Nimetoka kusuluhisha ugomvi mkubwa wa Mdogo wangu na mke wake

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
988
3,318
Mara kwa mara nimekuwa nikipenda kuweka visa vinavyogusa maisha yangu hata marafiki na ndugu zangu ili mpate kitu cha kujifunza hapa

Mdogo wangu wa kiume ana mwanamke ambae alimuoa mwaka 2017, ni binti mstaharabu sana mwenye heshima sana maana hata nyumbani ukweni anapendwa sana na wazee na dada zangu pia,

Sasa kuazia mwaka 2020 tukawa tunaskia visa vya chini chini tu kuwa mdogo wangu amekuwa akimnyanyasa sana huyo binti na unyanyasaji alio kuwa nao ulikuwa ni wivu kupitiliza na kufanya binti kuwa kama mfungwa maana alikuwa hataki afanye kazi yoyote wala kutoka nyumbani akiamini akitoka ataenda kupitiwa na wanaume wengine

Wiki iliyopita ulitokea ugomvi mkubwa dogo alimpiga yule binti nusu amuuwe ikabidi familia upande wa mwanume na kwao upande wa mwanamke tufunge safari kuja Dar kujua tatizo ni nini na kusuluhisha pia, hivyo tulivyofika kikawekwa kikako kikubwa ili lijulikane jambo lililopelekea Bro kufanya kitendo kibaya kama kile ambacho si jadi yetu.

Dogo alipopewa nafasi aeleze nini shida, akasema kuwa mwanamke wake, kwa muda wa mwezi sasa amekuwa akitaka watengane kwa amani ili migogoro na wivu uliopotiliza isiendelee na kila mtu awe na amani na maisha yaendelee, akasema kuwa kitendo hicho kilimfanya amuhisi mkewe kuwa tayari ana mwanaume mwingine hivyo alikuwa anatafuta sababu tu watengane na akiangalia kasha mgharamia vitu vingi hivyo akajikuta mkono umeteleza akamshushia kipigo lakini anajutia

Ikabidi tuje na kwa upande wa Binti tumskilize na yeye atoe maelezo yake tujue mwenye tatizo ni nani, hapa ndipo tulipoaibika maana mambo aliyoyaongea binti tulijikuta sisi kama upande wa mwanaume tunaaibika mbele ya ndugu wa mwanamke

Binti uvumilivu ukamshinda ikabidi afunguke yote, akasema kuanzia wameanza kuishi wote mwanaume alijiingiza kwenye matumizi ya mirungi sijui wanaita gomba kupitiliza, asasema akirudi kazini kazi yake ikawa ni kukaa nnje anasaga mirungi hadi sa tano au sita za usiku kila siku akawa anashindilia mirungi tu na Sigara, ndani anakuja kulala saa sita or saba usiku

Binti akasema kuwa aliendelea kumvumilia tu na kila alipomshauri aache kutumia hivyo vitu akawa anaambulia maneno makali

Akasema kuwa ikafika kipindi akawa amebadilika kabisa yani hata kitandani uwezo wa kufanya mapenzi hadi kumridhisha ukawa umepotea kabisa yaani akifika chumbani ni kulala tu hamu ya mapenzi na nguvu ya kufanya mapenzi ikapotea kabisa hvyo kilichofuatia yakawa ni maisha ya wivu tu sababu alikuwa hamridhishi kitandani.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili ikaonekana Mwanaume ndio ana matatizo tena sio madogo ni makubwa, Upande wa Binti ukagoma kusulihisha wakasema wanaondoka na mtoto wao wanaogopa atakuja kukatwa na mapanga aje auliwe huko mbeleni na wameondoka nae kweli.

Mzee kwa Hasira akamwambia Bwanamdogo kuwa amepoteza mwanamke mzuri kwa ajili ya uzembe wake, akamwambia kuwa yule mwanamke alivumilia sana pasipo kutafuta mapenzi nnje akiamimi atabadilika lakini Dogo hakubadilika.

Akamwambia kuwa akipata mwanamke mwingine kichaa kwa tabia zile atamletea mwanamme mwingine chumbani kwake pale pale atamsaidia kazi vizuri.

Wakuu tumeaibika sana hapa tupo kwenye basi na wazee tunarudi mkoa kwa aibu kali sana , tumeaibika sana, mzee wetu amekasirika sana anasema ni heri Bwanamdogo angemueleza tu ukweli kwenye Simu asingekanyaga ardhi ya Dar kufuata aibu kama ile
 
Sema veve ukiizoea ina addiction aseee ukifika ule mda wake unapata arosto mbaya mbovu.

Mkuu nyie ni Warangi? Maana hao watu wanapenda sana kuchanja veve/miraa/mirungi/gomba.
Aisee pale Kolo - Kondoa hali ni mbaya sana. Nilipita hapo jana karibu kila mtu anakula gomba aka mirungi! Yaan si bodaboda kijana au mzee wote midomo inatafuna vitu!
 
Kwa hiyo binti malalamiko ni kuwa haridhishwi. Hiyo ndiyo point ya msingi. Haridhiki na alitaka waachane. Mdogo wako pamoja na mapungufu na kuwa sababu ni yeye ya kutokuridhika kwa mwanamke ila yupo sawa kuhisi alilohisi.
Hamridhishi alafu hataki afanye kazi na anamshushia kipigo kamvumilia miaka 4, pasipo kumfanyia uhuni
 
Hivi kutafuna mirungi kuna faida gani, maana unakuta jitu limejaza majani mdomoni kama mbuzi
Mirungi huaribu sana nguvu za uume, wakati mwingine ktk hii dunia si kila kitu ni cha faida na chakuigwa.

Ona sasa Mke mwema kabisa anakosa Mume sahihi na kuachwa njia panda.

Mungu ni mwema sana kuniepusha na ulevi wowote wa sigara, bangi, kokein, shisha, pombe, pornography na uzinzi wa Wanawake na hata hii mitandao ya kijamii.
 
Mara kwa mara nimekuwa nikipenda kuweka visa vinavyogusa maisha yangu hata marafiki na ndugu zangu ili mpate kitu cha kujifunza hapa

Mdogo wangu wa kiume ana mwanamke ambae alimuowa mwaka 2017, ni binti mstaharabu sana mwenye heshima sana maana hata nyumbani ukweni anapendwa sana na wazee na dada zangu pia,
Mmeondoka bila kutatua tatizo lililowaleta! Mlitakiwa dogo mumpeleke hospitali ya serikali kwenye tiba ya mateja.
Pia kaka ungebaki nyumbani pao kumhamasisha dogo arudishe hamu asikiapo chaga za kitanda zikilia ukimgegeda shemeji yako, tiba hii ingemponya haraka sana kuliko maombezi.
 
Back
Top Bottom