya ni kumshikisha adabu na kumwonyesha kuwa kuna mipaka ambayo hatakiwi kamwe kuivuka. Siku nyingine atafikiria mara mbili kabla hajaamua kuvuka mpaka. Labda baada ya yeye kupokea kipigo na kuvunjwa mkono atajua ni maumivu kiasi gani anampatia huyo dada kwa kumpa vipigo na kumvunja mikono kila mara. Nadhani ningekuwa mimi katika viatu vyako ningetoa adhabu kama hiyo au hata zaidi kwa huyo jamaa.
 
Dodoma mbali halafu leo nimekuota tunapita milima na mabonde halfu kuna maua meeeeeeeeeeeengi ya rangi nyekundu na njano yaani we acha tu ukimaliza kusoma futa MJ1 asione maana muda kitambo najua TF atanitumia ila advance ya mahari ya Loner.

hahahahaha! Umeanza uchokozi heartbreaker. Ngoja nimwamshe MJ1 nikusemee.
 
Niliposoma heading nilidhani inazungumzia mtu ninayemfahamu, lakini seems matatizo yanafanana.
Shemeji yangu wa kike amenasa kwenye tundu bovu, na ndoa haina hata nusu mwaka lakini jamaa yake anamtenda kama msimuliaji anavyobainisha kwa dada yake. Ila shemeji yangu ameamua kufa na tai shingoni ( Jamaa anapiga wala hajali kama mkewe ana kiumbe tumboni)

Tatizo lililopo kwenye jamii ni namna hawa akina mama wanavyojua kuficha maovu ya watesaji wao ambapo huishia either kujeruhiwa ama kufa ama kupata ulemavu kabisa. Sheria ya ndoa ipo wazi kabisa kuhusu hizi brutality zinazoendelea kwenye bedrooms zetu. Women (and men) you must step out and speak it loud ili muweze kuokoa ndoa zenu na maisha yenu.
 
ubaya haulipwi kwa ubaya sangara. Kwani hakukuwa na namna nyingine ya kumaliza tatizo?

Husninyo, ulichoongea ni kweli kabisa lakini kuna mazingira ambapo reaction ya mtu inategemea sana na action iliyochochea reaction husika. Najaribu kuangalia mtiririko wa matukio katika mazingira haya naona kama huyo shemeji mtu hakumpa mysteryman option yeyote zaidi ya hiyo aliyoichukua.

Kila nikijaribu kutafakari kilichotokea sioni ni hatua gani nyingine huyo mysteryman angechukua. Wewe fikiria umekwenda kumtembelea dada yako ambaye anauguza jeraha la kuvunjwa mkono kwa kipigo cha mumewe. Wakati mnaongea anakuja shemeji yako na kuanza kukutupia maneno ya kashfa na matusi ikiwemo kuwa ataoa ukoo mzima - yaani na wewe ukiwemo. Kana kwamba hilo halitoshi anakumwagia chai na huyo mgonjwa uliyekwenda kumtembelea anapojaribu kuingilia kumsihi mme wake asiendelee kukudhalilisha na yeye anapokea kipondo kikali zaidi mbele yako bila kujali kuwa mkono wake umevunjika.

Option nyingine ingekuwa ni mysteryman kunyanyuka na kuondoka taratibu akimuacha dada yake akiendelea kuchukua kichapo toka kwa mumewe mbabe. Je huu ungekuwa ni uamuzi sahihi?
 
ishu ni kwamba uwepo wake pale umesababisha kwa kiasi kikubwa hayo yote yatokee. Kwanini huyu kaka asingetulia kwake? Dada mtu ameshajichagulia hayo maisha ya u-tyson. Jamaa anaona amemdhibiti shemeji lakini hiyo haitorejesha amani katika ndoa hata kidogo. Kifupi jamaa, shemeji na dada wote wana makosa. Sioni haja ya kumpongeza jamaa alichokifanya otherwise aje mwanasheria aniambie kisheria sister wako akidundwa kumvunja mguu na mkono shemeji inaruhusiwa.
Ngoja nitafute na watu wa imani waniambie.

Kwanza kaka mtu hajafanya makosa kwenda kumtembelea ndugu yake. Pili, hata kama dada mtu amejichagulia maisha ya ubondia basi mume angempiga mke in the absence of her brother kama tukiconsider privacy ya maisha yao! Tatu, presence ya kaka mtu haijasababisha ugomvi ila dharau za mume ndo zimepelekea mpaka hayo yote yatokee, nasema hivyo coz kulikua na kila sababu za mume kuendelea na shughuli zake binafsi bila hata kutoa kejeli kwa kaka mtu na kwakuwa mnyonge wake ni mkewe basi angesubiri kuwasilisha dharau zake kwa huyo huyo mkewe kama kweli alikuwa hataki ugomvi na shemejie! Nne, wote wamegombana ila shemeji mtu kazidiwa nguvu mpaka akavunjwa mguu hivo kuvunjika kwa mguu ni outcome ya purukushani za ugomvi(definatly) na wala kaka mtu hakuushika ule mguu akauvunja wakati shemeji mtu akiwa ametulia tu anaangalia mguu wake ukivunjwa! Finally, sidhani ka kuna sheria inayosema exactly kuwa dada yako akipigwa basi umvunje mguu shemejio but kuna exceptions. looking on the source provocation is applicable, and according to the circumstances of the fighting that is self defence!
 
Ifike mahali wanawake tuwe tunajitetea
inafikia unavunjwa mkono mara mbili bado
unaishi na katili kisa nimefunga nae ndoa.
Mkuu ulivyofanya ni sawa na kwenye kikao ukienda
usibabaike, eleza kilichotokea mpaka kufikia kuvunjana
mkono na mguu ulokataa kujiunga tena.
 
hapa nadhani kuna mlolongo wa matukio yanayohusu zaidi ya wanandoa (namaanisha ndugu) na inaonekana jamaa alipoenda kumsalimia dada yake mwanaume alihisi kuna uchochezi unaendelea au yawezekana jamaa anamjua kaka mtu jinsi alivyo kwa hiyo akaamua kuanza kumshambulia kwa kujua au kwa kujaribu kulinda nyumba yake ..

mkuu kwa hali ya namna hii ulitakiwa kutimka uwaachie wanandoa .. leo hii umemvunja shemejio mkono kesho ukimkuta amemshika dada yako kiuno na wanateta utachukua hatua gani??? kumbuka wewe ni ndugu na yule ni mme wa dadayo hivyo kila mmoja ana nafasi yake kwa wakati wake
 
Nashkuru sana wakuu kwa kila wazo ntayafanyia kazi na kikao ni saa nane nitawapa updates za kikao na kila kitachoendelea
 
hapa nadhani kuna mlolongo wa matukio yanayohusu zaidi ya wanandoa (namaanisha ndugu) na inaonekana jamaa alipoenda kumsalimia dada yake mwanaume alihisi kuna uchochezi unaendelea au yawezekana jamaa anamjua kaka mtu jinsi alivyo kwa hiyo akaamua kuanza kumshambulia kwa kujua au kwa kujaribu kulinda nyumba yake ..

mkuu kwa hali ya namna hii ulitakiwa kutimka uwaachie wanandoa .. leo hii umemvunja shemejio mkono kesho ukimkuta amemshika dada yako kiuno na wanateta utachukua hatua gani??? kumbuka wewe ni ndugu na yule ni mme wa dadayo hivyo kila mmoja ana nafasi yake kwa wakati wake

u mean kutimka na kumwacha dada akipata kichapo pengine kufa eti kisa ni wanandoa?? Ina mana unaweza kaa ukishangilia mwanao akichezea kichapo wewe....
 
Ifike mahali wanawake tuwe tunajitetea
inafikia unavunjwa mkono mara mbili bado
unaishi na katili kisa nimefunga nae ndoa.
Mkuu ulivyofanya ni sawa na kwenye kikao ukienda
usibabaike, eleza kilichotokea mpaka kufikia kuvunjana
mkono na mguu ulokataa kujiunga tena.

Natamani niwe wakili wake aisee...tena bure kabisa simdai hata shilingi! HUyo jamaa anatakiwa apo alipo moi awe na pingu na ulinzi akitoka tu Keko! khaa

Mi nadharau sana mwanaume anayejidai mwanaume kwa kumpiga mwanamke...mwanamke hapigwi kwa ngumi na mateke hili liko wazi...wana namna zao za kuwapiga au sio DaMie?
 
Niliposoma heading nilidhani inazungumzia mtu ninayemfahamu, lakini seems matatizo yanafanana.
Shemeji yangu wa kike amenasa kwenye tundu bovu, na ndoa haina hata nusu mwaka lakini jamaa yake anamtenda kama msimuliaji anavyobainisha kwa dada yake. Ila shemeji yangu ameamua kufa na tai shingoni ( Jamaa anapiga wala hajali kama mkewe ana kiumbe tumboni)

Tatizo lililopo kwenye jamii ni namna hawa akina mama wanavyojua kuficha maovu ya watesaji wao ambapo huishia either kujeruhiwa ama kufa ama kupata ulemavu kabisa. Sheria ya ndoa ipo wazi kabisa kuhusu hizi brutality zinazoendelea kwenye bedrooms zetu. Women (and men) you must step out and speak it loud ili muweze kuokoa ndoa zenu na maisha yenu.

Asee Paw pamoja na kusoma kwa woga woga hii post yako (haikawii kuwa ya kumpa mtu ban) unamaanisha kuwa anyefanya izo mambo ni kaka yako au ndugu wa damu? hebu fanya mpango bana umtoe huko kuzimu shemeji yako na hatakusau!
 
  • Thanks
Reactions: Paw

Paw anatisha eeh?
 
u mean kutimka na kumwacha dada akipata kichapo pengine kufa eti kisa ni wanandoa?? Ina mana unaweza kaa ukishangilia mwanao akichezea kichapo wewe....

je huwa unawatembelea mara kwa mara??
je walishawahi kukuhusisha katika magomvi mengine??
wewe maelewano yako na shemejio yakoje???
 
Yaani nakupongeza kwa ulichokifanya nadhani hiyo ni fundisho tosha kwa huyo shemejio akipona hatorudia tena na atasimulia hadi uzeeni kwake. Ila hao nduguzenu wanaomwabudu huyo shemejio ni wa******* yaani wanamwona wa maada sana kuliko damu yao hawana akili kabisa mwambie dada yako aenda TAMWA, Usawi wa jamii ama kweye hizNGO's zetu za mwasuala ya haki kwa wanawake atasikilizwa, na kama wazazi wenu wapo mwambie mama yenu asimamie kidedea kuhusu kunyanyaswa kwa bintie hao wanaoshabikia manyanyaso hayo kama ni wanawake basi hawajazaa na hawajui uchungu wa mwana ukoje na kama ni wanaume hawajui uchungu wakulea watoto. kwa mzazi yeyote mwenye kuzaa na kulea mtoto hawez kushabikia huu ujinga wa huyo shemejio...
 
Ndugu wa jamaa wamekuja na defender ya polisi tunaelekea polisi by now.....ntawajuza kinachoendelea
 
Back
Top Bottom